Thursday, 2 December 2021

KUOA/KUOLEWA NA MTU USIYE TARAJIA

🛑🛑 *UNAWEZA KUOA AU KUOLEWA NA MTU AMBAYE HUKUTARAJIA* 🛑🛑
_Imeandaliwa na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa, *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist and Counselor*)_
Whatsapp 0755444078
Facebook : Ev Elisha Kazimoto
.......
.......
_Nisuala la *Kisaikolojia* zaidi, Ni mara nyingi kuwasikia watu wakisema maneno haya ya Mshangao, *"Hivi ilikuwaje huyu akaoa mwanamke huyu, au akaolewa na mme huyu"* na hii inakuwa mshangao siyo tu kwa watu wanaotazama, ila Wakati mwingine inaenda mpaka kwa Muhusika Muoaji au muolewaji._
⛱️Hapa kuna mambo watu wanapaswa kujua mawili....., 
1️⃣Kwanza Mahusiano yanaweza kuanzishwa katika mstari wa Hisia za Mazingira( *_Mahusiano hatari haya kama watu wataendelea kwa muda mrefu hata kuingia kwenye ndo_*)...Nitachambua baadaye shika sana hiyo.
2️⃣Mahusiano yanaweza kuanzishwa katika Mstari wa Hisia za Malengo na Sababu( *_Mahusiano yenye heri na balaa_*) ntafafanua baadaye..Shika pointi hiyo
3️⃣Mahusiano yanaweza kujengwa katika Mstari wa Hisia za Tathmini na Nia ( *_Mahusiano bora na Imara_*)
⛱️Hizo hapo juu ni aina 3 za namna mahusiano yanweza kuanza kati ya baina ya watu 2.
⛱️Unajua mahusiano ni *_Nitendo la kutumikia Hisia za mwenzako zilizoibuliwa baada ya mazingira flani kutengenezwa baina ya watu 2_*
⛱️Kuna watu walijikuta wameanza mahusiano na watu ambao hawakutegemea kama wangekuwa kwwnye mahusiano au wangeoana au Wangelala pamoja ( kufanya mapenzi)
⛱️Kuna watu wanapoishi wanakuwa na *Nia au malemgo au wazo la kutamani mtu flani angekuwa mwenzi wake au mchumba wake au mpenzi wake* Hao watu hata wakianzisha mahusiano yanakuwa hayana shida sana kisaikolojia kwakuwa kuna mtu alikuwa na wazo na nia ya kufanya hivyo.
⛱️Lakini kuna watu ambao bila kujua, bila kutegemea, *Wanajikuta wapo kwenye mahusiano na mtu ambaye Hakudhamilia,hakumuhitaji, si wa ndoto zake kabisa* lakini wanajikuta wapo kwenye mahusiano na wanafurahia na baadaye kuoana au kusex pamoja, na kubebeshana mimba.
⛱️Nini kinafanyika mpaka mtu anakuwa kwenye mahusiano na mtu ambaye hakutarajia au hakukusudia au si wa ndoto zake....?
1️⃣MAZINGIRA yanaumba mahusiano ya Dharula na kupelekea Mahusiano au Ndoa Isiyotarajiwa.
🌹Kuna watu jinsia 2 tofauti walionekana kutovutiana, au humpendi,na wala umfikirii kwa lolote....Ila *Mazingira ya Ukaribu(DISTANCE/INTIMACY ) ikaumba hisia za upendo ndani yako kwakuwa mna share vitu flani kila mara pamoja bila migongano* mfano....Mahisiano haya yanatokea kwa watu walioko  _shuleni,vyuoni,kwenye kwaya,au watu wanaofanya kazi moja kwa muda mrefu pamoja kwa siku nyingi_
👉Watu hawa kama hawatakuwa na kuhitirafiana,magomvi, nk ujikuta kila mmoja anaanza kuvutiwa na mwenzake bila kujua.... Upendo unaozaliwa hapa Kisaikolojia tunauita *Functional Love* ni upendo wa majukumu.
👉Kwakadri mnavyotimiza majukumu na kusaidiana majukumu vyema na kuyafanikisha vema,upendo hukua,uongezeka, hata kuzalisha *Hisia za Thamani* yaani unaanza kumuona mwenzako mnaye fanya majukumu ni bora na mzuri sana kwako.
👉Na kanuni ya upendo inasema *Usitiri wingi wa Dhambi* yaani kwa kadri upendo unavyoongezeka ulotokana na majukumu ndivyo Sura mbaya, Shape mbaya,na mapungufu ya mwenzako yana futika unaanza kumuona mwenzako katika Upendo wa Kimapenzi wa *Muhitaji Kihisia* na hapo ndo watu ujikuta wana Sex na mtu asiyetarajia ambaye wala hawakupanga kuwa na mahusiano, wala hawajaombana urafiki, au unakuta wanaanzisha Uchumba moja kwa moja hata bila ya kuanza kutongozana,yaani urafiki wa kimajukumu unazalisha Utayari wa kuwa pamoja.
NB: _Ndiyo maana watu uwa wanapata wachumba /wapemzi kwenye field zao za kazi, wakiwa shuleni kwenye Discussion_
2️⃣MALENGO......ya mtu yanaweza zalisha mahusiano ambayo baadaye yakawa mazuri au yakaleta shida pale lengo litakaposhindwa kutimia au kubadirika.
👉Mfano mtu anaweza kuwa na shida ya *Pesa kufanya jambo flani* lakini uwezo wa kupata pesa ile haupo lakini akatokea mtu akamsaidia wala bila masharti ya kuanzisha mahusiano, lakini kutokana na aliyesaidiwa pesa kutimiza malengo yake, *Utaanza kuota upendo wa Kujari,na Kurudisha Fadhaira* na aliye toa kwa kadri anavyo heahimiwa na kuonwa kama Mwenye Kusaidia,na mwenye upendo mwingi ndivyo na yeye anajenga Upendo wa Imani(kuaminisha yeye ni bora zaidi) na hapo ndo *Mahusiano uanza kuota* na watu wakaamua kuoana au Kusex bila hata kutongozana na kuombana urafiki au uchumba.
3️⃣TATHIMINI, Mahusiano kadhaa uanza ikiwa ni matokeo ya watu, au mtu *_Kuchunguza sifa, ubora,uwezo,hisia na mwonekano wa mtu huyo pamoja na kuwa karibu,kuishi pamoja, kusoma pamoja, kufanya kazi pamoja lakini bado mtu anajizuia kujenga au kukubali, au kusema neno la Kihisia kwa mwenzake, akihofia kutokuwa na Taarifa kamili za mwenzake za kumfanya awe bora au muhimu kwenye mahusiano.....
👉Watu wa aina hii wakianzisha mahusiano uwa yanakuwa Imara,bora na yanadumu maana yamechanganuliwa kwa kujua nini sababu ya kuwa na huyo, anauzuri gani, ni bora kiasi gani kuzidi nani, na atamfaidisha namna gani.
NB _Hivyo ndivyo Mahusiano ya watu kuoa au kuolewa na watu ambao hawakuwatarajia ila ndo kmeisha kuwa hivyo._
*Imeandaliwana Mchambuzi wa Masuala ya Mahusianio Ev Elisha Kazimoto(psychologist & Counselor )*
Whatsapp 0755444078

