Thursday, 4 October 2018

BINTI AMEJIPANGIA MAHARI MIL2

♠♠ *Swali bintibanajipangia Mahari ni Milioni 2 huna kaa chini*♠♠
Ninaye rafiki wa kike. Nampenda sana. Ananipenda pia. Natamwani mwakani disemba nimuoe. Kwa ndoa ya kanisani na sherehe ndoogo tu ya kawaida. Ndog isiyojaza watu mia. Mwenzangu anataka kuolewa na mimi mwakani pia. Ilaa anadai km nispomlipia mahali mil 2 ambazo alijiwekea km ahadi kwa wazazi wake,kwamba nikimtolea mahali chini ya izo HATAISHI NA MIMI KWA FURAHA. alaf anaithamini sana harusi. Anataka iwe kubwa na watu wengi jambo ambalo kwa uchumi wangu naona haliwezekani. Maandalizi ya kama anavyotaka yeye labda nisogeze muda mwaja mmoja tena baadae wakat mi naona wakati sahihi wa kuoa ni mwakan disemba.

ndugu yangu,binti wa hivi ni mtafsiri vipi? Kuna lugha anajarbu kunieleza siielewi au ndio tayari ashajipatia kwigine mimi tu nd namchelewesha?
Wote tumeokoka
........................................
*_Anajibu Mchambuzi wa Masuala ya Mahusuano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto(whatsapp 0755444078)_*
........
........
*SI KILA UNAYE INGIA NAYE KWENYE MAHUSIANO ANAAKILI TIMAMU*(UTANIELEWA MWISHONI)
👉Kuna mambo mengi kwenye mahusiano yanafanyika mengine ukiyasikia unahisi *_Hapa ufahamu wa Kimungu ni mdogo,hapa Kisaikolojia hakuna kitu,hapa akili ya kawaida hakuna kabisa_* kuma matatizo mengine hayahitaji kuumwa njaa ya masaa 12,24,36,48 au 72 ukimuuliza Mungu huyu ni mtu sahihi au la,nipige chini au nibebe ndo maana Biblia ikasema TUTUMIE AKILI IPASAVYO.
Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe.

