*_Issue ya mawasiliano katika uchumba ni kitu kikubwa mno,ambacho kina hold safari yenu ya uchumba to ndoa,usipuuzie mawasiliano,kisaikolojia mawasiliano hupima kiwango cha upendo wa mtu kwako na Attention aliyo nayo kwako,na Area coverage uliyo nayo kwenye akili yake,sasa unapo kuwa kwenye mahusiano Rasmi ya uchumba au hata kwenye ndoa,unahitaji kujua Imekupasa kulipa Gharama ya muda ili ubebe na kuimarisha moyo wa mwenzako, tenga muda ukio mzuri,uwe wazi kwa mwenzako ajue ratiba zako vzr,lakini umwonyeshe ulivyo tenga dakika kadhaa za utulivu kwaajili yake._*
Sasa katika mawasiliano yenu kama ratiba zenu ni ngumu sana,ukipata hata dk 20 zitumieni vzr kupanga,au kutiana moyo na kufurahishana kwa story muhimu.....muda mwingine wa ubize tunieni hata texts kuwasiliana.
_Muda wa usiku sana kwa wachumba ni mzuri ika ni mtego kwenu,maana wengine hupitiliza mipaka hata humaliza mazungumzo wamejichafua miili yao,yaani wametokwa na uchafu wa ngono_ ndiyo maana ukiweza tumia usiku vizuri kupanga,kutiana moyo,kuombeana na kuzungumza mazungunzo mepesi.
*By Ev Elisha*
Friday, 27 January 2017
MAWASILIANO KWA WACHUMBA
MCHUMBA KULALA UKWENI
*_Issue ya kumtembelea expected mchumba wako,lipo katika kona mbili kulingana na tamaduni za kiafrika au kitanzania,unaenda kusalimia ukweni kwa binti na kulala....kwa kijana anaye jitambua,mwenye heshima zake hawezi kufanya hivyo,Jifunze kwa Yesu,ndugu zake walimwambia kajionyeshe kwa watu,akagoma,mama yake kamwambia hawa watu wameishiwa na divai,Yesu alimjibu....hivi..MAMA WAKATI WANGU BADO, kuba wakati wa kwenda kulala utapewa na heshima kubwa,na wewe utajisikia vzr,na mwenzako atajisikia vzr amepata mtu anaye heshimiwa hata na familia. Unajipeleka kisa wanajua huyu anaweza akawa mkwe,hujui unachorwa na kupimwa,mwisho unaondoka,wanaanza kumkandia mwenzako na kusema huyu hamna kitu....mnajiharibia....kitabu cha mithali anasema usiende kwa rafiki yako mara kwa mara asije akakuchoka,kama unahitaji kuichunguza familia,tuma maspy,ukienda wewe,siyo wewe ndo unawachunguza ila wao wanakuchunguza_
Mwishowe ufanye tukio la kujiabisha,huwezi pata nguvu za kurudi kutoa posa.
Watu wakikuzoea,na heshima inashuka....hauna maana wala faida yoyote kwenda kulala kwa fanilia ya binti au kijana kabla ya kuoana.
*_Kwanza amazing ni ile binti au kijana anakutambulishaa kwa familia rasmi kila mmoja ananyoosha shingo na kukodoa macho ili wakuone,halafu wee upo kimyaaa,halafu ubaondoka mapema hawajakujua wee ni mtu wa aina gani,mwongeaji,mpole au vipi....usiwape adui nafasi kukuwekea vigingi mapema_*
BY EV ELISHA
UMRI MPISHANO KWA WANANDOA
*_SUALA LA UMRI MPISHANO NA MWENZI WAKO_*
_Ni kisaikolojia,na kibiblia waba ndoa kupisha umri,na niki biblia na kisaikolojia mwanaume kumzidi mwanamke umri. Kitabu cha mwanzo kina twambia mpishanobwa umri,Adamu aliumbwa kwanza,baada ya muda kupita(unknown years)ndo Hawa akaumbwa,so Adamu ni mkubwa kwa Hawa,lakini tunaona Ibrahim na Sara ,walipishana miaka 10,Ibrahimu akiwa mbele miaka 10 hiyo ni kibiblia_
Kisaikolojia inashauliwa kijana amzidi mwanamke kuanzia miaka 2 mpaka 6,7 ikizidi sana 10.
-Kwa nini,mwanamke anakua haraka,lakini mwili wake unachamgamoto nyingi za mabadiliko ya ukuaji kuliko mwanaume,mfano, Mzunguko wa siku unaathiri mwili wake,mwanaume hana,kubeba mimba,mwanaune habebi,kunyonyesha,mwanaume hakuna...mambo hayo yanamfanya kubadirika sana kuliko mwanaume,kwahiyo unaweza hisi mke wako kachoka,au mkubwa kuliko wewe kumbe ni kwasababu ya mabadikiko yake._
Kwamaana hiyo,ukiolewa na mme anaye kuzidi miaka 2-5,6 unakuwa umebalance gap lile la mwili,ila mkilingana au ukampita,baada ya miaka 5-20,watu na wewe mdada utaonekana ni mama kwa mme wako,au dasa yake mkubwa.