Saturday, 11 September 2021

HATARI USIYOIONA KATIKA MAHUSIANO

🎣🎣 *HATARI USIYO IONA KATIKA MAHUSIANO KATI YA KIJANA WA KIKE NA WAKIUME* 🎣🎣
Imeandaliwa na Mchambuzi wa Musuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto*( Psychologist)
WhatsApp 0755444078
Facebook Ev Elisha Kazimoto
e-mail babaeve755@gmail.com
_Shalom vijana wote wenye ndoto za kimaisha za kiroho na za kimwili, na wote walio na mipango muhimu katika Ufalme wa Mungu kama kumtumikia Mungu katika huduma yoyote *mfano..Kuhubiri,Uimbaji,kupiga vyombo vya mziki na huduma nyinginezo* Somo hili litakufaa na kukukomboa na *Siri Usiyoijua na hatari usiyoiona iliyo nyuma ya Mahusiano uliyo nayo kati yako na rafiki yako huyo wa kike au wa kiume* Litakusaidia sana kutimiza ndoto zako na usipo jua basi utaishia njiani,utabaki na Historia *Nilikuwa* ila haitakuwa tena_
🎣🎣 *HATARI USIYO IONA KATIKA MAHUSIANO KATI YA KIJANA WA KIKE NA WAKIUME* 🎣🎣
Imeandaliwa na Mchambuzi wa Musuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto*( Psychologist)
WhatsApp 0755444078
Facebook Ev Elisha Kazimoto
e-mail babaeve755@gmail.com
_Shalom vijana wote wenye ndoto za kimaisha za kiroho na za kimwili, na wote walio na mipango muhimu katika Ufalme wa Mungu kama kumtumikia Mungu katika huduma yoyote *mfano..Kuhubiri,Uimbaji,kupiga vyombo vya mziki na huduma nyinginezo* Somo hili litakufaa na kukukomboa na *Siri Usiyoijua na hatari usiyoiona iliyo nyuma ya Mahusiano uliyo nayo kati yako na rafiki yako huyo wa kike au wa kiume* Litakusaidia sana kutimiza ndoto zako na usipo jua basi utaishia njiani,utabaki na Historia *Nilikuwa* ila haitakuwa tena_
ANDIKO KUU LA SOMO
LUKA 19:41-44
*41 Alipofika karibu aliuona mji, akaulilia,*
*42 akisema, Laiti ungalijua, hata wewe katika siku hii, yapasayo amani! Lakini sasa yamefichwa machoni pako.*
*43 Kwa kuwa siku zitakuja, adui zako watakapokujengea boma, likuzunguke; watakuzingira na kukuhusuru pande zote;*
*44 watakuangusha chini wewe na watoto wako ndani yako, wasikuachie jiwe juu ya jiwe, kwa sababu hukutambua majira ya kujiliwa kwako.Luka 19:44*
🎣Kwenye mistari hii kuna vitu kama 6.
1️⃣Kuna mji umeonekana(mtu)
2️⃣Kuna mtu anajua siri au ameona hatari juu ya mji(mtu) ambayo mji(mtu) haoni.
3️⃣Kuna mtu anaona uchungu kwa yajayo juu ya mji(mtu)
4️⃣Kuna kitu kibaya (Mji) haujui...(Laiti ungejua....)ila siri imefichwa
5️⃣Kuna nyakati za Uharibifu zinakuja juu ya mji(mtu)..Ambapo adui watazingira pande zote wafanye uharibifu
6️⃣Matokeo ya siri ikitimia ni Kufutika kabisa kwa mji(mtu)
🎣 *_Katika Tasnia ya Mahusiano kuna nguvu kubwa ya upendo na ushawishi uwa inajengeka ndani ya mioyo na akili za watu walio katika mahusiano_*
🎣Nguvu kubwa hiyo ya upendo na ushawishi Uongeza nguvu ya ( *Kuaminiana kwa kiwango cha Kutoshutukiana*)
🎣Kuaminiana kukiongezeka na kuimarishwa, utengeneza mazingira ya *Kuondoa mipaka flani flani* ya kujizuia kutofanya mambo flani flani ya kihisia, kuchochea hisia kwa mwenzako.
