Thursday, 31 October 2019

UZURI WA MUNGU KWETU NEW MONTH

🥦🥦 *HUU NDIYO UZURI WA MUNGU WETU KWETU*🥦🥦
*_Imeandaliwa na Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
       *NEW MONTH NOVEMBER 1.209*
................................................
        *_Tafakari ya Leo_*
_Shalom wana wa Mungu aliye hai. Leo ni tarehe 1.11.2019 ni mwanzo wa mwezi katika siku ya kwanza,nakutafakarisha uzuri wa Bwana_
*(21)Najikumbusha neno hili, Kwa hiyo nina matumaini.(22)Ni huruma za Bwana  hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.(23)Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.Maombolezo 3:21-23*
🥦Katika andiko hili, mstari (21)... Kuna jambo la kujifunza na kupata nguvu ya kuendelea mbele katika safari ya kuelekea mwisho wa Mwaka. Hapa yako mambo makuu 2.
1⃣Anasema _Najikumbusha Neno hili....._ Nimuhimu sana katika maisha kuwa na tafakari juu ya *Uliko Toka* Kujikumbusha, kwa lugha nyingine ni *Kurejea nyuma uliko pita, au kurudisha kumbukumbu za kilicho semwa,onwa* Vipi mpendwa Ukirejea nyuma uliko toka tangu tarehe 1.1.2019,unaona nini? Kama mpaka sasa upo ila unataarifa za watu wengi ambao mpaka sasa hatunao duniani,wengine ni wapendwa wetu wa karibu.... Hii Haikupi kuona kwamba *Bado Bwana ana Haja nawe Duniani?* Pamoja na Changamoto ngumu ulizopitia na tunazopitia lakini Uhai bado upo ndani yetu na Uhai ndo Injini ya Mabadiriko ya Maisha.
👉Jikumbushe ulivyo ponywa na Ajali ile mbaya, jikumbushe ulivyo pita kwenye lile pito zito mpaka ukakata tamaa, Lakini Ulipita, *Huo ndo uzuri wa Bwana*
👉Jikumbushe neno hili, Bwana wetu alivyosema *Sitakuacha wala kukupungukia* jitie nguvu sasa katika mwanzo mpya wa mwezi huu.
🥦Katika Mstari huo huo wa 21b, anasema _Kwa hiyo Nitatumaini_ Ukijikumbusha wema wa Mungu kwako, hutakuwa na Sababu ya *Kukata tamaa* na kuona kama Mungu amekuacha, aliye tenda yale ndo atatenda na *Hili* kwahiyo NITATUMAINI.
2⃣Katika mstari wa (22), amesema..... _Ni huruma za Bwana Hatuangamii_, Hakika ukikaa ukatafakari utajua ni Huruma tu za Bwana, adui ibirisi,mawakala wake wana lenga kila siku *Tuangamie* na wakati mwingine wanataka watumie nafasi ya *Udhaifu wetu* kutuangamiza ila HURUMA ZA BWANA zina tukinga.
_Hali halisi kwenye ulimwengu wa Roho kwako ni hii_
*13 Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini Bwana akanisaidia. Zaburi 118:13*
👉Kila siku, kila saa,kila dakika wapo *Wakusukumao sana* ili uanguke,lakini kwa nini hata sasa umesimama(Kiuchumi,kiafya,kindoa,kimahusiano,kieleimu,Kikazi,kihuduma nk) Ni *Huruma za Bwana* wakitusukuma anatusaidia kusimama.
🥦Tunaweza kuendelea kufurahia maisha ya kila siku,ni kwasababu tu *_Rehema za Mungu Hazikomi_* Na huo ndo usalama wetu, Rehema ni kiwango cha juu cha Kusamehewa na kuhurumiwa wakati ulikuwa unastahili adhabu.
3⃣Katika Mstari wa (23).... _Amesema, Ni Mpya Kila Siku Asubuhi_, tunatembelea kwenye mambo mapya ya Mungu, kawaida ya Mungu kwetu siyo *Kutulisha Viporo vya Jana* anatuandalia mambo mapya kila siku asubuhi.
🥦Kwa lugha hiyo walio cheka jana yako wata shangaa leo yako na kesho yako.... Maana utakuja na *Mambo mapya* yanayo toka kwa Mungu wetu. ( _Huu ndo uzuri wa Mungu_)
🥦Halafu anasema, _Uaminifu wake Mungu ni mkuu_, Hapa ndo huwa mioyo yetu inatulia kwa Bwana, yeye ni mwaminifu akiahidi atatenda,kazi yetu ni kumwamini na kuvumilia.
👉Huna sababu ya kumwacha Bwana, kuacha kumtumikia, kukatishwa tamaa na watu au mazingira, Uaminifu wa Bwana ni Mkuu,kiwango chake cha Kutimiza alicho sema ni cha Juu na Uhakika ndo maana yake.
_Unajua nini? Tumeanza mwezi huu na Bwana nao utaisha, Usiogope wala usiogopeshwe, ni mwisho wa Mwaka Utasafiri utatoka nyumbani salama na utafika uendako salama, Kafara za waovu Hazikuhusu wewe, sisi tunalindwa na Nguvu za Mungu kwanjia ya Imani( *1Petro 1:5*), Ni kweli mwisho wa Mwaka kuna matukio mengi ya Mauti na Ajali,Sema Hazinihusu mimi,wewe umeahidiwa na Mungu kwamba Bwana atakulinda na Mabaya Yote, tena atakulinda Utokapo na atakulinda Uingiapo ( *Zaburi 121:7-8*) Huna haja ya Kuogopa Tena_
Hii ndiyo Tafakari yetu leo katika mwanzo wa Mwezi huu wa 11,kwa kuwa ni Neno la Bwana, Litakufaa Leo,mwezi kesho na mwakani kila siku litakuwa jipya.
*_Ulikuwa nami Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto( WhatsApp 0755444078, Facebook Elisha Kazimoto)_*
              ©2019

