🎤🎤 *MAUMIVU YA KWENYE NDOA SWALI NA MAJIBU*🎤🎤
Bwana Yesu asifiwe Dady,nina changamoto naomba unipelekee kwenye group,kwa sasa sina MB,mme wangu hanishirikishi kwenye ratiba zake,yaan kuna siku namsikia tu anasema ,nimepanga kuwasomesha watoto wa ndugu zangu wawili,mara unaona kasain mikopo ya milion sita ,nane .Mwisho yaan ndugu zangu anawachukuliaje
..........................................
_Anajibu Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto*(Psychologist & Counselor )_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
.........
.........
*TUHITIMISHE MADA HII KWA KUANGALIA PANDE 2 YA MKE NA MME*
👉Kwanza kila changamoto,au tabia ina CHANZO chake au kichocheo chake aidha kutoka nje ya box au ndani ya box(maana kwamba kwa huyu aidha chanzo ni mwanamke - Nje ya box, au Mwanaume -Ndani ya box)
👉Shida kubwa ya kutatua migogoro ya ndoa au kushauri kwenye migogoro ya ndoa ni vigumu kupata Ushauri ulio suruhishi kwakuwa wana ndoa wengi wakileta mgogoro, analeta MATOKEO NA SI CHANZO,halafu Anazumgumzia kosa alilofanyiwa ila yeye alilo lifanya analificha au analihesabu kama si kosa.( hapo ndo huwa pagumu kushauri wana ndoa kama anayelalamika ni mmoja)
*TWENDE PAMOJA KWA TATIZO LA HUYU MAMA*
👉Mwana mama unahitaji kusoma NATURE na saikolojia ya mmeo vile vile mwanaume kusoma saikolojia ya mkeo ili mwende sambamba,ukishindwa hapo mtavurugana sana kwa vitu vidogo.
👉Hapa Tungejua kitu kimoja ingetusaidia sana, *Kwamba Tangu anamuoa huyu mama,mme amshirikishi kitu chochote?anaamua yeye mwenyewe au Imekuja hiyo tabia baada ya kuishi miaka 2,3,5....?*
👉Kama tangu anakuoa hakushirikishi kitu,anapanga tu mwenyewe.... Hapo tuta mtafsiri mwanaume katika nyanja zifuatazo.
1⃣Alikolelewa mfumo umemwathiri,katika makuzi yake hakuona mwanamke akithaminiwa na kupewa nafasi ya kupanga maisha so ni mwendelezo wa kifamilia damu ya utawala na ubabe
2⃣Ana makundi ya watu waliojengana fikra za kuwadharau wanawake kama viumbe visivyo na mchango wowote katika familia.
3⃣Ameoa mke asiye jishugulisha na chochote haingizi hata mia ni RECEIVER TU,halafu amekosa Ujanja wa kutumia nguvu ya mwanamke kumteka mme kimahaba mpaka akawa mtu wa kumshirikisha vitu vyote.
👉Kama tabia hii Imeanza baada ya wameisha ishi mwaka,1,2,3,5,.....Mwanamke ndo Amechangia, *Amezoea mazingira ameanza kupunguza huduma muhimu kwa mme.*
👉Niliongea vitu 2 juzi katika kutoa angalizo la mada hii.
👉Kosa kubwa wanawake wengi wanafanya ni Kutoa Adhabu isiyo sahihi kwa Kichwa cha familia., most of women Uona baada ya kukosewa eneo flani dawa pekee ya kumnyoosha mmewe ni KUMNYIMA SEX,bila kujua hapo ndo Unapandisha MASHETANI YA MWANAUME YEYOTE DUNIANI.(Kunyima kumegawanyika katika makundi 2)
1⃣Kunyima kwa kukataa kabisa
2⃣Kunyima kwa kutengeneza visababu sababu vyepesi, mara naumwa,mara sijisikii vzr,mara uende kutembea uchelewe,kuwa busy na watoto,kujipa kazi za ziada nakuzifanya hata kuchoka,kujipa usingizi fofofo wa uongo nk
👉Mwanaume anaakili sana ya kutambua hili unalofanya ni kwasababu umeambiwa sex sasa nikama hutaki.
👉Revenge ya mwanaume ni mbaya sana,akisha kuondoa kwenye Akili ataanza Kufanya mambo yake bila kukushirikisha na huyo awe ameokoka,ambaye hajaokoka vzr hapo anaenda na nje kupata sex.
👉Kinacho mpa nguvu ya kusikia moyo wa kukwambia kila kitu,kukushirikisha *NI MAHABA(SEX) NA HESHIMA UNAYO MPA* hilo ndo limewashinda wanawake waliokwenye ndoa ila WAKISHA ACHIKA NA KUWA MALAYA WANAYAWEZA(Hilo ndo malaya wote wanaoiba waume za watu wameweza)
👉Mpaka malaya aliyeiba mmeo anajua siri zote za mmeo,mipango yote nk kuliko wewe mwanandoa,SI DAWA,ni MAHABA NA HESHIMA ANAYOMPA MMEO vitu hivyo 2 vinafungua moyo wa mme Kusema yote *SI MJIFUNZE KWA DELILA NA SAMSONI* Umeona biblia imesema Delila alimpa Samson LIMBWATA ili aongee siri ya nguvu zake. NI PENZI TU(MME NI SEX,NARUDIA MME NI SEX NA HESHIMA KWISHA HABARI)
*_Sasa ninyi endeleeni kukaa rohoni sana msahau mahaba na heshima mtashangaa mmeo anaibiwa hivi hivi na anayemuiba unamzidi dashboard... Unashangaa kajamaa kanajua mipango yooote ya mmeo wewe hata 1 hujui na upo kwenye ndoa mwaka wa 10_*
Namaliza kwa kusema wamama wanaume hawa si wakorofi,wala jeuri,wala wajinga,Ujeuri,ujinga,na ukorofi mmeukuza ninyi, usipende kutawala hata kama wee unavheo na pesa mme hana,wee mfanye awe mtawala MPE MAHABA YA KUTOSHA,HESHIMA utaona kila kitu anakuuliza wewe kwanza ndo unampa mipango anaenda kutekeleza, UMEMTAWALA KIUTAALAMU.
*NARUDIA MAHABA(SEX)NA HESHIMA KWA MME NI DAWA YA MWANKE KUMTAWALA MME WAKE KIUJANJA NA AMANI NA FURAHA IKADUMU KWENYE NDOA NA UPENDO TELE.*
_Mchambuzi Ev Elisha Kazimoto(Psychologist & Counselor_
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
Thursday, 19 December 2019
MAUMIVU YA NDOA
Tuesday, 10 December 2019
HARUFU YA ZINAA KUWA MAKINI
Thursday, 31 October 2019
UZURI WA MUNGU KWETU NEW MONTH
🥦🥦 *HUU NDIYO UZURI WA MUNGU WETU KWETU*🥦🥦
*_Imeandaliwa na Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
*NEW MONTH NOVEMBER 1.209*
................................................
*_Tafakari ya Leo_*
_Shalom wana wa Mungu aliye hai. Leo ni tarehe 1.11.2019 ni mwanzo wa mwezi katika siku ya kwanza,nakutafakarisha uzuri wa Bwana_
*(21)Najikumbusha neno hili, Kwa hiyo nina matumaini.(22)Ni huruma za Bwana hatuangamii, Kwa kuwa rehema zake hazikomi.(23)Ni mpya kila siku asubuhi; Uaminifu wako ni mkuu.Maombolezo 3:21-23*
🥦Katika andiko hili, mstari (21)... Kuna jambo la kujifunza na kupata nguvu ya kuendelea mbele katika safari ya kuelekea mwisho wa Mwaka. Hapa yako mambo makuu 2.
1⃣Anasema _Najikumbusha Neno hili....._ Nimuhimu sana katika maisha kuwa na tafakari juu ya *Uliko Toka* Kujikumbusha, kwa lugha nyingine ni *Kurejea nyuma uliko pita, au kurudisha kumbukumbu za kilicho semwa,onwa* Vipi mpendwa Ukirejea nyuma uliko toka tangu tarehe 1.1.2019,unaona nini? Kama mpaka sasa upo ila unataarifa za watu wengi ambao mpaka sasa hatunao duniani,wengine ni wapendwa wetu wa karibu.... Hii Haikupi kuona kwamba *Bado Bwana ana Haja nawe Duniani?* Pamoja na Changamoto ngumu ulizopitia na tunazopitia lakini Uhai bado upo ndani yetu na Uhai ndo Injini ya Mabadiriko ya Maisha.
👉Jikumbushe ulivyo ponywa na Ajali ile mbaya, jikumbushe ulivyo pita kwenye lile pito zito mpaka ukakata tamaa, Lakini Ulipita, *Huo ndo uzuri wa Bwana*
👉Jikumbushe neno hili, Bwana wetu alivyosema *Sitakuacha wala kukupungukia* jitie nguvu sasa katika mwanzo mpya wa mwezi huu.
🥦Katika Mstari huo huo wa 21b, anasema _Kwa hiyo Nitatumaini_ Ukijikumbusha wema wa Mungu kwako, hutakuwa na Sababu ya *Kukata tamaa* na kuona kama Mungu amekuacha, aliye tenda yale ndo atatenda na *Hili* kwahiyo NITATUMAINI.
2⃣Katika mstari wa (22), amesema..... _Ni huruma za Bwana Hatuangamii_, Hakika ukikaa ukatafakari utajua ni Huruma tu za Bwana, adui ibirisi,mawakala wake wana lenga kila siku *Tuangamie* na wakati mwingine wanataka watumie nafasi ya *Udhaifu wetu* kutuangamiza ila HURUMA ZA BWANA zina tukinga.
_Hali halisi kwenye ulimwengu wa Roho kwako ni hii_
*13 Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini Bwana akanisaidia. Zaburi 118:13*
👉Kila siku, kila saa,kila dakika wapo *Wakusukumao sana* ili uanguke,lakini kwa nini hata sasa umesimama(Kiuchumi,kiafya,kindoa,kimahusiano,kieleimu,Kikazi,kihuduma nk) Ni *Huruma za Bwana* wakitusukuma anatusaidia kusimama.
🥦Tunaweza kuendelea kufurahia maisha ya kila siku,ni kwasababu tu *_Rehema za Mungu Hazikomi_* Na huo ndo usalama wetu, Rehema ni kiwango cha juu cha Kusamehewa na kuhurumiwa wakati ulikuwa unastahili adhabu.
3⃣Katika Mstari wa (23).... _Amesema, Ni Mpya Kila Siku Asubuhi_, tunatembelea kwenye mambo mapya ya Mungu, kawaida ya Mungu kwetu siyo *Kutulisha Viporo vya Jana* anatuandalia mambo mapya kila siku asubuhi.
🥦Kwa lugha hiyo walio cheka jana yako wata shangaa leo yako na kesho yako.... Maana utakuja na *Mambo mapya* yanayo toka kwa Mungu wetu. ( _Huu ndo uzuri wa Mungu_)
🥦Halafu anasema, _Uaminifu wake Mungu ni mkuu_, Hapa ndo huwa mioyo yetu inatulia kwa Bwana, yeye ni mwaminifu akiahidi atatenda,kazi yetu ni kumwamini na kuvumilia.
👉Huna sababu ya kumwacha Bwana, kuacha kumtumikia, kukatishwa tamaa na watu au mazingira, Uaminifu wa Bwana ni Mkuu,kiwango chake cha Kutimiza alicho sema ni cha Juu na Uhakika ndo maana yake.
_Unajua nini? Tumeanza mwezi huu na Bwana nao utaisha, Usiogope wala usiogopeshwe, ni mwisho wa Mwaka Utasafiri utatoka nyumbani salama na utafika uendako salama, Kafara za waovu Hazikuhusu wewe, sisi tunalindwa na Nguvu za Mungu kwanjia ya Imani( *1Petro 1:5*), Ni kweli mwisho wa Mwaka kuna matukio mengi ya Mauti na Ajali,Sema Hazinihusu mimi,wewe umeahidiwa na Mungu kwamba Bwana atakulinda na Mabaya Yote, tena atakulinda Utokapo na atakulinda Uingiapo ( *Zaburi 121:7-8*) Huna haja ya Kuogopa Tena_
Hii ndiyo Tafakari yetu leo katika mwanzo wa Mwezi huu wa 11,kwa kuwa ni Neno la Bwana, Litakufaa Leo,mwezi kesho na mwakani kila siku litakuwa jipya.
*_Ulikuwa nami Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto( WhatsApp 0755444078, Facebook Elisha Kazimoto)_*
©2019
Wednesday, 30 October 2019
SAIKOLOJIA YA MAWASILIANO
💢💢 *SAIKOLOJIA YA KINYWA(KUONGEA) KATIKA MAHUSIANO*💢💢
_Imeandaliwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, *Ev Elisha Kazimoto*(Psychologist & Counselor)_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
.......................................................
_Hello kijana wa kiume na kijana wa kike(binti),leo nikuongezee kitu kimoja muhimu sana katika mahusiano na Ndoa, ( *Mawasiliano/Kuongea*) tendo ambalo linatumika kila muda kila siku wakati wote wa maisha yako._
💢Kuongea ni njia moja wapo ya *Kufunua Uhalisia wako(Uzuri wako au Ubaya wako)* katikati ya watu wanao kuzunguka.
💢Nature ya mtu, Tabia ya mtu,nguvu ya mtu na udhaifu wa mtu, *Ufafanuliwa na Lugha yake(Maongezi yake)*
💢Kuna maeneo mawili makuu ambayo watu *Upima Uzuri na Ubaya wa mtu* Eneo la Kwanza *MAONGEZI YAKE(lugha) na Eneo la Pili ( MWONEKANO WAKE(Presentation)yake kwa watu(Personality)* hayo ndo maeneo makuu watu wanaweza ku Judge mtu kama anafaa au hafai kuwa mke au mme, au kuongoza au kusimamia eneo flani,ila hapa mimi naongelea mahusiano na Ndoa.
💢Ikumbukwe kuwa Lugha yako,(maongezi yako) *Yanaweza wasilishwa kwa Maneno ya sauti au kwa njia ya Maandishi* kupitia njia hizo kuu 2 watu wakajua wewe ni nani.
💢Unapo anza safari ya kutafuta mwenzi wa maisha( *Mke au Mme*), Anza na Safari ya Kurekebisha Maongezi yako na Mwonekano wako.
💢Unapo fanya maombi ya Kuombea mwenzi wako usiye mjua, ( *Anza pia kuombea Uwasilishaji wa Hisia zako kwa maneno na maandishi*) viwe vinavyo faa kwa watu.
💢Kisaikolojia na wanasaikolojia *Hauangaiki sana kujua Tabia ya mtu,kufaa kwa mtu, udhaifu wa mtu, endapo una Nafasi ya Kusikia maongezi yake na Kusoma Maandishi yake* hapo ndo unaweza Kujua huyu ni nani na Akili yake ikoje na moyo wake ukoje.
💢Lakini Uzuri wa Somo hili, Si Saikolojia pekee ilo bainisha haya, hata Biblia Takatifu imeweka wazi *Mtu ni nani,mtu ni Maneno yake* Yaliyo jaa moyoni ndiyo yatakayo semwa na ndiyo yatakayo tendwa.
*Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema, na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena yale yaujazayo moyo wake.Luka 6:45*
💢👆Hapa ndipo wana saikolojia wakafafanua zaidi, Kwamba Tabia ya mtu utaifahamu kwa kadri ya uwasilishaji wake wa hisia zake kwa watu kwa njia ya maneno au maandishi.