🎣Mipaka ya kuogopana na kuoneana Aibu ikianza kufutika....Kunazaliwa *Kujisahau*
🎣 KUJISAHAU....Ni *_hali ya mtu kuto tambua Nafasi yake, Heshima yake, mipaka yake, kushindwa kutambua hatari yoyote na kuona mambo yote ni sawa_*
🎣Hali ya kujisahau ikianza kukomaa inaweza zaa *Kutojizuia*..... Hali hii ni ile ambayo mtu *_Anaona jambo hili ni baya au halifai lakini kuna nguvu inayomsukuma kufanya hata kama anaona ni hatari_* maana nguvu ya Kujizuia imeisha ondoka ndani yake.
🎣Kwa mazingira hayo mtu anaweza anza kufanya ubaya wakati *Aupendi ubaya* anafanya ubaya kwakuwa Hana nguvu ya kujizuia, hawezi kujizuia kwakuwa alishaondoa mipaka.
🎣Mazingira haya yakifikiwa ndipo vijana/watu walio kwenye mahusiano wanaweza kufanya mambo yafuatayo
1.Kufanya *Romance*
2.Kuridhishana kihisia *kwa michezo ya kimahaba*(Kushikana shikana maeneo nyeti ya kihisia)
3.Kutumiana picha na video za uchi
4.Kushiriki Ngono...Tukio la mwisho hilo katika mchakato wa mahusiano.
*Na hii ndo Hatari iliyofichwa kwa vijana wengi* pamoja na kwamba wengi wana Imani ya Kujiamini kwamba wao wako Imara hawawezi Kufanya Ngono labda wawe wameamua.... Hiyo ji kweli kwa baadhi...Ila *Mchakato wa Kuanguka uwa hauendi Gafla* unaenda taratibu sana jambo ambalo uwezi kulishutukia kwa haraka.
ANGALIZO KWENYE MAHUSIANO, UKIONA MAMBO YAFUATAYO YAMETOKEA KATI YENU ITAKUGARIMU KUPONA.
_Ni vigumu kuelewa Elimu hii ya Kisaikolojia ninayo kupa ila ukikaa na kutajitazama utagundua kuna hatari tiyari umeisha ingia_
1.Ukianza Romance( Utakuja kuiacha) unaweza jizuia mara moja,mara mbili ila *Utarudia tu*(Msingi wa zinaa unaanza kujengwa taratibu)
2.Ukianza Kushika au kushikwa Maeneo yanayo ibua hisia(Utaacha,utarudia) maana mwili unazoea hisia za furaha. *Unaweza jikaza kujizuia kwa wengine ila kwa mtu wako wa karibu itakushinda*(huo ndo mwanzo wa kuisogelea zinaa)
3.Ukianza kutamani na kutumia mazingira ya kukaa peke yenu wawili msikoonekana na mtu mwingine, na nafsi zenu hazitamani kukaa mahali pa wazi, *Mtajikuta mmefanya matendo ambayo hamkutegemea kuyafanya* ila hamtaweza kujizuia.
3.Ukishazoelea mazingira ya kumtembelea mwenzako kwake, guest huwezi acha hata kama unahisi hatari,nguvu ya mahusiano itakusukuma kwenda tu.
*Ushauri wa Kiroho na Kisaikolojia kwako kijana kama ujaathirika na hali hii*
👉Usiruhusu upendo uzibe macho yako ya kuona hatari iliyombele zako ya kiroho na kisaikolojia.
👉Usiruhusu Maeneo yako ya mipaka yako yashikwe au usiruhusu hisia zako zikupelekee kushika maeneo yaibuayo hisia zako
👉Peaneni elimu na taadhari kama marafiki mliopo kwenye mahusiano ili mkae katika mipaka yenu
👉Kila mmoja jiwekee msimamo wa kutofanya makosa hayo uliyo yajua.
*Kama tayari Umeathirika,una kazi ya kifanya na inaumiza,na itakuchukua muda kuzoea* Fanya mazoezi ya kubadiri mazoea mliyozoeshana na rafiki yako ili ujinasue katika hatari ijayo.
*_Imeandaliwa na mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)_*
Whatsapp 0755444078
Facebook Ev Elisha Kazimoto