Wednesday, 30 October 2019

SAIKOLOJIA YA MAWASILIANO

💢💢 *SAIKOLOJIA YA KINYWA(KUONGEA) KATIKA MAHUSIANO*💢💢
_Imeandaliwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, *Ev Elisha Kazimoto*(Psychologist & Counselor)_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
.......................................................
_Hello kijana wa kiume na kijana wa kike(binti),leo nikuongezee kitu kimoja muhimu sana katika mahusiano na Ndoa, ( *Mawasiliano/Kuongea*) tendo ambalo linatumika kila muda kila siku wakati wote wa maisha yako._
💢Kuongea ni njia moja wapo ya *Kufunua Uhalisia wako(Uzuri wako au Ubaya wako)* katikati ya watu wanao kuzunguka.
💢Nature ya mtu, Tabia ya mtu,nguvu ya mtu na udhaifu wa mtu, *Ufafanuliwa na Lugha yake(Maongezi yake)*
💢Kuna maeneo mawili makuu ambayo watu *Upima Uzuri na Ubaya wa mtu* Eneo la Kwanza *MAONGEZI YAKE(lugha) na Eneo la Pili ( MWONEKANO WAKE(Presentation)yake kwa watu(Personality)* hayo ndo maeneo makuu watu wanaweza ku Judge mtu kama anafaa au hafai kuwa mke au mme, au kuongoza au kusimamia eneo flani,ila hapa mimi naongelea mahusiano na Ndoa.
💢Ikumbukwe kuwa Lugha yako,(maongezi yako) *Yanaweza wasilishwa kwa Maneno ya sauti au kwa njia ya Maandishi* kupitia njia hizo kuu 2 watu wakajua wewe ni nani.
💢Unapo anza safari ya kutafuta mwenzi wa maisha( *Mke au Mme*), Anza na Safari ya Kurekebisha Maongezi yako na Mwonekano wako.
💢Unapo fanya maombi ya Kuombea mwenzi wako usiye mjua, ( *Anza pia kuombea Uwasilishaji wa Hisia zako kwa maneno na maandishi*) viwe vinavyo faa kwa watu.
💢Kisaikolojia na wanasaikolojia *Hauangaiki sana kujua Tabia ya mtu,kufaa kwa mtu, udhaifu wa mtu, endapo una Nafasi ya Kusikia maongezi yake na Kusoma Maandishi yake* hapo ndo unaweza Kujua huyu ni nani na Akili yake ikoje na moyo wake ukoje.
💢Lakini Uzuri wa Somo hili, Si Saikolojia pekee ilo bainisha haya, hata Biblia Takatifu imeweka wazi *Mtu ni nani,mtu ni Maneno yake* Yaliyo jaa moyoni ndiyo yatakayo semwa na ndiyo yatakayo tendwa.
*Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.Luka 6:45*
💢👆Hapa ndipo wana saikolojia wakafafanua zaidi, Kwamba Tabia ya mtu utaifahamu kwa kadri ya uwasilishaji wake wa hisia zake kwa watu kwa njia ya maneno au maandishi.
💢 Tuna mjua mtu huyu ana Dharau, kwa maneno yake, mtu huyu Hajali, kwa maneno yake, mtu huyu ni Mkorofi kwa maneno yake, mtu huyu ana Hasira kwa maneno yake, mtu huyu ji Rough kwa maneno yake,mtu huyu ni mpole,muungwana,ana hekima kwa maneno yake, mtu huyu uwezo wake wa Kufikili,Kuamua mambo,ni mkubwa au mdogo kwa maneno yake( Anavyo yawasilisha kwa sauti au kwa maandishi)
💢 *KWA MSINGI HUU KIJANA WA KIKE NA WA KIUME HASA KATIKA ZAMA HIZI ZA TEKNOLOJIA YA MITANDAO YA KIJAMII*
1⃣Watu wengi wameshusha na watashusha Hadhi zao, watakataliwa sana,watachelewa kuoa au kuolewa kwasababu ya namna wanavyo wasiliana katika Magroup ya mitandao ya kijamii.
2⃣Watu wengi watafunua udhaifu wao na wanafunua udhaifu wao ambao ingekuwa vigumu kuujua, na kukulindia heshima yako,ila kwasababu ya kukosa Saikolojia ya Mawasiliano watu wanawasilisha Hisia zao kwa maandishi au kwa sauti bila kujiwekea Taadhari.
3⃣Watu wengi wanaweza na wataweza kuwahi Kuoa au Kuolewa, kugombaniwa na watu kwasababu ya Uwezo wao wa Kuwasilisha Hisia zao kwa maaandishi ana sauti, vinawa Promote zaidi kwa watu na kuonekana ni watu wa pekee.
💢 *ANGALIZO KATIKA SAIKOLOJIA YA  MAWASILIANO*
👉Kukaa kimya siyo tafsiri ya uwezo wako mzuri na mkubwa wa kuwasiliana, ila *Umepunguza kujulikana haraka kwa watu*
👉Kuongea sana katika kila kitu, Hakutafsiri uwezo wako wa kujua au uwezo wako mkubwa wa kuwasiliana, *Ila umewarahisishia watu kujua wewe ni nani*
💢Hayo mambo yaangalie sana yatakusaidia kwakuwa kila siku unaongea unaandika, unaonekana(Mwonekano wa nje - Personality)
🎀 *SAIKOLOJIA YA MAWASILIANO INAKUTAKA KUZINGATIA ALAMA ZIFUATAZO*🎀
1⃣Ongea kitu ulicho na uelewa nacho vizuri( Utaonyesha uwezo wako wa Akili)
2⃣Kabla ya Kujibu Hoja ya mtu, Angalia yeye Ameiwasiliaha katika hali gani(ya hasira, furaha,uzuni,upole,dharau nk) ukijua ameiwasilisha kwa Aina gani, Itakusaidia Kumjibu katika Nafasi iliyo nzuri itakayo funua Hekima yako na uwezo wako wa Kutafakari.
3⃣Kabla ya kujibu hoja ya mtu, Sikiliza ndani yako ile hoja uliyoisikia au isoma *Imeibua nini ndani yako*(Hasira,Furaha,Uzuni,Chuki nk) Ukijua aina ya msisimko uloibuliwa ndani yako, itakusaidia Kujibu kwa Umakini Maana utakuwa na Taadhari ya Kulinda Hisia zako.
4⃣Kabla ya kujibu hoja iliyokufikia kwa maandishi,au sauti.... *Angalia kwanza Nafasi yako kwa watu wanaokuzunguka(Status)* (Je, wewe ni kiongozi, Mkubwa Kiumri,mdogo,Una ndoa au huna) waza  athari zinazoweza tokea pale watu watakapo tafsiri ujumbe wako kama ndivyo ulivyo.... Hii itausaidia Kuongea au kujibu Umakini zaidi nanKutunza Heshima yako na kuonyesha *Kiwango cha Ukomavu wako*
_Ninapo maliza kwa leo yako mambo mengi ila leo niishie hapo, Lakini cha kujifujza hapa ni kwamba wewe mwenyewe unaweza jitengenezea *Kibali machoni pa watu au Kuharibu Kibali chako machoni pa watu* kutokana na uwasilishaji wako wa maneno kwa watu wanaokuzunguka_
💢💢 *_Uchambuzi huu umeletwa kwako na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, Mwanasaikolojia EV ELISHA KAZIMOTO, Ambaye ni Mkufunzi wa Masuala ya Kiroho(Neno la Mungu) na Masuala ya Kimahusiano na Ndoa na Saikolojia ya Maisha_*
Mawasiliano: WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto.
*NB: Ana Magroup ya WhatsApp 8 tofauti anayo yasimamia yanayotoa Elimu mbali mbali za Kiroho na Kisaikolojia*
ULIYE TAYARI KARIBU.
                 ©2019

Tuesday, 22 October 2019

TANGAZO LA KONGAMANO LA WHATSAPP

💒💒 *KONGAMANO LA KIHISTORIA LA MADINI ADIMU YA KISAIKOLOJIA,KIROHO KATIKA MAHUSIANO NA NDOA NA SIRI ZA UTUMISHI WA MADHANAHU*💒💒
💒Kongamano hili kimeandaliwa na Kamati kuu ya Umoja wa Magroup 8 ya WhatsApp yanayosimamiwa na Mtumishi wa Mungu na mwana Saikolojia *Ev Elisha Kazimoto(0755444078)* Kutoka mkoa wa Kagera.
🎀Hili litakuwa kongamano la kwanza na la Kihistoria kutokea,litakalo wakusanya watu kutoka mikoa yote Tanzania na Zanzibar na nje ya Tanzania.
💒Lengo kuu la Kongamano hilo ni *Kufahamiana,Kujifunza madini adimu ya Kisaikolojia na ya kiroho katika sekta ya Kimahusiamo,kindoa na kihuduma,bila kusahau kushare Experience za kiroho na kijamii* Lakini pia Utapata Fursa ya Kuhudhuria LIVE LECTURE na Kuuliza maswali ya papo kwa papo katika nyanja zote zilizotajwa.
💒Pia tutakuwa na Maombi Maalumu ya kuombea Vijana na Mahusiano,Wana ndoa na wale wenye Huduma mbali mbali za KIROHO.
💒Tutakuwa na mipango Mahususi kwaajili ya kuwa watu wenye Impact katika Kanisa na jamii katika kizazi chetu.
*_Hakuna kiingilio ni bure,kazi yako ni Kujisajili Kwa fomu maalumu yenye Maelekezo ili kujua umapatikana wapi,ili ujue eneo ambalo Kongamano litafanyika(Eneo utaambiwa litakuwa ni rahisi kufika kwawatu wote kutoka pande zote za nchi,tutakuwa na muda wa kutosha wa kujiandaa,Changamkia Fursa hiyo moja kwa mwaka 2020_*
Imetolewa na ofisi ya Maadmin waliochini ya Ev Elisha Kazimoto na kupitishwa na Senior Admin Ev Elisha Kazimoto(0755444078)
_Ulikuwa ukimfatilia mafundisho yake Facebook,WhatsApp na YouTube sasa Kukutana naye Live na kujifunza siri zote bure_.
                 ©2019

UTAMBULISHO NA USAJILI

🎀🎀 *TANGAZO MAALUMU KUTOKA OFISI KUU YA GROUP*🎀🎀
🎀 _Shalom members wote,tunaombwa kuzingatia Tangazo hili kwa umuhimu sana,ili kufanikisha maono makubwa yajayo mbele zetu_
🎀 Tutakuwa na Utambulisho Maalumu kwa members wote tulio humu, kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo
1⃣Picha yako ya sasa(current photo) *Picha yako iambatane na taatifa zote hizi chini* usitume picha bila maelezo hayo
2⃣Majina yote(full name)
3⃣Hali yako(Status) Single,Married,In relationship
4⃣Mkoa unakotokea(Regional) unakoishi kwa sasa
5⃣Wilaya unakoishi kwa sasa
6⃣Umeokoka au bado hujaokoka(be free)(KANISA UNAKO SALI)
7⃣Huduma yako(kanisani).
8⃣Mwajiliwa,Umejiajili,mwanafunzi.
*_Utambulisho huu niwa muhimu sana kwaajili ya mpango Mkakati wa maono ya Mwakani ya Uongozi wa Kuandaa Kongamano kubwa la Pamoja la LIVE LECTURE, pamoja na kufahamiana kama members wote wa Magroup 8 yaliyochini ya Mtumishi wa Mungu, na mwana Saikolojia Ev Elisha Kazimoto_*
🎀Mara baada ya utambulisho na kujua Idadi ya members kwa kila kanda tutarudi tena kupeana Maono Maalumu ya Kukutana kwa kongamano la Kihistoria.(Tuajadili pamoja,tutafikia Muafaka,tutaratibu, Tutatimiza,Tutaandika Historia ya Furaha maishani na katika ufalme wa Mungu)
*BY SENIOR ADMIN EV ELISHA KAZIMOTO*(0755444078)
_Imetolewa baada ya kikao maalumu cha Maadmin wote wa magroup yote 8 cha tarehe 22/10/2019_