💢 Tuna mjua mtu huyu ana Dharau, kwa maneno yake, mtu huyu Hajali, kwa maneno yake, mtu huyu ni Mkorofi kwa maneno yake, mtu huyu ana Hasira kwa maneno yake, mtu huyu ji Rough kwa maneno yake,mtu huyu ni mpole,muungwana,ana hekima kwa maneno yake, mtu huyu uwezo wake wa Kufikili,Kuamua mambo,ni mkubwa au mdogo kwa maneno yake( Anavyo yawasilisha kwa sauti au kwa maandishi)
💢 *KWA MSINGI HUU KIJANA WA KIKE NA WA KIUME HASA KATIKA ZAMA HIZI ZA TEKNOLOJIA YA MITANDAO YA KIJAMII*
1⃣Watu wengi wameshusha na watashusha Hadhi zao, watakataliwa sana,watachelewa kuoa au kuolewa kwasababu ya namna wanavyo wasiliana katika Magroup ya mitandao ya kijamii.
2⃣Watu wengi watafunua udhaifu wao na wanafunua udhaifu wao ambao ingekuwa vigumu kuujua, na kukulindia heshima yako,ila kwasababu ya kukosa Saikolojia ya Mawasiliano watu wanawasilisha Hisia zao kwa maandishi au kwa sauti bila kujiwekea Taadhari.
3⃣Watu wengi wanaweza na wataweza kuwahi Kuoa au Kuolewa, kugombaniwa na watu kwasababu ya Uwezo wao wa Kuwasilisha Hisia zao kwa maaandishi ana sauti, vinawa Promote zaidi kwa watu na kuonekana ni watu wa pekee.
💢 *ANGALIZO KATIKA SAIKOLOJIA YA MAWASILIANO*
👉Kukaa kimya siyo tafsiri ya uwezo wako mzuri na mkubwa wa kuwasiliana, ila *Umepunguza kujulikana haraka kwa watu*
👉Kuongea sana katika kila kitu, Hakutafsiri uwezo wako wa kujua au uwezo wako mkubwa wa kuwasiliana, *Ila umewarahisishia watu kujua wewe ni nani*
💢Hayo mambo yaangalie sana yatakusaidia kwakuwa kila siku unaongea unaandika, unaonekana(Mwonekano wa nje - Personality)
🎀 *SAIKOLOJIA YA MAWASILIANO INAKUTAKA KUZINGATIA ALAMA ZIFUATAZO*🎀
1⃣Ongea kitu ulicho na uelewa nacho vizuri( Utaonyesha uwezo wako wa Akili)
2⃣Kabla ya Kujibu Hoja ya mtu, Angalia yeye Ameiwasiliaha katika hali gani(ya hasira, furaha,uzuni,upole,dharau nk) ukijua ameiwasilisha kwa Aina gani, Itakusaidia Kumjibu katika Nafasi iliyo nzuri itakayo funua Hekima yako na uwezo wako wa Kutafakari.
3⃣Kabla ya kujibu hoja ya mtu, Sikiliza ndani yako ile hoja uliyoisikia au isoma *Imeibua nini ndani yako*(Hasira,Furaha,Uzuni,Chuki nk) Ukijua aina ya msisimko uloibuliwa ndani yako, itakusaidia Kujibu kwa Umakini Maana utakuwa na Taadhari ya Kulinda Hisia zako.
4⃣Kabla ya kujibu hoja iliyokufikia kwa maandishi,au sauti.... *Angalia kwanza Nafasi yako kwa watu wanaokuzunguka(Status)* (Je, wewe ni kiongozi, Mkubwa Kiumri,mdogo,Una ndoa au huna) waza athari zinazoweza tokea pale watu watakapo tafsiri ujumbe wako kama ndivyo ulivyo.... Hii itausaidia Kuongea au kujibu Umakini zaidi nanKutunza Heshima yako na kuonyesha *Kiwango cha Ukomavu wako*
_Ninapo maliza kwa leo yako mambo mengi ila leo niishie hapo, Lakini cha kujifujza hapa ni kwamba wewe mwenyewe unaweza jitengenezea *Kibali machoni pa watu au Kuharibu Kibali chako machoni pa watu* kutokana na uwasilishaji wako wa maneno kwa watu wanaokuzunguka_
💢💢 *_Uchambuzi huu umeletwa kwako na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, Mwanasaikolojia EV ELISHA KAZIMOTO, Ambaye ni Mkufunzi wa Masuala ya Kiroho(Neno la Mungu) na Masuala ya Kimahusiano na Ndoa na Saikolojia ya Maisha_*
Mawasiliano: WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto.
*NB: Ana Magroup ya WhatsApp 8 tofauti anayo yasimamia yanayotoa Elimu mbali mbali za Kiroho na Kisaikolojia*
ULIYE TAYARI KARIBU.
©2019
Tuesday, 22 October 2019
TANGAZO LA KONGAMANO LA WHATSAPP
💒💒 *KONGAMANO LA KIHISTORIA LA MADINI ADIMU YA KISAIKOLOJIA,KIROHO KATIKA MAHUSIANO NA NDOA NA SIRI ZA UTUMISHI WA MADHANAHU*💒💒
💒Kongamano hili kimeandaliwa na Kamati kuu ya Umoja wa Magroup 8 ya WhatsApp yanayosimamiwa na Mtumishi wa Mungu na mwana Saikolojia *Ev Elisha Kazimoto(0755444078)* Kutoka mkoa wa Kagera.
🎀Hili litakuwa kongamano la kwanza na la Kihistoria kutokea,litakalo wakusanya watu kutoka mikoa yote Tanzania na Zanzibar na nje ya Tanzania.
💒Lengo kuu la Kongamano hilo ni *Kufahamiana,Kujifunza madini adimu ya Kisaikolojia na ya kiroho katika sekta ya Kimahusiamo,kindoa na kihuduma,bila kusahau kushare Experience za kiroho na kijamii* Lakini pia Utapata Fursa ya Kuhudhuria LIVE LECTURE na Kuuliza maswali ya papo kwa papo katika nyanja zote zilizotajwa.
💒Pia tutakuwa na Maombi Maalumu ya kuombea Vijana na Mahusiano,Wana ndoa na wale wenye Huduma mbali mbali za KIROHO.
💒Tutakuwa na mipango Mahususi kwaajili ya kuwa watu wenye Impact katika Kanisa na jamii katika kizazi chetu.
*_Hakuna kiingilio ni bure,kazi yako ni Kujisajili Kwa fomu maalumu yenye Maelekezo ili kujua umapatikana wapi,ili ujue eneo ambalo Kongamano litafanyika(Eneo utaambiwa litakuwa ni rahisi kufika kwawatu wote kutoka pande zote za nchi,tutakuwa na muda wa kutosha wa kujiandaa,Changamkia Fursa hiyo moja kwa mwaka 2020_*
Imetolewa na ofisi ya Maadmin waliochini ya Ev Elisha Kazimoto na kupitishwa na Senior Admin Ev Elisha Kazimoto(0755444078)
_Ulikuwa ukimfatilia mafundisho yake Facebook,WhatsApp na YouTube sasa Kukutana naye Live na kujifunza siri zote bure_.
©2019
UTAMBULISHO NA USAJILI
🎀🎀 *TANGAZO MAALUMU KUTOKA OFISI KUU YA GROUP*🎀🎀
🎀 _Shalom members wote,tunaombwa kuzingatia Tangazo hili kwa umuhimu sana,ili kufanikisha maono makubwa yajayo mbele zetu_
🎀 Tutakuwa na Utambulisho Maalumu kwa members wote tulio humu, kwa kuzingatia vipengele vifuatavyo
1⃣Picha yako ya sasa(current photo) *Picha yako iambatane na taatifa zote hizi chini* usitume picha bila maelezo hayo
2⃣Majina yote(full name)
3⃣Hali yako(Status) Single,Married,In relationship
4⃣Mkoa unakotokea(Regional) unakoishi kwa sasa
5⃣Wilaya unakoishi kwa sasa
6⃣Umeokoka au bado hujaokoka(be free)(KANISA UNAKO SALI)
7⃣Huduma yako(kanisani).
8⃣Mwajiliwa,Umejiajili,mwanafunzi.
*_Utambulisho huu niwa muhimu sana kwaajili ya mpango Mkakati wa maono ya Mwakani ya Uongozi wa Kuandaa Kongamano kubwa la Pamoja la LIVE LECTURE, pamoja na kufahamiana kama members wote wa Magroup 8 yaliyochini ya Mtumishi wa Mungu, na mwana Saikolojia Ev Elisha Kazimoto_*
🎀Mara baada ya utambulisho na kujua Idadi ya members kwa kila kanda tutarudi tena kupeana Maono Maalumu ya Kukutana kwa kongamano la Kihistoria.(Tuajadili pamoja,tutafikia Muafaka,tutaratibu, Tutatimiza,Tutaandika Historia ya Furaha maishani na katika ufalme wa Mungu)
*BY SENIOR ADMIN EV ELISHA KAZIMOTO*(0755444078)
_Imetolewa baada ya kikao maalumu cha Maadmin wote wa magroup yote 8 cha tarehe 22/10/2019_
Thursday, 17 October 2019
ZINAA NA MCHUMBA WAKO NDOA MOTO
π£π£ *UKIONA UMEANGUKA KWENYE ZINAA NA MCHUMBA WAKO JIPANGE KWA YAFUATAYO KATIKA NDOA*π£π£
_Imeandaliwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto*(Psychologist & Counselor)_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto.
......................................................
_Hello kijana wa kiume, Hello kijana wa kike, Hello mwana Ndoa, nina Alama muhimu za Nyakati chache zikusaidie kwa Taadhari,au Kugundua Maangaiko yako,ujiponye au Upambane_
π£Mara nyingi tumekuwa tukichukulia kawaida suala la Mahusiano ya kirafiki na kiuchumba na kuona nikama kipindi cha Kujiachia,au cha Kujaribu jaribu kama kuna bahati yako au la, kumbe nikipindi Muhimu ambacho ni msingi wa ndoa ya mtu.
π£Ndoa nyingi zina machafuko yasiyokoma,ambayo masuluhisho mengi ya kwa wazazi,wasimamizi,wachungaji,mpaka na mahakama yamegonga mwamba hakuna kutulia,yametoka katika vyanzo vikuu 3, mimi nitazungumza 1, viwili vipo kwenye lecture zangu kama nimfatiliaji wa masomo yangu katika magroup mengi ya WhatsApp na Facebook. Machimbuko hayo 3 ni:
1⃣Ukosefu wa Maarifa ya Kisaikolojia ya kuendesha mahusiano ya uchumba au Ndoa (watu wanajikwaa katika mlima wa ujinga. HOSEA 4:6).
2⃣Kuto apata mtu sahihi(Uchaguzi usio makini) Unafoji ubavu.... (Jua hautakuja kutulia na mtu wa mwingine)
3⃣Msingi Mbovu wa Mahusiano yenye Harufu ya Zinaa.
π£Miongoni mwa vitu ambavyo wengi wa wanaofunga ndoa upuuzia nakuona ni kitu kidogo,ni *Ni wao kuanguka katika zinaa(Kushiriki ngono)kabla ya ndoa halafu wakaoana* wakiamini wanaendeleza Upendo,kumbe ndo wamefuta upendo.
π£Labda nikupe siri hii ya Kisaikolojia na kiroho *SEX INAPANDE MBILI ZA SHILINGI* Ni TAMU na Inaunganisha Nafsi za watu na kuwafanya wawe na Sura moja( *_Kama imefanyika katika muda muafaka kwa watu sahihi bila hatia_*)
19 Wakaondoka asubuhi na mapema, wakasali mbele za Bwana, kisha wakarejea na kufika nyumbani kwao huko Rama; Elkana akamjua mkewe Hana; naye Bwana akamkumbuka.
1 Samweli 1:19
ππSex ikifanyika kwa watu waliosahihi yaani mke na mme ina MKONO WA BWANA WA BARAKA.
πPili SEX inakawida ya *Kuwaachanisha watu nafsi,kufuta upendo,Amani,furaha kati ya watu Walioifanya Kinyume,nje ya muda na si watu sahihi*
10 Amnoni akamwambia Tamari, Kilete chakula chumbani, nipate kula mkononi mwako. Basi Tamari akaitwaa mikate aliyoifanyiza, akamletea Amnoni nduguye mle chumbani.
2 Samweli 13:10
11 Naye alipokwisha kuileta karibu naye, ili ale, Amnoni akamkamata, akamwambia, Njoo ulale nami, ndugu yangu.
2 Samweli 13:11
12 Naye akamjibu, La, sivyo, ndugu yangu, usinitenze nguvu; kwani haifai kutendeka hivi katika Israeli; usitende upumbavu huu.
2 Samweli 13:12
13 Nami nichukue wapi aibu yangu? Wewe nawe utakuwa kama mmoja wa wapumbavu wa Israeli. Basi, sasa, nakusihi, useme na mfalme; kwa maana hatakukataza kunioa.
2 Samweli 13:13
14 Walakini yeye hakukubali kusikiliza sauti yake; naye akiwa na nguvu kuliko yeye, akamtenza nguvu, akalala naye.
2 Samweli 13:14
15 Kisha Amnoni akamchukia machukio makuu sana; kwa kuwa machukio aliyomchukia yakawa makuu kuliko yale mapenzi aliyokuwa amempenda kwanza. Amnoni akamwambia, Ondoka, nenda zako.
2 Samweli 13:15
16 Naye akamwambia, Sivyo, kwa kuwa mabaya haya ya kunitoa ni makuu kuliko yale uliyonitendea. Lakini alikataa kumsikiliza.
2 Samweli 13:16
17 Ndipo akamwita mtumishi wake aliyemtumikia, akasema, Mtoe sasa mwanamke huyu kwangu, ukafunge mlango nyuma yake.
2 Samweli 13:17
ππWakati sex isiyo halali inakuwa ina vutia na inapofusha macho nikama unajituliza ila matomeo yake baadye INAFUTA KILA AINA YA FURAHA NA AMANI KATIKA NAFSI ZA WAWILI hawa,sasa ikisha futa na mkaoana *Hiki ndo kinatokea kwenye ndoa yenu* Kiroho na Kisaikolojia:
1⃣Uaminifu kati yenu ndo basi tena( Hakuna atakaye kuja kumwamini mwenzake daima)
πHapa hata mwenzako aone unatoa pepo,viwete wanatembea,unaimba mpaka unabubujika, Nafsi mwake *Hana Imani na wewe* ana ❓❓❓nyingi.( _Kwa nini,kwasababu ulikuwa na Ujasiri wa kuvunja uaminifu wako mbele zake katika ujana,kwa sasa ndo anaona huwezi shindwa vunja tena_) Mtaishi maisha ya kuwindana,kulaumiana sana.
πKawaulize wote walioangukia Kona hii hata kama ni watumishi wa Madhabahuni,wamalazimisha kuaminiana mdomoni ila Moyoni na Akilini *wanashutukana*
2⃣Thamani yako kwa mwenzako inashuka chini ya 50%. Ukiona umevua au umevuliwa nguo kabla ya ndoa na huyo huyo mkaoana, *Respect kati yenu inashuka chini ya nusu* kwa nini, Usiri wamiili yenu unabeba *Heshima ya mioyo na utu wenu* Mkisha vuana nguo Usitegemee, *Baba mwenye nyumba kupata full respect,au mama kupendwa full love* utakuwa na Partial.... Maana respect na love vilivuliwa moyoni mwako nje ya ndoa,hukuja navyo ndani ya ndoa
3⃣Kuna uwezekano wa KUACHANA kimwili (divorce) kwa nini vitu muhimu vinavyo shikilia Ndoa,hamkuingia navyo ndani mliviacha pale mlipovuana nguo( *Vitu kama, Usiri,Aibu,heshima,shahuku kwa mwenzako,*) kwa hiyo mgogoro ukianza ndani Hauzimwi unatafuta Kuachana.
