UZALIWA WA KWANZA WA MWILI WAKO UMEMUUZIA NANI
❤( Kijana Ongeza Umakini Hapa) ❤
Ev. Elisha Kazimoto
0755444078
💰Shalom, Shalom watakatifu wa Bwana, Leo ma kuletea ujumbe huu wa Uzaliwa wa Kwanza wa mwili wako, _Vijana wa kike na wa kiume ambao hamjaingia katika Ndoa, wazazi wenye watoto, watumishi mnaosimama madhabahuni (mnaolea kundi la Bwana) fatilia somo hili kwa umakini, ili Turudishe matumaini ya Ndoa takatifu, Wokovu sahihi wenye nguvu (Impacts) kwa ufalme wa shetani_
*Uzaliwa wa Kwanza Ulibeba Nguvu ya Baraka Kwa mtoto iliyoendesha maisha yake kwa mafanikio na furaha kuu*
*MWANZO 25:29-34*
29 _Yakobo akapika chakula cha dengu. Esau akaja kutoka nyikani, naye alikuwa amechoka sana._
30 _Esau akamwambia Yakobo, Tafadhali, unipe hicho chakula chekundu nile, kwa kuwa ninazimia mimi. Kwa hiyo walimwita jina lake Edomu._
31 *_Yakobo akamwambia, Kwanza niuzie leo haki yako ya mzaliwa wa kwanza._*
32 *_Esau akasema, Tazama, mimi ni karibu kufa, itanifaa nini haki hii ya uzazi?_*
33 _Yakobo akamwambia, Uniapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza._
34 *_Yakobo akampa Esau mkate na chakula cha dengu, naye akala, akanywa, kisha akaondoka, akaenda zake. Hivyo Esau akaidharau haki yake ya mzaliwa wa kwanza._*
⚽ *Ziko Aina 3 za Uzaliwa wa Kwanza*
1⃣ _Uzaliwa wa Kwanza wa Kutoka tumboni mwa mama kama mtoto wa kwanza katika Familia_ ( *Ukubwa*)
2⃣ _Uzaliwa wa Kwanza wa Wokovu tulio upata mara moja tu kwanjia ya Yesu Kristo( *Utakatifu*)
3⃣ Uzaliwa wa Kwanza wa Mwili wako/ ujana wako ( *Ubikra*)
⚽ Aina zote hizi zina nguvu kubwa katika maisha mtu kama atakuwa mwamunifu kutouza Uzaliwa wa Kwanza wowote katika aina hizo, maisha yake lazima yawe ya furaha, ushindi, na kufanikiwa.
⚽ _Lakini pia, ukiuza moja wapo, au zote wewe maisha yako yatakuwa ya majuto, kukataliwa, yasiyo na utulivu wa moyo, kujihukumu na kudharauliwa na kupoteza Ndoto zako zote._
⚽1⃣ *UZALIWA WA KWANZA WA UKUBWA KATIKA FAMILIA*⚽1⃣
🌲Huu ulibeba baraka za Mungu kupitia mzazi, na aliye barikiwa alitembea kwa ushindi katikati ya ndugu zake.
🌲 Tumeona Esau anauza Uzaliwa wa Kwanza kwa njaa ya Chakula cha siku moja, Biblia inasema *Akaudharau Uzaliwa wa Kwanza* chakula cha mlo mmoja, kikapoteza *mfumo mzima wa maisha yako zaidi ya miaka 80 umri tuliopewa kuishi.
🌲Wakati anauza uzaliwa wa kwanza hakuona shida, Shida ilitokea pale alipo hitaji kutumia uzaliwa wa kwanza kwa faida ya maisha yake.
*Mwanzo 27:26-34*
26 Isaka, baba yake, akamwambia, Njoo karibu sasa, ukanibusu, mwanangu.
27 Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu ya mavazi yake, akambariki akasema, Tazama, harufu ya mwanangu Ni kama harufu ya shamba alilolibariki Bwana.
28 Mungu na akupe ya umande wa mbingu, Na ya manono ya nchi, Na wingi wa nafaka na mvinyo.
29 Mataifa na wakutumikie Na makabila wakusujudie, Uwe bwana wa ndugu zako, Na wana wa mama yako na wakusujudie. Atakayekulaani alaaniwe, Na atakayekubariki abarikiwe.
30 Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo, na alipokuwa Yakobo ndiyo kwanza ametoka mbele ya Isaka, baba yake, mara Esau ndugu yake akaja kutoka katika kuwinda kwake.
31 Naye pia amefanya chakula kitamu akamletea babaye, akamwambia baba yake. Babangu na aondoke, ale mawindo ya mwanawe, ili roho yako inibariki.
32 Isaka, baba yake, akamwuliza, U nani wewe? Akasema, Mimi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza.
33 _Isaka akatetemeka tetemeko kuu sana, akasema, Ni nani basi yule aliyetwaa mawindo akaniletea? Nami nimekwisha kula kabla hujaja wewe, nikambariki; naam, naye atabarikiwa._
34 *_Esau aliposikia maneno ya babaye, akalia kilio kikubwa cha uchungu sana, akamwambia babaye, Nibariki na mimi, mimi nami, Ee babangu._*
🌲👆Usiche na kupoteza Uzaliwa wa Kwanza, Kinacho mliza Esau ni nini? _Anajua kabisa Dira ya maisha yake imepotea kabisa_chakula hakikumbukwi kwakuwa kilikuwa cha muda, ila Uzaliwa wa Kwanza unaoshikiria future, (maishabyake yote) ndo hana Tena, hicho ndo kilikuwa kilio kikubwa cha uchungu kwa Esau.
*_Shika sana huu mfano utatufundisha kwa aina 2 zilizo baki za Uzaliwa wa Kwanza_*
⚽2⃣ *_UZALIWA WA KWANZA WA WOKOVU_*⚽2⃣
🌲Neema ya Wokovu tuliyoipokea kupitia Yesu Kristo ni nguvu kubwa ya kuendesha maisha yetu ya kiroho na kimwili kwa ushindi. _Kupitia Wokovu (maisha matakatifu, tunaomba na kujibiwa maombi yetu na Mungu_ *Yohana 9:31*, *Mathayo 7:7*
🌲Kwa maisha safi ya Wokovu (Uzaliwa wa Kwanza) tunayashinda malango ya kizimu na maadui wote( *Mathayo 16:18*, *Luka 10:19*
🌲 _Ukipoteza uzaliwa wa kwanza(Utakatifu), ukauza Uzaliwa wa Kwanza huu kwa zinaa, rushwa, pesa nk, utapoteza mwelekeo wa maisha na hutokuwa na maisha ya ushindi Tena, utaonewa na nguvu za giza milele na mwisho ni majuto ya maisha ya motoni jehanamu_
*Kupoteza uzaliwa wa kwanza huu, Biblia inasema kitakuwa kilio na kusaga meno, zaidi za kilio cha Esau. Kuwa makini, usibadirishane Wokovu na kitu chochote*
No comments:
Post a Comment