Thursday, 17 October 2019

ZINAA NA MCHUMBA WAKO NDOA MOTO

💣💣 *UKIONA UMEANGUKA KWENYE ZINAA NA MCHUMBA WAKO JIPANGE KWA YAFUATAYO KATIKA NDOA*💣💣
_Imeandaliwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto*(Psychologist & Counselor)_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto.
......................................................
_Hello kijana wa kiume, Hello kijana wa kike, Hello mwana Ndoa, nina Alama muhimu za Nyakati chache zikusaidie kwa Taadhari,au Kugundua Maangaiko yako,ujiponye au Upambane_
💣Mara nyingi tumekuwa tukichukulia kawaida  suala la Mahusiano ya kirafiki na kiuchumba na kuona nikama kipindi cha Kujiachia,au cha Kujaribu jaribu kama kuna bahati yako au la, kumbe nikipindi Muhimu ambacho ni msingi wa ndoa ya mtu.
💣Ndoa nyingi zina machafuko yasiyokoma,ambayo masuluhisho mengi ya kwa wazazi,wasimamizi,wachungaji,mpaka na mahakama yamegonga mwamba hakuna kutulia,yametoka katika vyanzo vikuu 3, mimi nitazungumza 1, viwili vipo kwenye lecture zangu kama nimfatiliaji wa masomo yangu katika magroup mengi ya WhatsApp na Facebook. Machimbuko hayo 3 ni:
1⃣Ukosefu wa Maarifa ya Kisaikolojia ya kuendesha mahusiano ya uchumba au Ndoa (watu wanajikwaa katika mlima wa ujinga. HOSEA 4:6).
2⃣Kuto apata mtu sahihi(Uchaguzi usio makini) Unafoji ubavu.... (Jua hautakuja kutulia na mtu wa mwingine)
3⃣Msingi Mbovu wa Mahusiano yenye Harufu ya Zinaa.
💣Miongoni mwa vitu ambavyo wengi wa wanaofunga ndoa upuuzia nakuona ni kitu kidogo,ni *Ni wao kuanguka katika zinaa(Kushiriki ngono)kabla ya ndoa halafu wakaoana* wakiamini wanaendeleza Upendo,kumbe ndo wamefuta upendo.
💣Labda nikupe siri hii ya Kisaikolojia na kiroho *SEX INAPANDE MBILI ZA SHILINGI* Ni TAMU na Inaunganisha Nafsi za watu na kuwafanya wawe na Sura moja( *_Kama imefanyika katika muda muafaka kwa watu sahihi bila hatia_*)

19 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za Bwana, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye Bwana akamkumbuka.
1 Samweli 1:19
👉👆Sex ikifanyika kwa watu waliosahihi yaani mke na mme ina MKONO WA BWANA WA BARAKA.
👉Pili  SEX inakawida ya *Kuwaachanisha watu nafsi,kufuta upendo,Amani,furaha kati ya watu Walioifanya Kinyume,nje ya muda na si watu sahihi*
10 Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani.
2 Samweli 13:10

11 Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu.
2 Samweli 13:11

12 Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinitenze nguvu; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu.
2 Samweli 13:12

13 Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa.
2 Samweli 13:13

14 Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye.
2 Samweli 13:14

15 Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako.
2 Samweli 13:15

16 Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunitoa ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza.
2 Samweli 13:16

17 Ndipo akamwita mtumishi wake aliyemtumikia, akasema, Mtoe sasa mwanamke huyu kwangu, ukafunge mlango nyuma yake.
2 Samweli 13:17

👉👆Wakati sex isiyo halali inakuwa ina vutia na inapofusha macho nikama unajituliza ila matomeo yake baadye INAFUTA KILA AINA YA FURAHA NA AMANI KATIKA NAFSI ZA WAWILI hawa,sasa ikisha futa na mkaoana *Hiki ndo kinatokea kwenye ndoa yenu* Kiroho na Kisaikolojia:
1⃣Uaminifu kati yenu ndo basi tena( Hakuna atakaye kuja kumwamini mwenzake daima)
👉Hapa hata mwenzako aone unatoa pepo,viwete wanatembea,unaimba mpaka unabubujika, Nafsi mwake *Hana Imani na wewe* ana ❓❓❓nyingi.( _Kwa nini,kwasababu ulikuwa na Ujasiri wa kuvunja uaminifu wako mbele zake katika ujana,kwa sasa ndo anaona huwezi shindwa vunja tena_) Mtaishi maisha ya kuwindana,kulaumiana sana.
👉Kawaulize wote walioangukia Kona hii hata kama ni watumishi wa Madhabahuni,wamalazimisha kuaminiana mdomoni ila Moyoni na Akilini *wanashutukana*
2⃣Thamani yako kwa mwenzako inashuka chini ya 50%. Ukiona umevua au umevuliwa nguo kabla ya ndoa na huyo huyo mkaoana, *Respect kati yenu inashuka chini ya nusu* kwa nini, Usiri wamiili yenu unabeba *Heshima ya mioyo na utu wenu* Mkisha vuana nguo Usitegemee, *Baba mwenye nyumba kupata full respect,au mama kupendwa full love* utakuwa na Partial.... Maana respect na love vilivuliwa moyoni mwako nje ya ndoa,hukuja navyo ndani ya ndoa
3⃣Kuna uwezekano wa KUACHANA kimwili (divorce) kwa nini vitu muhimu vinavyo shikilia Ndoa,hamkuingia navyo ndani mliviacha pale mlipovuana nguo( *Vitu kama, Usiri,Aibu,heshima,shahuku kwa mwenzako,*) kwa hiyo mgogoro ukianza ndani Hauzimwi unatafuta Kuachana.
4⃣Fujo,magomvi,kunyimana tendo la ndoa haviwezi kukoma kati yenu....(Maana moyo wa Upendo uliisha chukuliwa na adui)mtasuluhisha ila muafaka haupo,wanacho laumiana ni kidogo sana ila kinakuzwa na mbegu ya zinaa iliyofanyika. Mwaweza ishi ila si kwa Amani na upendo,mtakuwa na vipindi vifupi vya furaha na kipindi kirefu cha dhoruba.
_Nini nataadharisha vijana ambao bado hamjaingia katika ndoa, Komaa mpaka mwisho,rafiki au mchumba akikushawishi kwa sex kimbia na PIGA ❌ kuanzia kichwani pake mpaka muguuni pake,usipo fanya hivyo uta enjoy kwa mwezi,wiki na siku ila Utajuta maisha ya ndoa Yote._
👉Mlioko kwenye Ndoa,Nahisi ukisoma haya utajua kuwa kama Ulipitia huko Haya ndo Maisha yako, *Huna heshima kwa mwenzako,Sex hupati inavyotakikana,upendo haba sana,Amani hakuna,Uaminifu hakuna,unahisi kumchoka mwenzako* nini Kifanyike Lazima mtibiwe wote Kiroho na Kisaikolojia ili mpunguze makali ya Maisha mnayoishi ila mbali na hapo  mpaka kaburini au Mtaachana tu.
*_Ulikuwa na mimi Mchambuzi wa Masuala ya Ndoa na Mahusiano Ev Elisha Kazimoto (Psychologist & counselor)_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

