🖤🖤 *SINTOFAHAMU YA KUOANA NA MPAGANI, NA UKAKASI WA DINI/IMANI ZINAZO ZALISHA WATU NILIOWAITA KWENYE POST YANGU "MAREHEMU WANAOTEMBEA" UFAFANUZI WAKE KWA WALIOPATA UKAKASI*🖤🖤
............
............
_Ev Elisha Kazimoto(Mjumbe Mkali *Mithali 17:11*)WhatsApp 0755444078_
..................
👆👉 Sasa niweke sawa Kuhusu Imani,na wokovu na Maana halisi ya post ya Marehemu.
*MTU YEYOTE AMBAYE HAJAOKOKA(NI MTENDA DHAMBI NI MAREHEMU ANAYE TEMBEA) NA HUU NDO MSIMAMO WA NENO LA MUNGU,SIPINDISHI WALA KUPUNGUZA MAKALI MTU YEYOTE AMBAYE NAFSI YAKE INA HATIA JUU YA DHAMBI,UOVU,MATENDO ANAYO YA TENDA SI YA KUMPEMDEZA MUNGU,HAIJALISHI UPO DINI GANI WALA DHEHEBU GANI WEWE NI MAREHEMU UNAYE TEMBEA.*
1 Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu;
Waefeso 2:1
2 ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi;
Waefeso 2:2
3 ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine.
Waefeso 2:3
👆 *Wokovu Ni Badiriko la Moyo na Matendo* kinachofuata baada ya Badiriko la moyo na matendo ni Kupata watumishi sahihi/Mahala sahihi panapo Fundisha NENO LA MUNGU HALISI SIYO MAPOKEO na maneno ya wanadamu. Na hapa Haijalishi dini gani,dhehebu gani, Uzuri kweli,huwa inajitenga na uongo na Yesu alisha sema mtawatambua kwa matunda yao, SI LAZIMA NIKUBAINISHIE kuwa dhahebu hili ni sahihi ili si sahihi.....TUNAJUA TU KWA KUTUMIA NENO LA MUNGU,kuwa huu ni utapeli,haya ni mapokeo ya wanadamu siyo MAAGIZO ya Mungu, ili NI NENO LA MUNGU.
1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani.
1 Yohana 4:1
2 Katika hili mwamjua Roho wa Mungu; kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.
1 Yohana 4:2
3 Na kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu. Na hii ndiyo roho ya mpinga Kristo ambayo mmesikia kwamba yaja; na sasa imekwisha kuwako duniani.
1 Yohana 4:3
👆Kwa hiyo imani yoyote tunaipima kama imekidhi matakwa ya Neno la Mungu, kama haikidhi matakwa ya Neno la Mungu, dhehebu hilo,imani hiyo, kanisa hilo, mchungaji huyo ANAZALIZA MAREHEMU WENGI WANAO TEMBEA.
Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa.
Ufunuo wa Yohana 3:1
👆Hilo ndo neno la Bwana.
Uzuri neno la Bwana limejikamilisha,halina mapungufu lina COVER maeneo yote kwa kipimo sawa.
5 Kila neno la Mungu limehakikishwa; Yeye ni ngao yao wamwaminio.
Mithali 30:5
👆Neno la Mungu limehakikishwa tena ni safi, linafaa kwa mafundisho na kutengeneza watu Hai walio uhishwa na Kristo kwa kumwamini kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yao.
6 Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba.
Zaburi 12:6
👉👆 *DINI NI NJIA TU,* ila njia yaweza kukupeleka shimoni,au eneo unalotamani kwenda.(NENO DINI NI LA KIARABU MAANA YAKE NJIA) umakini ni JE, NJIA HIYO INAKUPELEKA WAPI?
12 Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu, Lakini mwisho wake ni njia za mauti.