4⃣Fujo,magomvi,kunyimana tendo la ndoa haviwezi kukoma kati yenu....(Maana moyo wa Upendo uliisha chukuliwa na adui)mtasuluhisha ila muafaka haupo,wanacho laumiana ni kidogo sana ila kinakuzwa na mbegu ya zinaa iliyofanyika. Mwaweza ishi ila si kwa Amani na upendo,mtakuwa na vipindi vifupi vya furaha na kipindi kirefu cha dhoruba.
_Nini nataadharisha vijana ambao bado hamjaingia katika ndoa, Komaa mpaka mwisho,rafiki au mchumba akikushawishi kwa sex kimbia na PIGA ❌ kuanzia kichwani pake mpaka muguuni pake,usipo fanya hivyo uta enjoy kwa mwezi,wiki na siku ila Utajuta maisha ya ndoa Yote._
πMlioko kwenye Ndoa,Nahisi ukisoma haya utajua kuwa kama Ulipitia huko Haya ndo Maisha yako, *Huna heshima kwa mwenzako,Sex hupati inavyotakikana,upendo haba sana,Amani hakuna,Uaminifu hakuna,unahisi kumchoka mwenzako* nini Kifanyike Lazima mtibiwe wote Kiroho na Kisaikolojia ili mpunguze makali ya Maisha mnayoishi ila mbali na hapo mpaka kaburini au Mtaachana tu.
*_Ulikuwa na mimi Mchambuzi wa Masuala ya Ndoa na Mahusiano Ev Elisha Kazimoto (Psychologist & counselor)_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
Wednesday, 16 October 2019
NDOA INAHITAJI AKILI TIMAMU
🎀🎀 *NDOA NI TAASISI NYETI SANA INAYO HITAJI WATU WALIO NA AKILI TIMAMU NA KOMAVU*🎀🎀
_Imeandaliwa na Mwanasaikolojia na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto.
............................................
_Hello Hello wana ndoa na wana ndoa watarajiwa,nasema nanyi leo kuponya watu wachache wenye Akili Timamu ya Ki Mungu na ya Kisailojia,na wale waliogonjweka hii ni Saa ya Kupona ( *Kama ukitaka*) ila ukiona Huwezi Badirika, Amini unacho amini ila Historia Itajirudia HAUTAKUJA KUWA NA FURAHA MAISHANI kama wanayoipata wegine walioko kwenye NDOA_
🎀Kwanza, nimesema ndoa inahitaji watu wenye *Akili timamu* Kwa nini nasema akili timamu, _Kabla ya kufanya Maamuzi ya Kuoa au Kuolewa,inabidi uwe na uwezo wa kutambua mazingira yafuatayo ndo yanayoonyesha wewe una akili timamu ya Kindoa_
1⃣Naenda kuolewa au kuoa nimetaka mwenyewe, imenipasa kukabiliana na yoyote yatakayotokea huko kwa Busara.
2⃣Naenda kuoana na Binadamu na si Malaika, anamadhaifu kama mimi,atanikosea,nitamkosea ila inabidi niangalie namna ya kuishi naye kwa Amani.
3⃣Ndoa yetu(Makazi yetu) yatakuwa hapa hapa duniani na si Mbinguni,kwa hiyo kama dunia isivyo tambarale na maisha ya ndoa yetu hayawezi kuwa tambarale, lakini kuna watu waipenda ndoa yetu na wengine watatafuta namna ya kutugawa ila nijue namna ya kumlinda mwenzangu na kujilinda.
4⃣Kuoa na kuolewa ni Heshima kijamii(kwa Mungu ni kupata Kibali mbele za na baraka) *_Ila Kuachika,Kufukuza mke,Kutoka kwenye ndoa,kudai Talaka na Kutoa Talaka Ni Fedheha,na Aibu ya milele kwenye jamii na mbele za Mungu ni Laana_* Maana Mungu anasema ANACHUKIA KUACHANA.( yaani hapo hajaweka sababu yoyote Amesema ANACHUKIA, HIVI MUNGU AKICHUKIA UTASALIMIKA WEWE.
*Maana mimi nakuchukia kuachana, asema Bwana, Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema Bwana wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.Malaki 2:16*
🎀Lakini pia Unapoingia katika ndoa au kama wewe upo kwenye Ndoa Tunaona *Akili yako Imekomaa Kiasi gani,na Ulifaa kuoa au kuolewa kwasababu una akili komavu ya Kindoa pindi Utakapo kuwa na uwezo wa kufanya mambo Yafuatayo*
1⃣Kama utakuwa na uwezo wa kukaa na mtu ambaye si ndugu yako, mmekutana ukubwani, ukaweza Kuishi naye kwa hali yake yoyote, mkakaa kwa Amani na Furaha( *Yaani uwezo wa kutengeneza mazingira Rafiki ya amani*)
2⃣Kama utakuwa na uwezo wa Kukosewa na ukasamehe kabisa bila kulipa kisasi,au Ukakosea ukajua na kuomba samahani ili kulinda amani ya ndoa yako.
3⃣Kama utakuwa na uwezo wa Kuboresha madhaifu ya mwenzako mpaka akayaacha na kuwa vizuri,bila kumchoka na kumkatia tamaa.
4⃣Kama utakuwa na uwezo wa Kutimiza wajibu wako wa kijinsia na wa kindoa kwa mwenzako kwanza bila kusubiri UFANYIWE NDO UFANYE.
5⃣Kama utakuwa na Uwezo wa Kuhurumia Uzao wako,na kuwaonyeshea mfano mwema wa kuigwa ili nao wakue wakiwafurahia baba na mama na wawabariki hata muwapo wazee.
6⃣Kama utakuwa na uwezo wa kumpenda mwenzako hivyo alivyo, Mmejaliwa uzao au La, mnamali au mmefilisika, mzima au mgonjwa.
7⃣Kama una uwezo wa kuficha madhaifu yake watu wasiyajue bila sababu,na unauwezo wa kumwombea Mungu amsaidie awe vema.
8⃣Kama unauwezo wa Kuchukia KUACHANA na kupambana kwa namna yoyote ukae na mwenzako.
*_Hizo ndizo baadhi ya Kanuni za Kisaikolojia hasa katika Falsafa ya ndoa na Kibiblia(sija taja maandiko yako mengi) kama wewe Unajiita ni mtu wa Mungu, au kama unapenda kuishi nje ya Stress_*
NB: _Maamuzi yoyote ya wanandoa,jua mnapanda mbegu kwa uazo wenu wataishi maisha kama hayo hayo kwa vizazi 4(miaka 400baada yako) Usikurupuke kufanya maamuzi mabaya,utatesa uzao wako watakulaani hata kaburi lako_
(Fatilia wazazi walioachana,roho inawafuata hata watoto,Magomvi na kupigana,fatilia utaona kwa watoto, mama hamweshimu mmewe,fatilia watoto wake wa kike wakiolewa ni shida nk)
*TUPENDANE,TUJIFUNZE,TUREKEBISHANE HIZO NDO CHANGAMOTO ZA DUNIANI*
_Ulikuwa na Mwanasaikolojia na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa,Ev Elisha Kazimoto(WhatsApp 0755444078, Facebook Elisha Kazimoto)_.
Saturday, 12 October 2019
UFUNGUO 12
🗝🗝 *UFUNGUO WA 12: AMANI YA NDOA YETU INATOKA KWA MUNGU,TUKAE NA MUNGU VIZURI*🗝🗝
_Hello Hello wana Ndoa,kwa mara nyingine tunasogea katika meza ya Maarifa ya Kisaikolojia kwa wana Ndoa,upo nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, *Ev Elisha Kazimoto (Psychologist & Counselor)* karibu tuhitimishe kwa Ufunguo wa 12 wa ndoa yenye Furaha katika maisha._
🗝Mara nyingi watu wengi wanakuwa na mzigo mkubwa wa kuomba,kumtafuta Mungu wakati wanatafuta wenzi wa maisha,ila wakishawapata wanastarehe biashara ya kuomba,kuombeana,kuhimizana katika mambo ya Mungu inabaki ni kwa mtu binafsi na wakati Mwingine kila mmoja anaweka Silaha chini.
🗝Siri kubwa ya kuimarisha Ndoa yako na kuifanya kuwa ya Furaha,ni pale wana Ndoa mtaamua kukaa na kupanga namna yayay kuishi na Mungu katika ndoa yenu,namna ya kumtumikia Mungu katika maisha yenu ya ndoa,kubebana koroho na kuhimizana katika mambo ya Mungu.
🗝Ndoa inatoka kwa Mungu,hivyo inahitaji kurudishwa kwa Mungu kwa njia ya Maombi ili iwe salama.
🗝Miongoni mwa Taasisi yenye vita,inayowindwa na adui na inapigwa vita ni Ndoa, adui akifanikiwa kuwagawa katika Ndoa, *Amefanikiwa kushika uchumi wenu,kushika uzao wenu,kushika maendeleo yenu* na lolote laweza tokea lililo baya
🗝Mkifanikiwa kuwa watu wa vita,watu wa maombi, watu wa kumtumikia Mungu,watu wa kushirikishana mambo ya Ki Mungu,mtafanikiwa *Kulinda furaha,amani,na upendo* kati ya ndoa yenu.
🗝Wekeza nguvu kubwa ya kumwambia Mungu kila siku kwa maombi yako,kwamba Mungu linda mwenzangu,nilinde na mimi,upendo,uzuri na furaha niliyo iona kwake tangu siku ya kwanza nilipomuona,iendelee kudumu kati yetu,utupe uzee mwema,kataa vifo vya ujanani kwa watoto wenu na kwenu,kataa roho za migogoro,magomvi,mafarakano kati yenu, mwambie Bwana ifanye ndoa yetu iwe mfano wa kuigwa kwa watu wote.
_Mtu wa Mungu niishie hapa kwa leo,nikutakie baraka tele katika ndoa yenu na mkono wa Bwana uwaongoze katika kuishi maisha ya Furaha. Ndoa ni Njema kama wewe mwana ndoa ni mwema,na ndoa ni mbaya kama wewe mwana ndoa ni mbaya_
*Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.Tito 1:15*
_Ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto* (Psychologist & )_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
UFUNGUO WA 11
🗝🗝 *UFUNGUO WA 11:FURAHA YETU KATIKA NDOA NDO MWANGA WA MAKUZI MEMA YA WATOTO WETU*🗝🗝
_Hello Hello mwana Ndoa,kwa mara nyingine Mtaalamu wetu na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto* anakuletea ufunguo wa 11 wa ndoa yenye Furaha karibu_
🗝Kuna mambo ambayo wana ndoa wanaweza kuwa wanayafanya wao kama wao lakini hawatafakari kwa habari ya Uzao wao nini wana vuna kutoka katika Mahusiano ya ndoa yao.
🗝Mahusiano ya wazazi kama wana Ndoa ( *Yana nguvu kubwa katika Kuathiri Makuzi ya watoto na tabia za watoto wao*) hilo ndo jambo kubwa ambalo wanandoa wengi hawajui,na hawajali.
🗝Migogoro na magomvi kati yenu yanaathiri Saikolojia na tabia ya watoto wenu, kwa muda huo mwaweza kuona kama wako kawaida ila kuna mbegu mbaya imepandwa itakayo waendesha pale watakapo fikia umri wa kufanya Maamuzi binafsi,ndipo tabia zao, maisha yao yataonyesha Uhalisia wa Mahusiano ya wazazi wao jinsi yalivyo kuwa mabaya.
🗝Kama wana Ndoa watajutahidi kulinda Furaha katika ndoa yenu,na watoto wenu wakayaona Mahusiano yenu yalivyo mazuri tangu wakiwa watoto, kwanza *Mnawapa afya ya kiakili darasani, wanajengewa uwezo wa kutafakari na kufanya maamuzi sahihii,tabia njema inaumbika* lakini mnaetengeneza uwezo wa malezi safi ya uzao wenu.
🗝Wana Ndoa watoto wakiwa wadogo,mnaweza kila mtu kutojali,kila mtu anafanya kumkomoa mwenzake,hamuoni matokeo,ila kumbuka mnapanda mbegu ya *Mbuyu* watakapo kua watu wazima ambao wanaanza kufanya maamuzi yao binafsi na sikuamliwa 100% hapo ndipo mtakapo anza kuvuna matunda ya Magomvi yenu,visilani vyenu na ndipo mtaona Umuhimu wa Kusameana,kupendana na kuheshimiana kama wana Ndoa,lakini muda utakuwa umechelewa,mpaka kwa Neema ya Mungu aangilie kati ya uzao wenu ila mtakuwa na *Uzao mbaya usio na historia ya maisha ya kuigwa* Epuka Kulaaniwa na Watoto wako na kuburi lako kupigwa mawe, Lipa gharama ya kuhakikisha unalinda Mahusiano ya Furaha katika Ndoa.
_Niishie hapo kwa leo,ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, *Ev Elisha Kazimoto (Psychologist & Counselor)*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
UFUNGUO WA 10
ππ *UFUNGUO WA 10: MAKOSA HAYASAHIISHWI KWA MAKOSA* ππ
_Hello Hello wana Ndoa, kwa mara nyingine Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto* Anakuletea ufunguo wa 10 wa Ndoa yenye Furaha,karibu ufuatane naye katika Hoja hii_
πImekuwa kawaida ya watu wengi,iwe katika Mahusiano au katika maisha ya kawaida,wengi wametengeneza *Chuki,migawanyiko,magomvi na Migogoro* Kwa kushindwa kujua Saikolojia ya Mahusiano Inakataza Kutatua Makosa kwa kutumia makosa.
πKikawaida katika uwanja wa Kisaikolojia (Ambapo ndo makao ya Hisia) Mwenzako akikosea,ukamjibu kwa kosa jua Unaimarisha Mgogoro,au Unapanua mgogoro kati yako na yeye.
πKuitirafiana katika maisha kama wanadamu ni kawaida,kukosea kama wanadamu ni kawaida, shida matabaka,magomvi,kuachana kusingekuwepo,au kungekuwa kudogo sana na watu wangeishi kwa furaha.
πTatizo kubwa kwa watu ni pale mmoja Anapokosea, Mwenzake Anamjibu mwenzake kwa Makosa(kumkomoa) hapo haumbadirishi ila unamuongezea usugu.
πKila kosa,linahitaji Akili ya ziada ambayo ndani yake ina huruma,inakujali,inakuthamini,ina kupenda.palee ndo utaona mtu anatumia njia sahihi za kumwambia mwenzake *Jambo hili mke wangu,mme wangu linaniletea shida,waweza kulibadiri,kuliacha ili moyo wangu uwe na amani?* Kama wote wana akili ya Kisaikolojia,wamejifunza funguo za ndoa yenye furaha, hapo Watakuwa na Faragha ya kuzungumza,kurekebishana,kusaidiana na kupena mwanga mpya wa kuishi watatoka huko na majibu ya furaha na kuendelea kuishi kwa upendo.
_Niishie hapo kwa leo katika ufunguo huu wa 10, ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist & Counselor*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
UFUNGUO WA 9
🗝🗝 *UFUNGUO WA 9: KAMA MOYO WAKE UTAUMIA NA MIMI NITAUMIA*🗝🗝
_Hello wana Ndoa Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, Msaikolojia *Ev Elisha Kazimoto* Anakuletea ufunguo wa 9 kati ya 12 wa ndoa yanye Furaha, fuatana nami katika ufunguo huu,ili ufungue chumba chako cha Stress uingize furaha_
🗝Kuna vitu ambavyo ukishaingia kwenye ndoa inabidi kila mmoja Ujiulize ndipo utaruhusu chemi chemi za furaha katika ndoa yako.