_Lakini kisaikolojia haushauriwi kuzidiana zaidi ya miaka 10,hasa isizidi 6,7 hapa nikwa kulinda Psychological interests,mkipishana sana mtatofautiana kimawazo sana,kutakuwepo mwente mawazo ya kitoto mwingibe ya kiutu uzima na baadhi ya michezo na utani ya wana ndoa utaikosa na uhuru utapungua_
*By Ev Elisha*
Thursday, 26 January 2017
SEHEMU 7 ZA KICHWA(MWANAUME)
🚍 *MWANAUME KAMA KICHWA* 🚍
*_Ev. Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
🚗Tafsiri hii imechukuliwa kwa upeo wa chini sana na pande zote wanaume kwa wanawake, hali ambayo imepelekea ndoa nyingi kuyumba
🚗Tafsiri ya Mwanaume ni kichwa, wengine wameitafsiri kuwa Mwanaume ni mbabe katika familia, aliye Alfa na Omega, Dictator, asiyestahili kuheshimiwa, kushaurika nk
🚗Wengine wameitafsiri kuwa Mwanaume ni kichwa cha Kuhudumia Familia, kutafuta pesa, kulisha familia nk
🚗🚗Lakini kwa mtazamo wa Biblia na tafsiri halisi ya Mungu, mpaka Mwanaume kuitwa mfano wa Kristo Yesu, SI jambo dogo Kuna maana kubwa
🚗🚗Na kama wana ndoa watatumia, wataiangalia tafsiri ya biblia ndoa yao itakuwa Paradiso ndogo
🚗🚗Kiuhalisia na mtazamo wa Biblia, Mwanaume ameitwa ni kichwa cha mkewe na familia kwa ujumla, kama Yesu alivyo kichwa cha kanisa, kwa kutazama umuhimu na kazi za sehemu 7 za kichwa
🏢 *SEHEMU 7 ZA KICHWA NA KAZI ZAKE* 🏢
👦🏼Kichwa hiki unachokiona (Mwanamke kwa Mwanaume) ni kiungo kikubwa na kina kazi kubwa sana 7,
👦🏼Mwanaume ukitambua ulivyo wa pekee, na ukitumia kwa umakini sehemu hizo 7 ndoa yako utaifurahia milele
👦🏼Mwanamke ukitambua nafasi na umuhimu wa Mume wako kama kichwa na unatengeneza mazingira mazuri ya Heshima, Adabu, Utii na Unyenyekevu kwa mmeo, ndipo hizi sehemu 7 zitakuletea furaha, upendo na amani katika ndoa yako
👦🏼👦🏼Popote ukiona kichwa jua kina sehemu zifuatazo;Akili, Macho, Masikio, Pua, Ulimi, Mdomo (lips),na Meno haya ni maeneo muhimu sana
👦🏼👦🏼Utakuja kujua kwa nini Mungu alimpa Mwanaume nafasi au sifa ya kichwa na kumfananisha na Yesu Kristo
🏫 *SIFA NA KAZI ZA KICHWA* 🏫
🏡🏡UBONGO (AKILI):Kichwa kina ubongo ambayo ni injini ya maamuzi, fikra, tafakari ya mwanadamu
🏡Kazi kuu ubongo ni kuchanganua mambo kabla ya kufanya maamuzi, ni kuzalisha hekima na njia mbadala katika mambo magumu
🏡Mwanaume kama kichwa, unahitaji kutumia akili sana kufanya maamuzi ya faida kwa familia yako kwa amani, Biblia inasema hata Kuishi na mkeo kama mwili (uliobeba Moyo) unahitaji Kutumia AKILI SANA(1Petro 3:7)
🏡🏡MACHO:Macho ni kiungo muhimu sana, yana kazi kuu mbili, Kutazama na Kuona
🏡Kutazama, ni kutambua jambo likivyo ktk sura yake na Kuona ni Kuchanganua sura ya kitu na kukitendea kazi, kubaini ubora na mapungufu yake
🏡Mwanaume kama kichwa chenye macho unahitaji Kutazama na kuona mambo kwa mkeo na familia kwa ujumla, kuyachanganua, kujua yapi ni bora uyaboreshe na yasiyo bora utumie Akili kuyadhibiti
🏡Mwanaume macho yako (ya tafsiri ya kichwa) yakiwa mbovu ndoa itayumba (Mathayo 6:22-23)
🏡Macho yako kama Mwanaume (ya tafsiri ya kichwa) yakiwa vizuri, mkeo ataenjoy na ndoa yenu itakuwa salama. 🌏🌏MASIKIO:Masikio yana kazi ya kusikia na kusikiliza, hizo ni kazi kubwa na ngumu, kwa kuwa ndizo zinazo tengeneza mawazo na maamuzi
🌏Kusikia ni kupata sauti yoyote masikioni, iwe inamaana au haina,
🌏Kusikiliza ni kuweka umakini na utulivu, juu ya sauti unayoisikia na kujua ina maanisha nini na kwa nini isikike katika hali hiyo
🌏Mwanaume kama kichwa chenye masikio, ili ndoa yake iwe makini anahitaji Kuwa na uwezo mkubwa wa kutambua sauti ya mke wake na watoto wake, kujua hii sauti ya mke wangu inamaana gani na aifanyie maamuzi ya busara
🌏Mwanamke, anahitaji kujua mme wake anapata sauti nyingi huko na huko akiwa nje ya nyumba, akirudi ndani inabidi ni mpe sauti itakayo mfanya atulie, atabasamu na kunipenda zaidi.
🌏🌏PUA:Pua ni kiungo muhimu katika kichwa, ina mawasiliano na ushirikiano mkubwa na moyo na mapafu
🌏Lakini kazi ya pua ni kunusa(to detect) harufu nzuri na harufu mbaya na kufanya maamuzi ya kupokea harufu nzuri tu
🌏Mwanaume kama kichwa, unahitaji kunusa na kubaini harufu ya mambo yatakayo hatarisha ndoa na familia yako na kuyadhibiti, kunusa harufu za mambo mazuri mkeo abakufanyia uyaboreshe na kumtia moyo ili kulinda ndoa yenu.
🌏🌏Hayo yakizingatiwa mtaona kila siku mnacheka na kufurahiana daima..
🌏🌏Lakin Mwanamke ajue hasiruhu kuwa njia ya kupitisha harufu mbaya(kero) utaondoa amani kwa utaondo 🎒🎒MENO:Miongoni mwa viungo muhimu ktk kichwa, na msaada kwa tumbo ni meno, kazi kuu yake ni kuhakikisha usalama wa tumbo kwa vitu vyote vipitavyo kinywani
🎒Meno kazi yake ni kuvunja vunja vitu vigumu nakuviweka katika ulaini ili tumbo lipokee vitu salama
🎒🎒Mwanaume kama kichwa chenye meno, unahitaji kushughulika na mambo magumu, hatar kabla ya kumpasia mkeo, Hakikisha yakifika kwa mkeo hayata leta madhara
🎒Kuna mambo mengine ktk maisha, vifua vya kukabiliana nayo, tunatifautiana kati ya Mwanaume na Mwanamke, usipo Anglia utamfanya mkeo kukata tamaa
🎒Mwanamke mweshimu sana mmeo isimuone hivyo unavyo muona ukahisi ndo alivyo, Kuna vitu anamalizana navyo, anapambana, anaumia Makusudi wewe uwe na amani, ufurahi, maisha yaende
🎒Lakini wanawake wengine wanaweza kumdharau mme wake na kumbana muona wa kawaida sana, unakosea sana, yeye kana kichwa chenye meno anaumia kutafuna mambo magumu, ili wewe uenjoy maisha. 🚆🚆ULIMI:ulimi ni kiungo kikali sana, kinafanya kazi na akili, umasikio na macho ili kuhakikisha maelekezo yanayo tolewa na ulimi yako kamili
🚆Mwanaume kama kichwa chenye ulimi, unahitaji, kuonya mambo yasiyo na faida ktk familia yako yasiendelee, kufundisha mambo mapya ili kuisaidia ndoa yako,
🚆Kwa kutumia ulimi jua, ulimi una nguvu ya kujeruhi, na kuganga, hivyo unapoongea na mkeo onyesha kumjali, kumpenda na kumhurumia ili amani idumu
🚆Mwanamke unahitaji kujiadhari na tabia, vitendo vinavyo hudhi, ibua hasira,vitendo vya dharau, usimwonyeshee mmeo, ukivifanya atatumia ulimi vibaya kama kichwa na ATAKUJERUHI, na huo ndo utakuwa mwanzo wa migogoro mizito katika ndoa yenu.
*_By Ev Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
Friday, 20 January 2017
ZIBUA NJIA ZILIZO ZIBWA NA ADUI
*NI MAOMBI YA KUZIBUA NJIA ZILIZO ZIBWA NA ADUI*
_Shalom,shalom wewe mwana maombi,unayeitwa mtu wa vita,tukiwa katika usiku wa mkesha,ujumbe wetu wa leo,ni KUZIBUA NJIA Zilizo ZIBWA na maadui_
*_Ayubu 19 : 8 - Yeye ameiziba njia yangu nisipate kupita, Na kutia giza katika mapito yangu._*
✍Tukiwa katika mwaka wa Kwenda Mbali(KUTOKA 8:24-28)Neno la Mwaka 2017,wako maadui ambao kila siku hujipanga kwa hila Kuziba,njia zetu za mafanikio ya kiroho na kimwili.
