🔥🔥 *K̤̈Ṳ̈N̤̈Ä̤ G̤̈Ḧ̤Ä̤R̤̈Ä̤M̤̈Ä̤ K̤̈Ṳ̈B̤̈Ẅ̤Ä̤ Ÿ̤Ä̤ K̤̈Ṳ̈L̤̈Ï̤P̤̈Ä̤ B̤̈Ä̤Ä̤D̤̈Ä̤ Ÿ̤Ä̤ Z̤̈Ï̤N̤̈Ä̤Ä̤ Ï̤L̤̈Ï̤ Ṳ̈K̤̈Ä̤Ë̤ S̤̈Ä̤Ẅ̤Ä̤*🔥🔥
_B̺͆Y̺͆ E̺͆V̺͆.E̺͆L̺͆I̺͆S̺͆H̺͆A̺͆ K̺͆A̺͆Z̺͆I̺͆M̺͆O̺͆T̺͆O̺͆_
*0755444078*
_Shalom,shalom watu mlio na safari ya kwenda mbinguni,ili somo linakuhusu sana kijana na mwana ndoa,unaye ishi katika kizazi hiki kibaya, *Kinacho tembea na Zinaa maishani kama tendo la kunywa maji upatapo kiu* kizazi kinacho tukuza na kueneza zinaa kwa picha,matangazo,video za ngono na hata kwa mahusiano ya uchumba na ndoa_ Uliye na safaribya Uhakika ya kumuona Bwana Yesu,fuatana nami upate kiurejezwa na Bwana.( *_Mchambuzi wako ni Ev.Elisha Kazimoto(Mjumbe Mkali Mithali 17:11)_* Mungu akubariki usomapo.
🔥🔥 *USIJIFARIJI KWA HABARI YA DHAMBI YA ZINAA* 🔥🔥
🔥Dhambi, ni uasi kwa Mujibu wa Biblia (1 Yohana 3:4)
🔥Kila dhambi ni mbaya mbele za Mungu, na zote tiketi yake ni jehanamu (uongo, masengenyo, wizi, Uzinzi nk)
🔥Pamoja na tiketi ya dhambi ya kwenda jehanamu, Kuna dhambi ambazo Hubeba (MAPATILIZO/ADHABU HAPA DUNIANI) kwa kuwa dhambi hizo huambatana na UOVU
🔥Kama kijana, na kama mtu wa Mungu uliye okoka, USIJIFARIJI, kuwa dhambi zote ni sawa, ukatenda dhambi ya ZINAA ukahisi gharama yake, ya malipo, na Gharama ya TOBA ni sawa.
🔥Miongoni mwa Dhambi za Uchafu, Zinazo mkasirisha Mungu, zilizo beba Uovu na nguvu ya MAPATILIZO kutoka kwa Mungu, ni Dhambi ya Uchawi, Uuaji, na Zinaa.
🔥Kumbuka, Biblia inasema, mshahara wa dhambi ni Mauti (Rumi 6:23)dhambi yoyote ni mauti (Mauti ya pili yaani Ziwa la moto /jehanamu.. Ufunuo 20:14)
🔥Lakini yeye aliye zifanya dhambi zote kuwa sawa kwa kuwa na hukumu moja ziwa la moto, ndiye aliye zitaja dhambi hizi 3 kuzipa Adhabu /MAPATILIZO.
🌃🌃 *NGUVU YA ZINAA,* 🌃🌃
🌃Kabla ya kutenda dhambi, au kuwaza toba, angalia Gharama ya dhambi kufanyika, Biblia imesemaje kuhusu dhambi hiyo na toba yake
🌃Nguvu ya dhambi na hasara zake katika maisha ya kiroho na kimwili, ndiyo iliyo sababisha hata makanisa, wachungaji kuwa na sheria /utaratibu mkali wa kutenga na kufukuza watu wanao ingia ktk shimo la dhambi hiyo
🌃Kuna ushahidi wa kibiblia na kibinadamu juu ya nguvu ya dhambi ya zinaa, hasara zake, matokeo yake ktk maisha ya mtu, nayo ntayaeleza hapa ktk uchambuzi huu
😡😡 *ZINAA INAUA UTU WA NDANI*,... Katika dhambi biblia imetamka wazi kuzichukia ni ZINAA, kwa namna hiyo usitegemee na matokeo yake ni madogo na toba yake ni nyepesi kihivyo 👇🏻👇🏻👇🏻
18 Ikimbieni zinaa. Kila dhambi aitendayo mwanadamu ni nje ya mwili wake; ila yeye afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenye
*1 Wakorintho 6 :18*
32 Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa;Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake.