Wednesday, 16 October 2019

NDOA INAHITAJI AKILI TIMAMU

🎀🎀 *NDOA NI TAASISI NYETI SANA INAYO HITAJI WATU WALIO NA AKILI TIMAMU NA KOMAVU*🎀🎀
_Imeandaliwa na Mwanasaikolojia na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto.
............................................
_Hello Hello wana ndoa na wana ndoa watarajiwa,nasema nanyi leo kuponya watu wachache wenye Akili Timamu ya Ki Mungu na ya Kisailojia,na wale waliogonjweka hii ni Saa ya Kupona ( *Kama ukitaka*) ila ukiona Huwezi Badirika, Amini unacho amini ila Historia Itajirudia HAUTAKUJA KUWA NA FURAHA MAISHANI kama wanayoipata wegine walioko kwenye NDOA_
🎀Kwanza, nimesema ndoa inahitaji watu wenye *Akili timamu* Kwa nini nasema akili timamu, _Kabla ya kufanya Maamuzi ya Kuoa au Kuolewa,inabidi uwe na uwezo wa kutambua mazingira yafuatayo ndo yanayoonyesha wewe una akili timamu ya Kindoa_
1⃣Naenda kuolewa au kuoa nimetaka mwenyewe, imenipasa kukabiliana na yoyote yatakayotokea huko kwa Busara.
2⃣Naenda kuoana na Binadamu na si Malaika, anamadhaifu kama mimi,atanikosea,nitamkosea ila inabidi niangalie namna ya kuishi naye kwa Amani.
3⃣Ndoa yetu(Makazi yetu) yatakuwa hapa hapa duniani na si Mbinguni,kwa hiyo kama dunia isivyo tambarale na maisha ya ndoa yetu hayawezi kuwa tambarale, lakini kuna watu waipenda ndoa yetu na wengine watatafuta namna ya kutugawa ila nijue namna ya kumlinda mwenzangu na kujilinda.
4⃣Kuoa na kuolewa ni Heshima kijamii(kwa Mungu ni kupata Kibali mbele za  na baraka) *_Ila Kuachika,Kufukuza mke,Kutoka kwenye ndoa,kudai Talaka na Kutoa Talaka Ni Fedheha,na Aibu ya milele kwenye jamii na mbele za Mungu ni Laana_* Maana Mungu anasema ANACHUKIA KUACHANA.( yaani hapo hajaweka sababu yoyote Amesema ANACHUKIA, HIVI MUNGU AKICHUKIA UTASALIMIKA WEWE.
*Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.Malaki 2:16*
🎀Lakini pia Unapoingia katika ndoa au kama wewe upo kwenye Ndoa Tunaona *Akili yako Imekomaa Kiasi gani,na Ulifaa kuoa au kuolewa kwasababu una akili komavu ya Kindoa pindi Utakapo kuwa na uwezo wa kufanya mambo Yafuatayo*
1⃣Kama utakuwa na uwezo wa kukaa na mtu ambaye si ndugu yako, mmekutana ukubwani, ukaweza Kuishi naye kwa hali yake yoyote, mkakaa kwa Amani na Furaha( *Yaani uwezo wa kutengeneza mazingira Rafiki ya amani*)
2⃣Kama utakuwa na uwezo wa Kukosewa na ukasamehe kabisa bila kulipa kisasi,au Ukakosea ukajua na kuomba samahani ili kulinda amani ya ndoa yako.
3⃣Kama utakuwa na uwezo wa Kuboresha madhaifu ya mwenzako mpaka akayaacha na kuwa vizuri,bila kumchoka na kumkatia tamaa.
4⃣Kama utakuwa na uwezo wa Kutimiza wajibu wako wa kijinsia na wa kindoa kwa mwenzako kwanza bila kusubiri UFANYIWE NDO UFANYE.
5⃣Kama utakuwa na Uwezo wa Kuhurumia Uzao wako,na kuwaonyeshea mfano mwema wa kuigwa ili nao wakue wakiwafurahia baba na mama na wawabariki hata muwapo wazee.
6⃣Kama utakuwa na uwezo wa kumpenda mwenzako hivyo alivyo, Mmejaliwa uzao au La, mnamali au mmefilisika, mzima au mgonjwa.
7⃣Kama una uwezo wa kuficha madhaifu yake watu wasiyajue bila sababu,na unauwezo wa kumwombea Mungu amsaidie awe vema.
8⃣Kama unauwezo wa Kuchukia KUACHANA na kupambana kwa namna yoyote ukae na mwenzako.
*_Hizo ndizo baadhi ya Kanuni za Kisaikolojia hasa katika Falsafa ya ndoa na Kibiblia(sija taja maandiko yako mengi) kama wewe Unajiita ni mtu wa Mungu, au kama unapenda kuishi nje ya Stress_*
NB: _Maamuzi yoyote ya wanandoa,jua mnapanda mbegu kwa uazo wenu wataishi maisha kama hayo hayo kwa vizazi 4(miaka 400baada yako) Usikurupuke kufanya maamuzi mabaya,utatesa uzao wako watakulaani hata kaburi lako_
(Fatilia wazazi walioachana,roho inawafuata hata watoto,Magomvi na kupigana,fatilia utaona kwa watoto, mama hamweshimu mmewe,fatilia watoto wake wa kike wakiolewa ni shida nk)
*TUPENDANE,TUJIFUNZE,TUREKEBISHANE HIZO NDO CHANGAMOTO ZA DUNIANI*
_Ulikuwa na Mwanasaikolojia na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa,Ev Elisha Kazimoto(WhatsApp 0755444078, Facebook Elisha Kazimoto)_.

Saturday, 12 October 2019

UFUNGUO 12

🗝🗝 *UFUNGUO WA 12: AMANI YA NDOA YETU INATOKA KWA MUNGU,TUKAE NA MUNGU VIZURI*🗝🗝
_Hello Hello wana Ndoa,kwa mara nyingine tunasogea katika meza ya Maarifa ya Kisaikolojia kwa wana Ndoa,upo nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, *Ev Elisha Kazimoto (Psychologist & Counselor)* karibu tuhitimishe kwa Ufunguo wa 12 wa ndoa yenye Furaha katika maisha._
🗝Mara nyingi watu wengi wanakuwa na mzigo mkubwa wa kuomba,kumtafuta Mungu wakati wanatafuta wenzi wa maisha,ila wakishawapata wanastarehe biashara ya kuomba,kuombeana,kuhimizana katika mambo ya Mungu inabaki ni kwa mtu binafsi na wakati Mwingine kila mmoja anaweka Silaha chini.
🗝Siri kubwa ya kuimarisha Ndoa yako na kuifanya kuwa ya Furaha,ni pale wana Ndoa mtaamua kukaa na kupanga namna yayay kuishi na Mungu katika ndoa yenu,namna ya kumtumikia Mungu katika maisha yenu ya ndoa,kubebana koroho na kuhimizana katika mambo ya Mungu.
🗝Ndoa inatoka kwa Mungu,hivyo inahitaji kurudishwa kwa Mungu kwa njia ya Maombi ili iwe salama.
🗝Miongoni mwa Taasisi yenye vita,inayowindwa na adui na inapigwa vita ni Ndoa, adui akifanikiwa kuwagawa katika Ndoa, *Amefanikiwa kushika uchumi wenu,kushika uzao wenu,kushika maendeleo yenu* na lolote laweza tokea lililo baya
🗝Mkifanikiwa kuwa watu wa vita,watu wa maombi, watu wa kumtumikia Mungu,watu wa kushirikishana mambo ya Ki Mungu,mtafanikiwa *Kulinda furaha,amani,na upendo* kati ya ndoa yenu.
🗝Wekeza nguvu kubwa ya kumwambia Mungu kila siku kwa maombi yako,kwamba Mungu linda mwenzangu,nilinde na mimi,upendo,uzuri na furaha niliyo iona kwake tangu siku ya kwanza nilipomuona,iendelee kudumu kati yetu,utupe uzee mwema,kataa vifo vya ujanani kwa watoto wenu na kwenu,kataa roho za migogoro,magomvi,mafarakano kati yenu, mwambie Bwana ifanye ndoa yetu iwe mfano wa kuigwa kwa watu wote.
_Mtu wa Mungu niishie hapa kwa leo,nikutakie baraka tele katika ndoa yenu na mkono wa Bwana uwaongoze katika kuishi maisha ya Furaha. Ndoa ni Njema kama wewe mwana ndoa ni mwema,na ndoa ni mbaya kama wewe mwana ndoa ni mbaya_
*Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.Tito 1:15*
_Ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto* (Psychologist & )_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