✍Siku zote,Njia ndiyo mahali pa kupitia kuelekea pale uliko kusudia kwenda,njia ikiwepo safari ipo,njia ikizibwa,safari inakuwa na utata. *_Ndiyo maana kwasababu tunakusudia kwenda mbali mwaka huu,lazima pia tujipange KUZIBUA chanel(njia zetu)za mafanikio zinazo zibwa na maadui siku kwa siku._*
✍Kinacho fanywa maadui zako(wachawi na mapepo)nikuweka vikwazo katika njia zako, magonjwa,kufuta kibali chako,umasikini na uhitaji,mafarakano na migogoro,tabia ngumu na matukio yaumizayo ndiyo mawe yao ya kiziba njia yako ili wakupunguzie kasi ya safari(speed).
*_Maombolezo 3 : 9 - Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa; Ameyapotosha mapito yangu._*
✍Siku zote mtendee adui kile anacho kusudia kutenda,mtendee na zaidi ya kilee..sasa kwakuwa adui anaziba njia zetu kwa mawe yaliyo chongoka ili atuumize,sisi tunaziba njia yake kwa MIIBA,tunamzuia kupita kabisa kwa jina la Yesu.
*_Hosea 2 : 6 - Basi kwa ajili ya hayo, angalia, nitaiziba njia yako kwa miiba, nami nitafanya kitalu juu yake, asipate kuyaona mapito yake._*
Hatulegei,hatupunguzwi speed,ila kasi yetu ni ile ile tunaenda mbali,kiuchumi,kiroho,kindoa,kitaaluma na kiafya kwa jina la Yesu.
*_By Ev Elisha Kazimoto_*
*@2017*
*0755444078*
Sunday, 15 January 2017
KUOANA NA MTU WA IMANI TOFAUTI
*UKWELI KUHUSU KUTAKA KUOANA NA MTU WA IMANI NYINGINE*
👉Kwanza naomba ifahamike kuwa ndoa ni Taasisi nyeti sana isiyo hitaji kubumba bumba mambo,na hapa lazima kweli ya Mungu iwe dhahiri ili kama unafanya maamuzi ufanye maamuzi ukijua madhara au faida ya ndoa *MIXTURE* Maamuzi yako ya sasa ndo maisha yako ya baadaye.
_Ziko sababu nyingi za kwa nini Usioane na Mtu wa Imani Tofauti na wewe hasa kama wewe ni wa Imani ya Wokovu kwanjia ya Yesu Kristo na unayahishi maisha hayo ya wokovu_
2KORINTHO 6:14-17
14 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?
15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari? Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini?
16 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.
17 Kwa hiyo, Tokeni kati yao, Mkatengwe nao, asema Bwana, Msiguse kitu kilicho kichafu, Nami nitawakaribisha.
👉Mstari wa 15, Kuamini ni nguzo kubwa katika imani na ndicho hutofautisha imani moja na NYINGINE,dini moja na nyingine na hapa ndo kutofautiana katika mwelekeo.
👉Suala la wote ni Wakristo halina nguvu katika imani,maana humo humo kwa Kristo hutofautiana katika Imani(kuamini)
*_Kuna wanao amini maombi kwa wafu,wengine hapana,wengine wanaamini katika kuwa watakatifu ni baada ya kufa,wengine wanaamini utakatifu ni hapa duniani Zaburi 16:3,wengine wanaamini katika kuwaombea walio kufa waingizwe peponi,wengine mtu akifa amekufa ataenda sawasawa na alivyoishi duniani,wengine wanaamini ubatizo wa watoto,wengine watu wazima waliokiri kwa kinywa kumpokea Yesu,wengine wanaamini ujazo wa roho mtakatifu na kunena kwa lugha,wengine haina haja,wengine wamaamini ukifa imeishia hapo,wengine kuna maisha ya kufa,wengine tutakaa duniani milele,wengine kuna mbingu mpya na nchi mpya(mbinguni),_*
Haya ndo baadhi ya mambo yanayo tofautisha Ukristo,yako mengi ni muda tu umezuia,sasa ona athari hizi....
👉Hapa si zungumzii Uana Dini(yaani kuwa Mkristo) nazungumza Mtu aliyefanya maamuzi binafsi ya Kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yako kwa kutubu na dhambi zako na kuziacha,si suala la kuabudu kwakuwa nimekuta wazazi wangu walokole...hiyo ni uana dini ndo huwa wanashika dini ya baba na mama na hawataki kuihasi,ila Si kwba w all ikuta na Injili ikachoma mioyo yao wakaamua kkimbilia Yesu na kuacha njia zao mbaya w an epokea imani kwa wazazi huo si wokovu wala haupo kwenye biblia( Hao wanaweza oana na mtu yoyote wa aina hiyo,haijalishi wa dhehebu gani au dini gani)
👉Katika Imani ya Wokovu wa Yesu Kristo(Kuokoka) ina msingi huu katika kuoana...
*_Amosi 3 : 3 - Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?_*
Kama hampo imani moja,hamuamini katika imani moja(sawasawa *Waefeso 4:1-6* hamuwezi kuoana labda kama wote mna wokovu wa Kifafa,yaani anaye sema ameokoka wokovu wake ni kifafa huyo anaweza fanya maamuzi hayo)
👉Tatizo linalo wasumbua na kuwachanganya vijana wengi sasa, *Kwa sasa kila dhehebu wanasema na sisi tumeokoka* lakini kwa uhalisia *Hawajaokoka wala hawana mpango wakuishi maisha ya wokovu* ila lugha hii ya kuokoka imezuka miaka ya hivi karibuni 10 tu kutoka sasa,kabla ya hapo ilikuwepo lugha ya Mimi dini yangu ni hii,na hao ni dini ya walokole (walokole) sasa ona shida hii...
👉Kuna uongo na utapeli wa kujifichia nyuma ya *Mungu,Amani ya Kristo,Roho kasema,Kufunuliwa* ifahamike kabisaa hakuna hata chbe ya ukweli Mungu,Roho mtakatifu kusema na mtu wa Mungu kuoana na mtu Asiye Amini(Okoka),Mungu si maskini kiivo mpaka aazime mtu upande wa pili kpatia mtu wake mtu Asiye sawa kiimani,lakini Issue ya amani,kuna *Amani ya Nafsi,Amani ya Shetani,Amani ya Hisia,na Amani ya Roho wa Kristo* je unajua kuzotofautisha?au ndo kumpakizia Mungu?
👉 Kuoana na mtu wa imani tofauti(yaani mnaamini tofauti) mfano 1 nitumie... *Wewe waamini ubatizo wa mtuzima na maji mengi(mke),na mme anaamini ubatizo wa watoto na maji machache* saaa fikiria mkipata mtoto anaishi imani ipi,je,nani anakubali kuipoteza imani yake aifuate ya mwenzake? Na endapo unaamua kuipoteza imani yako kwaajili ya ndoa, *Inaama imani yako ilikuwa Batili na wewe ulikuwa batili* Ndo zile imani za kukuta baba na mama wanaabudu imani flani na wewe ukadaka hiyo(si zungumzii dhehebu...mfano EAGT,TAG,FPTC haya ni madhehebu ila imani ni moja)no peoblem au (RC na Karithematic)ni kitu kimoja.