1 Wakorintho 15:34
👉👆Ndoa,ni makubaliano ya watu 2,binti na kijana,walopendana na kuamua kuishi pamoja ( *Yaani kuacha familia zao,na kuunda familia yao*)
👉Kikawaida(katika akili timamu, *Wachumba wanafahamiana hali zao za kuuchumi,na famikia zao* lakini hawa watu wawili wana kazi ya *Kujenga Familia yao iwe na nguvu kiuchumi ili wazisaidie familia zao* kwa watu wenye akili timamu.
👉Pili suala la Mahari,ni Mgao unaofanywa na familia ya binti kwa kijana anaye mtaka bibti yao, na mgao huo *Kimantiki haulengi kuwa mtaji wa sendoff,au biashara,au kuuza,au kufidia gharama za matunzo* ni zawadi na heshima ya shukrani ya kijana kwa wazazi wa binti.(kiafrika) lakini kimaendeleo na kimaana halisi( *Familia ya binti na ya kijana zijipinde kuwatafutia kiwango cha uchumi wa kianzio cha maisha,hawa wanaanza maisha,ninyi ndo mnakaribia kumaliza maisha,nani anamzigo?* yule anaye anza.
👉Binti mwenye akili timamu ya kimaisha na kisaikolojia anacheza *midfield* kuhakikisha mme wake mtarajiwa *Haumii kwa mahari* maana akiumia si kwamba anaumia kijana,ila wote mnaumia maana si unaolewa naye,kama madeni si mtalipa wote?kwani wee utaishi wapi?kama kula vibaya mtakula vibaya mpaka deni liishe. Ok anayway nini nasema hapa kulipa mil 2,siyo shida hata kama 10,je mmeo mtarajiwa anauwezo?
*KABLA SIJA HITIMISHA NIKUPE SIFA ZA BINTI HUYU NA KAMA UNATAMANI NDOA YA AMANI PIGA CHINI HUYU HARAKA SANA KABLA WEWE HUJAWA REMOTE*
1⃣Ni binti mwenye dharau kubwa, dharau yake imepita viwango kiasi cha kujuonyesha thamani yake ikoje tofauti na unavyoweza kuwa unamtazama.
2⃣Ni binti mwenye jeuri na moyo wa kutawala, huyu dada kumuoa unaweza jikuta unatawaliwa badala ya kutawala. Mdada anayejipangia Mahari aisee huyu hafai kuolewa ila kupiga *umalaya*(unielewe,neno gumu ila waweza likumbuka baada ya kuishi si zaidi ya miaka 3.
3⃣Ni binti mwenye moyo wa ushindani wa kipumbavu. Aisee huyu ni miongoni mwa wanawake wanaoshindana na watu kuvaa,kula,mitindo bila kujali *Uchumi wa familia yake ukoje* huyu ukioa umeumia.( yaani mtu anayejipangia mahari kisa anataka kushindananadada zake walotangukia kuolewa,awapite kiwango cha mahari,huyu hamna kutu)
4⃣Ni binti mwenye misimamo isiyo faa, yaani, *Amejiwekea kuolewa kwa mil 2* hapo haijalishi kijana anauwezo gani huyu ni hafai kwa familia.
*LABDA NI MUHOJI HUYU DADA KIDOGO*
👉Ulipiwe mahari mil 2,kwakuwa una nini *Kipya* ambacho hakioatikani kwa wengine ili mtu apambane na hicho.
👉Kuwa na bikira ndo kuwa na tabia njema⁉,ndo kuwa na akili ya kuendesha familia? Bikira ni upekee?wapo wengiii wenye bikira ila wametulia,sanapanga na kuelewana na wachumba zao kulingana na hali zao za kiuchumi.
👉Kwani unahisi mil 2 ni pesa nyiiiingi kiasi kwamba ukiolewa kwa mahari ya mil 2 utakuwa wapekee⁉ wakati wenzako mil 2 *Nipesa ya pete tu za harusi* ndo unalilia iwe mahari yako(mpaka hapo unaonyesha level ya familia yenu kiuchumi)
👉Nikusaidie, wewe huna haki ya kupanga chochote,kabda mmeo mtarajiwana wazazi wako,yaani wewe jeuri huna,maana unasubiri kutafutwa,na unaweza kuachwa leo na akapata mwingine wiki moja,ila wewe kupata mwingine na mwaka waweza isha.
*_Mwisho,huyu kijana anaweza pata tabu sana kuoana na huyu mdada,yaani hapa hapahitaji maombi ya kufunga,huyu nikumuita nakumwambia ukweli kwamba masharti yako siyawezi,na kwa hari hii kwenye ndoa ndo nitakuwa house boy,tafuta atakaye weza lipa mil 2 za mahari, na kufanya harushi kuubwa,mimi nitatafuta wa kuendana na uwezo wangu_*
NB: _Ukipenda usiwe kipofu na kiziwi,usione athari za baadaye, heri kuvunja uchumba kuliko ndoa_
Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto* (whatsapp 0755444078)

