*UKIONA MWENZAKO ANAMAMBO HAYA NA HABADILIKI PIGA CHINI,USIJIKAZE KUINGIA NAYE KATIKA NDOA*
Ev Elisha Kazimoto
Whatsapp 0755444078
*_Kuna jambo moja na la muhimu watu wengi katika mahusiano linawapiga chenga, ni Kuchunguza Mwenzake anayetaka kuingia naye katika ndoa, kubaini Vitabia sumu ana viashiria vya migogoro ya ndoa,kuvibaini na kuvifayia maamuzi magumu mapema ili kuepusha changamoto kwenye ndoa_*
👉Ni heri kuvunja mahusiano kuliko kuvunja ndoa au kuishi kwa kujikaza kwenye ndoa.
👉Ukishindwa kumbadirisha mwenzako katika mahusino yenu usije ukajidanganya kuwa utambadirisha ndani ya ndoa.
Kauli ni hii *Ukiona Vijitabia hivi mwenzako haiviachi ana ving'ang'ania PIGA CHINI huyo*
✍Ana mambo ya siri,si muwazi,anakuficha ficha vitu sana...Huyo mtu piga chini,utaumiza moyo wako bure kwa kukosa ushirikiano katika ndoa
✍Anazira zira mara kwa mara pale unapomkosea tu kidogo.... Anaye zira zira piga chini.
✍Ukiona ana kiburi sana,jeuri hata akikosea anakuwa mzito kukuomba msamaha,hataki kabisa piga chini huyo ni mwiba.
✍Anakulinganisha na wavulana au wasichana wengine pale anapokukosoa,piga chini...Wewe ni wewe wala huwezi kuwa kama flani.
✍Hapendi kushauriwa,anataka afanye anachotaka yeye,anachojua yeye ndo kizuri wewe mawazo yako hamna, huyo piga chini....
✍Ana Masharti mengi mengiii yasiyo na msingi, huyo piga chini....
✍Anayeendesha mahusiano kwa kusikiliza nyumbani wamesema hivi au vilee,huyo piga chini....
✍Hataki kujishugulisha na kazi atafute pesa,...Anapenda kuulamba tu....Huyo piga chini.
✍Mkali sana,hataki umzoee muwe kama rafiki piga Chini,ndoa siyo kituo cha polisi.
✍Anahitaji umsikilize yeye tu na ufuate mambo yake,ila yeye hakusikilizi,Piga Chini, ndoa siyo jeshi haiendeshwi kwa Amri ya Amili jeshi,ni mazungumzo na makubaliano.
✍Mvivu kwa mambo ya Mungu hata ukimuhimiza, huyo atakuwa mzigo kwako kwenye ndoa usiobebeka. huyo piga chini Haraka sana Uvivu wa kiroho na hatari kuliko uvivu wa kimwili,kimwili wewe waweza pambana ukamtunza ila kiroho kila mtu anambingu yake lakini majibu mnapokea kama mwili 1.....PIGA CHINI.
✍Mara kwa mara anakuambia mambo ya X friend wake, huyo piga chini.....
*_Hayo ni baadhi ya mambo very critical ya kisaikolojia,usiyapuuze yatakugharimu_*
_Ukipenda na Usiwe na macho ya kuona madhaifu na kuyakwepa,jiandae kuishi jela la maisha na furaha ya maisha hutaiona_
Mwanasaikolojia Ev Elisha Kazimoto
0755444078