Mtoto huyu mtampoteza,malezi yatakuwa feki,kuna mmoja aliye na nguvu atalazimisha afuate misingi yake,mtoto atakuwa kama yatima mwenye mzazi mmoja na andiko la Mithali 22:6 halita timia kwake. Kwanini mchome kizazi chenu watoto wasiyo na hatia kisa mahaba yenu yasiyotokana na Mungu? Oana na mtu wa IMANI MOJA kama ni wapagani wapagani,kama wana dini,wana dini,kama Mlio wateule wa Kristo muwe wote wateule wa Kristo.
*_By Ev Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
Thursday, 12 January 2017
UTATA WA UMRI NA NDOA
*CHANGAMOTO YA UMRI KATIKA KUOA/KUOLEWA*
*_Ev Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
_Shalom watu wa Mungu,vijana na wazazi wenye vijana umri ya ujana,niwakaribishe katika uchambuzi huu wa *Presha ya Umri kwa Vijana katika kuelelea kwenye NDOA* Upo na mimi Mtaalamu wa Saikolojiana Mchambuzi wa Masuala ya Saikolojia *Ev Elisha(Baba Eve)* karibu sana_
🌹Kwanza niseme,Suala la kuoa na kuolewa ni suala la Kiroho(Kimungu) na ni suala la Kihisia(Kisaikolojia) kwa hiyo unapo anza kuhisi unaweza kuingia,kuhitaji ndoa unahitaji kujipanga sana Kiroho na Kisaikolojia,kwani Kujisahau katika haya mawili kunaweza *_Kusogeza Mbali Muda wako wa kuoa/kuolewa nje ya muda ulo tamani kuingia katika ndoa_*mfano ulitamani kuingia katika ndoa below 30 years,ukaja kuingia above 30years.
🌹 _Kisaikolojia,ufahamu wa kijana wa kike au wa kiume huanza kutamani mahusiano ya jinsia nyingine sana kati ya umri wa miaka *15-19*( siyo kutamani ndoa,ni kutamani mahusiano ya kimapenzi na jinsia nyingine) na Kutamani Ndoa kwa hisia za chini huanza kati ya miaka *20-25*, na kati ya miaka *26-29* kiwango cha kutamani ndoa huwa cha juu,na kati ya miaka *30-35*Hofu utanda na wasiwasi mkubwa uingia wa kupata mtu wa kuingia naye katika ndoa, na kati ya *35-40*Matumaini huanza kupotea wa kuoa au kuolewa,japo mtu hakati tamaa kabisa ya kutokuwa na mwenzi,na kati ya miaka *45-55*mtazamo huanza kuwa wakuwa na maisha binafsi na ndoa huwa suala la bahati na sibu_
*NINI TABIA ZA KILA MUHULA NA CHANGAMOTO ZAKE*
_Hapa naomba uwe makini na utazame kwa makini katika vipindi hivi vilivyo ainishwa pale juu,Tabia hizo zinaweza kuusogeza muda wako wa kuingia katika ndoa, *Baadaye ntaongea kuhusu muda wa Mungu,unavyo weza sogeza muda wako wa kuingia katika ndoa,hapa naanza na Tabia za Kisaikolojia*_ karibu upo na mimi Mtaalamu wa Saikolojia Ev Elisha(Baba Eve)
✍ Katika ule muda wa kutaka mahusiano ya kimapenzi na si ndoa( *15-19*) huu muda wengi wanasukumo wa *_Kijiachia katika mapenzi kwa kila anaye mtamani,aliye na pesa,au vitu vya kushawishi, mzuri wa sura,muda wa kufanya mapenzi na kila mtu atakaye taka kufanya mapenzi,hajali Promise ya ndoa anajali kutimiza tamaa za mwili_* kwa sababu hiyo wengi hasa (Wadada)huchezewa sana na kujeruhiwa mioyo na vijana wa kiume. *_Mbaya zaidi katika kipindi hiki hakuna Anaye waza au kufikiria Thamani ya ndoa,au kufikiria kuwa maisha yake hayo anavyo jiachia yanaweza athiri mpango mzima wa yeye kupata mtu sahihi wa kuingia naye kwenye ndoa_* Athari ya Tabia za kipindi hiki;
1⃣Ni kueneza sifa yako mbaya ya kutothamini mwili wako.
2⃣Kueneza Uchi wako kwa kila mtu(upo vizuri au vibaya,una mapungufu kitandani au uko vizuri)kumbuka _uzuri wako kitandani katika kipindi hiki hakukupi tiketi ya kuingia katika ndoa,bali kukushusha thamani na kuonyesha wewe kahaba_ na ubovu kitandani ndo unakuzika kabisa na kukimbiwa.
3⃣Kupata Alama ya kupoteza kibali cha kuwahi kuolewa( _mfano kupata mtoto kipindi hiki,utapata shida sana kumpata mtu wa kuoana naye ukiwa na mtoto_)
✍ Katika kipindi cha kutamani ndoa kwa hisia za chini Miaka 20-25,( *Hapa wengi ndo huvuruga mambo na muda wao halisi wa kuolewa au kuoa,kwani ni muda wa Uzuri huongezeka,kujitambua huongezeka,shape hukaa sawasawa,Elimu uanza kuonekana,pesa kidokidogo huanza kuonekana,Ajila hupatikana,* _Kwa sababu hizi kufukuzia wadada,au kuwindwa na vijana huwa kiwango cha juu,Foleni ya Requests huwa kali, na wengine vijana ndo hupanga wadada 5,7,10.....kuwaweka sawa kuwaoa,kwa kisingizio wanaangalia the best kati ya hao wote,mwusho huishia kuto pata hata mmoja,maana kisaikolojia huwezi kuwamiliki watu zaidi ya 2 vizuri kiasaiklojia kwenye mapenzi mpaka ukaonekana unafaa kuwa mme wake_
_Na kwa upande wa Wadada hapa ndipo *Hujipoteza kabisa na kujipa sifa ya kutoolewa* ambapo huanza Kujiona,kuchagua kijana wa kumuoa,hupanga vigezo visivyo wezekana katika mazingira yake,hupanga vigezo bavyo jata yeye hana,huwatimua vijana wanao kuja kuwachumbia kwa GIA ISIYO YA USTAARABU, dharau huongezeka,hutegemea kuolewa na watu wazito,well off ,walofanikiwa sana,huwakwepa vijana wasio na kazi ya kuingiza pesa mwisho wa mwezi(Ajila),huwauliza wanao kuja kuwachumbia swali la Una nini cha ziada,nyumba,usafiri,unaishi kijijini au mjini,familia yenu mko wengi au wachache,kama mpo wengi na una wadogo zako wengi kama 4 na kuendelea,hata ukiacha kumsumbua,wanaogopa kusomesha ndugu huku ana watoto wake, *Lakini nao huwapanga vijana kama 3-5 na kutazama nani ana mwelekeo mzuri wa kimaisha* shida yao huwa hawapendi kuwa wawazi sana kwa kijana, ANAMTAKA-HAMTAKI,hali hii ya kuzungushwa vijana huwafanya kumfutikia mbali na kutafuta mwingine,na kujikuta wote wamemwacha kimya kimya au kuvunja mahusiano naye._
Pia kwa kipindi hiki vijana wote wa kike na kiume *Huwa na Misimamo isiyo na tija* mfano aina ya mavazi,urembo,mwili (huna six park,huendi gym umekosa mtu tayari)kabila,Carrier flan kama wewe si mfanyakazi wa carrier flan hutakimbiwa na kila mtu.