UFUNGUO WA 11

🗝🗝 *UFUNGUO WA 11:FURAHA YETU KATIKA NDOA NDO MWANGA WA MAKUZI MEMA YA WATOTO WETU*🗝🗝
_Hello Hello mwana Ndoa,kwa mara nyingine Mtaalamu wetu na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto* anakuletea ufunguo wa 11 wa ndoa yenye Furaha karibu_
🗝Kuna mambo ambayo wana ndoa wanaweza kuwa wanayafanya wao kama wao lakini hawatafakari kwa habari ya Uzao wao nini wana vuna kutoka katika Mahusiano ya ndoa yao.
🗝Mahusiano ya wazazi kama wana Ndoa ( *Yana nguvu kubwa katika Kuathiri Makuzi ya watoto na tabia za watoto wao*) hilo ndo jambo kubwa ambalo wanandoa wengi hawajui,na hawajali.
🗝Migogoro na magomvi kati yenu yanaathiri Saikolojia na tabia ya watoto wenu, kwa muda huo mwaweza kuona kama wako kawaida ila kuna mbegu mbaya imepandwa itakayo waendesha pale watakapo fikia umri wa kufanya Maamuzi binafsi,ndipo tabia zao, maisha yao yataonyesha Uhalisia wa Mahusiano ya wazazi wao jinsi yalivyo kuwa mabaya.
🗝Kama wana Ndoa watajutahidi kulinda Furaha katika ndoa yenu,na watoto wenu wakayaona Mahusiano yenu yalivyo mazuri tangu wakiwa watoto, kwanza *Mnawapa afya ya kiakili darasani, wanajengewa uwezo wa kutafakari na kufanya maamuzi sahihii,tabia njema inaumbika* lakini mnaetengeneza uwezo wa malezi safi ya uzao wenu.
🗝Wana Ndoa watoto wakiwa wadogo,mnaweza kila mtu kutojali,kila mtu anafanya kumkomoa mwenzake,hamuoni matokeo,ila kumbuka mnapanda mbegu ya *Mbuyu* watakapo kua watu wazima ambao wanaanza kufanya maamuzi yao binafsi na sikuamliwa 100% hapo ndipo mtakapo anza kuvuna matunda ya Magomvi yenu,visilani vyenu na ndipo mtaona Umuhimu wa Kusameana,kupendana na kuheshimiana kama wana Ndoa,lakini muda utakuwa umechelewa,mpaka kwa Neema ya Mungu aangilie kati ya uzao wenu ila mtakuwa na *Uzao mbaya usio na historia ya maisha ya kuigwa* Epuka Kulaaniwa na Watoto wako na kuburi lako kupigwa mawe, Lipa gharama ya kuhakikisha unalinda Mahusiano ya Furaha katika Ndoa.
_Niishie hapo kwa leo,ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, *Ev Elisha Kazimoto (Psychologist & Counselor)*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

UFUNGUO WA 10

🗝🗝 *UFUNGUO WA 10: MAKOSA HAYASAHIISHWI KWA MAKOSA* 🗝🗝
_Hello Hello wana Ndoa, kwa mara nyingine Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto* Anakuletea ufunguo wa 10 wa Ndoa yenye Furaha,karibu ufuatane naye katika Hoja hii_
🗝Imekuwa kawaida ya watu wengi,iwe katika Mahusiano au katika maisha ya kawaida,wengi wametengeneza *Chuki,migawanyiko,magomvi na Migogoro* Kwa kushindwa kujua Saikolojia ya Mahusiano Inakataza Kutatua Makosa kwa kutumia makosa.
🗝Kikawaida katika uwanja wa Kisaikolojia (Ambapo ndo makao ya Hisia) Mwenzako akikosea,ukamjibu kwa kosa jua Unaimarisha Mgogoro,au Unapanua mgogoro kati yako na yeye.
🗝Kuitirafiana katika maisha kama wanadamu ni kawaida,kukosea kama wanadamu ni kawaida, shida matabaka,magomvi,kuachana kusingekuwepo,au kungekuwa kudogo sana na watu wangeishi kwa furaha.
🗝Tatizo kubwa kwa watu ni pale mmoja Anapokosea, Mwenzake Anamjibu mwenzake kwa Makosa(kumkomoa) hapo haumbadirishi ila unamuongezea usugu.
🗝Kila kosa,linahitaji Akili ya ziada ambayo ndani yake ina huruma,inakujali,inakuthamini,ina kupenda.palee ndo utaona mtu anatumia njia sahihi za kumwambia mwenzake *Jambo hili mke wangu,mme wangu linaniletea shida,waweza kulibadiri,kuliacha ili moyo wangu uwe na amani?* Kama wote wana akili ya Kisaikolojia,wamejifunza funguo za ndoa yenye furaha, hapo Watakuwa na Faragha ya kuzungumza,kurekebishana,kusaidiana na kupena mwanga mpya wa kuishi watatoka huko na majibu ya furaha na kuendelea kuishi kwa upendo.
_Niishie hapo kwa leo katika ufunguo huu wa 10, ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist & Counselor*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

UFUNGUO WA 9

🗝🗝 *UFUNGUO WA 9: KAMA MOYO WAKE UTAUMIA NA MIMI NITAUMIA*🗝🗝
_Hello wana Ndoa Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, Msaikolojia *Ev Elisha Kazimoto* Anakuletea ufunguo wa 9 kati ya 12 wa ndoa yanye Furaha, fuatana nami katika ufunguo huu,ili ufungue chumba chako cha Stress uingize furaha_
🗝Kuna vitu ambavyo ukishaingia kwenye ndoa inabidi kila mmoja Ujiulize ndipo utaruhusu chemi chemi za furaha katika ndoa yako.
🗝Kumekuwa na kawaida ya wana ndoa kutojali Maumivu ya mwenzake,kwa hiyo anaweza fanya lolote kwake akidhani *Anamkomoa mwenzake* anashindwa kujua kwamba kwenye Ndoa Mungu alisha sema ninyi ni MWILI MMOJA, Kauli hii Kisayansi tunaipata kwa bwana mmoja mwana FIZIKIA(PHYSICS) anaitwa Archimedes,kwenye *Third Law of Motion, anasema "To Every Action,there's equal and opposite Reaction"* mwisho wa kumnukuu.... Akimaanisha kwamba _Kwa kila tendo kuna usawa na kinyume cha tendo hilo_ mfano mwenye baiskeli akigongana uso kwa uso na gari, Wote wanaumia sawa japo sisi tutaona wa baiskeli kakanyagwa kanyagwa na kufa...ila kikanuni ya mwendo na gari limeumia sawa na baiskeli.
🗝Sasa katika Ndoa,watu wanasahau kwamba Mwenzako Akiumia moyo wake kwa majeraha uliyo yatengeneza mwenyewe,jua na wewe *Utavuna au utakula sehemu ya maumivu hayo* yeye hawezi umia wewe ukacheka. Kuna vitu utavikosa vya Kihisia kutokana na Kuumia kwake.
🗝Ndiyo maana tunasema katika ndoa,kila mmoja kimbizana na kutafuta namna gani *Uuburudishe moyo wa mwenzako* ili nawe Uburudike.
🗝Ni vigumu kucheka na mtu aliye jeruhika moyo, ni vigumu kutoka out ma mtu aliyejeruhika moyo,ni vigumu kumsifia mtu aliyejeruhika moyo,ni vigumu kufanya mipango na mtu aluyejeruhika moyo,ni vigumu Kushiriki tendo la ndoa na mtu mwenye majeraha ya moyo.( hivyo ni baadhi tu)
🗝Kwa mazingira hayo,Epuka Kumezea,kutemgeneza mazingira ya maumivu kwa mwenzako,na umigundua umemuumiza, Ebu tafuta namna ya kuuganga moyo wake airudie hali yake ya furaha. *_Mwenzako akifurahi,nawe utafurahi,na mtaishi maisha ya Ushindi katika ndoa_*
_Mimi kwa leo niishie hapo niseme kwamba Ndoa ni Tamu kama utaamua wewe uitengenezea mazingira ya utamu,na ndoa ni chungu kama wewe utaamua kuiandalia mazingira ya uchungu_.
*Ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa _Ev Elisha Kazimoto(Psychologist &Counselor_)*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