WACHUMBA WALOANGUKA

🖤🖤 *Swali la Wachumba waloanguka kwenye Zinaa*🖤🖤
Alikua kweny mahusiano na huyo mdada wote ni born again christians
Katika mahusiano yao walikuwa hawa date kipendwa Namaanisha walikuwa Wameangk kweny dhambi ya Uzinzi .Ila Sasa huyo kaka Kamshauri mdada wake wakatubu kanisani na Waweke wazi kwa mchungaji na wazee wa kanisa hiyo dhambi Ili watubu .Swali linakuja hawa watu baada ya hapo Wavunje uchumba Kila mtu amwombe Mungu ampe mwingine au Waendelee na mahusiano Yaliyo ya mipaka nasio kama ya mwanzo Ya kuhusisha dhambi hapo inakaaaje .
.......................................
*_Anajibu mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp 0755444078)_*
(Mjumbe Mkali- *Mithali 17:11*)
........
........
*NI HITIMISHE HII MADA*
_Kwanza kabisa, nawapa polee kwa kushindwa KIPIMO CHA UAMINIFU WAO KATIKA UCHUMBA KITAKACHO WAGHARIMU HATA KATIKA NDOA wawe wametubu au hawakutubu,watafauru sehemu A,ila sehemu B itawagharimu_
Pili, niweke sawa kwanza msimamo wa Kiroho na kisaikolojia. *Hatutoi Faraja Feki kwa watu walioshindwa kwa Kigezo cha Mungu anasamehe,au Kuna Reference za watu walioanguka dhambini nawakatubu kama DAUDI. Isitoshe kizazi hiki hakuna mwenye hata robo ya moyo wa TOBA KAMA DAUDI,kijana wa sasa akiambiwa afanye toba kama aloifanya Daudi ATAACHA WOKOVU,kwa hiyo kiufundi Usijilinganishe hata kidogo kwa mtu ambaye hata theruthi ya viwango vyake Huna*
👉Andiko la Daudi kuanguka na mke wa Uria wamelitumia vijana wengi( *wahuni na wachafu*)kujihalalishia ZINAA kabla ya ndoa, na kujifariji eti watatubu kama Daudi.....Hivi mnauelewa wa Toba ya Daudi⁉ ukiielewa Toba ya Daudi utatetemeka, Lakini *Mnasomaga Majibu ya Mungu baada ya Toba ya zinaa,Alivyo Gharimika kwa zinaa ile pamoja na kuomba Toba⁉*
👉God is not cheap like people assuming. Daudi Alisamehewa ila Alilipigia gharama ya zinaa, soma Bible uone,mtoto wake alobebesha mimba Mungu *Alimuua*,lakini ikawepo laana kwa uzao wake *NDUGU WAKA BAKANA*(Tamari na Amnoni),tena akaambiwa mchana kweupe watu watalala nawakeze..... *Usijifariji kwa Zinaa*
👉Tatu, Zinaa kabla ya ndoa inafanya kazi kuu 2 kwenye ndoa yenu kiroho na kisaikolojia.
1⃣Hamtaaminiana kamwe mpaka mnazeeka(hiyo ni Biblically )hata mkitubu mtasamehewa,ila Moyo wa uaminifu *Unaondolewa kwenu* (Ninashuhuda nyingiii)kwa watu walofoji ndoa, hawakuwa salama,hata kama mnapendana namna gani, hii ni Kanuni ya Mungu( *Uaminifu kati yenu nimatokeo ya kutunza siri ya miili yenu mpaka mruhusiwe rasmi*)mkiindoa HAKUNA MUUJIZA,WALA MAOMBI YAKUOMBEA AMANI,WALA UAMINIFU KATI YENU, mtakula matunda ya kazi yenu(kiroho kama mtatubu toba ya kweli,aaha ninyi watakatifu na mbinguni mnaenda,ila ishu za amani na uaminifu mta struggle sana)
👉 *NIWASHAURI SASA HAWA*
*_Fanyeni toba kamilifu,ntatuma lecture ya zinaa kama 2,3 zisome vizuri,kama kuna mtu mwingine alihisi afanye atatubu,KIMBIA,SI RAHISI KIVILE,unaweza ukatubu,hata miaka 10 bado hupati amani,na kila kitu unaona hakiendi._* na kwakuwa wanapendana WAOANE kwasababu kuachana eti kila mtu atafute mwingine ni KUENDELEZA UHALIBIFU,ukienda kwa mwingine ukamwangusha naye?maana wee mzoefu,utaacha wangapi? Lakini ukichumbiwa au kuchumbia ambaye hajawahi kuanguka na bahati mbaya tamaa ileile ikainuka ukamwangusha,umeongeza kundi la majeruhi.
*Ni heri bhana mkachukuana mlofoji marks pamoja za mtihani* kila mtu abebe mzigo wake( Na hapa Tusiweke ukiroho kupita Yesu,kwamba nikunyanyapaa,tukitubu tumekuwa kiumbe kipya,kiumbe kipya cha wapi, *Upya wa wapi wa roho au kimwili,au vyote*? Kama wa kiroho, *Roho anahusika nayo Mungu,mume au mke anahitaji upya wa mwili* mambo ya upya wa roho mpelekee Yesu Kristo aliye mbinguni,ila hapa duniani,tuletee mwili mpya.
🎁👆Kwanini nasema haya yote, *Watu wameirahisha Zinaa sanaaaaa,na kutuumizia mabibti zetu,na vijana wetu, eti tuta Tubu*
KAURI YANGU USIFANYE ZINAA NA MCHUMBA WAKO,AU RAFIKI YAKO KWA NAMNA YOYOTE. Na HAKUNAFA BAHATI MBAYA YA ZINAA...Haipo.
*HAWA WAOANE,WAZIDI KUSAIDIANA MUDA HUU WASIANGUKE TENA,JAPO NI KAZI KUBWA,KUONJA HALAFU USIENDELEE,ILA WAWEKEANE MIPAKA,JAPO HESHIMA MPAKA SASA HAKUNA,WANAONANA KAWAIDA SANA,ILA WAJITAHIDI KUMPENDA MUNGU SANA ILI MZIGO WAO UWE MWEPESI*
By Ev Elisha Kazimoto(whatsapp 0755444078)
Mithali 17:11(Jina la Kazi)