✍Katika kipindi cha kuitamani ndoa kwa hisia za juu yaani miaka 26-29( *Kwa kijana wa kiume ni mzuri sana kwa kuwa yeye ni mtafutaji,ila kwa wadada ni muda wa heartbeat kwenda speed,hofu inaanza kui gia hasa kama hayupo kwenye mahusiano imara(serious ) wanapata shida sana* Lists ya watu wa kuulizia au kuuliza huanza kupungua, taarifa za Awali huanza kuhukumu maisha yako ya sasa na ya baadaye( _yaani ulivyo tumia vipindi viwili vilivyo pita huanza kuathiri uhitaji wako wa sasa na baadaye_),Watu huanza kujitia wale walio wakwepa,au kuwapiga vibuti, huanza kuwa wapole,waelewa,wastaarabu,wasikivu wa kila ombi na kujibu kwa Adabu,hukirudia kipindi cha kwanza,hutamani mahusiano na kila mtu,hutafuta mawasiliano ya watu,marafiki wote wazamani na wapya,na hutega sikio kwa walio bado single kama anaweza pata mtu wa kumkubali au kumwambia neno la kumuoa. (Si kipindi kizuri sana kisaikolojia kwani kinakutaka ujipendekeze kwa kila mtu)
✍ Katika kipindi cha hofu na wasiwasi, miaka 30-35( *Kipindi hiki hofu kwa muhusika na familia yake huanza kuingia juu ya uwezekano wa kupata mtu,Mvuto wa ujana huanza kufifia,utu uzima huanza kutokezea,kwa mabinti ni kipindi ambacho kama ni kufanya mahusiano au kiliki no za simu, ANA DELETE VIJANA WOTE WALO CHINI YA UMRI WAKE, si rahisi kuolewa na kijana unaye mzidi miaka 2,3,4,5....huanza kuwafikilia walio juu yake kiumri,kichagua hupungua,vigezo hupungua,kutojiamini huanza,kwa upande wa vijana wasicha wadogo huanza kuwakimbia kwa kuogopa umri mkubwa*) na Wengi hapa vijana kwa wadada huwa na *_Kigugumizi cha kutaja Umri wake_*
✍Katika kipindi cha Matumaini kupotea miaka 35-40( _Hali huwa tete,lawama nyingi hutupwa juu ya muhusika kutoka kwa familia na watu walo mfahamu kwa rika ya ujana mbichi,kujilaumu huongezeka,wengine huamua kutoolewa tena au kutooa tena,wengine huamua kutafuta mtoto angalau mmoja kwa njia zisizo rasmi,wadada huanza kuwaganda wanaume akimtania_.
*_Katika mambo yote,muda wako wa kuingia katika ndoa unaweza kusogezwa mbele kwa kusudi la Mungu,si kweli kuwa kila anaye chelewa kuingia katika ndoa amefanya uzembe,ila kusudi la Mungu_* Haya yanaweza kuwa mambo muhimu ya kusogezwa mbele kwa ndoa yako.
👉 Bado mtu wako,au wewe katila ulimwengu wa roho haja kaa katika Position (nafasi) ya kuibeba ndoa na kukufanya uendelee kumpendeza Mungu.
👉Bado hujakamilisha vema utumishi wako wa ujana ukiwa huru,ndoa itakunyima uhuru na kushindwa kulitimiza kusudi la Mungu
👉Muda wako wa kuingia katika ndoa katika ulimwengu wa roho bado
👉Ni jaribu lako unaloliweza,lakini utafanyika ushuhuda mkubwa kwa wengine
👉Mkuu wa Uajemi(Anga)amepingana nawe sana na kumzuilia mwenzako usimuone.
NB: _Usiingie kwenye ndoa kwa kuwa umri wako umeenda utaumia,utapata mwiba mbingu utaikosa kisa ndoa,Usiingie katika ndoa kisa marafiki zako wote wameoa na kuolewa,we sikama hao utapoteza mwelekeo waaisha. Tulia na mtegemee Mungu ndoa ipo tu,punguza na kuondoa makosa kwenye maisha yako ya kiroho na kimwili
*_Nini ukifanye kama kijana ili kukabiliana na changamoto hizi zote za miroho na kisaikolojia, moja kuwa mtu wa kumpenda Mungu nyakati zote na tumika kwa moyo na bidii sana kwa Mungu,kuwa mtu wa maombi na kushughulikia vikwazo vyote katika ulimwengu wa roho, Jivue vazi la kuto kubalika na kataa roho ya kukataliwa na kukosa kibali kwa watu, Pili,kusa makini na tabia zako,lugha zako,presentation yako kwa watu,usiruhusu hali yako mfn,elimu,pesa,status yako na familia yako iwe na sauti kubwa kuliko utu wako_*
_Ulikuwa na mimi Mtaalamu wa Saikolojia na Mchambuzi wa Mahusianl na Ndoa Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve ) 0755 444078_ ✍Facebook Elisha Kazimoto
✍Blog Material Adimu University
✍Whatsapp (Gropu Material Adimu University-Chuo cha Mahusiano na ndoa)
✍Whatsapp no. 0755444078
*_Huko kote utakutana na Mafundisho ya kina_*
Monday, 9 January 2017
NGUZO ZA MAHUSIANO IMARA
*NGUZO ZA MAHUSIANO IMARA NA NDOA*
_Kuna mambo ya kuwa nayo makini unapo anzisha mahusiano,kisaikolojia ili yadumu,msichokane kuwa makini kufanya haya yafuatayo na usipo yafanya hata kama ulimuona mwenzako mzuri uramchoka_
1. *Hakikisha mnawasiliana mara kwa mara* _Mawasiliano yanavuta Attention ya mtu kukaa kwenye akili yako,na kitu kilicho kwenye akili mara kwa mara si kwa ubaya upendwa_
2. *Hakikisha mkihitirafiana,usifanye maamuzi magumu ya kumuumiza mwenzio,kumuadhibu,kumkomoa,kumsusia,au kukaa kimya kwa muda mrefu bila kutatua hitirafu ile* _Mkihitirafiana,jua ni ubinadamu,mrekebishe kama ni uchumba,au ndoa,kwa uchumba kama harekebishiki achana naye,kwenye ndoa,Ingia garama ya maombi,na kuendelea kumfundisha na kumwelekeza._
3. *Epuka kumlaumu mwenzako mara kwa mara kwa kila kosa* Lawama zina vunja moyo na kushusha nguvu ya hisia za upe do.