33 Atapata jeraha na kuvunjiwa heshima;Wala fedheha yake haitafutika.
*Mithali 6:32-33*
🔥🔥Tafuta katika biblia, dhambi ambayo imesema Kuna kitu hakitafutika 🙅🏻, unajua dhambi nyingi hazina majeraha yasiyo futika, isipo kuwa dhambi ya zinaa,
🔥Usije ukasema, nikitubu tu mambo yamekuwa sawa, ni kweli ukifanya toba ya Dhati, unasamehewa, ila Jeraha, kovu, outcomes za hiyo dhambi hazifungwi utazitumikia
🔥(mfano mtu aliye pata HIV/AIDS ktk zinaa, akiomba toba ya dhambi yake anasamehewa, na akifa mbinguni anaingia, ila toba yake na msamaha haumuondolei Jeraha, malipo ya zinaa (HIV) labda kwa rehema tu za Mungu
😡😡 *ZINAA INAFUTA FUTURE YAKO* Miongoni mwa dhambi za kuku fanya upoteze vision uliyo kuwa nayo ya maisha ni ZINAA, ina nguvu ya kukuondolea nguvu ya kutimiza vision yako
🔥Yusufu alipo jikuta yupo mikononi mwa shimo la ZINAA, Alisema, Nifanyeje ubaya huu mkuu ni mkosee Mungu wangu, tafsiri ya hapo Yusufu alikuwa hasemei dhambi kama dhambi, alikuwa anasemea kupoteza ndoto zake (ZINAA inavuruga vision yako)
6. Akayaacha yote aliyokuwa nayo mkononi mwa Yusufu; wala hakujua habari za kitu cho chote chake, ila hicho chakula alichokula tu.Naye Yusufu alikuwa mtu mzuri, na mwenye uso mzuri.
7 Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami.
8 Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.
9 Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?
10 Akawa akizidi kusema na Yusufu siku baada ya siku, lakini hakumsikia alale naye, wala aongee naye.
11 Ikawa, siku moja, akaingia nyumbani atende kazi yake, wala hapakuwa na mtu katika watu wa nyumbani humo ndani;
12 huyo mwanamke akamshika nguo zake, akisema, Lala nami. Yusufu akaiacha nguo yake mkononi mwake, akakimbia, akatoka nje.
😡😡 *ZINAA INAKUONDOLEA UJASIRI WA KUKEMEA DHAMBI NA KUIPINGA DHAMBI KWA NGUVU,* Zinaa ni sumu ya Nafsi na moyo, wote walio anguka katika dhambi ya zinaa wana sura mbili
🔥Sura ya kutetea udhahifu wa mwili, kuona mwili una nguvu na unaweza kukukosesha, hivyo usijilaumu, au kumlaumu mtu, kushindwa kuisimamia kweli kuhusu kuipinga dhambi, Kushindwa kuikemea dhambi ya zinaa wazi wazi na kwa ujasiri kwa sababu wana hatia ndani ya wao Kushindwa ktk eneo hilo
🔥Sura ya kuikemea dhambi ya zinaa kwa uchungu na kutahadharisha wengine, wakiangalia hasara walizo pata kwa sababu ya kuanguka ktk zinaa 👇🏻👇🏻👇🏻
20 ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote.
21 Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu;
22 na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake.
👆🏻👆🏻Watu wengi walio anguka katika dhambi ya zinaa, wana hali ya *HATIA KUU* mioyoni mwao, hata wakitubu hawajiamini kama wamesamehewa, hii inawanyima ujasiri wa kuikemea dhambi ya zinaa kwa watu, na mara nyingi wanajihesabia kuwa wadhahifu kimwili
🙏🙏 *TOBA YA ZINAA NA UTARATIBU WA KANISA KUHUSU ZINAA* 🙏🙏
🙏Ikimbukwe kuwa, dhambi ya zinaa *HAINA BAHATI MBAYA*
🙅🏻🙅🏻, dhambi ya zinaa, ni mpango mkakati unao husisha, akili, macho, masikio, kinywa ulimi, miguu, mikono, Gharama ya muda na pesa, na Gharama ya kufunua nguo na kuizika Aibu ya mwili wako mbele za mwenzako, na Kuanza zinaa kuondoa tofauti zenu na kujiungamanisha miili, akili na maji ya mwili,
🙏Kwa Uzito wa Gharama za dhambi hiyo, hasara zake, makanisa yameiwekea sheria kali itokanayo na Neno la Mungu kuithibiti, malengo si kuwakomoa walio tenda dhambi, ila kuzuia mlolongo wa watu Kuingia ktk shimo la dhambi hiyo ya zinaa, na kupata hasara kubwa ya maisha, na kanisa kwa ujumla
🙏 *TOBA YA ZINAA*, kwanza usijutubishe, dhambi kwa kufunga na kuomba ili usamehewe, toba ya Dhati ni kuiabisha dhambi, kama ilivyo fanywa kwa siri, iaibishwe wazi ktk toba ndipo utaishinda
🙏wengi wa watu walio anguka katika dhambi ya zinaa, wakajitubisha, wamejikuta wakaanguka tena, na tena, na tena, wamebaki kuiona ya kawaida, au ni jaribu kwao, au udhahifu wao