Tuesday, 2 October 2018

JENGA MOYO NA NAFSI YAKO

🎾SOMO: *UJENGE MOYO WAKO NA NAFSI YAKO KATIKA UWEZO WA KUTO YUMBISHWA NA TUFANI YOYOTE*🎾
_By Ev Elisha Kazimoto(whatsapp 0755444078)_
🎁 *_Utangulizi Wa Somo_*🎁
*28 Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Mathayo 11:28*
🥦Kwenye andiko hili kuna mambo ya kuzingatia kama 4,ambayo yatakusaidia kama mwamini wa Yesu Kristo Kuujenga Moyo wako na Nafsi yako.
🥦Hapa kuna mwito wa Yesu kwa watu wote( walio nje na walio ndani ya Kanisa)
🥦wanaoitwa na wale wenye kusumbuka,wenye masumbufu maishani mwao
🥦Kundi lingine ni wale waliolemewa na Mizigo(mizigo ya aina yote)
🥦Lakini pia kuna jibu la Yesu au Suluhisho la Yesu ni kuwapumzisha.
*_Sasa kwa mujibu wa andiko hili Mizigo siyo dhambi tu,au magonjwa tu, hapa mizigo ni Hali zote,zilizoongezwa kwenye maisha yako ambazo Hukuumbiwa na Mungu,chochote kinacho Athiri amani yako alokuumbia Mungu ni mzigo_*
🎁KUNA MAENEO MATATU YANAYO HUSIKA NA KUBEBA MIZIGO HIYO KATIKA MAISHA YA MWANADAMU🎁
1⃣ *MOYO* ni kiti cha mizigo yote ya Maamuzi mabaya. Matendo yote yasiyo ya haki,yaletayo hatia, matendo yote yanayolenga kuumiza mtu, matendo ya kutendewa kinyume na matarajio yako ni *Mzigo wa Moyo*.

20 ikiwa mioyo yetu inatuhukumu; kwa maana Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu naye anajua yote.
1 Yohana 3:20

21 Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu;
1 Yohana 3:21
👉👆Kuna watu usema moyo unaniuma,mapigo ya moyo yanaenda kwa kasi,pressure,kifua kubana,kutenda mambo kwa Hasira,kuzira na kununa ni matokeo ya Moyo kubeba Mizigo Isiyo stahili.
2⃣ *AKILI/NAFSI* Hiki ni kiti cha kubeba mizigo yote inayotoka kwenye mazingira kwa kuona au kusikia mambo magumu yasiyo na majibu kwa muda huo unao hitaji majibu. *_Ni mawazo Makali yasiyoonyesha mlango wa kutokea_*
🎁👆 Kuna watu anasema kichwa kinauma bila ugonjwa,kichwa kizito,macho yanauka,machozi yanalengalenga,hasira kwenye uso,majibu makali naya mkato,kutukana na kizunguzungu, hayo ni matokeo ya *Akili/Nafsi kubeba jambo lisilo na Majibu wakati huo unaohitaji majibu*