4. *Epuka kumwesabia makosa mwenzako* _kwamba hapa yamefika 2,3,6,.......samehe,likijirudia usirikumbushie kuwa umewahi kufanya,kukumbushia huonyesha na wewe huna roho ya msamaha,kwa hiyo na wewe ni mpuuzi_
5. *Kauli nzuri katika kuongea na kuwasiliana* _Usiwe na majibu ya mkato,kuongea ovyo mpaka unachosha_
6. *Weka tofauti ya Thamani kati ya mkeo/mmeo na watu wengine* _Hakikisha mwenzako anafahamu jinsi unavyo mchukulia wa tofauti na watu wengine katika kila eneo,onyesha kuheshimu na kumthamini,usi mfananishe na wengine. Kila unachoweza fanya kwa wengine yeye mzidishie_
7. *Sifa na zawadi*, _tambua uzuri,au kupendeza kwa mwenzako kila siku ( *Kila siku*) msifi kwa uziri,akivaa,akisuka au kunyoa,akipika nk, vina boost upendo_
8. *Neno Nakupenda lisiwe zito kwako* _Aliye naakili ya kulinda ndoa,na alichagua mwenza wake hakuchaguliwa na mtu hakikisha neno hili mwenzako analisikia kila siku,hutakuja kumchoka au kuchokwa_
9. *Usifanye maamuzi makubwa binafsi* _mfano kununua kiwanja,kujenga nyumba,kununua usafiri nk,mshirikishe mwenzako,inampa moyo wa kuona amethaminiwa_
10. *Kuwa makini na familia yalo na ya mwenzako* _Usiwe na upendeleo wa watu wa kwako,be fare,usiruhusu kilamoja atoe kauli kwa familia yenu,au kumsema ovyo mwenzako,mlinde atakupenda daima_
11. *_Msiache kuombea ndoa yenu au mahusiamo yenu shetani ni Adui wa furaha,amani na Upendo_*
*BY EV ELISHA*
KWELI KUHUSU TENDO LA NDOA
*KWELI KUHUSU TENDO LA NDOA*
" *SWALI* _Hivi ni halali kwa wana ndoa kunyonyana sehemu za siri(Uume au Uke),Imekaaje Kiroho?_"
( *Mjibu swali:Ev Elisha*)
✍ Kwanza kabisa nikupongeze muuliza swali kwa ujasiri wa kutaka kuweka mambo sawa katika maisha ya ndoa,ili uweze kuwa na mahusiano mazuri na Mungu wako.
✍ _Nianze kwa kusema Tendo la ndoa ni pana sana,lakini kama jina lake lilivyo tendo la ndoa ni kwa wana ndoa tu,siyo kwa vijana wasio kwenye ndoa( Huo ni Uasherati-dhambi kubwa)au siyo nje ya mke/mme wako huo ni Uzinzi-dhambi na laana kubwa_ kwa hiyo *Sex* ni tendo halali kwa wana ndoa.
✍Ukilizungumza tendo la ndoa siyo tendo la kukutanisha viungo vya uzazi tu(in- and out) tu,bali ni pamoja na maandalizi ya michezo ya kimahaba( *Sex Plays*) zikiwemo romance(busu zito/denda),kutomasana,na michezo mingi ya kuibua hisia,kuamsha mwili ili uwe tayari kwa tendo la viungo kukutana kwa uzuri,wepesi,na kuleta raha kwa washiriki( _Ndiyo maana vijana ambao hamjaoa wala kuolewa ni marufuku kufanya michezo hii inayoibua hisia za kufanya ngono,lengo la michezo hiyo siyo kwasababu ni rafiki,au ni upendo mkuu kwa mwenzako,ni kuuamsha mwili wake uwe tayari na mwepesi kwa ngono,kwa hiyo mkiicheza hata msipo kutanisha viungo vya uzazi uume na uke,tayari mmezini,mmesheratika kwa mawazo,na Mungu ahukumu matendo tu ila mawazo yazaayo matendo mabaya_)
✍Sasa, *Kunyonyana viungo vya Uzazi(uume na Uke ni Sahiii kwa wana ndoa?*
Mtazamo wangu ni huu, Lazima kwanza tujue aina za tendo la ndoa(ngono) Types of Sex.
1. *Genital sex*( ngono ya kutumia viungo vya uzazi uke na uume kuingiliana )Halali kwa Mungu,ndiye aliye umba na akatoa kazi yake *Zaeni* Mwanzo 1:26-28, kwa aina hii haina maswali ni moja kwa moja inajulikana.(Japo tendo la ndoa si kwaajili ya kuzaa tu,ni pamoja na kustareheshana wana ndoa,na kutuliza mawazo)
2. *Anal sex*(ngono ya Aja Kubwa)mwanaume kumwingilia kimwili mwanamke au mwanaume kwa nyuma,(kinyume na maumbile)( *Ulauwiti au Ufilaji*) Hii ni dhambi kubwa,laaana,imaleta ghababu ya Mungu haraka sana(matendo ya sodoma na gomora)
*_1 Wakorintho 6 : 9 - Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti._*
Kwa hiyo iwe kwa wana ndoa hamuruhusiwi,tumieni maumbile yenu,wengine huvunja mipaka ya Mungu kisa ni wana ndoa,wanafanya ngono hata ya nyuma kinyume na maumbile(Haja kubwa haikuumbiwa kuzalisha raha ya tendo la ndoa,unakosea sana).
3. *Oral Sex*(ngono ya mdomo) kama ilivyo ngono ya haja kubwa ndo ilivyo ngono hii,ila hii yaweza kuwa mwanaume au mwanamke,kutumia mdomo wake kunyonya na kumtosheleza mwenzi wake kingono. (hii nayo siyo Sahiii japo watu hupinga kwa kusema mbona kunyonyana ndimi(romance,siyo vibaya?iweke kunyonya nyeti ndo vibaya?)hoja nzuri( *Ni vizuri tujue kunyonyana ndimi ni mdomo kwa mdomo,viungo vinavyo fanana,vinavyo fanya kazi sawa vimetumika,siyo kimyime na maumbile*) tunge shangaa kama tungeona mtu ana nyonya kulamba haja kubwa tungesema ni kinyume na maumbile.
✍ _Mwana ndoa usibadili matumizi ya asili Mungu atawaacha......_
*WARUMI 1:21-28*
21 kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kumshukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza.
22 Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika;
23 wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu kwa mfano wa sura ya binadamu aliye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo.
24 Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao.
25 Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.
26 Hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu, hata wanawake wakabadili matumizi ya asili kwa matumizi yasiyo ya asili;
27 wanaume nao vivyo hivyo waliyaacha matumizi ya mke, ya asili, wakawakiana tamaa, wanaume wakiyatenda yasiyopasa, wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.
28 Na kama walivyokataa kuwa na Mungu katika fahamu zao, Mungu aliwaacha wafuate akili zao zisizofaa, wayafanye yasiyowapasa.
