Sunday, 26 November 2017

SWALI: STYLE ZA SEX NANI AANZISHE

Swali: *Hivi ni vibaya mwanamke kuanzisha style mpya ya sex kwa mume wake? Au anatakiwa atumie mbinu gan kuianzisha?*

Anajibu: Ev Elisha Kazimoto(Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na ndoa)
WhatsApp 0755444078
_Kwanza Ndoa ni uwanja wa watu wawiliwa amani,furaha na upendo na uhuru, mwana ndoa anahitaji kuwa huru kwa mwenzake,na kila linalofanyika ni la kwenu wawili, sasa maudhui ya umoja wa wana ndoa yakibadirika ndoa inakuwa chungu,na ndoa ikiingiwa tu na mdudu uwezekano wa kwenda mbinguni,unaanza kuwa mdogo_
👉 Kweli ni kwamba ndoa ni mlango, ni chombo kizuri cha usafiri kwenda mbi guni au jehanamu, ambao hamjaoa au kuolewa, kwenye ndoa hupaswi kuishi katika ndoa kwa kujikaza au kiugumu, jua mbingu una asilimia 10 kati ua 100 kuiona. Ndiyo maana tunawashauri vijana usiingie kwa ndoa kutafuta sex, tafuta kusudi la Mungu, usitamfute mtu wa mitoko na kukidhi mahitaji ya kiuchumi, tafuta na omba mtu atakaye kusogeza karibu na Mungu na kukufanya utimize kusudi la Mungu.
👉Unapo kwenda kuoa au kuolewa jua ndoa yaweza kuwa ngumu au nzuri(nyepesi)kutokana na aina ya ndoa utakayo chagua kuishi.
Kuna aina 3 za ndoa, *Moja , Ndoa ya Kirafiki, pili Ndoa ya Kitoto, tatu Ndoa ya kibosi* wengi hasa wasiopenda kujifunza na hasa walokole(siwasemi vibaya maana miongoni mwa walokole mimi ni namba moja najivunia neema hii) ila wengi wao maarifa ya kidunia wameyatupilia mbali kwa kisingizio cha wanajua tu maarifa ya biblia nayo hawako vizuri,kwa hiyo kote hawako vizuri ndo maana ndoa zinakuwa ngumu sana wengi wao wana ndoa za KIBOSI hapo ni amri,uchifu, nk lakini ndoa ya kitoto ni kucheza na kufurahi na kusameana,ndoa ya kirafiki ni kusaidiana ka hivyo ku mshave mwenzako,kumuogesha,kusaidiana vikazi vya haoa na pale kwa upe do si kwa kuagizana.
Kuna kawimbi ka wahuni wa imani, kutafuta namna gani ya kutengeneza vitisho kwa watu,au tofauti ya imani nawe uwe ni mwana imani iliyo tofauti na wengine,bila kuzingatia neno la Mungu na Nature of Creation.(  _Wanasema wana ndo kufanya tendo la ndoa kwa style mbalimbali ni dhambi, ni style moja tu ya chali mama baba juu ndo takatifu_) Huu niuhuni mkubwa wa kiroho.
Mungu alipotuumba alitupa intelligence(Akili) . Sasa imani ya style hii takatifu na hii dhambi ni mavumbuzi ya wanadamu,Ukisema neno dhambi ni Katazo la Kimungu. Sasa sijawahi soma aina ya style kwenye biblia, ila intelligence ya uumbaji inatusaidia  kutafuta pozi zuri la kufurahia sex. Kwani nani alikupa agizo la ukilala ulalie mkono wa kulia au kushoto,au chali...kwa nini huwa unajigeuza ukilala? Ni katika kutafuta pozi la kuenjoy usingizi alotuumbia Mungu hivyo hivyo na styyle za sex.
