Tuesday, 29 November 2016

USICHEZEE MWILI WAKO TENA

🏹🏹 *USICHEZEE MWILI WAKO TENA*🏹🏹
   *_By. Ev. Elisha Kazimoto_*
    *0755444078*
🏹 _Haleluya watu mlio kombolewa na Yesu Kristo Bwana wetu, leo niseme na wewe juu ya thamani kubwa ya mwili wako huo, unaokufanya uendelee kufanya hayo yote unayo yafanya, yawe mema au mabaya_
🏹 Kuna wingu kubwa nyakati hizi la ushawishi kwa nguvu kubwa kutoka kuzimu la watu kuchezea miili yao kama mtoto achezeavyo matope, *Si vijana wa kiume, mabinti, watoto wa sekondari, primary siyo wana ndoa ni Rika zote* uharibifu umetanda na unaongezeka kwa kasi kubwa, watu wana Haribu miili yao, nini shetani anatafuta?  Anatafuta haya, *_Ukiharibu mwili wako, umeharibu makazi ya Roho wa Mungu, na makazi ya Roho wa Mungu yakiharibiwa mambo matatu yanatokea, 1⃣ Mauti ya Kiroho, 2⃣ Mauti ya mwili 3⃣Mauti ya mwili na roho._* Hii ndo hatari kubwa.( _Somo hili limeandaliwa na Ev Elisha Kazimoto-Mjumbe Mkali MITHALI 17:11_). Tusome andiko letu kuu👇👇👇
*1 Wakorintho 3:16-17*
_16 Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu?_ 

*_17 Kama mtu akiliharibu hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa maana hekalu la Mungu ni takatifu, ambalo ndilo ninyi._*
🏹Unajua kuwa mwili huo ulopewa ni vazi, linalo kaliwa na Roho wa Mungu alowekwa ndani yako, muda wowote vazi hilo likichakaa, likiwa chafu Linavuliwa na kutupwa? Halafu roho yako inaenda kuhukumiwa? ( *Kwa nini unachezea mwili wako? Unahisi unamamlaka na huo mwili? Tembelea makabulini tena ya watu maarufu ujue jinsi ambavyo hakuna mwenye mamlaka na huo mwili, isipokuwa Mungu*)
🏹 _Kwa nini unauchosha mwili kwa zinaa_? Imefikia hatua watu wameona kawaida kuvua nguo👉�👙kwa kila mtu, ili mradi mwili umehitaji, umekuwa na uhitaji wa pesa, mchumba ametishia kukuacha usipo mpa, mke/mme hakutoshelezi.. Kweli? Kweli? Unajua Thamani ya mwili wako hiyo na gharama aliyoilipa Yesu kukupa wokovu (uzima) ili pumzi yake ikae kwenye vazi safi na tulivu? Makusudi uishi miaka mingi ya furaha.👇👇👇👇