✍Cheza michezo yote lakini zingatia matumizi ya asili ya viungo vyenu
✍ *_Isitoshe mambo haya,yamekuja ikiwa ni maendeleo ya sayansi na technolojia,utandawazi ambapo wafanya ngono za biashara,wafanyao uchafu na machukizo,hufanya ngono,na kuona haitoshi shetani akaongeza mbinu chafu ikiwa imepakwa rangi ya utundu wa kitandani,kuwafanya watu wazidi kumchukiza Mungu hata wana ndoa,waingilane kinyume cha maumbile,nyuma na ndomoni,ikaongezwa nyingine ili kuzidi kuvuta ghadhabu ya Mungu,ikalewa ya usagaji,ushoga nk...tusipo kuwa makini tutakuta vyote tunaviona halali....lakini hayo yote ni matokeo ya Video za Ngono zinazo zidi kuja na navumbuzi mengi yaliyo jaa machukizo kwa Mungu_*
_Ni hitimishe kwa kusema,Ni udanganyifu mkubwa wa shetani,kuona kuwa unaweza kumtosheleza mwenzako au kumfanya anogewe na mahaba kwa kushiriki naye ngono ya mdomo(Kunyonyana Nyeti zenu)_
*_Unaonaje,Mungu akisitisha uwezo wa kuingiliana kwa viungo vyenu,uume na uke,mkabakiza kunyonyana nyeti zenu...Lengo na furaha ta ndoa na tendo la ndoa itafikiwa?_
*Tafakari Chukua Hatua*
_Mchambuzi Ev.Elisha Kazimoto(Baba Eve)_
*0755444078*
Monday, 2 January 2017
USIJITENGENEZEE MATATIZO
💣💣 *ỦS̉ỈJ̉Ỉ̉T̉ẺN̉G̉ẺN̉ẺZ̉ẺẺ M̉ẢT̉ẢT̉ỈZ̉Ỏ T̉ẺN̉Ả*💣💣
*_B̉ỷ Ẻv̉ Ẻl̉ỉs̉h̉ả K̉ảz̉ỉm̉ỏt̉ỏ@2017_*
*0755444078*
_S̉h̉ảl̉ỏm̉ w̉ảt̉ủ m̉l̉ỏp̉ảt̉ả ̉n̉ẻẻm̉ả k̉w̉ả M̉ủn̉g̉ủ k̉ủv̉ủk̉ả m̉w̉ảk̉ả 2016 n̉ả k̉ủỉn̉g̉ỉả 2017 k̉w̉ả ủs̉h̉ỉn̉d̉ỉ,h̉ảỉj̉ảl̉ỉs̉h̉ỉ ủm̉ẻỉn̉g̉ỉả 2017 ủk̉ỉw̉ả k̉ỉt̉ản̉d̉ản̉ỉ,g̉ẻr̉ẻz̉ản̉ỉ,ủn̉ảl̉ỉả ảủ ủn̉ảc̉h̉ẻk̉ả,h̉ảỷỏ ỷỏt̉ẻ n̉ỉ s̉ẻh̉ẻm̉ủ ỷả m̉ảỉs̉h̉ả,b̉ảd̉ỏ ủn̉ả n̉ảf̉ảs̉ỉ k̉ủb̉w̉ả ỷả k̉ủb̉ảd̉ỉr̉ỉs̉h̉ả m̉ảỉs̉g̉ả ỷảk̉ỏ k̉ủl̉ỉk̉ỏ ỷủl̉ẻ ảl̉ỉỷẻ ̉k̉ảt̉ả r̉ỏh̉ỏ 2016 k̉ảt̉ỉk̉ả s̉h̉ỉd̉ả h̉ỉz̉ỏ,d̉h̉ảm̉b̉ỉ h̉ỉz̉ỏ,m̉ảt̉ẻs̉ỏ h̉ảỷỏ n̉k̉,w̉ẻw̉ẻ ủn̉ả n̉ảf̉ảs̉ỉ k̉ủb̉w̉ả k̉ủf̉ản̉ỷả m̉ảp̉ỉn̉d̉ủz̉ỉ_
Ndo maana mtaalamu wako wa Saikolojia na mchambuzi wa masuala ya Mahusiano na ndoa *_Ev Elisha Kazimoto @2017_* mwanzoni kabisa mwa mwaka nakuletea Miwani👓 ya kukusaidia kuchungulia maisha yako ya mahusiano yako na Mungu,na Mchumba wako,na Mme/mke wako ili usiingie kwenye Matatizo na Stess zilizo kukumba 2016. *_sasa fuatana nami katika uchambuzi huu_*
*_Yohana 5 : 14 - Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi._*
✈ Nianze kwa kukutafakarisha, unakumbuka nini na nini 2016? Ukifumba macho🙈unaona nini, ukitafakari🙇🏻🙇🏻♀ unakumbuka nini?, Katika yale unayo yakumbuka yanakupa kufurahi😃😃😃au yanakupa kusikitika na kulia☹☹😭😭? Je,hayo yanayo kuhuzunisha yalikuja kama majaribu au uliyasababisha mwenyewe? Yanayo kupa furaha na kucheka yalikuangukia bila kutegemea au uliyatengenezea mazingira? *_Mpaka hapo najua umetafakari_*, Lengo langu ni uvae miwani👓 utazame vizuri siku 362 zilizo mbele yako ili *Usijitengenezee Matatizo Tena* Safiri nami
💎💎 *KIJANA/BINTI ULIYE KWENYE MAHUSIANO*💎💎
✍ Binti ulipewa promises nyingi na zawadi na kuahidiwa kuolewa 2016,umeishia kutumiwa tu kama chombo cha starehe,kwa sasa unalaumu na kulalamika na kulaani wavulana, Acha Kulalamika *_Acha kugawa mwili wako ovyo kama bigijii_* 2017 jiheshimu utaheshimika.
✍Kijana wa kiume, 2016 umepanga wadada wa watu foleni zaidi ya 7,wana hamu ya kuingia katika ndoa,mwaka umeisha hawajui hatima yao ni ipi, *Mbaya zaidi Umewatumia,umewavua nguo,mpaka huna hamu na hata mmoja huna mpango wa kumuoa* hiyo laana itakutafuna, 2017 Usiongeze laana,futa laana yasije yakakukumba mabaya zaidi.
✍Wewe mdada,ambaye 2016 kila aliye kuomba urafiki ulikubali,aliyekuahidi kukuchumbia ulimvulia nguo👙,2016 imeisha kwa kuvua nguo tu hujavalishwa hata pete ya urembo💍,unahisi kisaikolojia huko timamu? _Kisaikolojia umevurugwa wa kukuoa anakazi kubwa ya kukurudisha katika hali ya ubinadamu_. *2017 Usivue nguo kujiletea matatizo ya kisaikolojia yatakayo kufanya uchukie wanaume wote duniani*
✍Wewe Kijana, Umekwepa mimba ngapi ulizo wapa wa dada wa watu 2016,walikuamini kwa udanganyifu wako,umewaondolea sifa za kuitwa wadada,na sasa wanaitwa wamama wasio na waume. Uchungu huo ulo usababisha kwao usiuendeleze 2017, *_usijitengenezee matatizo makubwa ukawa na mwaka mbaya._*
*Mlio kwenye mahusiano*
✍Usiendelee na mahusiano ya kuvuana nguo👙kabla ya ndoa utajiletea laana ya kuto pata mtu sahii.
✍Msitende unyama wa kutoa mimba kwa sababu ya zinaa yenu kabla ndoa,kisa mnakwepa aibu,..Mtapewa aibu kubwa na Mungu baada ya kuua kiumbe hicho.
✍Acha mchezo wa kupotezeana muda wa tutaoana,kumbe unamuenjoy mwenzako huna mpango naye, hiyo itakugharimu huwezi kuwa na ndoa nzuri.