Zipo zaidi ya style 100 za sex ila nyepesi 15,inategemea na flexibility ya miili yenu wotw wawili.
NB: *_Kilicho marufuku na dhambi kwa raha zenu zoote,kwa mifumo yenu yote, style zenu zote msifanye machukizo ya kuingiliana kinyume na maumbile(msibadiri matumizi ya asili ya mwanamke au mwanamme)neno limesema hivyo._*
👉Kwa suala la nani wa kuanzisha zoezi la kunlbadiri style kati ya mwanamke au mwanamme ni yeyote ila Kisaikolojia, kabla ya tendo la ndoa mwanamke anakuwa na aibu, na akili inashuka, wakati huo mwanaume hana aibu,aikili inachaji asilimia mia, sex ikianza in and out...mwanaume anapoteza akili(akili inashuka) mwanamke ujasiri unaongezeka na akili inaongezeka, na controller wa game ni mwanamke ... Shida maarifa kwa wana ndoa zero,hakuna watu wa kujitoa muhanga ku calculate mambo ya mahusiano kwa kina, tunaishia kufundishana kanisani MSINYIMANE,MTII MMEO NA MPENDE MKEO semina zote. Hii ndo Shida .Uliza wana ndoa wenye umri miaka 15 mpaka 50 kwenye ndoa, usikie haya tunayo fundisha na kufundishwa kizazi hiki kama wao waliyapata. Kwanza  kujadiri mambo haya ya sex enzi hizo ni dhambi kubwa,ukiyasikia unaingia maombi ya kufunga siku 3 kujitakasa. Mmmh shida kweli. Ndoa zilitembelea kwenye neema ya Mungu tu 100% bila maarifa mengine, sasa dunia ya sasa siku za mwisho maarifa yameongezeka,usipo kuwa nayo ndoa utaichukia.
👉Tendo la ndoa lina nogeshwa na vitu vingi tangu kuandaliwa na wakati linafanyika. Vitu kama kiss,romance,sex play nk.
Nijambo la kushangaza kukwepa romance ya mke wako au mmeo, moja ni dalili ya kutokomaa kisaikolojia katika ndoa, lakini kuna mambo ya msingi kwa wana ndoa kuyaweka vizuri, USAFI WA KINYWA, ili usiwe kero kwa mwenzako harufu mbaya. Pili busu haiwi ya fujo, iwe ya kitaratiibu,yakimahaba, iwe na maandalizi ya gentle touching,sex touch & sex play ndo romance inakuja automatically, siyo unavamia kichwa cha ntu na kuromance.
👉 Ndoa nyingi watu wanaishi kwa fujo kukuru kakara, hawana vionjo vipya,hawajui jipya,hilo hilo waliloanza nalo mpaka kuzeeka ndo hilo,mpaka ndoa inachosha, kazi za walimu,wasomi na watumishi wahubiri kunusurisha ndoa za wana wa Mungu kwa kufundisha kwa kina.
👉 *_Sasa tuhitimishe hii topic hivi, Tendo la ndoa kwa wana ndoa kwanza ni Huru, ni la raha,si la kulazimishana, siyo la kuibiana ni suala la makubaliano baina ya watu wawili, linahitaji kugusa feelings,kuongea kuhusu hisia zako kwa mwenzako, unataka akufanyie nini,ashike wapi, akaeje, tendo la ndoa halifanywi kibubu, gizani,ghafla linahitaji maandalizi ya kisaikolojia na kimwili,hakuna mwenye hati miliki ya tendo kuliko mwenzake wote mnapaswa kufurahia na kufikishana kwenye kilele cha raha_*