20 Akamwambia, Mwalimu, haya yote nimeyashika tangu utoto wangu.
Marko 10:20

21 Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa na neno moja. Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kisha njoo unifuate.
Marko 10:21

22 Walakini yeye akakunja uso kwa neno hilo, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali nyingi.
Marko 10:22
🎁👆Akili ikikosa majibu inatoa picha nje haraka kwenye uso kuwa hapa majibu hakuna kwa muda huu,ni baada ya kusikia inapelekea mzigo wa akili.
3⃣ *MWILI* Hiki ni kiti cha mizigo itokanayo na hali ya hewa,vita ya kiroho,au changamoto za dunia.
🎁👆Kuna watu anasema Mwili wangu hauko vizuri,naumwa,hauko kawaida,sijui nimekuwaje,au anakuonyesha Jeraha la mwili,au anajiona mnyonge sana,wa chini,hafai kati ya watu, hayo yote ni matokeo ya Mizigo itokayo katika mazingira,adui kama wachawi na mapepo juu ya mwili wake.
3 Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu; naye hata sasa anashikamana na utimilifu wake, ujapokuwa ulinichochea juu yake, ili nimwangamize pasipokuwa na sababu.
Ayubu 2:3

4 Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Ngozi kwa ngozi, naam, yote aliyo nayo mtu atayatoa kwa ajili ya uhai wake.
Ayubu 2:4

5 Lakini sasa nyosha mkono wako, uuguse mfupa wake na nyama yake, naye atakukufuru mbele za uso wako.
Ayubu 2:5

🥦Kwa mtazamo wa hapo juu,utagundua *Kila mwanadamu aliye duniani,ana mizigo,awe kanisani au nje ya kanisa ila tunatofautiana aina ya mizigo, kuna mizigo inayokuumiza ila Haikuzuii uzima wa milele,japo yaweza kukukwamisha,na kuna mizigo ambayo inakuzuia moja kwa moja kumuona Mungu* Hapa ndo utaona umuhimu wa Kanisa na watumishi wa Mungu.
🥦Kanisa ni Mahali ambapo tunakuja Kutuliwa mizigo yetu yote, na Neno la Mungu ndilo nyenzo ya kutua mizigo ya watu.
🥦Kwa kadri unavyosikia au nenwa Neno la Kristo,katika uimbaji,kuabudu,kusifu mahubiri vikimnena YESU KRISTO automatically mizigo yako inashushwa, na kwa Kadri yakinenwa matatizo,watu mizigo inaongezeka.
🥦Na hapa ndo Mtihani na Huku kwa wasimamao madhabahuni pa Bwana,mwimbaji,mwombaji,muhubiri Yesu Asikike sana kuliko hali,vitu na maisha. Mizigo itatuliwa.
*_Msingi wa Somo_*
👉 _Maisha ya wokovu ni safari yenye mwanzo wa safari na mwisho wa safari._ *Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu; Wafilipi 1:6*
👉Na mfumo wa safari ya wokovu kuna vituo rasmi na vituo visivyo rasmi, kila kituo kina mchango wake katika safari yako. ( *_Vipo vituo vya kupumzika na kustarehe,vituo vya uchungu, vituo vya kujifunza, vituo vya kukatisha tamaa,na vituo vya kutiwa moyo na nguvu_* vyote vipo katika safari yako moja ya wokovu.)
*58 Basi, ndugu zangu wapendwa, mwimarike, msitikisike, mkazidi sana kutenda kazi ya Bwana sikuzote, kwa kuwa mwajua ya kwamba taabu yenu siyo bure katika Bwana. 1 Wakorintho 15:58*
👉Uwezo wa kutambua utofauti wa vituo katika safari,ndiyo nguvu yako ya kufika mwisho wa safari yako salama.
20 Bwana akasema, Mimi nimewasamehe kama neno lako lilivyokuwa;
Hesabu-Numbers 14:20