🗝Kumekuwa na kawaida ya wana ndoa kutojali Maumivu ya mwenzake,kwa hiyo anaweza fanya lolote kwake akidhani *Anamkomoa mwenzake* anashindwa kujua kwamba kwenye Ndoa Mungu alisha sema ninyi ni MWILI MMOJA, Kauli hii Kisayansi tunaipata kwa bwana mmoja mwana FIZIKIA(PHYSICS) anaitwa Archimedes,kwenye *Third Law of Motion, anasema "To Every Action,there's equal and opposite Reaction"* mwisho wa kumnukuu.... Akimaanisha kwamba _Kwa kila tendo kuna usawa na kinyume cha tendo hilo_ mfano mwenye baiskeli akigongana uso kwa uso na gari, Wote wanaumia sawa japo sisi tutaona wa baiskeli kakanyagwa kanyagwa na kufa...ila kikanuni ya mwendo na gari limeumia sawa na baiskeli.
🗝Sasa katika Ndoa,watu wanasahau kwamba Mwenzako Akiumia moyo wake kwa majeraha uliyo yatengeneza mwenyewe,jua na wewe *Utavuna au utakula sehemu ya maumivu hayo* yeye hawezi umia wewe ukacheka. Kuna vitu utavikosa vya Kihisia kutokana na Kuumia kwake.
🗝Ndiyo maana tunasema katika ndoa,kila mmoja kimbizana na kutafuta namna gani *Uuburudishe moyo wa mwenzako* ili nawe Uburudike.
🗝Ni vigumu kucheka na mtu aliye jeruhika moyo, ni vigumu kutoka out ma mtu aliyejeruhika moyo,ni vigumu kumsifia mtu aliyejeruhika moyo,ni vigumu kufanya mipango na mtu aluyejeruhika moyo,ni vigumu Kushiriki tendo la ndoa na mtu mwenye majeraha ya moyo.( hivyo ni baadhi tu)
🗝Kwa mazingira hayo,Epuka Kumezea,kutemgeneza mazingira ya maumivu kwa mwenzako,na umigundua umemuumiza, Ebu tafuta namna ya kuuganga moyo wake airudie hali yake ya furaha. *_Mwenzako akifurahi,nawe utafurahi,na mtaishi maisha ya Ushindi katika ndoa_*
_Mimi kwa leo niishie hapo niseme kwamba Ndoa ni Tamu kama utaamua wewe uitengenezea mazingira ya utamu,na ndoa ni chungu kama wewe utaamua kuiandalia mazingira ya uchungu_.
*Ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa _Ev Elisha Kazimoto(Psychologist &Counselor_)*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
Friday, 11 October 2019
UKIUMIZWA MOYO,USIJIUMIZE NA WEWE
🖤🖤 *UKIUMIZWA MOYO KATIKA MAHUSIANO, EPUKA KUJIUMIZA NA WEWE*🖤🖤
............................................
*_Na Ev Elisha Kazimoto(Psychologist & Counselor)_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
.................
.................
_Hello Hello vijana kwa mabinti ambao mpo katika safari ya Mahusiano yakuelekea ndoa, na wengine mpo katika Mahusiano yakuelekea katika ndoa, leo nataka niseme nawe kwa ufupi, Lugha hii Tata ya Kisaikolojia ili Nikusaidie Kutoendeleza Historia ya Maumivu katika moyo wako unapoendelea kuishi,lugha hii Niirudie tena, *"Ukiumizwa Moyo katika Mahusiano, Epuka Kujiumiza na Wewe* Huu umekuwa Ugonjwa kwa watu wengi, Je wewe wewe weza kupona Leo?_ Sentensi yangu kwako ni Alama ya ( Rudi nyuma Fikiri kabla ya maamuzi - 🔙)
🔙Kila anayeanzisha mahusiano(anayeingia) Ana matarajio ya kukidhi Hisia zake za Furaha zilizo msukuma kuingia kwenye Mahusiano,japo Anaweza Kushida Kuziongoza Hisia zake zifikie matamanio yake.( *Kosa la kwanza*)
🔙Kila anayeingia kwenye Mahusiano,anaingia na mtu ambaye Anahisi ana vitu au kitu ambacho kwa nafsi yake na hisia zake zilimwonyesha Anaweza Kupata Furaha,na kutimiza ndoto zake za Kimaisha, Japo Anaweza kushindwa Kuusoma Ukweli wa Maneno,matendo ya mwenzake hata kupelekea Mahusiano kuvunjika mapema,au baada ya muda mrefu.( *Kosa la Pili*)
🔙Kila mtu aliyeingia katika Mahusiano na mtu,aliamini huyo ndiye mtu pekee wa Kuzigusa hisia zake na kuleta matarajio yake katika Uhalisia alioutamani tangu zamani, ndiyo maana ukamfuata,au ukamkubali, Japo Waweza Kushindwa Kuchochea Uzuri huo uliouona ili uendelee kutimiza hisia zako,ukapelekea kuachana kwa shari au kwa wema( *Kosa la Tatu*)
🔙Kila mmoja anayeingia katika Mahusiano huwa anaangalia Dhamira yake ilivyo njema,na alivyo sahihi katika Mahusiano na alivyo dhamilia kufikia hatima ya ndoa, Ambapo wengi Usahau na Ushindwa Kutambua Madhaifu yao na Makosa yao yanaweza changia wasifike mwisho wa safari. Kushindwa kujua udhaifu wako katika Mahusiano ni kosa kubwa la kisaikolojia ( *Kosa la nne*)
🔙Kila anayeingia katika Mahusiano Uamini aliyeingia naye katika Mahusiano anauwezo mkubwa wa kumfurahisha na si Kumkosea,Japo watu Usahau huyo naye ni mwanadamu kama wewe anachumba cha hisia chanya na hisia hasi,kwa hiyo jipange ukiingia chumba chake hasi wewe ingia ukiwa chanya, ukiingia chumba chake chanya,wewe ingia ukiwa chanya japo yeye anaweza kuonamo hasi kadhaa. Ukishindwa kanuni hiyo Mahusiano yatavunjika( *Kosa la tano*)
🔙Kila anayeingia katika Mahusiano,Uingia akijiona yeye ndo Mkweli na si rahisi kukosea ila mwenzake ndo si Mkweli na ndo mkosaji, ndiyo maana Wengi wa walioingia katika Mahusiano na kutoka katika Mahusiano (Break up mbali mbali) *Uwalaumu jinsia nyingine,au umlaumu mwenzake* Si Rahisi kusikia Anaanisha Makosa yake yaliyochangia Kuvunjika kwa Mahusiano,ndo maana kumekuwa na mwendelezo wa kuumizwa na huyu, na yule, na yule mpaka unachukia Mahusiano ( *Kosa la sita*) kwasababu Hujijui ubovu wako, udhaifu wako.
⚖ *Laiti ungerudi nyuma Ukajipima kwenye Uzani wa Mahusiano Kisaikolojia,Ungeweza kuendesha Mahusiano yako vizuri na Kutibu Majeraha yako ya Moyo*⚖
🎀Kama Ukijua kuwa Unapoingia kwenye Mahusiano una Hisia za Matarajio yako,lakini na mwenzako ana Hisia za Matarajio yake ambazo hizi zote za wewe kutofautiana,au kulandana,ungeweza kulinda Mahusiano yako kwa furaha, ila kwasababu unatafuta kutimiza hisia zako tu huangaiki na za mwenzako, Break up,kuumizwa kutaendelea mpaka pale moyo wako utakapo Uruhusu kukubali hali zote za Mahusiano.( *Utakuwa umeshinda kujiumiza mwenyewe*)
🎀Siku utapo jua,kitu kizuri ulichokiona kwa uliyempenda huyo,kinahitaji kuchochowa,kuboreshwa,Kulindwa na ukatia bidii kufanya hivyo utakuwa Umezuia Kuumizwa.
👉Lakini pia Ukipenda usiwe kipofu nakiziwi ruhusu macho yako yaone mazuri na mabaya,mazikio yako yasikie ukweli na uongo wake, na Ipe akili kazi ya Kutafsiri kufaa kwakwe na kutofaa kwake na ushugulikie mapema taarifa hiyo kabla ujaumia zaidi. ( kuendelea kujikaza wakati unajua ukweli hamuendi popote ni Kuendelea Kujiumiza wakati umeisha umizwa. ( *Hiyo ndo tiba ya kutojiumiza mwenyewe*)
🎀Wengi wetu katika Mahusiano,tunapenda kufayiwa mema zaidi,ila siyo sisi kuwafanyia mema watu wetu,Ndiyo maana Tukiumizwa nasi tunatafuta mwanya wa Kuumiza, hapo ndo Unazidi kujiumiza mwenyewe. Ikitokea Uliyoyatarajia kwa mwenzako Kuyapata,hukuyapata 🔙Rudi nyuma tazama wapi Wewe Ulikosea,ulichangia katika kuumizwa kwako,Ulishindwa Kuchochea Uzuri wake,uli relax? Ili kama mkiyatengeneza au ukipata mwingine Usiumizwe tena, Usipo Rekebisha kwanza, Utajiumiza mwenyewe tena na tena( *Hiyo ndo tiba ya kutojiumiza mwenyewe*)
🎀Ukitaka Mahusiano yako yaishi, uwe Mwepesi wa Kujua madhaifu yako na makosa yako unayo yafanya katika Mahusiano kwa mwenzako,na uwe mwepesi Kuyakwepa yasiwe yakujirudia rudia,hapo utakuwa Umeshinda Kujiumiza mwenyewe, Usipo jua hilo,utakuwa wakuumizwa kila mtu na utawachukia wanaume wote au wanawake wote kumbe ni wewe unaye jiumiza kila mara baada ya kuumizwa mara moja. ( *Hiyo ndo tiba ya Kukiumiza mwenyewe*)
🎀Usisahau kuwa tuna *Date na wanadamu wenye mapungufu yao, Si malaika* Kwa hiyo uwe Mwepesi kujua kuwa naweza kukosewa,nami naweza Kumkosea,ila kama nimeona uzuri wake unao nifaa,nifanye nini ili nisimpoteze? Punguza kujihesabia haki kila wakati,msaidie ajue udhaifubwake na Kuushinda ( *Tiba ya kutojiumiza*) mbali na hapo Utakuwa unajiumiza mwenyewe kila mara kwa kuona wanaume au wanawake ni Matapeli.
🆒 *Labda nikusaidie Acha Kupandisha Joto lako la Kihisia kwa Kutafsiri vibaya Changamoto yako yakimahusiano*🆒
🆒Kama Uliumizwa, Tulia Usiendelee Kuumiza nafsi yako kwa kuona Wanaume au wanawake wote ni Wasaliti, Hiyo haikusaidii bali Inaua na kutafuna Hisia zako za upendo na furaha,maana kutafsiri kwako huko Hakubadirishi Mapungufu yako,wala hakuondoi Uzuri wanaouona watu walio na Wanawake au Wanaume kwenye Mahusiano yao. Utaumia wewe ila wao wanazidi kufurahi,na ukisema wanawake wabaya au wanaume wabaya *Wanakuona Waajabu*
🆒Ukiumizwa,jua uwenda Huyo hakuwa size yako au Kilikuwa kipimo chako cha ukomavu wa akili ya Mahusiano,usiendelee kulalamikia Kosa lile ulilotendewa, halitakusaidia Kuhurumiwa na watu ili Wajitolee kukuoa au kuolewa nawe ili usiendelee kuumia. Tulia jua huo ulikuwa niukurasa wenye maandishi yake,subiri kurasa ijayo isome kwa utulivu,au iandike kwa utulivu.
🆒Ukiumizwa,Unapo jipanga kuingia kwenye Mahusiano mapya, Usibebe Hisitoria za maumivu yako na kuhamishia kwenye kurasa mpya, Utaumizwa tena, jifunze kuandia mambo mapya kwenye kurasa mpya.
🆒Ukiumizwa usijipandishe joto kwa kwa kujumuisha watu wa jinsia hiyo na kuwaona ni wabovu, wewe ndo *Utakuwa mbovu wa Kupindukia* kwakuwa ujui kila chapter ina sentensi zake,lakini kila mmoja ana Asili yake na uzuri wake na udhaifu wake.
🆒Ukiumizwa Usiape kutoyarudia Mahusiano, Haumkomoi aliyekuumiza, Unajiumiza mwenyewe.... Apa wewe mmwenyewe kutorudia Makosa uliyochangia,na kuboresha uzuri wako.
*_Niishie kwa kusema kwamba, Usipo kuwa mkomavu Kisaikolojia katika Mahusiano,Utakuwamtu wa kujuta katika Mahusiano,ongeza Maarifa juu ya Mahusiano,ongeza ubora wa upekee wako,Hitirafu za Kimahusiano zione darasa la kukomaa Kimahusiano,uta Enjoy Maisha, Hakuna Mtu mbaya katika Mahusiano,ila watu Wanakosa Mbinu sahihi za Kuendesha na Kulinda Mahusiano_*
_Ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, *Ev Elisha Kazimoto*( Psychologist & Counselor)_
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
Wednesday, 9 October 2019
FANYA KAZI NA MUNGU
🛢🛢 *FANYA KAZI KATIKA OFISI SALAMA NA BOSS MWAMINIFU* 🛢🛢
*_Ujumbe huu umeandaliwa na Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto(Mjenzi wa Maisha ya Kiroho)_*
🛢 _Shalom mtakatifu wa Mungu uliye katika ufalme wa Bwana wetu Yesu Kristo, Neema na rehema za Mungu wetu ziwe juu yako. Shahuku yangu leo ni kukufunulia Siri iliyo katika Ofisi ya Bwana Yesu ili unapoamua kufanya kazi katika ofisi hii uwe na Matumaini katika maisha yako kuwa Unafanya kazi katika Ofisi Salama na kwa boss Mwaminifu kwako._
*28 Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Warumi 8:28*
🛢Katika mstari huu,tunapata kuona *Mungu(boss mwenye ofisi) anatoa taarifa kuwa anafanya KAZI pamoja na watu wale wa mpendao* Lakini katika KAZI hiyo wanayoifanya Anawapatia Mema Yote(Mshahara) wale walioitwa Kwa Kusudi lake.
🛢Maisha ya kumtumikia Mungu yamebeba Hatima na Heshima ya maisha yako kama mwanadamu.
*26 Mtu akinitumikia, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.Yohana 12:26*
🛢Kuna siri kubwa katika kuyatoa maisha yako kwa Mungu Umtumikie, ndani yake kuna Neema yaziada asiyokuwa nayo mtu mwingine, hapa amesema BABA atakuheshimu. ( _Neno Heshima hapa linawakilisha maisha yenye Heri,ulinzi,kibali,mpenyo kwako_) Mungu akikuheshimu dharau za wanadamu zinakoma, waliokuhesabia siku za kutofanikiwa wanashangaa kuona zinapita, nawe upo unasonga mbele.
🛢Kila aliyejitia Nia ya kukaa katika Ofisi ya Mungu, maisha yake yalibadirishwa, maana Mungu si dhalimu Akiahidi Kukuheshimu,anakuheshimisha kweli kweli katikati ya mataifa.( Huo ndo uzuri wa Kumtumikia Mungu).
*10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la Bwana, nao watakuwa na hofu kwako. Kumbukumbu laTorati 28:10*
🛢Faida ya Kumtumikia Mungu katika Roho na Kweli,kwa uaminifu mkuu.... Bwana anaachilia Neema yake juu yako,katika ulimwengu wa Roho na katika ulimwengu wa mwili Utukufu wa Bwana,kibali cha Bwana,na Utisho dhidi ya maadui zako unawekwa juu yako.