Kwa wakati wa tendo ongeeni raha unayo ihisi,unatamani uhisi nini zaidi,sema na mwenzako tukae hivi sasa,muulize mkao huo anahisi raha au kuchoka na kuumia,hapa ni mtu yeyote kuongea.
Shida watu tangu siku ya kwanza ya ndoa sex ni kifo cha mende,mpaka first born,2,5,.   Huu ni ushamba na kuchokesha ndoa na miili yenu.
Wana ndoa wengi wanafanya tendo la ndoa kama WAJIBU ,au kutimiza hisia zao ila si kama ENJOYMENT.

Badirika usiwe Regidy,Static, conservative utamchoka mwenzako.
*_By Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp 0755444078

Friday, 10 November 2017

UZUSHI KATIKA UCHUMBA

MADA SWALI

...hivi upo ktk mahusiano na mtu mmoja tu lakin ikatokea habari zinazoeneaenea kidogo kuwa u mzinzi upo na mahusiano na waschana wanne na huyo mmoja wa ukweli akiwemo!! Ukizingatia wewe ni mtu mwenye wadhifa Fulani wa kiongoz ktk kanisa,na wapo wanaokuamin na kukuheshimu sana!! Na yule Mwenzako wa ukweli yeye anaelewa na anakuamin sana kuwa u mwaminifu!!na ni kweli mwaminifu...

Je, utafanyeje??

Anajibu: Ev Elisha Kazimoto
WhatsApp 0755444078

Kwa kuhitimisha mada hii, tuyaangalie mahusiano haya katika jicho la wawili kwanza kabka ya watutu

Mara nyingi watu 2 mlo kwenye mahusiano ndo mna hatima ya kuamua mahusiano yenu yawe na harufu gani kwa watu.(kwa kuwa ameuliza nini kifanyike katika hali ambayo imeisha kuwepo,basi nitakazia upande huo.
👉Kwanza binti na kijana wakae pamoja wafanye Psychological Cross-checking ya mazingira ya mahusiano yao(maadamu wamethibitisha WANAAMINIANA) basi wakae waongee humu kanisani,ofisini,au mtaani tulimo watu wagani wamo?(wadada wengi? Vijana wakiume ndo wengi?wanawake?au wanaume?)....eqution .....(i)
(Wanaoongelea mahusiano yetu kwa wingi na kuzusha maneno hayo ni watu gani(wadada? Wakaka?wamama?au wababa?au wote?)........ Equation......(ii)
Wanaoongea wana msakama nani(binti/mkaka)..... Equation .....(iii)
Uongeaji wao watafuta nini kwetu( kutuachanisha, kutuchafua,kutusaidia kiroho,au kupata nafasi ya kupendwa wao?)......Equation......(iv)
Baada ya kusolve Equation hizo by substitution mtagundua maisha gani muishi,na agenda gani muibebe.
Tukianza kufanya Substitution katika Equations zetu
👉Equaton (i)kama wamo wengi wadada au wakaka jua mpo kwenye competition kubwa ya kutafuta nafasi ya kuoa au kuolewa(hapo ninyi kazeni kamba kuziba masikio wasiwagawanye kisaikolojia) maana hapo formula inayowasumbua kwenye mazingira ni Scarcity of Resources (girls/boys)to marry
👉(ii) kama ni wadada au wakaka (kila mmoja wenu achunguze past zake)kama ziko swa jua hao wanatafuta mpenyo.... Na kama ni wamama au wababa(jiulize nani ana binti mkubwa au kijana mkubwa umei wa kuoa au kuolewa)kama yupo tafakari mvuto wako kwa watu upo juu ? Kama huyupo tulieni.
👉Equation (iii)anaye sakamwa kaka ni mkaka(mdada ongeza ulinzi,kama ni mdada mkaka ongeza ulinzi)ulinzi wa kuwa mwaminifu,na kuongeza viwango vya kumpenda huyo,na kumsaidia mwenzio asiporwe
👉Equation ya (iv)lengo laazungumzo mtalijua kama watu wanawafuata kuwambia au unasikia wanaongea huko.(tendea kazi mazunhumzo yao)
By Ev Elisha Kazimoto
WhatsApp 0755444078

Tuesday, 7 November 2017

MDADA KUSEMA NO INAMAANA GANI

Mada ya kuna athari gani kuoa mke ulombembeleza akakukataa kwanza baadaye akakukubali, vipi athari zake kwenye ndoa