21 lakini hakika yangu, kama niishivyo, tena kama dunia hii nzima itakavyojawa na utukufu wa Bwana;
Hesabu-Numbers 14:21

22 kwa sababu watu hawa wote, ambao wameuona utukufu wangu na ishara zangu, nilizozitenda huko Misri, na huko jangwani, pamoja na haya wamenijaribu mara hizi kumi, wala hawakuisikiza sauti yangu;
Hesabu-Numbers 14:22

23 hakika yangu hawataiona hiyo nchi niliyowaapia baba zao, wala katika hao wote walionidharau hapana atakayeiona;
Hesabu-Numbers 14:23

24 lakini mtumishi wangu Kalebu, kwa kuwa alikuwa na roho nyingine ndani yake, naye ameniandama kwa moyo wote, nitamleta yeye mpaka nchi hiyo aliyoingia; na uzao wake wataimiliki.
Hesabu-Numbers 14:24
*KIINI CHA SOMO*
*_4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha.Yakobo 3:4_*
👉 _Katika somo letu kuna mambo muhimu kama 5 unapaswa kuya fahamu vema ili somo hili liwe baraka na nguvu na ufunguo wa maisha yako ya kiroho na kimwili_
1⃣Kujenga moyo wako.
2⃣Kujenga Nafsi yako
3⃣Uwezo
4⃣Kuto yumbishwa
5⃣Tufani yoyote
👉 *Kujenga Moyo wako* ni kuuzoeza moyo wako ambao ni Kisima cha Maamuzi, Kujua kuwa Mfumo wa maisha yako Unaratibiwa na Mungu na si Mazingira wala Mtu yeyote na kwa maana hiyo *Hakuna mwenye uwezo wa kubadiri Hatima yako* iliyopangwa na Mungu.
*23 Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. Mithali 4:23*
👉 *Kujenga Nafsi yako* Ni Kuizoeza Akili yako ambayo ni Lango(barabara) ya Matukio yote yatokayo katika milango mitano ya fahamu kuupelekea moyo ufanye maamuzi,kujua yakuwa Si kila Tukio uonalo lina Maana, Si kila sauti(maneno)usikiayo yote yanakufaa wewe,sikila hisia zikujiazo ni sahihi bali Kila jambo lina maana yake kwa muda wake CHAMBUA LA KUKUFAA.
*3 Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo 2 Wakorintho 11:3*
👉 *Uwezo* ni Nguvu ya kubeba mazito yanayokulemea moyoni na akilini na ukaonekana hukubeba kitu,pia ni nguvu ya kufanikisha lengo lako katika vikwazo vingi, nguvu inayo kusaidia kunyamaza wakati unatakiwa kusema, na kusema wakati unatakiwa kunyamaza( *Huo ndio Uwezo*)
1 Mara kulipokuwa asubuhi wakuu wa makuhani walifanya shauri pamoja na wazee na waandishi na baraza nzima, wakamfunga Yesu, wakamchukua, wakamleta mbele ya Pilato.
Marko 15:1