Thursday, 26 August 2021

UHODARI NA USHUJAA WETU MSINGI WAKE

💪💪 *ILI KUSHINDA UNAHITAJI MAMBO 2..UHODARI NA USHUJAA*💪💪
Mnenaji: *Ev Elisha Kazimoto*
ANDIKO KUU: *2Mambo ya Nyakati 13:1-18* 👇👇👇👇👇 _Ukisoma mistari hiyo kwa utulivu halafu njoo hapa kwenye Ufafanuzi wa Roho Mtakatifu_
👉Kila mtu aitwaye mshindi, maana yake *Amepita kizuizi kilicho lenga kumzuia asiende alikokusudia* kwenda.
👉Kushinda pia ni kupata,kuona ulichokuwa unakitarajia......Ikiwa ni baada ya kuzuiliwa na kitu,mtu,mazingira au hali,iliyowekwa maalumu kwaajili yako kukuzuia.
💪 *UHODARI* ni Tabia  au hali ya *Kujiamini* kutokana na mafunzo,mazoezi,kinga au mtu aliye nyuma yako kukusaidia.
👉Kila mtu aliye Hodari ana namna ya wapi anapata nguvu ya kujiamini.
👉Kwa ujumla UHODARI ni KUJIAMINI.
💪USHUJAA....Ni hali na moyo wa Mapigano yazaayo Ushindi.
👉Mtu shujaa maana yake ana Rekodi ya kupigana na kushinda mpinzani wake.
👉Ushujaa ni moyo uliotayari kupigana na kushinda.
NB1,: *_Msingi wa Imani yetu ya watu tuliookoka ni Sisi ni Hodari(kwakuwa aliyenyuma Yetu ana nguvu kuliko yeyote na chochote kikwazo,au adui tutakaye kutana naye kutuzuia,au kutudhuru_*
KUMBUKUMBU LA TORATI 31:1-6