*_1 Wakorintho 6 : 20 - maana mlinunuliwa kwa thamani. Sasa basi, mtukuzeni Mungu katika miili yenu._*
🏹Umeanza zinaa ukiwa shule ya msingi, saizi uko chuo, hivi unahisi bado una ubora kama mtu ambaye amejitunza ameikataa zinaa? Haina haja ya kukufariji, *_Umechoka wewe, hata kama unavaa unapendeza, wewe ni mchovu tu! Unajitutumua na kuimba, kuhubiri ila wewe ni mchovu tu kiroho na kimwili, kaangalie jembe lililo lima kwa muda wa miaka 3,4,5...na yaweke pamoja na jembe jipya uone kama vinafanana!_*
🏹 Yaani umekuwa radhi, kiurahisi, kizembee kujiungamanisha mwili wako na kahaba? Hujui viungo vyako vyote vya mwili ni Mali ya Kristo? Sasa mbona umempa kahaba wa kike/kiume? ( _Maneno haya ni Roho tena Uzima, Ev Elisha Kazimoto mjumbe wa Bwana na Kuonya Badirika Utunze Mwili wako_).Tuendelee na somo,....Soma hapa👇👇👇👇👇
*_1 Wakorintho 6 : 15 - Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!_*
🏹 Unasikia raha unapopewa promise ya kukutana guest ili ufanye ngono na kahaba wako unaye mwita Girlfriend /Boyfriend au Mchepuko? _Unahisi huo mwili wa udongo ulijivika mwenyewe na unaweza kukomaa nao roho isiuache? Nakupa polee,_ maana kwanza umeisha choka, na bado wewe uliye kijana unaomba Mungu akupe mme/mke mwema mwaminifu, hiyo biashara mbona mahesabu yake hata mtoto wa chekechea anakupa jibu?  *(Utapata Kahaba mwenzio/Tapeli wa mapenzi)* upo kwenye ndoa unachepuka, na kwaya unaendelea kuimba, na Album umetoa, na  injili unahubiri, unahisi Mungu kasafiri nchi za nje na Usafiri wa kumrudisha ni mgumu maana kuna foleni, akija kurudi utakuwa umetubu!! Umejitapeli mwenyewe utavuliwa vazi hilo ghafla na ufikie kwa hukumu ya🔥🔥🔥🔥moto
🏹 Kuna lugha nyingi sana za kujifariji, mimi sikufariji, nakwambia kweli ya Mungu upone kama wewe niwa kupona,  _Kuna lugha za Nikajikuta Nimeanguka kwenye Zinaa, Nikazidiwa, Nashindwa Kujizuia_ *Hii ni faraja yenye sumu ndani yake, zinaa haishtukizi kama mtu anaye tembea kwenye utelezi akaanguka, dhambi ya kutendwa na watu wa wili ni Mpango(Process), inamaandalizi yakutosha, inamakubaliano, mpaka una chojoa nguo zote hata nguo hii👉�👙 ya ndani unasema bahati mbaya, nimejikuta! Usijifariji katubu umrudie Mungu* huwezi salimika. ( *_Tafuta somo langu la ZINAA SI YA BAHATI MBAYA nimeelezea hatua 11 zinazofuatwa kabla mpaka mwisho wa zinaa, huwezi sema Nikajikuta,_*)Utajikutaje wakati umepita Milango 11? Tafuta somo hilo By *Ev Elisha Kazimoto*
🏹 Biblia imesema wazi, kwa habari ya kuulinda mwili wako usichoke, usiharibu makazi ya Roho wa Mungu, Biblia imekupa Option ya kuikimbia zinaa👇👇👇👇
*_1 Wakorintho 6 : 18 - Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe._*
🏹Mara ngapi umeikimbia zinaa, pale ulipoambiwa tusipo fanya mapenzi nakuacha, ulichukua hatua gani? Ulipo ambiwa usipo lala nami kazi hakuna ulifanyeje, uliposhikwa maziwa na kiuno ulifanyeje, ulipo rushiwa sh. Laki 1ukaambiwa ya soda na hujaifanyia kazi ulifanyeje,? 👇👇👇
*_Waebrania 12 : 4 - Hamjafanya vita hata kumwagika damu, mkishindana na dhambi;_* You are entertaining the sin, that's a simple language.
🏹Makanisani injili inahubiriwa, kwenye media, and social media kama hizi hapa mafundisho yanapita, ila umekomaa nakujifariji eti _Mungu anajua mke wangu, mme wangu hanitoshelezi hapo kuchepuka lazima, eti amenisaidia sana, kunilipia ada ya chuo, shule, pango la nyumba siwezi mnyima sex, wewe umelaaniwa na unaharibu mwili wako sana, utaharibiwa muda si mwingi usipo badirika_ ( Hizo ndo umeziona sababu kubwa za kufanya Umtelekeze Roho wa Mungu atoke ndani yako ili ukamilishe shida zako hizo,Tubu ndugu na Uanze upya na Bwana)
