๐ช๐ช *ILI KUSHINDA UNAHITAJI MAMBO 2..UHODARI NA USHUJAA*๐ช๐ช
Mnenaji: *Ev Elisha Kazimoto*
ANDIKO KUU: *2Mambo ya Nyakati 13:1-18* ๐๐๐๐๐ _Ukisoma mistari hiyo kwa utulivu halafu njoo hapa kwenye Ufafanuzi wa Roho Mtakatifu_
๐Kila mtu aitwaye mshindi, maana yake *Amepita kizuizi kilicho lenga kumzuia asiende alikokusudia* kwenda.
๐Kushinda pia ni kupata,kuona ulichokuwa unakitarajia......Ikiwa ni baada ya kuzuiliwa na kitu,mtu,mazingira au hali,iliyowekwa maalumu kwaajili yako kukuzuia.
๐ช *UHODARI* ni Tabia au hali ya *Kujiamini* kutokana na mafunzo,mazoezi,kinga au mtu aliye nyuma yako kukusaidia.
๐Kila mtu aliye Hodari ana namna ya wapi anapata nguvu ya kujiamini.
๐Kwa ujumla UHODARI ni KUJIAMINI.
๐ชUSHUJAA....Ni hali na moyo wa Mapigano yazaayo Ushindi.
๐Mtu shujaa maana yake ana Rekodi ya kupigana na kushinda mpinzani wake.
๐Ushujaa ni moyo uliotayari kupigana na kushinda.
NB1,: *_Msingi wa Imani yetu ya watu tuliookoka ni Sisi ni Hodari(kwakuwa aliyenyuma Yetu ana nguvu kuliko yeyote na chochote kikwazo,au adui tutakaye kutana naye kutuzuia,au kutudhuru_*
KUMBUKUMBU LA TORATI 31:1-6
NB2: _Maisha yetu sisi watu tuliookoka, niya USHUJAA kwakuwa sisi ni watu wa vita,mapigano kwenye ulimwengu wa roho na Tunashinda kabla ya pambano kwakuwa *Vita si yetu ni ya Bwana* hivyo Ushindi ni Lazma_
*Waefeso 6:10-12, Warumi 8:31,37, 1Samweli 17:46-47*
Imendaliwa na *Ev Elisha Kazimoto*
Whatsapp 0755444078