Friday, 11 October 2019

UKIUMIZWA MOYO,USIJIUMIZE NA WEWE

🖤🖤 *UKIUMIZWA MOYO KATIKA MAHUSIANO, EPUKA KUJIUMIZA NA WEWE*🖤🖤
............................................
*_Na Ev Elisha Kazimoto(Psychologist & Counselor)_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
.................
.................
_Hello Hello vijana kwa mabinti ambao mpo katika safari ya Mahusiano yakuelekea ndoa, na wengine mpo katika Mahusiano yakuelekea katika ndoa, leo nataka niseme nawe kwa ufupi, Lugha hii Tata ya Kisaikolojia ili Nikusaidie Kutoendeleza Historia ya Maumivu katika moyo wako unapoendelea kuishi,lugha hii Niirudie tena, *"Ukiumizwa Moyo katika Mahusiano, Epuka Kujiumiza na Wewe* Huu umekuwa Ugonjwa kwa watu wengi, Je wewe wewe weza kupona Leo?_ Sentensi yangu kwako ni Alama ya (  Rudi nyuma Fikiri kabla ya maamuzi - 🔙)
🔙Kila anayeanzisha mahusiano(anayeingia) Ana matarajio ya kukidhi Hisia zake za Furaha zilizo msukuma kuingia kwenye Mahusiano,japo Anaweza Kushida Kuziongoza Hisia zake zifikie matamanio yake.( *Kosa la kwanza*)
🔙Kila anayeingia kwenye Mahusiano,anaingia na mtu ambaye Anahisi ana vitu au kitu ambacho kwa nafsi yake na hisia zake zilimwonyesha Anaweza Kupata Furaha,na kutimiza ndoto zake za Kimaisha, Japo Anaweza kushindwa  Kuusoma Ukweli wa Maneno,matendo ya mwenzake hata kupelekea Mahusiano kuvunjika mapema,au baada ya muda mrefu.( *Kosa la Pili*)
🔙Kila mtu aliyeingia katika Mahusiano na mtu,aliamini huyo ndiye mtu pekee wa Kuzigusa hisia zake na kuleta matarajio yake katika Uhalisia alioutamani tangu zamani, ndiyo maana ukamfuata,au ukamkubali, Japo Waweza Kushindwa Kuchochea Uzuri huo uliouona ili uendelee kutimiza hisia zako,ukapelekea kuachana kwa shari au kwa wema( *Kosa la Tatu*)
🔙Kila mmoja anayeingia katika Mahusiano huwa anaangalia Dhamira yake ilivyo njema,na alivyo sahihi katika Mahusiano na alivyo dhamilia kufikia hatima ya ndoa, Ambapo wengi Usahau na Ushindwa Kutambua Madhaifu yao na Makosa yao yanaweza changia wasifike mwisho wa safari. Kushindwa kujua udhaifu wako katika Mahusiano ni kosa kubwa la kisaikolojia ( *Kosa la nne*)
🔙Kila anayeingia katika Mahusiano Uamini aliyeingia naye katika Mahusiano anauwezo mkubwa wa kumfurahisha na si Kumkosea,Japo watu Usahau huyo naye ni mwanadamu kama wewe anachumba cha hisia chanya na hisia hasi,kwa hiyo jipange ukiingia chumba chake hasi wewe ingia ukiwa chanya, ukiingia chumba chake chanya,wewe ingia ukiwa chanya japo yeye anaweza kuonamo hasi kadhaa. Ukishindwa kanuni hiyo Mahusiano yatavunjika( *Kosa la tano*)
🔙Kila anayeingia katika Mahusiano,Uingia akijiona yeye ndo Mkweli na si rahisi kukosea ila mwenzake ndo si Mkweli na ndo mkosaji, ndiyo maana Wengi wa walioingia katika Mahusiano na kutoka katika Mahusiano (Break up mbali mbali) *Uwalaumu jinsia nyingine,au umlaumu mwenzake* Si Rahisi kusikia Anaanisha Makosa yake yaliyochangia Kuvunjika kwa Mahusiano,ndo maana kumekuwa na mwendelezo wa kuumizwa na huyu, na yule, na yule mpaka unachukia Mahusiano ( *Kosa la sita*) kwasababu Hujijui ubovu wako, udhaifu wako.
⚖ *Laiti ungerudi nyuma Ukajipima kwenye Uzani wa Mahusiano Kisaikolojia,Ungeweza kuendesha Mahusiano yako vizuri na Kutibu Majeraha yako ya Moyo*⚖
🎀Kama Ukijua kuwa Unapoingia kwenye Mahusiano una Hisia za Matarajio yako,lakini na mwenzako ana Hisia za Matarajio yake ambazo hizi zote za wewe kutofautiana,au kulandana,ungeweza kulinda Mahusiano yako kwa furaha, ila kwasababu unatafuta kutimiza hisia zako tu huangaiki na za mwenzako, Break up,kuumizwa kutaendelea mpaka pale moyo wako utakapo Uruhusu kukubali hali zote za Mahusiano.( *Utakuwa umeshinda kujiumiza mwenyewe*)
🎀Siku utapo jua,kitu kizuri ulichokiona kwa uliyempenda huyo,kinahitaji kuchochowa,kuboreshwa,Kulindwa na ukatia bidii kufanya hivyo utakuwa Umezuia Kuumizwa.
👉Lakini pia Ukipenda usiwe kipofu nakiziwi ruhusu macho yako yaone mazuri na mabaya,mazikio yako yasikie ukweli na uongo wake, na Ipe akili kazi ya Kutafsiri kufaa kwakwe na kutofaa kwake na ushugulikie mapema taarifa hiyo kabla ujaumia zaidi. ( kuendelea kujikaza wakati unajua ukweli hamuendi popote ni Kuendelea Kujiumiza wakati umeisha umizwa. ( *Hiyo ndo tiba ya kutojiumiza mwenyewe*)
🎀Wengi wetu katika Mahusiano,tunapenda kufayiwa mema zaidi,ila siyo sisi kuwafanyia mema watu wetu,Ndiyo maana Tukiumizwa nasi tunatafuta mwanya wa Kuumiza, hapo ndo Unazidi kujiumiza mwenyewe. Ikitokea Uliyoyatarajia kwa mwenzako Kuyapata,hukuyapata 🔙Rudi nyuma tazama wapi Wewe Ulikosea,ulichangia katika kuumizwa kwako,Ulishindwa Kuchochea Uzuri wake,uli relax? Ili kama mkiyatengeneza au ukipata mwingine Usiumizwe tena, Usipo Rekebisha kwanza, Utajiumiza mwenyewe tena na tena( *Hiyo ndo tiba ya kutojiumiza mwenyewe*)
🎀Ukitaka Mahusiano yako yaishi, uwe Mwepesi wa Kujua madhaifu yako na makosa yako unayo yafanya katika Mahusiano kwa mwenzako,na uwe mwepesi Kuyakwepa yasiwe yakujirudia rudia,hapo utakuwa Umeshinda Kujiumiza mwenyewe, Usipo jua hilo,utakuwa wakuumizwa kila mtu na utawachukia wanaume wote au wanawake wote kumbe ni wewe unaye jiumiza kila mara baada ya kuumizwa mara moja. ( *Hiyo ndo tiba ya Kukiumiza mwenyewe*)
🎀Usisahau kuwa tuna *Date na wanadamu wenye mapungufu yao, Si malaika* Kwa hiyo uwe Mwepesi kujua kuwa naweza kukosewa,nami naweza Kumkosea,ila kama nimeona uzuri wake unao nifaa,nifanye nini ili nisimpoteze? Punguza kujihesabia haki kila wakati,msaidie ajue udhaifubwake na Kuushinda ( *Tiba ya kutojiumiza*) mbali na hapo Utakuwa unajiumiza mwenyewe kila mara kwa kuona wanaume au wanawake ni Matapeli.
🆒 *Labda nikusaidie Acha Kupandisha Joto lako la Kihisia kwa Kutafsiri vibaya Changamoto yako yakimahusiano*🆒
🆒Kama Uliumizwa, Tulia Usiendelee Kuumiza nafsi yako kwa kuona Wanaume au wanawake wote ni Wasaliti, Hiyo haikusaidii bali Inaua na kutafuna Hisia zako za upendo na furaha,maana kutafsiri kwako huko Hakubadirishi Mapungufu yako,wala hakuondoi Uzuri wanaouona watu walio na Wanawake au Wanaume kwenye Mahusiano yao. Utaumia wewe ila wao wanazidi kufurahi,na ukisema wanawake wabaya au wanaume wabaya *Wanakuona Waajabu*
🆒Ukiumizwa,jua uwenda Huyo hakuwa size yako au Kilikuwa kipimo chako cha ukomavu wa akili ya Mahusiano,usiendelee kulalamikia Kosa lile ulilotendewa, halitakusaidia Kuhurumiwa na watu ili Wajitolee kukuoa au kuolewa nawe ili usiendelee kuumia. Tulia jua huo ulikuwa niukurasa wenye maandishi yake,subiri kurasa ijayo isome kwa utulivu,au iandike kwa utulivu.
🆒Ukiumizwa,Unapo jipanga kuingia kwenye Mahusiano mapya, Usibebe Hisitoria za maumivu yako na kuhamishia kwenye kurasa mpya, Utaumizwa tena, jifunze kuandia mambo mapya kwenye kurasa mpya.
🆒Ukiumizwa usijipandishe joto kwa kwa kujumuisha watu wa jinsia hiyo na kuwaona ni wabovu, wewe ndo *Utakuwa mbovu wa Kupindukia* kwakuwa ujui kila chapter ina sentensi zake,lakini kila mmoja ana Asili yake na uzuri wake na udhaifu wake.
🆒Ukiumizwa Usiape kutoyarudia Mahusiano, Haumkomoi  aliyekuumiza, Unajiumiza mwenyewe.... Apa wewe mmwenyewe kutorudia Makosa uliyochangia,na kuboresha uzuri wako.
*_Niishie kwa kusema kwamba, Usipo kuwa mkomavu Kisaikolojia katika Mahusiano,Utakuwamtu wa kujuta katika Mahusiano,ongeza Maarifa juu ya Mahusiano,ongeza ubora wa upekee wako,Hitirafu za Kimahusiano zione darasa la kukomaa Kimahusiano,uta Enjoy Maisha, Hakuna Mtu mbaya katika Mahusiano,ila watu Wanakosa Mbinu sahihi za Kuendesha na Kulinda Mahusiano_*
_Ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, *Ev Elisha Kazimoto*( Psychologist & Counselor)_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