🛢 *Katika Utumishi wako waweza kukutana na Changamoto nyingi za kukukatisha tamaa,kukurudisha nyuma*
👉Safari ya Utumishi inaweza kuwa na changamoto nyingi za *Usizimie moyo kwa mapito hayo* Unapaswa kujua Nani unamtumikia,nani Alikuita katika utumishi wako huo,huuo ndo wa kumwangalia,huyo ndo wakumsikiliza kila wakati.
👉Yawezekana wengine wakasema *Hukuitwa na Mungu, maneno mengi ya kejeli juu yako,kukudharau, wengine hata kukuwekea Vikwazo vikali ili Kuziba kibali chako,Kuficha Neema yako isionekane kwa watu* Uhitaji kupambana nao,Unahitaji kukaa katika Wito wako na Kumwomba Mungu Neema ya Kuvuka pito lako hilo. *Hakuna kitu kilichowekwa na Mungu ndani ya mtu kinaweza kuzuiliwa na Mwanadamu (Anakuwa anatafuta balaa katika maisha yake na Utumishi wake)*
👉Mtu wa kushindana nawe,pambana nawe katika kuzuia kusudi la Mungu lisitimizwe, Hashindani nawe,hazuii kazi yako, Anazuia kazi ya Mungu, Mungu Akiamua kuingilia kati Ataaibika aibu kuu wakati wewe ukipandishwa.
*_Ninachosema nawe ni Amina na kweli, jambo kubwa jihakikishe je,Umesimama na Mungu wa Kweli? Unatumika bila Hila?_* Tulia kanuni hii itatenda kazi...
*29 Maana wale aliowajua tangu asili, aliwachagua tangu asili wafananishwe na mfano wa Mwana wake, ili yeye awe mzaliwa wa kwanza miongoni mwa ndugu wengi.Warumi 8:29*
*30 Na wale aliowachagua tangu asili, hao akawaita; na wale aliowaita, hao akawahesabia haki; na wale aliowahesabia haki, hao akawatukuza.Warumi 8:30*
👉Huna sababu ya kuumizwa kichwa,kulia na watu Wasiojua *Asili yako,ambao hawakukuchagua,wala hawana uwezo wa kukutukuza* Unahitaji kushikamana na Bwana Anayejua Asili yako, aliyekuchagua kabla haujazaliwa na huko huko akakutukuza.
🛢👉Habari njema kwako mtumishi wa Bwana,ni kwamba kilicho tukuzwa na Bwana hata ungefanya harakati zote za kukichafua,kukizima,kukiharibu Hakizimiki,hakichafuki,wala Hakipotei yeye aliyeanzisha KAZI ndiye anayeitimiza.
*Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu;Wafilipi 1:6*
👉Nikutie moyo,kazi tuliyo nayo ni kubwa na Inachanua,na kwakawaida Mizabibu ikichanua Lazima Vimbweha vidogo vidogo viibuke kwaajili ya kupukutisha Maua yake yasilete matunda,... Hapo ndo Neno la Bwana linasema....
*15 Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua. Wimbo Ulio Bora 2:15*
👉Kwenye maombi yako, shika Mbweha hao wadogo wadogo,(kwanini wameitwa wadogo wadogo,kwakuwa hawana Uwezo wa Kubadiri Hatima yako) Wageuzie hayo yote wanayoyapanga juu yako,na mwambie Bwana lilinde kusudi lako ndani yangu nami nikae katika kusudi lako.
🛢👉Uzuri wa Ofisi ya Utumishi wa Kimungu chini ya Boss wetu Yesu Kristo ni Kulinda Haki za watumishi wake, siku zote ukikaa katika haki na kutenda haki Kusudi la Mungu kwako ndilo litakalo simama daima siyo makusudi ya wanadamu.
*Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.Mithali 19:21*
🛢👉Nimalize kwa kusema kuna faida kubwa kukaa na Mungu vizuri na kumtumikia yeye kwa Uaminifu, *No matter what you are facing, Breakthrough is there* Utapenya kwa Mkono wa Bwana .
*_Ulikuwa na mimi mtumishi wa Mungu, Ev Elisha Kazimoto(Mjumbe wa Matengenezo ya Kiroho)_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
JIKUBALI DADA UMEUMBIKA
💚💚 *NIMEUMBWA KWA KUSUDI JEMA LA MUNGU,WACHA NIJIVUNIE HILO*💚💚
*_Ujumbe huu umeandaliwa na kuletwa kwako na Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto_*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
_Shalom mtu wa Mungu,unaye pendwa na Bwana,leo nataka nizungumze na wewe Dada(Malkia Esta wa zama hizi)_
*Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha. Matendo yako ni ya ajabu, Na nafsi yangu yajua sana, Zaburi 139:14*
💚Nataka nikusemeshe uzuri wako,waweza kuwa umekata tamaa pengine unapoona umechelewa kuingia katika ndoa,au mahusiano yako yanaishia njiani waweza kuwa na maswali nafsini mwako, *_Hivi mimi ni mbaya?, Siwavutii wanaume,au mimi nimeumbwaje?_* Neno la Mungu limetupa jibu wewe Umeumbwa kwa *Jinsi ya Ajabu mno* ambayo Unafaa mbele za Mungu na mbele za Mme wako atakaye kuoa.
💚Unacho paswa kujua ni kuwa Uzuri wako si kwaajili ya wanaume wote, na si wote wa kuuona uzuri wako, na wakiuona wengine *Wasio wako, hawatakupenda bali watakutamani* na wakikutamani watakuchezea na kuumiza moyo wako maana safari yako itaishia kwenye mahusiano si ndoa.
💚Leo na kufundisha Uzuri wako uliowekwa kwenye kwenye chemba ya Moyo wa Mme wako Usiye mjua bado kwa sasa,huyo ndo aliyebeba sura yako,tabasamu lako,chozi lako,furaha yako,huyo akifunuliwa kwako tu *Lazima moyo wako Ulipuke kwa furaha* Na yeye huyo Atakupenda,atalinda moyo wako,hisia zako na huyo ndo atafuta machozi ya mapito yako, na huyo ndo *Atasimulia na kuelezea Uzuri wako* Ulivyo na ndiye ataujua Uzuri wako, hatakama wengine watasema No kwako, yeye atasema Yes, wengine wakikuambia Haufai, yeye Atasema wewe ndo wa Pekee katika wana wake wote.
*Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote,Mithali 31:29*
💚Mwanaume wa aina hii mwenye lugha hii, Atapatikana tu pale utakapo *_Jituliza kwa Bwana,na kuzama magotini kwa maombi na Utumishi mbele za Mungu_* Na hapa ulipo ni mahali sahii pa Kupata waume wema,kwakuwa Tunasema MUNGU NIPE UBAVU WANGU,siyo mazingira,elimu,kabila,baba au mama,tumesema MUNGU,kwa lugha nyingine *Group hili tumejipanga kumtafuta Mungu kwa Bidii mpaka ajibu watu wake* Na tumeona,tunaushuhuda kwa maombi yetu watu wamejibiwa maombi wamepata wachumba sahii na wengine Wamefunga ndoa tiyari... Mungu wetu Anajibu.
*USITISHWE NA UPEPO WA KUKOSA WACHUMBA, AU WENGINE KUKUACHA*
👉Mungu wetu huyu uwa ni Mungu anaye fanya mambo kwa kusudi lake,na kwa wakati wake, wakati unalalamika unasema *WHY ME?* Upande wa pili kuna *Wema wa Mungu ulio kuzunguka na kukuepusha na Majuto makuu* ila hukuona,umeona tu tukio la kuachwa,au kuchelewa kuolewa,kumbe upande wa pili Mungu amekuepusha na *Kuwa mjane ukiwa bado mdogo,Amekuepusha na Divorce katika umri mdogo wa ndoa,Amekuepusha na kuishi wa Migogoro isiyo isha,Amekuandalia mtu wakutimiza ndoto zako za kihuduma,kiuchumi na kimaisha kwa ujumla*
💚Binti yangu, Kila mahusiano Unayopitia ni darasa tosha kwaajili ya maisha yako ya baadaye.
💚Wengine mebeba nafsi za watu wengi maishani mwenu ambao wanahitaji kufundishwa,kushauriwa,kuepushwa katika majanga ya kindoa na kiahusiano, nani awezaye kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkuu wakati hana *History ya Mapito ya ushindi?*
Utawasaidia watu kwa ubora zaidi ikiwa Ulipita na ukashinda..... _You have a living testimony_
*Daudi akasema, Bwana aliyeniokoa na makucha ya simba, na makucha ya dubu, ataniokoa na mkono wa Mfilisti huyu. Sauli akamwambia Daudi, Enenda, na Bwana atakuwa pamoja nawe. 1 Samweli 17:37*
💚Wajuaje wewe ni mtu mkubwa utakaye ponya kizazi cha mabinti wengi wajao nyuma yako, walio nyumbani mwa Bwana? Watoto wako?washirika wako? Wajuaje utakuwa Great Figure in the world utakaye kuwa ukisema na ulimwengu mzima,taifa zima,mkoa mzima, wajuaje utaolewa na mme ambaye ni mtumishi mkuu wa Mungu asimamaye mbele za maelfu wengi?.
💚Mara nyingi tunatishwa na muda wetu ambao kwa mtazamo wetu twa hisi ndiyo sahihi,lakini pamoja na kuona muda wetu ndiyo sahihi, *Sisi kama wanadamu twaona karibu mno* wala hatuyajui ya baada ya dakika moja, lakini Mungu wetu anaona mbali,anajua yote na yote anayotuwazia ni Mema,kwa hiyo *_Anaweza kwenda kinyume na Muda wetu,siyo ili atuumize,bali aulete Utukufu mkuu wa muujiza katika maisha yetu_* ili tuwe na furaha timilifu ndani yake.
1 Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake.
Yohana 11:1
3 Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema, Bwana, yeye umpendaye hawezi.
Yohana 11:3
6 Basi aliposikia ya kwamba hawezi, alikaa bado siku mbili pale pale alipokuwapo.
Yohana 11:6
💚Kuchelewa kwa Mungu kukupa hitaji lako, kwa Tafsiri ya Kiroho, *_Ni Mungu kukuthamini mno nakutaka kukupa kitu bora zaidi_* In fact Mungu achelewi,(hiyo nikatika mtazamo wa Muda wetu)ila katika Muda wa Mungu huo ndo wakati na majira yako yanayo faa kupokea Zawadi hiyo ya Mungu.
💚Wakati mwingine watu wanao tuzunguka wanaweza *Kuwa changamoto,kwa kukukatisha tamaa,au kukupandisha hamasa ya kutaka kuingia katika ndoa kwa namna yoyote* unaona wengine walio chini ya umri wako wanaolewa wanakuacha.... *USI PANIC* Subiri muda wako,huo ni muda wao.... Usifanye maamuzi ya Kubebwa na yeyote, subiri ubebwe na *Mtu maalumu*.
*Kwa nini ni Hofu wakati najulikana na Mungu tangu zamani?*
💚Ni muhimu kulisoma Neno la Mungu na kulitumaini maishani mwako kwakuwa limebeba majibu ya maisha yetu.
💚Huna sababu yakuwa na hofu na kuhisi Umepoteza mwelekeo, _Mungu aliyekuumba,mwenye maamuzi ya mwisho juu ya maisha yako anasema anakujua wewe hata kabla hujazaliwa_ kwa maneno mengine hakuna jipya linalotokea maishani mwako hajui.....
*4 Neno la Bwana lilinijia, kusema, Yeremia 1:4*
*5 Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.Yeremia 1:5*
💚Kukujua kwake,si kwa bure,anasema Anataarifa zako za kwa nini uchelewe,na atafanya nini katika kuchelewa kwako.
💚Mungu Hawi na Taarifa zetu mapema ili Atuchekiiii na kutuacha, Anakuwa na taarifa zetu kwa misingi yakuweka mazingira sawa ya mapito yetu ili Tupate vitu vinavyo tufaa.
💚Uzuri wa pekee wa Mungu wetu ametufanya tuishi maisha ya Historia kwa Mungu,kwetu ni mapya ila kwake ni History, angalia anavyosema.....
9 kumbukeni mambo ya zamani za kale; maana mimi ni Mungu, wala hapana mwingine; mimi ni Mungu, wala hapana aliye kama mimi;
Isaya 46:9
10 nitangazaye mwisho tangu mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado; nikisema, Shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu yote.
Isaya 46:10
💚Kama Mungu anatangaza *_Mwisho wako tangu mwanzo(tangu unazaliwa,tangu unaanza mchakato wa kuomba mchumba)Mungu anatangaza mwisho wako(ndoa ya heshima) kwa hiyo wewe kabla huja kata tamaa Mungu alishatangaza mwisho wako wa utukufu, kazi yako ni Kuvumilia na kumtumaini yeye_* mpaka uufikie Muda wako wa furaha.
_Nimalize kwa Kusema,wewe unathamani kubwa sana machoni pa Bwana,na Hayuko tiyari aone Ukiabika kama mtoto wake,atafanya na mlango wa kutokea ili Uvikwe taji ya utukufu,
*_Unachotakiwa kama Dada wa KiKristo, katika mchakato wa kuielekea ndoa Takatifu uwe na sifa hizi,au fanya haya_*
1⃣Tengeneza Profile ya maisha yanayo someka kwa ubora na sifa njema( Attractive life)
2⃣Ibua vitu pekee ukivyo navyo ndani yako vifaye kwa bidii uwe tofauti na wengine( Be Unique and Potential)
3⃣Hata siku moja Usijidharau ulivyo,thamini nature yako jikubali ulivyo.
4⃣Jijue mapungufu yako uyarekebishe yasiendelee kuwa ukuta,au kuchafua Profile yako ya maisha.
5⃣Mwombe Mungu,mwamini Mungu,Mungoje Mungu wa kwako yupo atakuja kwa wakati.
*NB: _Katika kuomba hakikisha unamwambia Bwana fungua sura yangu katika ulimwengu wa Roho ionekane katika uhalisia wa ulivyoniumba ili mme wangu auone Uzuri wangu ulioniumbia_*
Nikutakie Maombi mema,na matengenezo mema ya maandalizi yakuingia katika ndoa njema ya Baraka.
_Ulikuwa nami mnenaji wa siri hizi Mtumishi wa Mungu, *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist & Counselor)*
Facebook Elisha Kazimoto
WhatsApp 0755444078
Monday, 18 February 2019
MAAJABU 6 YA WANA NDOA
❓❓ *MAAJABU SITA (6) YA WANA NDOA*❓❓
_Haya ni maajabu ya kisaikolojia,waweza yaona ya kawaida ila ndo hivyo kama umekamatwa hapo huwezi kuwa na furaha,kwa namna yoyote unaishi kiugumu ugumu_
1⃣Huwezi mwamini mkeo au Mmeo, ila unakubali kulala naye kitanda kimoja na shuka moja❗
2⃣Huwezi mwambia nakupenda mke wangu au mme wangu, ila Unazaa naye watoto.❗
3⃣Huwezi muaga mkeo au mmeo popote unapo kwenda, ila Unamuomba Tendo la ndoa kwa sura ya upole.❗
4⃣Huwezi ongozana naye,wala kumtambulisha kwa watu kuwa huyu ni mpenzi wangu(wife/husband ),ila unaweza eneza ubaya wake kwa watu na bado mnakaa wote nyumba moja.❗
4⃣Huwezi kukaa na mmeo au mkeo mkazungumza kama marafiki,na kubadirishana mawazo, ila unapenda mkae muda wa kutosha kwenye tendo la ndoa.❗
6⃣Huwezi kumthamini mwenzako kama mtu mwenye umuhimu kwako,dhaifu sana hana uwezo wowote, ila Unamuita Baba/mama wa watoto wako.❗
_Haya yanashangaza sana, na Yajayo yanafurahisha_
*Raha ni kujipa mwenyewe na Stress ni Kujitengenezea*
#Mwanasaikolojiahazeeki.