2 Pilato akamwuliza, Wewe ndiwe mfalme wa Wayahudi? Akajibu, akamwambia, Wewe wasema.
Marko 15:2

3 Nao wakuu wa makuhani walikuwa wakimshitaki mambo mengi.
Marko 15:3

4 Pilato akamwuliza tena akisema, Hujibu neno? Tazama ni mambo mangapi wanayokushitaki!
Marko 15:4

5 Wala Yesu hakujibu neno tena, hata Pilato akastaajabu.
Marko 15:5
👉 *Kutoyumbishwa* Ni namna unavyozidi kukaa katika Tumaini,Imani yako,lengo lako pindi inapotokea chamgamoto za kiroho au kimwili,au kimazingira za kukutoa katika Njia yako.( *To Stay Focused No Matter what circumstances  come across*) huko ndo kutoyumbishwa.
👉 *Tufani yoyote* Tufani ni chamgamoto,vikwazo,hali ya kukatisha tamaa,hali ya kuleta uzuni, vitu vyote vinavyo tishia Hali yako ya uthabiti na kufanikiwa na kusonga mbele ni *Tufani* Usiyumbishwe.
31 Saa ile ile Mafarisayo kadha wa kadha walimwendea, wakamwambia, Toka hapa, uende mahali pengine, kwa sababu Herode anataka kukuua.
Luka 13:31

32 Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilika.
Luka 13:32
👉 *_Kutoyumbishwa siyo kiburi,siyo dharau ni uwezo wa kupangua hoja dhaifu zinazo lenga kukudhahofisha utoke kwenye lengo la tumaini la wito wako_*
👉Sasa waweza kujua na kuona wapi tunaelekea katika somo letu na sasa utakuwa na hamu ya kusogea hatua nyingine ili uwe hodari katika maisha yako ya kiroho na kimwili. _Andiko letu kuu tulisome ili tuanze uchambuzi_
*4 Tena angalieni merikebu; ingawa ni kubwa kama nini, na kuchukuliwa na pepo kali, zageuzwa na usukani mdogo sana, ko kote anakoazimia kwenda nahodha.Yakobo 3:4*
👉Yakobo kuna kitu kikubwa hapa anajaribu kukifunua na kutupa ufunuo mpya kupitia chombo( *Merikebu, Usukani na Bahari na mawimbi yake na Nahodha*) hapa kuna siri kubwa ya maisha ya kiroho ukielewa itakusaidia sana.
👉 *Naodha* ndiye mwenye nia na lengo la safari yake inaanzia wapi na kuishia wapi. ( _Nahodha ni wewe mtu wa Mungu_)
👉 *Merikebu*  ni chombo kinacho beba abiria(watu)ambao imewapasa kutoka eneo moja kwenda lingine( _Chombo ni Wokovu wako_) na abiria ni mfumo wako wa maisha kama( Ndoa,uchumi,afya,elimu,huduma,nk)ambayo vipo kwenye Merikebu kubwa ya wokovu inabidi vifike salama mwisho wa safari yako Nahodha.
👉 *Usukani* _Uwezo wako_ wa Kiroho na Kiakili wa kuratibu mambo,kusikiliza,kuona,kuhisi na Ukayatolea maamuzi kwa kadri ya Nia yako,imani yako mbele za Mungu bila Kubadirishwa na Mazingira,watu,hali ili ufike uliko kusudia,uishi sawa sawa na ulivyo kusudia.
👉 *Bahari* ni ulimwengu huu ambao tunaishi wenye *Mawimbi* maudhi,vikwazo,changamoto nyingi.... Laini *_Nahodha anakokusudia kwenda anakwenda_* pamoja na misukosuko yote ya mawimbi,merikebu haifuati mawimbi ila inafuata Usukani ulioshikiliwa na Nahodha mwenye lengo la Merikebu inaenda wapi.
👉Katika safari yoyote ya kimaisha,ili usiharishe safari au kwenda mwelekeo ambao *Hukukusudia kwenda* tambua kuwa *_Si kila anayekuona kwenye safari anajua ulianzaje safari,nia ya kusafiri ni ipi, unasafiri na nini(ulivyo beba)na unaelekea wapi mwisho wako_* hivyo huna haja ya kupambana na msafiri mwenzako,kudharau,au kumuona kawaida, unamjua ni msafiri kwenye gari moja ila hujui ni nani katika safari hiyo,umuhimu wake kwako na anaishia wapi.
👉 Abiria wengine *Ni wezi, wengine  wana uwezo na taaluma ya Uokoaji pale chombo kinazama,wengine ni wabishi na wakorofi,wengine ni watu wema tu* hao wote ili ufike salama lazima ujue kucheza kwenye maeneo yao kulingana na hali zao.
👉 Kwa *Abiria wezi* tunza mizigo yako vizuri(na nena kwa habari ya mambo ya kiroho)
👉Kwa *Abiria wakorofi na wabishi* Kaa Kimya Usijibu hoja zao, utaharibu Radha ya safari yako na utaonekana nawe ni mpumbavu kama alivyo mpumbavu. ( *_Watu Dhaifu ujibu kila Neno, watu Hodari Unyamaza ili kupata hekima ya Kujibu sahihi_*)  Kanuni hii usipo ijua kiroho utakuwa mtu wa Kurudi nyuma kiimani kila mara.
👉 Kwa *Abiria wenye uzoefu wa uokoaji* Huwezi kuwajua mpaka itokee dhoruba na upate matatizo ya kuzama na wakuokoe katika kuzama( _Kwa maana hiyo hapo Unahitaji kutengeneza sura ya amani kwa kila mmoja,usiwe Kero kwa abiria wenzako safarini,maana nani wa kukuokoa humjui_) wezi hawajulikani,na waokokaji hawajulikani ila wakorofi na wabishi hujionyesha kwa maneno yao ndani ya merikebu.
48 Yesu akamwambia, Yuda, wamsaliti Mwana wa Adamu kwa kumbusu?
Luka 22:48