🏹 Wengine wala hakuna kishawishi chochote chenye nguvu, ila umeuendekeza mwili wako tu, kiasi kwamba wanaume hawakutafuti, ila unawatafuta wewe, au kijana umemaliza uchumi wako kuhonga tu wanawake ulale nao, na wengine  *mnatumia nafasi zenu za Kipaji ulicho nacho kwa kuwa we mkali wa kupiga vyombo vya mziki, Producer, mtume, nabii, pastor mwimbaji mkali wa sauti, umewaangusha wengi,* laana hiyo itakutafuna usipo badirika. (Wewe ni Mbweha katikati ya kondoo muda si mrefu utakufa na moto unakusubiri)
🏹 Mimi sina lugha ya kukushawishi ila ukweli ni kwamba *Acha Kuchezea Mwili Wako*, _Acha Zinaa_ unachosha mwili, unaharibu mwili, Uliye bado kijana kwa nini kuharibu ndoto zako mapema?  *_Unahisi kwa nini kila anaye tafuta mtu wa kuaona naye anataka bikra? Asiye kahaba? Walozoea zinaa Ni Misiba kwenye ndoa(majanga matupu) unajipa stress kwenye ndoa,_* sasa kwa nini usitulie?
🏹Jambo lingine, Achana na Kahaba wako huyo, wa kike au wa kiume siyo kwa kubembeleza au kimya, kimya, mwambie Nimeacha zinaa na wewe nimerudi kwa Mungu wangu, wala sihitaji maswali, usimshawishi huyo mchumba mpagani aokoke ili muoane utajuta kwenye ndoa. ( *_Halafu ninyi walokole wa wokovu wa KIFAFA, Umekomaa na Mchumba Mpagani unajifanya na kujifariji eti mimi Naweza tumika kumuokoa,ntambadirisha mchumba wangu, wee Nimarehemu wa Kiroho unayetembea. Wee umekuwa Yesu,Ulisha kutana na Agizo la Yesu ka ENENDENI ULIMWENGUNI MWOTE MKAHUBIRI NDOA KWA KILA KIUMBE? Wee ni mpagani tu asilimia 100_*) Tumeambiwa Injili kwa kila kiumbe,na Injili yetu Si ya Ushawishi.(Ukinipenda nipende ukinichukia nichukie ndo Mjumbe Mkali EV ELISHA KAZIMOTO-MITHALI 17:11)
🏹Usiwe na mazoea tena ya karibu na huyo mlokuwa mnazini pamoja.
🏹Epuka lugha tata za mapenzi, na kutembelea, kutembelewa na jinsia nyingine mkiwa wawili peke yenu mtarudia zinaa
🏹Usimwamini huyo anaye kwambia basi tuendelee na urafiki ila hatuta zini tena, upendo utawasukuma tena mtazini
🏹Usiruhusu kushika au kushikwa mwili wako na jinsia nyingine wakati ulishazoea mahaba ya kushikwa mpaka kuanza ngono. Utarudia zinaa
👉Eti wachumba wanasema tunaishia Romace na kutomasana tu(wee usichezee mwili wako,subiri ndoa utafanya yote kwa uhuru)
🏹Kuwa busy na mambo ya Mungu na kuwa msomaji wa neno na maombi.
_Kuwa makini Yesu yu karibu, usichezee mwili wako tena, usiwe mtumwa wa mwanadamu atumie mwili wako kila akiuhitaji, na mwisho anatumbukiza kwa UKIMWI, Kipigo cha fumanizi, Kulogwa kwa kuiba mme/mke wa mtu, usaliti na stress za kuachwa_👇👇👇
*_1 Wakorintho 7 : 23 - Mlinunuliwa kwa thamani; msiwe watumwa wa wanadamu._*
🏹 _Ukiona maneno haya ya somo hili yanakuhusu fanya harakati haraka za kutubu kabla hujavuliwa vazi la mwili wako huo mapema sana_
🏹🏹🏹🏹🏹🏹🏹
*_Ulikuwa nami mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na ndoa na Maisha ya Kiroho na Huduma Ev Elisha Kazimoto,pata masomo mengi kwa Magroup yangu ya Whatsapp 0755444078,facebook Elisha Kazimoto ziko page kama Hazina ya Maarifa,nk_*
(ONYO:Unaye fanya Editing ya Masomo ya watu kwa kuondoa Anuani za mwandishi na namba za mawasiliano, Unawanyima watu fursa ya kupata msaada wa karibu kutoka kwa waandishi,acha tabia hiyo mara moja nao huo ni USHETANI- MITHALI 17:11)
    *By Ev. Elisha Kazimoto*
       _0755444078_

No comments:

Post a Comment