Sunday, 17 February 2019
WAWEZA KUKAA BILA SEX
*JE, KUNA UWEZEKANO WA MTU MWANAUME AU MWANAMKE KUKAA MUDA MREFU BILA KUSEX?*
_Suala hili hatuwezi lipa jibu ya mtazamo mmoja ili kulipa majibu ya uhakika lazima tuangalie Kisaikolojia linatafsiriwa vipi na kiroho linatafsiriwa kivipi_
✍Kwanza sex ni suala la Kihisia linalo ratibiwa na Hormones ( hisia zinaweza kutibuliwa na mazingira kwa kuona au kushikwa/contacts).
✍Shahuku/uhitaji wa sex kwa mwanaume na mwanamke unatofautiana, Kisaikolojia mwanaume anahitaji sana sex kuliko mwanamke japo( *Kuna wanawake wana kiwango kikubwa sana cha hamu ya sex kama au zaidi ya wanaume*) walio wachache....
✍Ila wanaume wanauwezo mdogo wa kuhimili kukaa bila sex kuliko wanawake kwasababu hawana njia mbadala ya regulation of body kama wana wake isipo kuwa kwenye ndoyo nyevu au wale wanaofanya Uharamu wa Masterbation.
✍Kwanini wanaume wanashindwa kustahimili kukaa bila sex kwa muda murefu? *Ni kwasababu Tamaa yao ipo kwenye Macho, kwa hiyo mara kwa mara wanatibuliwa Hisia zao kwa kutazama* tofauti na wanawake ambao hisia zao Utibuliwa kwa *Kushikwa shikwa na Kusifiwa saana na kwa sauti ya mahaba* jambo ambalo kwa halifanyiki mara kwa mara linatokea kwa nadra kwa muda maalumu. Kwa msingi huo kisaikolojia wanaume Sex kuikwepa ni nadra sana.
✍ *NB: Uwezo wa kijana kukaa bila sex muda mrefu bila shida ni mkubwa kuliko Mwanaume aliyeoa au Yule ambaye alisha onja sex* Aliyeonja sex uwezo wake wa kisaikolojia umeathiriwa kulinganisha na ambaye hajawahi kugusa.
✍ *Kiroho hapa ambapo penye msingi wa usalama kwa watu walio na Mungu* Udhibiti wa miili upo katika Nguvu za Roho Mtakatifu (Wafilipi 4:13....Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.) Kwa maana hiyo kuhimili kutofanya sex si kwamba kunashindikana ila Umeshikiliwa na nini....? Kama umeshikiliwa na Pepo,hisia tabia mazingira hutaikwepa zinaa ila kama Umeshikiliwa na Roho mtakatifu kuna nguvu ya KUSHINDA. Watu waliookoka kweli kweli wanajua Siri hii ya KUSHINDA kama, kiroho hauko vizuri HUWEZI JUA ninacho SEMA.
✍Ila kwa siri hii ya Nguvu ya KUSHINDA tunapewa na Roho mtakatifu ndo maana watu *wanaoa na kuolewa miaka 25,30,35,40 BILA KUGUSA SEX.* si kwamba hawana hisia,hawaoni SITES za kusex,wanaziona ila ndani yao wanapigiwa ALARM NA ROHO WA BWANA.
7 Ikawa baada ya mambo hayo, mke wa bwana wake akamtamani Yusufu, akamwambia, Lala nami.
Mwanzo 39:7
8 Lakini akakataa, akamwambia mke wa bwana wake, Tazama, bwana wangu hajui kitu kilichowekwa kwangu nyumbani, na vyote alivyo navyo amevitia mkononi mwangu.
Mwanzo 39:8
9 Hakuna mkuu katika nyumba hii kuliko mimi, wala hakunizuilia kitu cho chote ila wewe, kwa kuwa wewe u mkewe. Nifanyeje ubaya huu mkubwa nikamkose Mungu?
Mwanzo 39:9
👆👉 Kwa hiyo KUSHINDA kwetu kunatoka ndani.
✍ *NB* KUSHINDWA KWA MTU MMOJA SIYO KWAMBA WOTE WAMESHINDWA.
*_Kufanya sex ni maamuzi na kukaa bila kufanya sex ni maamuzi, na dhambi ngumu kuliko zote na yenye mazingira magumu ya kuitimiza ni sex_*
By Ev Elisha Kazimoto
©2019
Friday, 15 February 2019
KUSANYA YALOYO TAWANYWA
🔺🔺 *MKESHA WA MAOMBI YA KUKUSANYA YALIYO TAWANYWA NA ADUI*🔺🔺
Mnenaji: Ev Elisha Kazimoto
WhatsApp(Anointed)
*0755444078*
.......
.......
*8 Bwana MUNGU, akusanyaye waliofukuzwa katika Israeli asema, Pamoja na hayo nitamkusanyia na wengine, zaidi ya ao walio wake waliokusanywa.Isaya 56:8*
_Haleluya mwombaji na mtu unaye utafuta uso wa Mungu daima, ni haki kwetu kukutana na mahitaji yetu tuyaombayo mbele za Bwana_
✍Kila anayeingia katika maombi anapeleka haja za moyo wake kwa Bwana( HOJA ZENYE NGUVU) na Bwana ameahidi kutimiza,au kutupa matakwa yetu.
✍Tunapo zidi kumwomba Mungu juu ya *Safari yetu ya mwaka huu* kuna kazi moja na ya msingi tunahitaji kuifanya katika maombi yetu, nayo ni *Kuomba maombi ya Kukusanya Maishani mwetu*
✍ Yaliyo kusanywa ni maisha ya ushindi, maisha yenye kibali cha Bwana na utukufu,ni baraka zako ziko kapuni mwako lakini zikitawanywa shida inaingia katika mfumo wa maisha yako.
✍Angalia kwa nini tuombe maombi ya KUKUSANYA.
1⃣Ndoa ikitawanywa, amani inatoweka na migogoro inaingia(migogoro ya mahusiano,uchumba na ndoa ni matokeo ya Adui kutawanya Upendo kati yenu).
2⃣Uchumi ukitawanywa, maangaiko na madeni yasiyoisha na yasiyo na sababu yanaingia na Umaskini unajenga makao.
3⃣Elimu yako ikitawanywa,nguvu ya ujinga,kufeli inangia na matokeo yako ya kitaaluma yanadorola.
4⃣Kanisa likitawanywa, Migogoro,mafarakano,malumbano yanaanza, huduma za kiroho zinaanza kuwa KAVU,ibada zinasuasua,watu kurudi nyuma kiimani,watu kutookoka,lakini Mpenyo wa Kiroho na hali ya ulimwengu wa Roho wa kanisa kutokuwa swari.
✍Kumbuka, Adui ushugulika na ulimwengu wa roho kutawanya vitu *Vilivyo kusanywa na Maishani mwako* akifanikiwa kutawanya matokeo ndo yanaonekana huku katika ulimwengu wa kawaida hali kuwa Mbaya.
✍Sasa kama wana wa Mungu,wana maombi, *Wana wa Vita* Usiku wa Leo tusimama kwa Neno la Bwana kama alivyosema kwenye Neno lake, *_Anakusanya waliofukuzwa,na siyo hao tu atakusanya na wengine/mengine yaliyo zaidi ya hayo yaliyo kusanywa_* hiyo ndo kazi ya Bwana tukimwomba.
🤝Tunashimana,kama wana Kanisa,wana Ndoa, Wachumba,wana Familia, tunasema _Bwana Yesu wewe ni Bwana wa Utosherevu,adui ametawanya mambo yetu mengi,na mengine anawaza kuyatawanya,ila leo kwa Mamlaka ya Jina la Yesu Tunakusanya,tunaleta karibu,tunarudisha mahara pake,tunaita Kila kilicho tawanywa,rudi mahara pake kwa jina la Yesu,tunafunga njia zilizo tumika na zinapangwa kutumika kutawanya maisha yetu kwa damu ya Yesu,naifungua njia ya Bwana ya kukusanya mahitaji yangu(yetu), na Bwana Anikusanyie *Na zaidi ya hayo yaliyo tawanywa* ili maadui zangu waone kuwa nimejazwa,nimetosheka na msifu Bwana katika jina la Yesu,Leo na Kesho Bwana atakusanya na kutawanywa Kumekoma katika jina la Yesu AMEN_
✍👆Ikiwa umeomba maombi haya kwa Imani amini kuna vitu mbingu zinaanza kushugulika kwaajili yako Kukusanya na kukufunika kwa utukufu mkuu.
*USIACHE KUOMBA,OMBA UKIKUSANYA WIKI HILI LOTE*
_Ulikuwa nami mnenaji wa SIRI za Bwana wa Majeshi EV Elisha Kazimoto(Anointed)_
*WhatsApp 0755444078*
©2⃣0⃣1⃣9⃣
OMBA BWANA AKUFICHE
🖥 *MKESHA WA MAOMBI YA KUOMBA KUFICHWA NA BWANA MBALI NA MIPANGO YA SIRI YA MAADUI ZETU*🖥
*_Mnenaji: Ev Elisha Kazimoto(Anointed)_*
WhatsApp 0755444078
.........
.........
_Shalom mwombaji,ni wiki lingine tunaendelea na vita,tunajipanga kwa safu mpya kila wiki Bwana anayo siri ya kutupa kuwaendea maadui zetu na kuwashinda na kuziteka baraka zetu. Leo twende *Mafichoni pa Bwana* huko kuna usalama mkuu.
1 Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu; Unilinde uhai wangu na hofu ya adui.
Zaburi 64:1
2 Utanificha mbali na shauri la siri la watenda mabaya, Mbali na ghasia ya watu wafanyao maovu;
Zaburi 64:2
3 Waliounoa ulimi wao kama upanga, Wameielekeza mishale yao, maneno ya uchungu,
Zaburi 64:3
4 Wapate kumpiga mkamilifu faraghani, Kwa ghafula humpiga wala hawaogopi.
Zaburi 64:4
5 Walijifanya hodari katika jambo baya; Hushauriana juu ya kutega mitego; Husema, Ni nani atakayeiona?
Zaburi 64:5
6 Hutunga maovu; husema, Tumefanya shauri kamili; Na mawazo ya ndani ya kila mmoja wao, Na moyo wake, huwa siri kabisa.
Zaburi 64:6
7 Kwa hiyo Mungu atawapiga shabaha, Kwa mshale mara watapigwa.
Zaburi 64:7
👉👆Maombi ya Daudi,ilokuwa ni kumsihi Bwana asikie sauti yake. *_Ndugu yangu ni kwambie siri moja, hakuna mwanadamu wa kusikiliza sauti yako na malalamiko yako muda wote, ni Mungu tu wa kuomba asikie Sauti yako_*
👉Mara ngapi sauti yako imesikika mbele za watu uliowategemea lakini hukuona jibu? Mwambie Bwana leo naomba usikie sauti yangu.
👉Lakini mstari wa 2, Daudi anaomba kwa Bwana *Amfiche mbali na mashauri ya siri ya wabaya* Ndugu hujawahi kujua ya kuwa kuna wanaokupangia mipango Kinyume nawe unavyotamani kuwa?
👉Mipango ya siri ina lenga kukwamisha, kuua,kudhohofisha,kuteka,kuaibisha,kuangusha ndiyo maana inapangwa kwa siri,na inapangwa na watu wabaya na waovu.
👉Wakiwa katika mikakati na kupanga *_Kuua uchumba wako, uzao wako,ndoa yako,biashara yako,elimu yako na Huduma yako,kanisa kako_* sisi usiku huu nasi tunamwomba *Baba wa miujiza,mkausha bahari,mtuliza Dhoruba,tunamwambia TUNAOMBA UTUFICHE mbali na mipango yao miovu juu yetu mwaka huu* hapo ndipo tutakuwa tumewashinda ushindi wakishindo.
👉Kufichwa ni kuhifadhiwa,kutunzwa,kwa matumizi ya sasa na ya baadaye, kilicho *Fichwa* ni kazi kukipata mpaka aliye kificha akwambie nimekificha eneo hili.
👉Mungu anapo tuficha,anawafanya maadui zetu wapoteze muda wakitutafuta,wakati wanaangaika na Kujua tupo wapi,sisi tuko Safari ya mbali.
👉Unaonaje familia yako, kazi yako, huduma yako,mambo yako viwe mevikwa vazi la Maficho na Bwana, halafu maadui wanaangaika kuvipata wanakupita tu hawavioni,wanajikwa na kuanguka wee unasonga kwa ushindi,unatamani Yesu asirudi mapema..... *Ebu tuombe pamoja leo Nguvu ya maficho ya Bwana* Hatuhitaji kuwa wazi kwa adui zetu mwaka huu, tunamambo mengi ya kufanya watatuchelewesha.
" _Bwana Yesu weeni Bwana wa usalama,nakuja mbele zako,na vitu vyangu vyote,na maisha yangu yote na kuomba nifiche pamoja na wote walio nami, nisionekane mbeleya watesi,mashauri yao ya siri yashindwe kutekelezwa, mkono wako unitegemeze niwe salama,katika jina la Yesu AMEN_"
*Mnenaji alikuwa mimi mjumbe wa Bwana: Ev Elisha Kazimoto(Anointed) WhatsApp 0755444078*
©2019
Wednesday, 30 January 2019
MIAKA YA KUCHANUA NA KUSINYAA
_Swali: Kwa nini wadada ambao uwakataa watu waliowachumbia,wakikaa bila kuolewa uwarudia na kuomba au kutengeneza mazingira ya kurudiana?_
Anajibu: Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto(0755444078)
*HAPA KUNA MAMBO MAKUBWA 2 YA KUANGALIA, KISAIKOLOJIA NA KIROHO*
👉Kuolewa na kuoa ni jambo la kiroho na kisaikolojia linaloenda na muda na kusudi.
👉Nianze na KISAIKOLOJIA.
👉Nikizungumza kisaikolojia najifanya kama kiroho sijatazama,ila mwisho nitayaunganisha nikisha chambua na kiroho.....
1⃣Kuoa na kuolewa kisaikolojia kunaenda na muda na mvuto wa hisia.....
1⃣Miaka 15-18, wadada wanakuwa wanapenda sanaa jinsia ya kiume(au mapenzi) hapa ni shida kwa wazazi yaani binti anafukuzia wakaka anaye hisi anampenda, hapa ndo unakuta mtu ana marafiki wa kiume hata 10,au wapenzi 10 na wore anawamudu.
2⃣miaka 19-25 anaanza kujiona mzuri sana anavyopendwa, hapa anakuwa na majibu ya dharau maana muda huu anamvuto mkubwa wa sura,kimaumbile (shape imekaa sawa) Anaanza kuchambua wanaume wapi wa kumuoa na hapa anapandisha vigezo vya mtu wa kumuoa,vigumu gumu na kujiona kama Malkia wa dunia, wanaume wote wanamtazama yeye tu.