​Anajibu​ ​Ev Elisha Kazimoto​
WhatsApp 0755444078
👉Si kila mkatao wa mwanamke umemaanisha kukukataa usiwe mme wake, mkatao huo unakuwa na maana kama mbili tatu, moja.. Bado saikolojia yake haijakusoma iambatane nawe(kubuka mwanamke,hapendi mpaka apandiwe wazo la kupendwa,yeye alizungushe akilini ili lizae wazo la Yes au No.
👆kwa sababu hiyo No inaweza kuja muda huo au muda wote ambao bado akili yake haijazungusha na kupata jibu la moja la ndiyo au hapana. Na mwanamke mpaka ashawishiwe, kumbuka wewe kijana ndo uliyejiridhisha kwa binti ndo maana ukaamua kumfuata na kutaka kuwa naye, unampandia wazo jipya,ambali hakuwa nalo, kwa hiyo ulinzi wake wa kutafuta jibu sahihi la hisia zake ni (NO, AU NTAKUPA JIBU)
👉Pili mkatao ule unaweza kuwa Unalenga kupima NIA YAKO ni muoaji au ni mwenye tamaa ya kumtumia( Are you a real husband to be or a boy of enjoyment) mara nyingi a real husband akipenda, moja hatakata tamaa kufatilia mpaka amekubaliwa, pili hata tafuta short cut kuomba basi sex kama hutaki tuoane, tatu ni msitaarabu kufatilia kwake si kwa kero,bali kwa upendo. Kwa maana hiyo wadada husema No mpaka aone nia yako ya ndani ni ipi,inaendana na shahuku yake?
👉Mkatao mwingine unalenga kukupa taarifa ya Kajipange kimaisha, wanawake wengi huwa wana ​worry about life style​ kabla ya kumkubali mtu wanataka wajiridhishe uwezekano wa kutunzwa na kuishi maisha ya furaha na amani. Kwa sababu hiyo akisema No mara ya kwanza baadaye akakukubali ni kwamba alikuwa anakupa message ya kajipange kimaisha uwe well off then come, ndo maana wengine usipo onyesha badiriko la kimaisha tangu ume propose ukirudi utaikuta No, ila ukienda ukajipanga ukirudi unakuta Yes.
👉Mkatao mwingine unamaanisha Si Muda Muafaka, wengine wadada wamejiwekea malengo ya nitaanza relationship ya kuingia kwenye ndoa nikiwa na umri kadhaa,au nikiwa level flani ya elimu, au uchumi,nk sasa ukienda kabla ya muda utakuta No mpaka muda wake ukifika ndo utaikuta Yes.
👉Mkatao mwingine niwa Kusibiri Mlinganisho,( inamaana kuwa wapo wadada wasemao No,wakisubiria wafike watu 2,3,4 ili waone kama nani yuko best kuliko wengine ndo aseme Yes kwako, akikosa atasema yes,wakija akaona umewazidi sifa waliokuja atasema yes
👉Kuna mkatao wa ​TOTALLY I DON'T LOVE YOU​ huu ni mkatao wa you dont fit to me, sasa mkatao huu una viashiria vyake, moja hutaheshimiwa kwa namba yoyote,utakatiwa simu zako zote,au hutajibiwa simu zako au ataku block,hatakusema vizuri kwa marafiki zote,utapewa majibu ya mkato tu,utaambiwa live mapungufu yako, hatapokea offers zako, na akizipokea bado hata kuomba kitu
​Sasa mtu wa namba hii kijana ukitumia ushawishi mkubwa wa pesa,zawadi,wazazi wake,ndugu zake,marafiki zake ili akukubali, siku akikukubali mkaingia ndani akikisha unajipanga kwenda naye kwa taadhari, ila athari utapata heshima kidogo,lakini itabidi maea kwa mara uwe mpole kwake,utaporwa position yako ya kichwa​
Jifunze kusoma ishara ya upendo ndo uokomaye naye,asiye na upendo hatakama ni Angel piga kona kwenye ndoa sura yake hutaiona, uraona matendo korofi, utajuta.
Ev Elisha Kazimoto
WhatsApp 075544078