*WEWE MWANA NDOA WA 2017*
✍Usijitengenezee stress kwenye ndoa kwa kutotimiza wajibu wako kama mama kwa mme wako au kwa mke wako.
✍Acha kujitengenezea matatizo ya kukosa amani kwenye ndoa kwa kusikiliza majungu ya vijiweni,wenzako wanapigana busu vyumbani mwao wewe na mwenzako mnalala mzungu wa nne. linda mwenzako daima.
✍Unahisi ukiwa mbabe kwa mwenzako ndo unamkomoa ili wewe uenjoy au na wewe ndo walewale wenye akili fupi ya kukuta tawi alolikalia yeye na mwenzake.!.Usijiletee matatizo 2017,tulia ufurahie mwaka.
*Wewe Msimama Madhabahuni*
✍Wewe uloaminiwa na Mungu na kanisa,acha udanganyifu wa kuimba kwenye praise team,kwaya huku wewe ni mzinifu wa hali ya juu,acha kuichafua Madhabahu ya Bwana,2017 yanaweza kukuta makubwa,aibu ya mwaka. 2016 umefanya zinaa kwa kujificha sana na umefanikiwa,kuopoa vibinti vya praise team,kwaya..vijana wengi umewaangusha hata mchungaji wako umemwangusha, *STOP* usijiletee matatizo makubwa.
✍Enyi Makuhani wa Mungu mloibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, *_Mwahubiri mafanikio tu na miujiza,dhambi hamuzioni?Mbona mmegeuza wadada wanao hudumu ofisini kwenu na nyumbani kwenu mmewageuza Wake zenu wa pembeni? Wana kwaya na Praise team unao zunguka nao kwenye huduma mbona wawavua nguo?Mmewatelekeza Mama wachungaji nakuwaona hawafai mnaruka na vidada vidogo🤔🤔._* Acha 2017 inakuja kama moto usije pata aibu ya mwaka.
*NI HITIMISHE HIVI*
_Mungu amekuhurumia 2016,umevuka lakini pia amekuvumilia sana kwa maovu mengi,kwa nini mwaka huu usibadirike? Umekuwa na mwaka mgumu 2016,umeumizwa,umelia,umeachiwa jeraha na kovu la kudumu katika hisia na mahusiano yako,lakini wewe mwenyewe umekuwa mchangiaji mkubwa wa matatizo yako hayo,sasa Ushauri wangu kwa mwaka 2017_ 👇👇👇
*_Yohana 5 : 14 - Baada ya hayo Yesu akamkuta ndani ya hekalu, akamwambia, Angalia, umekuwa mzima; usitende dhambi tena, lisije likakupata jambo lililo baya zaidi._*
*By Ev Elisha Kazimoto @2017*
*0755444078*
NENO LA MWAKA 2017
✈✈ *MWAKA 2017 NI MWAKA WA KWENDA MBALI*✈✈
*By Ev Elisha Kazimoto*
*0755444078*
*_Bwana Yesu asifiwe sana wale wenye tumaini katika Bwana,huu ndio ujumbe alionisemesha Bwana tarehe 31/12/2016 mnamo majira ya saa 2 usiku,baada kumsihi Mungu nini Mungu anasema kwangu kuhusu mwaka 2017,kama ambavyo amekuwa akinisemesha kila mwisho wa mwaka akinipa neno la Mwaka mzima la kusimamia,mfano mwaka 2014 tarehe 30/12/2014 Mungu alinisemesha kuhusu 2015 kuwa utakuwa Mwaka wa Kicheko..AYUBU 8:20-21,na hakika kwa wote na mahali pote nilipo nena neno hili tangu kwangu hata kwa watu walio liamini neno la Bwana( 2Wafalme 7:1), lilitimia kwao.Tarehe 31/12/2015 nikapewa neno la mwaka 2016 kuwa utakuwa mwaka wa...Kupanua Mipaka yako(Isaya 54:2)..na sasa tarehe 31/12/2016 nimepewa neno la Mwaka 2017 kuwa utakuwa mwaka Wa kwenda Mbali_*
( *KUTOKA 8:25-28*)
_25 Farao akawaita Musa na Haruni akawaambia, Endeni mkamtolee Mungu wenu dhabihu ndani ya nchi hii._
_26 Musa akasema, Haitupasi kufanya hivyo; kwa kuwa tutamchinjia sadaka Bwana, Mungu wetu, na hayo machukizo ya Wamisri; je! Tutachinja sadaka ya hayo machukizo ya Wamisri mbele ya macho yao, wasitupige kwa mawe?_
*_27 La, tutakwenda safari ya siku tatu jangwani, tumchinjie dhabihu Bwana, Mungu wetu, kama atakavyotuagiza._*
_28 Farao akasema, Mimi nitawapa ruhusa mwende, ili mmchinjie dhabihu Bwana, Mungu wenu, jangwani;_
*lakini hamtakwenda mbali sana; haya niombeeni.*
✈Wewe uliye okoka,unamwitaji Mungu na nguvu zake ili kwenda mbali mwaka huu, *_Ni lazima kwenda mbali,ila kuna ushindani mwingi sana katika ulimwengu wa roho,changamoto nyingi zinazo kusudia kuto enda mbali,kutopiga hatua,kurudisha nyuma_* Ndiyo maana nakushauri mtu wa Mungu katika mwaka huu, *Kaa na Mungu sawasawa* watakao kuwa na uwezo wa kwenda mbali ni wale, *Walio wa Mungu kweli* wasio kubaliana na usemi wa adui, wasiokubaliana na changamoto za mazingira kuwakatisha tamaa, yaani *_Watu Ving'ang'anizi wa Imani hao 2017 Wataenda mbali kiroho na kimafanikio ya kimwili._*
✈ Ukisoma andiko letu pale la Farao na Musa na Haruni,uangalie mchuano wao,waruhusiwa watoe dhabihu lakini katika nchi ya Misri humo humo, na hawa lengo lao ni kutoka Misri, *Siku zote adui Hataki utoke mikononi mwake, anatamani aendelee kukuona katika vifungo alimo kuweka* Lakini na hawa watumishi wa Mungu hawakukubali changamoto ya mazingira hayo,wakasema *_Imetupasa kwenda mwendo wa siku tatu_* siyo hapa Misri,tunahitaji tutoke twende mbali.
✈ _Huwezi kufanikiwa,kupata heshima ukiwa bado ndani ya teso,huzuni,vita hiyo inayokuumiza ya tangu mwaka/miaka iliyo pita._ unahitaji kukataa ndo Mungu aingilie kati utoke uende mbali.
✈ *_Huu ni ujumbe mfupi,lakini ni mpana sana katika kuutafakari,Mungu akupe neema,2017 usijisahau,fanya maamuzi ya kuwa Rafiki wa Mungu na Mtu faida katika ufalme wa Mungu,utaenda mbali sana 2017, lakini pia wale waliozoea kudharau mambo ya Mungu,kuwa busy na mambo yao,mwaka huu unaweza kuwa mgumu kwao_*
✈✈ _Nikutakie safari njema ya siku 365 uende mbali katika jina la Yesu Amen_✈✈
*By Ev Elisha Kazimoto*
*0755444078*