Na hapa ni muda wa foleni ta wanaume kumchumbia, mambo yanageuka hapa Wanaume wanatiririka kumchumbia,kumtongoza wamchezee, siyo yeye kuwatafuta.( *Huu muda binti anahitaji kuwa makini sana, maana kwenye foleni inayokuja waweza poteza hata wa kwako) maana kipindi hiki ndo wadada ukataa kila mwanaume, anaye mkubali ni *Kwa kumtega kuona kama atakidhi vigezo vyote,siyo baadhi vyote*(Hapa wadada ujiona bado wadogo na wana take headlines za wavulana)
3⃣miaka 26- 30 wadada kama hana mchumba maalumu wanaanza kushtuka shutuka, kupunguza vigezo vyao, *Foleni ya wanaume inaanza kupungua* Muda huu uanza kujiona wamekuwa,uanza kuogopa kusema umri wao halisi, uanza kutafuta no au mwasiliano ya wanaume waliowahi mcuumbia kujua kama ameoa tayari, anaanza kutafuta urafiki kama kipindi cha miaka 15-18.
4⃣31-40 hiki ni kipindi kigumu sana kwa wadada, foleni za wanaume Ukata kabisa,mvuto aliokuwa nao mwanzo uanza kupotea, suraya kukomaa uanza kutokea,wamaume(vijana uanza kumpita mbali,anaanza kuheshimia kama mtu mzima., uanza kujilaumu, upunguza vigezo vyote ubakiza kigezo 1 tu cha awe ni MWANAUME aliyeokoka, wengine ubakiza mwaume tu.
👉Muda huu niwaupweke,wa kuomba sana mme,uanza kujutia makosa aloyafanya ya kukataa wanaume.
5⃣Miaka 40 kuendelea....muda huu niwakusuburia Neema za Mungu na Muujiza wa Bwana, saikolojia inakuwa imeisha koma kufanya kazi.
👉Kwa Upande wa Kiroho, ndoa inaenda na muda wa kusudi ka Mungu, kwa hiyo nimuhimu kukaa na Mungu vizuri,ili foleni ya wanaume inapokuwa nyingi,ujue nani kakusuduwa na Mungu au hayupo. Ukilitupilia mbali kusudi la Mungu akipita ndo imetoka hiyo,itakugharimu sana kumtafuta Mungu akutengenezee ubavu wako tena,au na mwanaume kule afungwe mje kukutana ukubwani huko.
*_Kwa hiyo kinacho sababisha kukaa wadada bila kuolewa kipo kiroho na kisaikolojia_*
By Ev Elisha Kazimoto(Anointed)
WhatsApp 0755444078
©2019
Friday, 25 January 2019
HUWEZI BADIRISHA NAFASI YANGU
🛤🛤 *MAOMBI YA KUZUIA MAADUI KUBADIRISHA BARAKA ZAKO MWAKA HUU*🛤🛤
_Mkesha Wa Maombi ya Nguvu ya Kuporomosha Nia Ovu ya Maadui dhidi yako katika Mwaka huu wa Baraka_
*Mnenaji: Ev Elisha Kazimoto(Anointed)*
WhatsApp 0755444078
.................
.................
8 Israeli
wana wa Yusufu, akasema, Ni nani hawa?
Mwanzo 48:8
9 Yusufu akamwambia babaye, Hawa ni wanangu, Mungu alionipa hapa. Akasema, Tafadhali uwalete kwangu nami nitawabariki.
Mwanzo 48:9
13 Yusufu akawaweka wote wawili, Efraimu katika mkono wake wa kuume, kuelekea mkono wa kushoto wa Israeli; na Manase katika mkono wake wa kushoto, kuelekea mkono wa kuume wa Israeli, akawasogeza karibu naye.
Mwanzo 48:13
14 Israeli akanyosha mkono wake wa kuume akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, huku akijua atiavyo mikono; maana Manase ndiye aliyezaliwa kwanza.
Mwanzo 48:14
15 Akambariki Yusufu, akasema, Mungu ambaye baba zangu, Ibrahimu na Isaka, walienenda mbele zake, yeye Mungu aliyenilisha, maisha yangu yote, hata siku hii ya leo,
Mwanzo 48:15
16 naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Ibrahimu na Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.
Mwanzo 48:16
17 Yusufu alipoona kwamba babaye anaweka mkono wake wa kuume juu ya kichwa cha Efraimu, ikawa vibaya machoni pake. Akauinua mkono wa babaye auondoe katika kichwa cha Efraimu, ili auweke juu ya kichwa cha Manase.
Mwanzo 48:17
18 Yusufu akamwambia babaye, Sivyo, babangu, maana huyu ni mzaliwa wa kwanza; weka mkono wako wa kuume kichwani pake.
Mwanzo 48:18
19 Babaye akakataa, akasema, Najua, mwanangu najua, yeye naye atakuwa taifa, yeye naye atakuwa mkuu; lakini ndugu yake mdogo atakuwa mkubwa kuliko yeye, na uzao wake watakuwa wingi wa mataifa.
Mwanzo 48:19
🛤Kuna wakati unahitaji kusimama katika nafasi yako kwenye Maombi kushugulikia Nguvu za maadui wanao Kusudia mabaya katika maisha yako, _Kuwazuia wasibadirishe mpango mzuri wa Mungu kwako_
🛤Siri moja ni hii, kila mmoja Mungu anao mpango mzuri kwake, ziko packages za baraka kila msimu,kila mwaka ambazo Mungu anaziachilia kwenye ulimwengu wa roho zikupate katika ulimwengu wa mwili.
🛤Ila kuna mchezo mchafu waweza fanyika katika ulimwengu wa roho na hata katika ulimwengu wa mwili Shetani kwa kutumia mawakala wake na watu, *Wenye Nafasi* iwe ofisini, iwe kwenye biashara, elimu,Kihuduma, kijamii *Watumike kubadirisha baraka zako* Lakini Habari njema kwa Watu wamtumainio Mungu ni kwamba, *_Harakati zote za siri na za Wazi Haziwezi fanikiwa kwakuwa Mkono wa Bwana uko juu yako hakuna wa Kuubadirisha_* Na leo tunasimama kwenye Maombi kuwa piga hao walioshikilia mpango Ovu juu yako ubatirishwe na Bwana wa Majeshi.
🛤Yusufu hakujua kuwa Efraimu *Tayari ana Alama ya Mungu ya kubarikiwa* akataka abadirishe mbaraka wake, Akamweka Mkono wa Kushoto kwa yeye abarikiye(Yakobo) na Manase akamweka mkono wa Kuume akijua huyu ndo anastahiri kubarikiwa.....Sikiliza mawazo ya wanadamu na kutazama kwa wanadamu Si kama Mungu aonavyo, Yakobo akiwa katika Roho *Alizuia Mission ya Yusufu ya kumbadirishia Efraimu baraka zake* Nami nataka nikwambie Kwa Maombi haya ya leo Tunaharibu Mission ya Maadui ya kujaribu kubadirisha baraka zako, Ndoa yako,uchumba wako, uchumi wako,elimu yako na Huduma yako, katika jina la Yesu watakomeshwa wao na mwisho itakuwaaibu yao.
🛤Sikiliza mtu wa Mungu,sijui kama *Efraimu alikuwa anatambua anachokifanya baba yake Yusufu* lakini alitulia( Tunahitaji Kutulia kwa Mungu acheze game na maadui zetu) Alisha sema Hakuna Hila ya ya mwanadamu itafanikiwa juu yako,ni kusudi la Mungu ndo litakalo fanikiwa.
*Mna hila nyingi moyoni mwa mtu; Lakini shauri la Bwana ndilo litakalosimama.Mithali 19:21*
🛤Kataa hila juu yako kufanikiwa kwa jina la Yesu, mwambie Bwana kusudi lako litimizwe kwangu mwaka huu.
🛤Ujasiri mkuu tulio nao ni kwamba, Mkono wa Mungu ukinyooshwa juu yetu hakuna mwanadamu wa kuurudisha nyuma, *Watatumia Mbinu zoote wazijuazo kukudhohofisha, hawatafanikiwa* Neno hili ni Hakika ni amina na kweli atatutetea kwa mkono wake wa nguvu.
24 Bwana wa majeshi ameapa, akisema, Hakika yangu kama vile vilivyoazimia, ndivyo itakavyokuwa; na kama nilivyokusudia, ndivyo itakavyotokea;
Isaya 14:24
27 Maana Bwana wa majeshi amekusudia, naye ni nani atakayelibatili? Na mkono wake ulionyoshwa, ni nani atakayeugeuza nyuma?
Isaya 14:27
🛤Tunapo funga mwezi huu kwa maombi,tunamwambia adui,na wanadamu wote waliokubali kutumika kama mawakala waadui,kuwambia *Pisha njia katika mwaka huu,Usiangaike kushikilia Kibali changu,Nafasi yangu,Uchumi wangu,Huduma yangu Uzao wangu....Mungu atakapo Ipinga Hila yako Utaumia* Huu ni Usiku wakutanga Maachilio katika ulimwengu wa Roho juu ya maisha yetu katika mwaka huu.
🛤Yakobo akamwambia Yusufu Mchezo unao ucheza juu ya Efraimu Naujua,unakusudia awe mdogo ila ndo Atakuwa mkubwa,na Manase unaye mwazia awe mkubwa ndiye atakaye kuwa mdogo..... *NAJUA NIWEKAVYO MIKONO JUU YAO KUWABARIKI*
🛤Unacho hitaji kama mwana maombi na mtu wa Mungu ni kuzingatia mambo makubwa 3 maishani mwako:
1⃣Jitambue na jihakikishe Uko sawa na Mungu,unaotaka nini maishani mwako,una nini maishani mwako kama Neema ya Mungu ndani yako.
2⃣Jitenge na Uovu(usimkose Mungu)lindi uchaji wako kwa Mungu hiyo ndo nguvu ya kuwasambaratisha wenye hila juu yako.
3⃣Kaa kimya(Zama kwenye maombi)usipambane na watu kimwili pambana nao katika maombi ushindi wetu unaanzia kwenye ulimwengu wa Roho. *Yuko Bwana wa Kumkemea adui yako* na Baraka zako zikakukalia daima, na lile uliloandikiwa na Bwana likatimia kwako.
*_Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu.Mwanzo 31:42_*
_Nimalize kwakukutia moyo wewe mtumishi wa Mungu ,ondoa Hofu na Mashaka kuhusu Kesho yako,anaiangaikia Bwana,haijalishi Vitawekwa Vigingi vingapi mbele yako,haijalishi ni kwa muda gani umepambana ila uoni mpenyo, saa yako ikaribu,na mwaka huu tunautangaza kuwa wa Bwana kutimiza,kulinda heshima yetu Kazi yetu ni Kukaa vizuri na Mungu,kumtafuta uso wake, Baraka,nafasi za wana wa Mungu wenye chapa ya Mungu malongo yao Hayafungwi na mtu yatakuwa wazi Daima,wanao angaika kukufungia Wanapoteza muda wao bure wewe ni Mzao wa Kifalme, Taifa takatifu la Mungu Ulinde Uraia wako wa Mbinguni Ushindi Nilazima, *Huu ni Mwaka wa Bwana Kutufanyia Nafasi na Kutuzidisha sana* Inuka acha kulia,acha kusononeka uwe kama Efraimu, uwe kama Yakobo, uwe kama Daudi na wengine waliotetewa na Bwana_
*_Nakutakia Mwaka wa Ushindi na mwezi mwingine wa kuuendea Muujiza na Nafasi yako katika jina la Yesu. Amen. By Ev Elisha Kazimoto(Anointed)_*
WhatsApp 0755444078
Monday, 21 January 2019
UFUNGUO WA 8
🔑🔑 *Ufunguo wa 8: Nahitaji Kujiona Sura yangu ndani ya moyo wa Mke au mme wangu*🔑🔑
_Huu ni mwendelezo wa Funguo 12 za ndoa yenye Furaha na Amani,ukiwa na mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa na Mwanasaikolojia *Ev Elisha Kazimoto(Anointed)* WhatsApp 0755444078_
🔑Kuna vitu vinasahaurika kwa watu kwakuwa wanaviona si vya muhimu,na kuna mambo yanajengeka mioyoni ambayo hayakutarajiwa, lakini yote ni kwa sababu kuna kitu kimoja cha Kisaikolojia kimepigwa teke na wahusika aidha kwa kutojua,au malezi au mazingira yamewafanya wajivue ufahamu wa kufanya yaliyo ya msingi na washikilie yasiyo ya msingi.
🔑Furaha ya ndoa Siyo Muujiza,ni *Mchakato wa Hiyari* wa kutumia akili na maombi(kwa wale wanaoamini katika Mungu).
🔑Umewahi kujiuliza kupindi *Mnachumbiana na huyo mwenzako* moyoni mwako na akilini mwako kulikuwaje? Kulikuwa *Kumejaa Sura yake* ndiyo maana mawasiliano ya barua,ya simu,ya kutafuta kuonana yalikuwa makubwa na ya mara kwa mara sana, angaiko la moyo Usipo muona au Kusikia sauti yake kwa muda lilikuwa linakutokea. Kilicho kuwa kina fanya hayo yote ni SURA YAKE ILIJAA MOYONI MWAKO, NA YAKO ILIJAA MOYONI MWAKE.
🔑Kilicho sababisha sura yake ijae kwako na yako ijae kwake ni nini? *Jibu rahisi sana, ni Kila mmoja alikuwa anatafuta kufanya kile anacho hisi mwenzake atapendezwa nacho, na kujizuia kufanya kileambacho anahisi kitamuumiza au muudhi mwenzake.* Ila kwa sasa Sura ya mwenzako Imefutika moyoni mwako au sura yako imefutika moyoni mwake, na kama ipo basi *Haionekani vizuri ina kivuli vuli* kwa nini? _Kwasababu, haujali tena Hisia za kufurahi au kuchukia kwa mwenzako_ bali unafanya unalo hisi una utashi wa kulifanya, unasema bila kujali kama lugha hiyo ni tamu kwa mwenzako au ni chungu,inajeruhi au inaganga moyo wake.
🔑Ila ujue sura yako ikifutika ndani ya mwenzako jua *Hamtokuja kutulia kwenye Ndoa, migogoro itapoa mwezi, ujao inaanza,mwaka, ujao inaanza....* Nini mwenzako HAJIONI SURA YAKE NDANI YAKO
🔑Kulinda Furaha na Amani ya ndoa yako hakikisha unatumia ufunguo huu, *Nataka nijione Sura yangu ndani yake* ukimwangalia unaona *_Huyu ndo chaguo sahii langu, huyu ananifaa, Nisinge mpata huyu nisinge fanikiwa,amenisahaurisha machungu yangu_* Usipo ona hayo utaona Neno kubwa jeusi kwenye Paji la Uso wake linalosomeka hivi... *"Laiti ningejua Nisinge Mchagua huyu"* Sura hiyo ikisha someka moyoni mwako mtaishi ndani kwa Maigizo bila Matumaini.
_Ndoa ni yako tu haina jirani wa kukubebea, ifanye uonavyo vyema waweza ifurahia_
*By Msaikolojia na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto (Anointed)*
WhatsApp 0755444078
©2019
Saturday, 19 January 2019
AINA ZA MAHUSIANO 5
💝💝 *UKIANZISHA MAHUSIANO HAKIKISHA UNAJUA HATIMA YAKE KWANZA*💝💝
_Uko Nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa na Mwanasaikolojia *Ev Elisha Kazimoto*_
WhatsApp 0755444078
.........
.........
Leo nipo kutibu majeraha ya Stress zisizo za Lazima zinazotengenezwana ukosefu wa Maarifa ya Saikolojia ya Mahusiano. *Special kwa Vijana wakike na wakiume* mlio katika Mahusiano na mtakao anzisha Mahusiano.
✍Unapo anzisha Mahusiano na mtu, jambo la kwanza *Hakikisha unajua haya mahusiano ni ya nini? Hatima yake niya nini?* Kujua ahatima ya Mahusiano yako itakusaidia kujipanga, kupalilia Mahusiano au Kuvunja Mahusiano yasije kukuletea Stress za bure na kuku haribia Sifa,muda na Malengo.