Mithali 14:12
👆Suala hapa si kuangalia *Dini/Dhehebu langu limefananishwa na nini...... Suala ni NJIA YANGU NINAYOTEMBELEA INA VIGEZO VYA KUNIFIKISHA MBINGUNI*? Mimi liwe kanisa langu,dhehebu langu lifananishwe na nini, Hainihusu swala ni YESU WANGU AMEFANANISHWA NA NINI maana Yesu ndo Sura ya Uhai,dini hakuna uhai..... *DHEHEBU/DINI NISAWA NA MWILI WA MTU PASIPO ROHO* Huu mwili wangu ikiondoka Roho nitaitwa Marehemu, Roho ndo inanifanya niitwe EV ELISHA, vivyo hivyo DINI/DHEHEBU kama HAKUNA ROHO WA BWANA (ROHO MTAKATIFU-NA NENO LA MUNGU LILILO HAI)dini au dhehebu linabaki kuitwa KUSANYIKO MFU.
27 Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa.
Yakobo 1:27
👆Kama njia(mtu)hajilindi na dunia PASIPO MAWAA(dhambi na uovu) hiyo dini(mtu)ni Marehemu.
*UKWELI NI HUU*
_Wale watu wa zamani kidogo kuanzia utawala wa mkapa mpaka nyerere,mmtajua jambo hili na ntaleta lecture kama 2 juu ya Imani,dini,wokovu...... MADHEHEBU KADHAA unayoyajua mengi yalikuwa HAYAAMINI KWA HABARI YA WOKOVU,NA MTU KUWA MTAKATIFU AKIWA DUNIANI LABDA AKISHA KUFA,ndo atatangazwa kuwa mtakatifu._ Sasa *Huu ni Utapeli wa shetani na Kwenda kintume na NENO LA MUNGU NA NDO UMAREHEMU UNAANZIA HAPO KUZALISHWA, kwakuwa wanakiuka andiko hili la Mungu anapendezwa na watakatifu WALIOPO DUNIANI siyo waliokufa*
3 Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.
Zaburi 16:3
👆Miaka ya hivi karibuni kuanzia miaka ya 2000 ndo kumeanza kushika kasi ya KILA MTU KUSEMA AMEOKOKA,KILA DINI,DHEHEBU KUSEMA NA SISI TUMEOKOKA, vikumdi vya UHAMSHO, vya kiinjili kuanzishwa na kuwa kanisa B ndani ya kanisa A..... Kumbe WOKOVU UPO, ningekuwa group la Be strong ningeeenda ndani zaidi na kutoa historia ya vikundi vyote na aababu ya kuanzishwa, dhehebu moja badala ya lingine,ila hapa na jibu hoja kwa jumla kuhusu KUOANA NA MAREHEMU(MPAGANI)....
*HOJA SIYO DHEHEBU WALA DINI, HOJA HAPA NI 2 TU*
1⃣Wewe mtu binafsi UMEOKOKA? Unaishi maisha MATAKATIFU? Nafsi yako haikupigii kelele kuwa wewe HAPANA NI TAPELI(unafanya hivi,hivi,hivi Mungu hapendi?)
3 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.
1 Yohana 3:3
4 Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi.
1 Yohana 3:4
5 Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.
1 Yohana 3:5
6 Kila akaaye ndani yake hatendi dhambi; kila atendaye dhambi hakumwona yeye, wala hakumtambua.
1 Yohana 3:6
8 atendaye dhambi ni wa Ibilisi; kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.
1 Yohana 3:8
9 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
1 Yohana 3:9
10 Katika hili watoto wa Mungu ni dhahiri, na watoto wa Ibilisi nao. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala yeye asiyempenda ndugu yake.
1 Yohana 3:10
20 ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote.
1 Yohana 3:20
21 Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu;
1 Yohana 3:21
👆👉Mistari muhimu ya mtu binafsi kujipima wala hapa uhitaji kuambiwa wewe ni MAREHEMU AU HAI,binafsi unajihukumu kwa NAFSI YAKO. Japo ukitaka kujitetea ili ujulikane umwema utazuga kwa watu lakini nafsi inasema wewe HAPANA HUJAOKOKA.