Wednesday, 9 October 2019

FANYA KAZI NA MUNGU

🛢🛢 *FANYA KAZI KATIKA OFISI SALAMA NA BOSS MWAMINIFU* 🛢🛢
*_Ujumbe huu umeandaliwa na Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto(Mjenzi wa Maisha ya Kiroho)_*
🛢 _Shalom mtakatifu wa Mungu uliye katika ufalme wa Bwana wetu Yesu Kristo, Neema na rehema za Mungu wetu ziwe juu yako. Shahuku yangu leo ni kukufunulia Siri iliyo katika Ofisi ya Bwana Yesu ili unapoamua kufanya kazi katika ofisi hii uwe na Matumaini katika maisha yako kuwa Unafanya kazi katika Ofisi Salama na kwa boss Mwaminifu kwako._
*28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Warumi 8:28*
🛢Katika mstari huu,tunapata kuona *Mungu(boss mwenye ofisi) anatoa taarifa kuwa anafanya KAZI pamoja na watu wale wa mpendao* Lakini katika KAZI hiyo wanayoifanya Anawapatia Mema Yote(Mshahara) wale walioitwa Kwa Kusudi lake.
🛢Maisha ya kumtumikia Mungu yamebeba Hatima na Heshima ya maisha yako kama mwanadamu.
*26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.Yohana 12:26*
🛢Kuna siri kubwa katika kuyatoa maisha yako kwa Mungu Umtumikie, ndani yake kuna Neema yaziada asiyokuwa nayo mtu mwingine, hapa amesema BABA atakuheshimu. ( _Neno Heshima hapa linawakilisha maisha yenye Heri,ulinzi,kibali,mpenyo kwako_) Mungu akikuheshimu dharau za wanadamu zinakoma, waliokuhesabia siku za kutofanikiwa wanashangaa kuona zinapita, nawe upo unasonga mbele.
🛢Kila aliyejitia Nia ya kukaa katika Ofisi ya Mungu, maisha yake yalibadirishwa, maana Mungu si dhalimu Akiahidi Kukuheshimu,anakuheshimisha kweli kweli katikati ya mataifa.( Huo ndo uzuri wa Kumtumikia Mungu).
*10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. Kumbukumbu laTorati 28:10*
🛢Faida ya Kumtumikia Mungu katika Roho na Kweli,kwa uaminifu mkuu.... Bwana anaachilia Neema yake juu yako,katika ulimwengu wa Roho na katika ulimwengu wa mwili Utukufu wa Bwana,kibali cha Bwana,na Utisho dhidi ya maadui zako unawekwa juu yako.
🛢 *Katika Utumishi wako waweza kukutana na Changamoto nyingi za kukukatisha tamaa,kukurudisha nyuma*
👉Safari ya Utumishi inaweza kuwa na changamoto nyingi za *Usizimie moyo kwa mapito hayo* Unapaswa kujua Nani unamtumikia,nani Alikuita katika utumishi wako huo,huuo ndo wa kumwangalia,huyo ndo wakumsikiliza kila wakati.
👉Yawezekana wengine wakasema *Hukuitwa na Mungu, maneno mengi ya kejeli juu yako,kukudharau, wengine hata kukuwekea Vikwazo vikali ili Kuziba kibali chako,Kuficha Neema yako isionekane kwa watu* Uhitaji kupambana nao,Unahitaji kukaa katika Wito wako na Kumwomba Mungu Neema ya Kuvuka pito lako hilo. *Hakuna kitu kilichowekwa na Mungu ndani ya mtu kinaweza kuzuiliwa na Mwanadamu (Anakuwa anatafuta balaa katika maisha yake na Utumishi wake)*
👉Mtu wa kushindana nawe,pambana nawe katika kuzuia kusudi la Mungu lisitimizwe, Hashindani nawe,hazuii kazi yako, Anazuia kazi ya Mungu, Mungu Akiamua kuingilia kati Ataaibika aibu kuu wakati wewe ukipandishwa.
*_Ninachosema nawe ni Amina na kweli, jambo kubwa jihakikishe je,Umesimama na Mungu wa Kweli? Unatumika bila Hila?_* Tulia kanuni hii itatenda kazi...
*29 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.Warumi 8:29*
*30 Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.Warumi 8:30*
👉Huna sababu ya kuumizwa kichwa,kulia na watu Wasiojua *Asili yako,ambao hawakukuchagua,wala hawana uwezo wa kukutukuza* Unahitaji kushikamana na Bwana Anayejua Asili yako, aliyekuchagua kabla haujazaliwa na huko huko akakutukuza.
🛢👉Habari njema kwako mtumishi wa Bwana,ni kwamba kilicho tukuzwa na Bwana hata ungefanya harakati zote za kukichafua,kukizima,kukiharibu Hakizimiki,hakichafuki,wala Hakipotei yeye aliyeanzisha KAZI ndiye anayeitimiza.
*Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;Wafilipi 1:6*
👉Nikutie moyo,kazi tuliyo nayo ni kubwa na Inachanua,na kwakawaida Mizabibu ikichanua Lazima Vimbweha vidogo vidogo viibuke kwaajili ya kupukutisha Maua yake yasilete matunda,... Hapo ndo Neno la Bwana linasema....
*15 Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua. Wimbo Ulio Bora 2:15*
👉Kwenye maombi yako, shika Mbweha hao wadogo wadogo,(kwanini wameitwa wadogo wadogo,kwakuwa hawana Uwezo wa Kubadiri Hatima yako) Wageuzie hayo yote wanayoyapanga juu yako,na mwambie Bwana lilinde kusudi lako ndani yangu nami nikae katika kusudi lako.
🛢👉Uzuri wa Ofisi ya Utumishi wa Kimungu chini ya Boss wetu Yesu Kristo ni Kulinda Haki za watumishi wake, siku zote ukikaa katika haki na kutenda haki Kusudi la Mungu kwako ndilo litakalo simama daima siyo makusudi ya wanadamu.
*Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.Mithali 19:21*
🛢👉Nimalize kwa kusema kuna faida kubwa kukaa na Mungu vizuri na kumtumikia yeye kwa Uaminifu, *No matter what you are facing, Breakthrough is there* Utapenya kwa Mkono wa Bwana .
*_Ulikuwa na mimi mtumishi wa Mungu, Ev Elisha Kazimoto(Mjumbe wa Matengenezo ya Kiroho)_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