🙏Andika hili linatoa picha ya hatua za kushughulikia dhambi kanisani 👇🏻👇🏻
9 Naliwaandikia katika waraka wangu, kwamba msichangamane na wazinzi.
10 Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang’anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia.
11 Lakini, mambo yalivyo, naliwaandikia kwamba msichangamane na mtu aitwaye ndugu, akiwa ni mzinzi au mwenye kutamani au mwenye kuabudu sanamu au mtukanaji au mlevi au mnyang’anyi; mtu wa namna hii msikubali hata kula naye.
12 Maana yanihusu nini kuwahukumu wale walio nje? Ninyi hamwahukumu hao walio ndani?
👫Kama mkianguka ktk zinaa, haraka sana ombeni toba kwa Mungu ninyi kama ninyi
👫Toba yenu iwe ya Dhati, yaani muhakikishe hamurudii tope hilo
👫Kimbieni kwa mchungaji wekeni wazi dhambi hiyo, na muwe tayari kufuata ushauri mtakao pewa kuhusu anguko hilo
👫Ombeni Rehema Juu ya maisha yenu na ndoa yenu
👫Msihi Mungu abatirishe roho ya kutoaminiana kati yenu
👫Wekeni mipaka mikali ya kujilinda msirudie tena ktk anguko
👫Kubaliana na matokeo ya tendo lenu la ZINAA kama ni mimba ilee, funga ndoa mkiwa mmeweka wazi hali hiyo, msifunge ndoa kimya kimya, kumbe mmeisha haribu mtapata laana kubwa
✔ *EPUKA MAJUTO KATIKA NDOA* ✔
✔Sina uhakika kama kweli mtazamo nilio nao, picha ninayo pata kwa neema ya Mungu aliyo nipa, na sehemu ya maarifa niliyo pewa kama na watu wengine hasa vijana wamepewa
✔Lakini kwa kutambua hivyo ndo maana namshukuru Mungu kwa neema hiyo, pia anaye tufanya tushirikishane mambo mbali mbali, uliyo nayo sina, niliyo nayo huna
✔Kwa sababu hii, Leo nakuongezea Siri nyingine za kujenga, kulinda ndoa yako
✔Usisome na kufurahi tu, tafakari chukua hatua, usije ililia ndoa yako, au ujana wako au maisha yako
✔Siku zote, huwa nasema, tamani kupata maarifa, ni utajiri mkuu, utawafanya hata wenye pesa na Mali kusujudu au kukuheshimu daima
💥Unahitaji ndoa ya maana, nzuri, baraka, utulivu, basi *_"USICHEZEE UJANA WAKO"_*
💥Nivigumu kuelewa sentensi hii niliyo sema hapo juu" *_USICHEZEE UJANA WAKO"_* usiitazame katika mwonekano wake, itazame katika upana wake, utaelewa uchambuzi huu.
💥Ndoa nyingi zinaleta shida makanisani mpaka Talaka zimeingia kanisani, kuachana na kuolewa, kuoa kupo makanisani, Kuto oa au kuolewa kupo makanisani, hivi unahisi nini chanzo chake??