Ndo maana siku ya hukumu Mungu hatahitaji Shahidi kama mahakamani No unaye shahidi wako NAFSI YAKO inaongea kila te do,kila wazo,na kila njia yako.(sasa hapa haijalishi upo dhehebu gani wala dini gani) MAANA WENGI UKIKBILIA KUSEMA NA KWA WALOKOLE WAPO WATENDA DHAMBI WAKUBWA KULIKO WAPAGANI......Jibu jepesi sana nikweli kwani *Hata Yesu likuwa na wanafunzi 12 ila moja alikuwa Yuda msaliti na Yesu hakuwahi kusema si mwanafumzi wangu ila hakwenda mbali panga la haki lilimpitia,ila alionywa kila mara....Yesu alisema kati yenu mmoja atanisaliti* na ndicho kinahubiliwa huko kwa walokole ACHA DHAMBI wakusikia anasikia asiye sikia njia yake ni fupi.
2⃣Hoja ya pili ni *ALIYE MBELE YAKO,AU ENEO LAKO LA IBADA LINAIFUNDISHA KWELI? Lina kemea dhambi?lina imiza maisha matakatifu? Kama hayo hakuna linapita kwa mwaka mara 1 tayari unajua watu gani wanazalishwa. Maana kuna madhehebu mengine na imani nyingine.... Dhambi kwao siyo agenda,ndo maana mtu anaweza kwenda nyumba ya ibada akiwa na promise ya Ngono baada ya ibada,au anatoka ibada anapitia Bia na sigala,hawala nk, anaenda ibadani KUPUNGUZA DHAMBI, SIYO KUKUTANA NA MUNGU.
👉Imani zingine zinaenda ibadani kupata nafasi ya kuzikwa atakapo kufa aombewe aende mbinguni siyo kuyaandaa maisha yake ya baadaye akiwa hai.....
27 Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu;
Waebrania 9:27
👆Hilo andiko hawalisomi na hawalioni.
*SHIDA NI MOJA NA ITABIDI NIISHIE HAPA MAANA HUMU NI MAHUSIANO NA NDOA ILA KISAIKOLOJIA NAKIROHO*
_Watu wengi sana wakisha Penda wanahitaji na Mungu apende kama wanavyopenda,wanataka Mungu awafuate matakwa yao siyo wao wafuate mapenzi ya Mungu,ndo maana mtu anaweza sema SI NIKIOANA NA MPAGANI MIMI NAWEZA MBADIRISHA AKAOKOKA AKAMJUA MUNGU?_
*NOTE*. Msingi wa wokovu SIYO MAPENZI NI msimgi wa wokovu NI MOYO WA TOBA ULOTAMBUA HATIA YA DHABI NA UOVU, kumleta mtu wa Yesu kwa msingi wa mapenzi nisawa na KUMTUNUKU PhD kondakita wa gari akiyeishia darasa la 2 halafu ukaaza kujisifu kwamba huyu ni msomi hatari ana PhD ni mtaalamu wa uchumi huku ukijua wewe ndo umempa hiyo phd hewa.
Kwa Mungu hakunaga kufoji.
Shida ya pili watu wanahitaji wasikie maneno laini na ya uongo yakuwafurahisha siyo kweli inayo choma ili kubadirika.
9 Kwa maana watu hawa ni watu waasi, watoto wasemao uongo, watoto wasiotaka kuisikia sheria ya Bwana;
Isaya 30:9
10 wawaambiao waonaji, Msione; na manabii, Msitoe unabii wa mambo ya haki, tuambieni maneno laini, hubirini maneno yadanganyayo;
Isaya 30:10
👆👉Hii ndo shisa na kizazi cha sasa na kilichokuwepo tangu zamani.
...........
...........
*_Ev Elisha Kazimoto(Mjumbe Mkali -Mithali 17:11) WhatsApp 0755444078_*