✍Zipo aina za Mahusiano yanayo anzishwa kwa lengo husika, ni muhimu kujua: *Kijana Sikia,Binti tulia kwa makini* usipo kuwa makini Utaishia kuumua na kulaani wakaka au wadada.
1⃣Mahusiano ya Kujioyesha.( *Show up*) _Haya haendi popote ni kwaajiliya yakujionyesha kwawatu kuwa nawe una mtu wa kukuweka busy kimahusiano_
👉Mahusiano ya mitoko zaidi, story nyingi, *I love you* nyingi ila HAKUNA NDOA.
2⃣Mahusiano ya Kutojiamini( *Partial Relationship*) _Mahusiano haya niya kupotezeana muda, mwanzilishi wa mahusiano,au aliye katika uhusiano Hana uhakika kama aliye naye ndo chaguo sahihi lake_ kuna wakati anaonyesha kuwa ndo yeye chaguo,kuna wakati anakuwa na wasiwasi anajivuta kama anataka asitishe ila anakosa namna ya kusitisha. *Mahusiano haya Uishia na ukaa kwenye lugha za I love you tu* hakuna Step yakuonyesha Kuna sehemu tunaekekea,umebaki muda flani tuoane, kila siku nikama ndo naanza Mahusiano.( WAWEZA ZEEKEA HUMUBIKA NDOA) lugha ni nzuri ila vitendo hewa.
3⃣ Mahusiano ya Ngono( *Sexual Relationship*) _Mahusiano haya yanadumu kwa kupena sex,lakini utumika lugha ya tutaoana kwakuwa nimejua uzuri wako,radha yako sitakuacha,lakini ukweli wake, pale mdada anapo onyesha kuhutaji Engagement kijana umzungusha,ndipo vituko uanza hata kukata mawasiliano,matusi ya uzembe wa sex uanza na hamu ya kijana kuingia katika ndoa uisha._ Hapa kama ni kijana atamtumia binti sana ila ndoa atakwepa kwepa.
4⃣Mahusiano ya Kitoto( *Childish Relationship*) _Mahusiano haya wahusika ni kama watoto wanaochezea tope na mikojo,wanatumia gharama,zawadi,muda,kuitana majina ya Mtarajiwa,kuambizana nakupenda lakini wanaweza maliza hata miaka 5 *Hakuna hatua,mipango maalumu inayoonyesha wanaingia kwenye ndoa lini* hawauishia kuachana huku wakipendana baada ya kuona muda unasonga ila hakuna dalili ya ndoa._
5⃣Mahusuano ya Ndoa ( *Marriage Relationship*) _Haya ni Mahusiano muhimu,yenye mipango,yenye malengo,yenye heshima,yenye kulinda hisia,yenye kulinda heshima,na yenye kumtanguliza Mungu_ Hapa muhusika Kijana *Utoa mwelekeo wa kuekekea ndoa* uonyesha harakati za michakato mahususi ya kuingia katika ndoa. Wakati huo huo mdada umtia moyo mwenzake,na kumwonyesha ushirikiano wa namna inavyowezekana kuifikia ndoa.
*_Kwenye Mahusiano haya wote wanakuwa wanataarifa wako wapi,wafanye nini na lini wanaingia kwenye ndoa_* wanakuwa na ujasiri wote wakuelezea Uhai wa mahusiano yao na Nia yao, mawasiliano yao yako juu.
NB: _Ukiona unapata ukakasi,utata wa kuelezea uhai,uimara wa mahusiano yako, jua mahusiano yako hayapo no 5,yatafute no 1 hadi 4._
*_Ulikuwa nami mchambuzi wa masuala ya Mahusiano na ndoa Mwanasaikolojia Ev Elisha Kazimoto(Anointed)_*
WhatsApp 0755444078
©2019
Wednesday, 16 January 2019
KUOANA NA MROMANI HAPANA
ππ *Swali: Me nilikuuliza kwamba ni sahihi mfano mtu kama mim nimkristo niliye okoka kuolewa na mroma au katoliki namaanisha*ππ
........
........
Anajibu Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto(Anointed)*
WhatsApp 0755444078
*SWALI LA WAZI LA KIIMANI NAMI NITALIJIBU KWA WAZI KIIMANI SIKISAIKOLOJIA*
_Wapendwa kuna wimbi kubwa na la kutisha katika kizazi cha sasa cha KUPANDIKIZA MACHOTARA wa Kiroho(Spiritual Mulattoes) Negro Christians who has double sides in faith, because of seeking Marriage_ sasa nitegee sikio nijibu kwa uwazi mkubwa sawa sawa na muuliza swali alivyo uliza.
π Note: Sipo kukwambia dhehebu lako ni mbaya au ni nzuri, ila ni uchambuzi wa swali kwa Kadri ya muuliza swali ila kupitia uchambuzi huu waweza PONA na ukasimama na Mungu.
*Fuatana nami Mchambuzi Ev Elisha Kazimoto(0755444078)* Utaweza kufunguka na kupata ufahamu juu ya maamuzi yako.
1⃣Kwanza tuelewe ( *Wale mliookoka, si kwa usanii na kivuli*) Ndoa ni Mpango wa Mungu na mwanzilishi ni wa ndoa Ni Mungu mwenyewe ndiye anayetoa KIBALI cha kuoa au kuolewa tukimwomba,tukikaa sawa naye... Siyo harakati zetu za kujitafutia mtu tunayeoana anaweza timiza ndoto zetu za maisha, Ila _Mungu anatupa mtu wa kutimiza kusudi lake kwenye maisha yetu._
18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
Mwanzo 2:18
ππ Mungu ndo wa kwanza kuoana Uhitaji wa ndoa kwa mwanadamu,si mwanadamu kuona uhitaji wa ndoa kabla ya Mungu ( *Hapo ndo tunaingiaga kwenye mfumo wa zoazoa yoyote*) ilimradi Anaweza kidhi Matarajio yako si Mapenzi ya Mungu ( *Ndo chimbuko la kuzoa Imani nyingine tofauti na yako, au kuiacha imani yako ili uoe au uolewe*)nayo hii ni Laana ya Kizazi cha sasa.
2⃣Pili,Mungu kusema atafanya msaidizi wa kufanana naye alikuwa anamaana kubwa ya kiroho na kiusalama, kuepusha mgongano wa Kiimani,Kufyonzwa nguvu za kiroho, Kuiandama miungu mingine badala ya Mungu aliye hai, Kuepusha kuzaa Machotara wa Kiroho wasio na upande wa kusimamia kiimani.
*_Kauli ya Mungu tangu zamani ni kutembea na kubariki watu watakao weza kuwafundisha watoto wao Imani ya Mungu wao Mungu wa Isaka na Yakobo_* sasa ninyi mlio imani Tofauti by NATURE mtawarithisha watoto wenu nini?
siku ile uliyosimama mbele za Bwana wako huko Horebu, Bwana aliponiambia, Nikusanyieni watu hawa, nami nitawasikizisha maneno yangu, ili wajifunze kunicha mimi siku zote watakazoishi duniani, wakapate na kuwafundisha watoto wao.
Kumbukumbu la Torati 4:10
ππ Si kwamba tunakataa Kuoana na Imani zingine kwasababu ya dhehebu,kwasababu ya uimbaji na kucheza ni *Kwa Maslahi ya Imani yako na watoto wako* Kama wazazi mna mashina mawili tofauti ya Imani,nani atawafundisha watoto niia ya Bwana? Wakati Malezi ni ya Pande mbili baba na mama walio mwili mmoja? Wakati kila mmoja wenu anaona imani yake ndo bora?
πBiblia imesema mlee mtoto katika njia ipasayo naye hata iacha hata atakapo kuwa mzee... Sasa mnalea mtoto kwa Imani ipi( kulingana na muuliza swali *Imani ya Kipentekoste/Kilokole au Kiromani?*) au unataka kusema mmoja ataamua kubadirika kumfuata mwingine... Kubadiri Imani kwaajili ya ndoa ni sawa na Kupata mtiani mark 10% wewe ukajiongezea 0 ikawa 100% halafu ukahisi umewin....kwenye karatasi watakaoona wataona umewin sana ila KIMANTIKI akilini mwako kuna 10% shida ni pale utakapo kuja mtiahani wa Taifa usio badorishwa, usiorudishiwa karatasi ndo 10 yako itaonekana,na utakuwa umefyonzwa akili na ujinga wa kujilewesha na kujidanganya haitakuwa 10 tena ila 05% na hapo ndo utahisi Maumivu makubwa na hasara kuliko maumivu na hasara ulizo kwepa darasani kupokea karatasi ya mark 10 na kutafuta kwa nini nimepata 10? Ukarekebisha ili upate 100 ya uhalali.
π *KIIMANI si sahihi wewe uliyeokoka,kuolewa/Kuoa Mromani wala Mromani Si sahihi wewe kuoa au kuolewa na Mlokole au mtu wa imani ya Kipentekoste unaichafua imqni yako na utazalisha NEGROES na utakutana na shida kubwa katika ndoa* kwa nini ni kwasababu ninyi wawili Misingi ya imani inayofautiana mbali sana, na Biblia imesema hivi, wasiopata wataendaje pamoja?
3 Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, wasipokuwa wamepatana?
Amosi 3:3
ππ Hebu tujiulize na wewe uliye uliza swali..maswali haya machache:
1⃣Mromani anaamini na anaomba maombi kupitia kwa Mama wa Yesu Mariamu( Sala ya mama wa Mungu utuombee) *Ukitafuta kwenye Biblia hakuna mawasiliano kati ya aliye kufa na aliye hai* (Lakini Biblia imesema Wazi mwombezi wetu wanadamu Ni Roho Mtakatifu) (Imani ya Kipentekoste inaamini hivyo)
26 Kadhalika Roho naye hutusaidia udhaifu wetu, kwa maana hatujui kuomba jinsi itupasavyo, lakini Roho mwenyewe hutuombea kwa kuugua kusikoweza kutamkwa.
Warumi 8:26
ππHapa kuna shida kubwa, mtasimamaje pamoja kumwita Mungu juu ya ndoa yenu,watoto,mipango yenu na kupambana na nguvu za giza? Huyu anaombewa na Mariamu mama wa Yesu huyu anaombewa na Roho mtakatifu......(Jibu inabidi turudi kwenye Biblia mwongo wa Kikristo nani anastahili kuomba,na nani mwombezi).
2⃣Imani ya Romani *Haiamini kama kuna Kuokoka hapa Duniani* inaamini mtu akifa ndo anaokoka ndo anakuja kupewa Cheo cha Mtakatifu flani baada ya kupitia katika hatua kadha wa kadha...anatunukiwa cheti cha mtakatifu alisha kufa zamani.. Na Imani ya Kipentekoste kwa Mujibu wa Neno la Mungu Tunaamini wokovu ni hapahapa duniani wakati bado uko hai.
3 Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao.
Zaburi 16:3
ππHilo ni miongoni mwa maandiko mengi sana yanayo zungumzia watakatifu wapo duniani siyo waliokufa, kama kuna waliokufa ni watakatifu sawa nao niwatakatifu ila si kwamba wanafanywa watakatifu baada ya kufa, Neno la Mungu linamuhusu Aliye hai ndo maana anasema *Kumcha Bwana ni kuchukia uovu Mithali 8:13* Marehemu hachukii uovu hivyo amchi Bwana,kama hakumcha akiwa duniani huyo No more time. *Msingi wa Kipentekoste ni kusisitizia utakatifu wa maisha yako ukiwa hapa duniani ndo Vasi lako la kujiandaa kumuona Bwana* Sasa hii si Imani ya Romani mtaishije watu mnaotofautiana mtazamo na Imani?
14 Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao;
Waebrania 12:14
ππImani ya Kipentekoste inaamini andiko hilo na kulitendea kazi, lakini Imani ya Romani inasema ni Uongo, Huwezi kuwa Mtakatifu ukiwa Duniani hapa, wanasahu na *Wafilipi 4:13, inayosema Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu* lakini nenda ukasome mwenyewe *YOHANA 5:1-15* Uone nguvu ya utakatifu tunaitoa wapi.
3⃣Mromani anaamini *Sala kwa aliyekufa na kutolewa sadaka kuhamishwa kutoka kwenye mateso na kupokelewa na Mungu hata kama alikufa kwenye dhambi* Imani hii wapentekoste Haipo, Wapentekoste(Walokole wanaamini katika andiko la *Waebrania 9:27, linalosema baada ya kufa ni hukumu* hakuna sadaka wala sala za kubadiri nafasi ya marehemu kama ni mwenye dhambi motoni,mwenye haki mbinguni...Sasa mnaoana ili muandaaneje kwenda kwa Bwana mbinguni.?
4⃣Mromani anaamini Kumbatiza mtoto mdogo kwa kumwondolea dhambi ya asili, lakini Imani ya Kipentekoste inaamini ubatizo ni kwa mtu mzima, aliyekiri kwa kinywa chake na kumpokea Yesu moyoni mwake ndoa anabatizwa.(Kwa lugha nyingine inaanza Toba ndo unafuata ubatizo kwa mtu mzima mwenye akili timamu)
38 Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.
Matendo ya Mitume 2:38
ππSasa watoto wenu watafuata ya nani,? *_Haya ni baadhi katika uchambuzi huu,ila Hatushauri na Hakuna kusudi la Mungu la Kuoana watu wa Imani tofauti. Huo ni Ukengeufu na Upagani wa yule anaye jihita Ameokoka maana yeye Anaijua Kweli yote,ika anajifanya hajui_*
πKuna Biashara ya UTAPELI ya kuokokeshana ili muoane kwa mwenye Maarifa ya Kimungu hatufanyi hiyo biashara isiyo zaa kununua Samaki aliye China ila unasema nitambanika na kumwekea vitunguu na nyanya nyingi nipoteze harufu, Haina shida Gharama zako,usumbu wako,harufu yako, hasara yako...muuzaji hana shida shida ni wee mlaji, Sisi tunanunua Samaki Fresh *Na tunamchunguza sana mpaka kwenye masikio, ili tusiingie hasara na gharama zisizo tarajiwa,huku tumetoa pesa yetu* Kama umeelewa mfano huu uheri. Ukitaka kufanya utapeli mwambie okoka tuoane sawa, yakiwabana,mkivurugana, yakikushinda kwani sisi Tuna hasara gani, kwani Mungu ana hasara gani, kwani utakapo kuwa unazunguka kwenye Maombezi na kuandika Vikaratasi vya kuombea ndoa yako, mmeo au mkeo au watoto wako, gharama tutakuwa tunatoa sisi Wahubiri, mkifukuzana kwenye ndoa ukarudi kwenu au mke akakuacha kwani Sisi tunaumia nini? Si ulichagua? Sometimes sisi wahubiri tunapambana sana kuvaa uhalisia wa wahuni tunaumia, Ukweli uko pale pale Ndoa ni yako, yakikushinda ni wewe ulichagua, Mungu niwademokrasia anasema CHAGUA, ila yeye anakushauri chagua Uzima ukichagua mauti Kufa umetaka mwenyewe. Ila hatutaacha kusema kweli.
*_NB: Kuchelewa kuolewa,au kuoa Siyo sababu ya Kuzoa Yeyote, Ghara ya kukwepa kuvumilia muda wa Mungu ulimgharimu Ibrahimu na Sara akazaa na Kijakazi, imetuletea shida mpaka sasa duniani kisa nimechelewa, umechelewa Unajua utaishi miaja mingapi? Unajua sababu ya kucheleweshwa? Vumilia pate mema ya Mungu_*
Nadhani nimejibu swali la muuliza swali mchambuzi alikuwa:
*Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto(Anointed)*
WhatsApp 0755444078
©2019