💥Kwanza nikufungue macho unaye taka kuoa au kuolewa, juu ya vijana wa kike na wakiume walio makanisani,
💥Wapo vijana *"MATAPELI"* kanisani, wanahudumu ktk mazingira mbali mbali, lakini ni Matapeli wakuu katika mahusiano
💥Wako Mabinti *"WAHUNI"* wanasifa zote za kiroho kwa kuigiza lakini ni sumu kali katika maisha ya mahusiano
💥Usipo kuwa makini, ukipambana na mmoja wa wavulana au Wasichana hao, utajitwisha mikono daima katika ndoa
🔥Sumu ya maisha yako ya ndoa Nitabia yako ya sasa ukiwa kijana❗
🔥Vijana wa kike kwa kiume, wanaendekeza *"NGONO"* kama Ajira yao, hofu imetoweka ya kuogopa ngono, ngono katika maisha nje ya ndoa (kabla ya ndoa) imekuwa kawaida lifestyle❗
🔥Watu kuanzisha mahusiano ya uchumba kwa kutumia kipimo cha Ngono imekuwa kawaida, hakuna anaye mtafuta Mungu aseme naye nani amuoe au aolewe naye, kigezo kimerudi, "we mkali wa mapenzi" tuoane❗
🔥Ni nani katika vijana wa kike na wakiume, mwenye kiapo mbele za Mungu na katika maisha yake, asemaye *_"SITA MVULIA NGUO KIJANA AU BINTI NIMJUE KIMWILI MPAKA MME WANGU AU MKE WANGU"_* ❓❗
🔥Imekuwa ni Hadithi kusikia au kuona Binti anaye sema *"MIMI NI BIKRA NA KWELI AKAWA NI BIKRA*" ❗
🔥Imefikia hatua vijana wa kike na wakiume, uwezo wa Kusimamia Neno la Mungu la " *IKIMBIE ZINAA*" wengi wanaogopa, wamebaki kuhalalisha kuwa dhambi zote ni sawa ❗❗
🔥MIJADALA katika makanisa kwa vijana imekuwa si ndoa yangu iwe ya ushindi na baraka bali iwe ya wenye pesa, gari, nyumba na elimu ya juu, kwa njia hiyo wamekuwa radhi Kufanya zinaa na mtu ambaye atasababisha mazingira hayo anayo yatamani yawepo
👑Vijana wengi wanajiuliza, kwa nini wameshuhudia ndoa za kale zimedumu sana mpaka uzeeni, watu wanapendana, wanaheshimiana, wanajaliana?
👑Watu walikuwa makini na *KUTO JIINGIZA KATIKA ZINAA KABLA YA NDOA*
👑Niutamaduni UPI mpaka sasa wanaweka mashuka meupe kwa siku ya kwanza kwa wana ndoa, ili wathibitishe Ubikra wa msichana aliye olewa, wazee wapi wanakagua mashuka hayo kwa sasa?
👑Hata sasa makanisani watu wanachumbiana hawaaminiani, kila mmoja anasema vyovyote itakavyo kuwa basi, ndiyo maana tabia ya kuonjana imeshamiri mpaka makanisani, hakuna anaye hisi huyu ni Bikra nimgoje aje kwangu tuanze na moja pamoja
👑Kwa sasa ukisema namtaka kijana Bikra asiye mjua mke, Mabinti watakushangaa, hivyo hivyo kijana ukisema namuomba Mungu anipe msichana Bikra watu watakucheka
👑Kwa nini, Ngono Imekuwa ndo KISHIKA uchumba wa watu, Badala ya Uaminifu na Mungu
👑Vijana wengi, wa kike na wakiume, hawapendi kuzungumza msimamo wao kuhusu mapenzi au zinaa, wanahisi ukisema yakakushinda kuvumilia itakuwaje?!
👑Huu ni udhahifu mkubwa na maandalizi ya Anguko la mara kwa mara ktk zinaa
👑Niliwahi kusema, na sifichi, na hii ndo Imani yangu kwa Mungu na kwa mke wangu mtarajiwa, " _HAITATOKEA KABLA YA KUOA KUMJUA MSICHANA YEYOTE, HAITATOKEA BAADA YA KUOA NIMJUE MKE MWINGINE ZAIDI YA MKE WANGU"_
👑Biblia inasema tutakula matunda ya vinywa vyetu,(Mithali 12:14)si kujiona, kujiaminisha, kujisifu, _NAYAWEZA MAMBO YOTE KATIKA YEYE ANITIAYE_ nguvu" *wafilipi 4:13*
*_Ukijua madhara ya zinaa na Gharama yake katika Toba,hutathubutu kuvua👉👙ili ufanye zinaa.Utajilinda,usubiri ndoa yako,lakini pia kama umeharibu,fanya matengenezo ya kweli,Toba ya kweli ili urudi mbele ya Mungu uwe na nguvu na ujasiri rohoni mwako unapo mwendea Mungu wewe binafsi_*
_Ulikuwa na mchambuzi wa mahusiano na Ndoa,Ev.Elisha Kazimoto_
*0755444078*