NB2: _Maisha yetu sisi watu tuliookoka, niya USHUJAA kwakuwa sisi ni watu wa vita,mapigano kwenye ulimwengu wa roho na Tunashinda kabla ya pambano kwakuwa *Vita si yetu ni ya Bwana* hivyo Ushindi ni Lazma_
*Waefeso 6:10-12, Warumi 8:31,37, 1Samweli 17:46-47*
Imendaliwa na *Ev Elisha Kazimoto*
Whatsapp 0755444078

Thursday, 7 January 2021

MWAKA WA KUACHILIWA 2021

🎁2️⃣0️⃣2️⃣1⃣ *MWAKA WA KUACHILIWA(MWAKA WA MAACHILIO)* 2️⃣0️⃣2️⃣1⃣🎁
_Mnenaji Ev Elisha Kazimoto(0755444078)_
_Shalom watu wa Mungu mliopata neema ya Mungu Kuingia katika mwaka mpya wa 2021,Heri ya Mwaka Mpya kwako unaye soma Ujumbe huu na *Neno la Kinabii* la mwaka huu. Kila mwaka Bwana amekuwa akinipa neno la Mwaka mzima,na katika mwaka huu hili ndilo Bwana ameninong'oneza katika usiku wa tarehe 31.12.2020 katika mkesha wa Mwaka mpya,tukiwa katika maombi ya kumshukuru Bwana na kuukaribisha mwaka mpya 2021, *Nikanong'onezwa na Roho wa Bwana akisema, Huu mwaka mnaouingia ni mwaka wa Kuachiliwa(Maachilio)* tangu muda huo maombi yangu yalibadirika nikaanza kuunena mwaka tunaouingia niwa Kuachiliwa kwa vitu vingi Vilivyo shikiliwa muda mrefu, sasa nikukaribishe katika ujumbe huu kama unaamini Neno la Bwana utashuhudia mwenyewe kabla ya mwaka huu kuisha mambo mangapi yako yaliyokuwa yamezuiliwa sasa YAMEACHILIWA_
*_1 Bwana akamwambia Musa, Liko pigo moja bado, nitakaloleta juu ya Farao na juu ya Misri; baadaye atawapa ninyi ruhusa mtoke huku; naye hapo atakapowapa ruhusa, atawafukuza mtoke huku kabisa kabisa.Kutoka 11:1_*
🌲Watu wengi muda umepita,miaka imepita hawaoni wanayoyaomba,pamoja na kwamba wakijichunguza wanaona wako vizuri na Mungu,siyo hivyo tu ila kama kuomba na kuombewa wameomba na kuombewa ila *Mambo hayatokei,bado yamezuiliwa* 
🌲Ndivyo ilivyokuwa hata kwa wana wa Israeli,miaka mingi wako chini ya mateso,mkombozi amekuja (Musa) ameanza harakati za kuomba(maombi) kibali cha kutoka,siyo kwa hisia zake no kwa maelekezo ya Mungu, fanya hivi mtatoka(MTAACHILIWA) Lakini wapi(tangu sura ya 3 ya kutoka Mungu anakiri kuona kilio chao na kusema sasa nimeshuka kuwaokoa,mpaka sura ya 11 Mungu anasema sasa Liko pigo 1 nikilileta huyu aliye wang'ang'ania ATAWAACHILIA KABISA KABISA,haikuwa kazi ndogo na muda ulikuwa umesonga.
👉Nataka niseme nawe unayesoma ujumbe huu wa Kinabii, 2020 nakurudi nyuma ulitembelea ndani ya kipindi cha ( *Sura ya 3 hadi 10 ya Kitabu cha kutoka*) mwaka huu ulipoanza(2021) UMEINGIA SURA YA 11 SURA YA MAACHILIO.
🌲Mungu anamwambia Musa pigo hili litamfanya Farao AWAACHILIE nanyi mtatoka huku KABISA KABISA.
👉Kuna sehemu utatoka kabisa kabisa mwaka huu, *_Mwaka huu unatoka katika masimango ya wanadamu,unatoka katika magonjwa,unatoka katika utasa,unatoka katika kutooa au kuolewa,unatoka katika dimbwi la madeni na umaskini, Vitu vyako vinaachiliwa katika jina la Yesu_*