JIKUBALI DADA UMEUMBIKA

💚💚 *NIMEUMBWA KWA KUSUDI JEMA LA MUNGU,WACHA NIJIVUNIE HILO*💚💚
*_Ujumbe huu umeandaliwa na kuletwa kwako na Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
_Shalom mtu wa Mungu,unaye pendwa na Bwana,leo nataka nizungumze na wewe Dada(Malkia Esta wa zama hizi)_
*Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana, Zaburi 139:14*
💚Nataka nikusemeshe uzuri wako,waweza kuwa umekata tamaa pengine unapoona umechelewa kuingia katika ndoa,au mahusiano yako yanaishia njiani waweza kuwa na maswali nafsini mwako, *_Hivi mimi ni mbaya?, Siwavutii wanaume,au mimi nimeumbwaje?_* Neno la Mungu limetupa jibu wewe Umeumbwa kwa *Jinsi ya Ajabu mno* ambayo Unafaa mbele za Mungu na mbele za Mme wako atakaye kuoa.
💚Unacho paswa kujua ni kuwa Uzuri wako si kwaajili ya wanaume wote, na si wote wa kuuona uzuri wako, na wakiuona wengine *Wasio wako, hawatakupenda bali watakutamani* na wakikutamani watakuchezea na kuumiza moyo wako maana safari yako itaishia kwenye mahusiano si ndoa.
💚Leo na kufundisha Uzuri wako uliowekwa kwenye kwenye chemba ya Moyo wa Mme wako Usiye mjua bado kwa sasa,huyo ndo aliyebeba sura yako,tabasamu lako,chozi lako,furaha yako,huyo akifunuliwa kwako tu *Lazima moyo wako Ulipuke kwa furaha* Na yeye huyo Atakupenda,atalinda moyo wako,hisia zako na huyo ndo atafuta machozi ya mapito yako, na huyo ndo *Atasimulia na kuelezea Uzuri wako* Ulivyo na ndiye ataujua Uzuri wako, hatakama wengine watasema No kwako, yeye atasema Yes, wengine wakikuambia Haufai, yeye Atasema wewe ndo wa Pekee katika wana wake wote.
*Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote,Mithali 31:29*
💚Mwanaume wa aina hii mwenye lugha hii, Atapatikana tu pale utakapo *_Jituliza kwa Bwana,na kuzama magotini kwa maombi na Utumishi mbele za Mungu_* Na hapa ulipo ni mahali sahii pa Kupata waume wema,kwakuwa Tunasema MUNGU NIPE UBAVU WANGU,siyo mazingira,elimu,kabila,baba au mama,tumesema MUNGU,kwa lugha nyingine *Group hili tumejipanga kumtafuta Mungu kwa Bidii mpaka ajibu watu wake* Na tumeona,tunaushuhuda kwa maombi yetu watu wamejibiwa maombi wamepata wachumba sahii na wengine Wamefunga ndoa tiyari... Mungu wetu Anajibu.
*USITISHWE NA UPEPO WA KUKOSA WACHUMBA, AU WENGINE KUKUACHA*
👉Mungu wetu huyu uwa ni Mungu anaye fanya mambo kwa kusudi lake,na kwa wakati wake, wakati unalalamika unasema *WHY ME?* Upande wa pili kuna *Wema wa Mungu ulio kuzunguka na kukuepusha na Majuto makuu* ila hukuona,umeona tu tukio la kuachwa,au kuchelewa kuolewa,kumbe upande wa pili Mungu amekuepusha na *Kuwa mjane ukiwa bado mdogo,Amekuepusha na Divorce katika umri mdogo wa ndoa,Amekuepusha na kuishi wa Migogoro isiyo isha,Amekuandalia mtu wakutimiza ndoto zako za kihuduma,kiuchumi na kimaisha kwa ujumla*
💚Binti yangu, Kila mahusiano Unayopitia ni darasa tosha kwaajili ya maisha yako ya baadaye.
💚Wengine mebeba nafsi za watu wengi maishani mwenu ambao wanahitaji kufundishwa,kushauriwa,kuepushwa katika majanga ya kindoa na kiahusiano, nani awezaye kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkuu wakati hana *History ya Mapito ya ushindi?*
Utawasaidia watu kwa ubora zaidi ikiwa Ulipita na ukashinda..... _You have a living testimony_
*Daudi akasema, Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na Bwana atakuwa pamoja nawe. 1 Samweli 17:37*
💚Wajuaje wewe ni mtu mkubwa utakaye ponya kizazi cha mabinti wengi wajao nyuma yako, walio nyumbani mwa Bwana? Watoto wako?washirika wako? Wajuaje utakuwa Great Figure in the world utakaye kuwa ukisema na ulimwengu mzima,taifa zima,mkoa mzima, wajuaje utaolewa na mme ambaye ni mtumishi mkuu wa Mungu asimamaye mbele za maelfu wengi?.
💚Mara nyingi tunatishwa na muda wetu ambao kwa mtazamo wetu twa hisi ndiyo sahihi,lakini pamoja na kuona muda wetu ndiyo sahihi, *Sisi kama wanadamu twaona karibu mno* wala hatuyajui ya baada ya dakika moja, lakini Mungu wetu anaona mbali,anajua yote na yote anayotuwazia ni Mema,kwa hiyo *_Anaweza kwenda kinyume na Muda wetu,siyo ili atuumize,bali aulete Utukufu mkuu wa muujiza katika maisha yetu_* ili tuwe na furaha timilifu ndani yake.
1 Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake.
Yohana 11:1

3 Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi.
Yohana 11:3

6 Basi aliposikia ya kwamba hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo.
Yohana 11:6
💚Kuchelewa kwa Mungu kukupa hitaji lako, kwa Tafsiri ya Kiroho, *_Ni Mungu kukuthamini mno nakutaka kukupa kitu bora zaidi_* In fact Mungu achelewi,(hiyo nikatika mtazamo wa Muda wetu)ila katika Muda wa Mungu huo ndo wakati na majira yako yanayo faa kupokea Zawadi hiyo ya Mungu.
💚Wakati mwingine watu wanao tuzunguka wanaweza *Kuwa changamoto,kwa kukukatisha tamaa,au kukupandisha hamasa ya kutaka kuingia katika ndoa kwa namna yoyote* unaona wengine walio chini ya umri wako wanaolewa wanakuacha.... *USI PANIC* Subiri muda wako,huo ni muda wao.... Usifanye maamuzi ya Kubebwa na yeyote, subiri ubebwe na *Mtu maalumu*.
*Kwa nini ni Hofu wakati najulikana na Mungu tangu zamani?*
💚Ni muhimu kulisoma Neno la Mungu na kulitumaini maishani mwako kwakuwa limebeba majibu ya maisha yetu.
💚Huna sababu yakuwa na hofu na kuhisi Umepoteza mwelekeo, _Mungu aliyekuumba,mwenye maamuzi ya mwisho juu ya maisha yako anasema anakujua wewe hata kabla hujazaliwa_ kwa maneno mengine hakuna jipya linalotokea maishani mwako hajui.....
*4 Neno la Bwana lilinijia, kusema, Yeremia 1:4*
*5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.Yeremia 1:5*
💚Kukujua kwake,si kwa bure,anasema Anataarifa zako za kwa nini uchelewe,na atafanya nini katika kuchelewa kwako.
💚Mungu Hawi na Taarifa zetu mapema ili Atuchekiiii na kutuacha, Anakuwa na taarifa zetu kwa misingi yakuweka mazingira sawa ya mapito yetu ili Tupate vitu vinavyo tufaa.
💚Uzuri wa pekee wa Mungu wetu ametufanya tuishi maisha ya Historia kwa Mungu,kwetu ni mapya ila kwake ni History, angalia anavyosema.....
9 kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi;
Isaya 46:9

10 nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.
Isaya 46:10
💚Kama Mungu anatangaza *_Mwisho wako tangu mwanzo(tangu unazaliwa,tangu unaanza mchakato wa kuomba mchumba)Mungu anatangaza mwisho wako(ndoa ya heshima) kwa hiyo wewe kabla huja kata tamaa Mungu alishatangaza mwisho wako wa utukufu, kazi yako ni Kuvumilia na kumtumaini yeye_*  mpaka uufikie Muda wako wa furaha.
_Nimalize kwa Kusema,wewe unathamani kubwa sana machoni pa Bwana,na Hayuko tiyari aone Ukiabika kama mtoto wake,atafanya na mlango wa kutokea ili Uvikwe taji ya utukufu,
   *_Unachotakiwa kama Dada wa KiKristo, katika mchakato wa kuielekea ndoa Takatifu uwe na sifa hizi,au fanya haya_*
1⃣Tengeneza Profile ya maisha yanayo someka kwa ubora na sifa njema( Attractive life)
2⃣Ibua vitu pekee ukivyo navyo ndani yako vifaye kwa bidii uwe tofauti na wengine( Be Unique and Potential)
3⃣Hata siku moja Usijidharau ulivyo,thamini nature yako jikubali ulivyo.
4⃣Jijue mapungufu yako uyarekebishe yasiendelee kuwa ukuta,au kuchafua Profile yako ya maisha.
5⃣Mwombe Mungu,mwamini Mungu,Mungoje Mungu wa kwako yupo atakuja kwa wakati.
*NB: _Katika kuomba hakikisha unamwambia Bwana fungua sura yangu katika ulimwengu wa Roho ionekane katika uhalisia wa ulivyoniumba ili mme wangu auone Uzuri wangu ulioniumbia_*
Nikutakie Maombi mema,na matengenezo mema ya maandalizi yakuingia katika ndoa njema ya Baraka.
_Ulikuwa nami mnenaji wa siri hizi Mtumishi wa Mungu, *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist & Counselor)*
Facebook Elisha Kazimoto
WhatsApp 0755444078