👉👆 _Mme wako anaachiliwa kutoka kwa makahaba,mtoto wako anaachiliwa,elimu yako inaachiliwa,ofisi yako inaachiliwa,ndoa yako inaachiliwa,mume wako,mke wako,mahusiano yako YANAACHILIWA KATIKA JINA LA YESU_
🌲Sijui kama unaelewa na unaona ninachokiona,kama kukata tamaa ilibidi Musa akate tamaa haraka, maana alikuwa anaambiwa na Mungu fanya Ishara hii Farao atawaachia, anafanya na FARAO HAWAACHII,anarudi kwa Mungu mbona amegoma kutuachia?Mungu anampa ishara na pigo lingine anafanya,Farao anagoma kuwaachilia Israeli watoke kwenye mateso, ila sura ya 11 Mungu anasema LIMESALIA PIGO 1 HILO NI LA MAACHILIO, wacha *Mungu mwaka huu ampige adui yako pigo moja la mwisho,PIGO LA MAACHILIO naye ATAKE ASITAKE ATAACHILIA mipango yako na maono yako na huduma yako* 
🌲Kwanini una mashaka? Kwakuwa umeomba sana na kuombewa,?umetabiriwa sana hujaona? Wewe ungekuwa Musa ungewatoa Israeli kweli Misri? Aaah Huu ndo Muda wa Mungu unaposoma ujumbe huu SAA YA KUACHILIWA IMEFIKA...Anza maandalizi ya kutoka,weka mipango yako sawa,andika maono yako ya mwaka mzima sasa,fanya ulilolikusudia 2021 ni mwaka wa *Kuachiliwa kwa vitu vilivyo shikiliwa*
🎁 _16 Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina lake. Malaki 3:16_
*_17 Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye.Malaki 3:17_*
👉Mungu yuko kazini mwaka huu kushugulikia watu wake na mambo yao ambayo yalikuwa yameshikiliwa muda mrefu sasa anasema  Ataachilia. Hakuna adui wa kuendelea kukuchezea akishikilia vitu vyako,kazi yako ni *Kukaa na Mungu sawa sawa na kumwamini na neno lake* Mwaka wa Maachilio.
🎁 _20 Basi Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni kinyume cha hirizi zenu, ambazo kwa hizo mnaziwinda roho za watu kama ndege, nami nitazitoa katika mikono yenu kwa nguvu; nami nitaziachilia roho zile mnazoziwinda kama ndege.Ezekieli 13:20_
_21 Na leso zenu nazo nitazirarua, na kuwaokoa watu wangu katika mikono yenu, wala hawatakuwa katika mikono yenu tena kuwindwa; nanyi mtajua ya kuwa mimi ndimi Bwana.Ezekieli 13:21_
👉👆Kwa namna yoyote waliyokuwa wamekushikilia adui zako,iwe kwa uganga,mahirizi,walikufunga leo usione uendako na usionekane, Mwaka huu Bwana anasema ATAZIRARUA LESO HIZO walizokufunga ili Akuachilie wewe.
_Nimalize kwa kusema hivi, Suala la Kuona kile Mungu alichosema na watumishi wake kwa unabii,haliko mikononi mwa Mungu,bali mikononiwa Asikiaye neno la Mungu,ukiliamini na kulifuata UTAONA,ukidharau na kutoamaini HUTAONA BADILIKO LOLOTE ila waliomgoja Bwana Muda mrefu na wamesikia na wanaamini sasa NATANGAZA KATIKA JINA LA YESU  KITU CHAKO KILICHOSHIKILIWA KWA MUDA SASA KUACHILIWA MWAKA HUU 2021 Hilo ndilo neno la Bwana,mwenye kulipokea na kuliamini Pokea nguvu ya Maachilio katika jina la Yesu Amen_
🎁Ulikuwa nami mnenaji wako, Mtumishi wa Bwana na mjumbe wa matengenezo wa nyakati za mwisho, *Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp 0755444078)*
Facebook Ev Elisha Kazimoto.
          ©️2️⃣0️⃣2️⃣1⃣