49 Na wale waliokuwa karibu naye walipoona yatakayotukia, walisema, Bwana, tuwapige kwa upanga?
Luka 22:49

50 Mmoja wao akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio la kuume.
Luka 22:50

51 Yesu akajibu akasema, Mwe radhi kwa hili. Akamgusa sikio, akamponya.
Luka 22:51
👉 Kwa *Abiria waungwana* kaa nao kwa sura ya uungwana maana hao ndiyo wanaoifanya safari yako Usiboreke.( *_hawa hawanaga muda na mambo ya watu,wao wanamuda na mambo yao,hata itokee nini wao kimyaa safari iende hadi mwisho_*
👉Unapaswa kujua anayejua *Thamani ya safari yako,na mizigo muhimu uloibeba ni wewe mwenyewe* wala si Abiria mwingine, ndo maana Abiria aweza kukanya mzigo wako,begi lako ili avuke apite atoke nje,maana hajui ukicho beba, yeye anaona ni gunia,au begi tu la kawaida, wewe huoni begi, *Unaona vitu vya thamani na muhimu ulivyo beba* Unaangaika kulikwepesha begi lisikanyagwe au kurushwa rushwa Ovyo.( *_Thamani ya wokovu wako na huduma yako, maisha yako unaijua wewe,kwepesha kwepesha wasiojali wasikanyage au kurusha rusha ovyo_*)
17 Basi, wapenzi mkitangulia kujua hayo, jilindeni nafsi zenu, msije mkachukuliwa na kosa la hao wahalifu mkaanguka na kuuacha uthibitifu wenu.
2 Petro 3:17

18 Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu na Mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.
2 Petro 3:18
*ILI USIENDELEE KUYUMBISHWA KATIKA SAFARI YAKO YA WOKOVU NA MAISHA JIULIZE MASWALI HAYA*
1⃣ Kwa nini nilianza safari hii?(huwezi ishia njiani au kupotezwa njia na wapuuzi kama unajua Lengo la kuanza safari hiyo na umuhimu wa kule uendako)
2⃣Nimeanza safari na nani? (hapa utajua safari inakuhusu wewe na si watu wengine) hii itakulinda usikatishwe tamaa na abiria waendao karibu hawafiki mwisho wa safari
3⃣Jiulize abiria wote ni kama mimi? (utajua kuwa abiria wanatofautiana sana pamoja nakuwa gari moja ila tabia ni tofauti) Hii itakusaidia usiangaike na abiria na kuumiza kichwa na tabia zao safarini angaika na uwezekano wako wa kufika salama(Vumilia maudhi niya muda, wengine wanaishia njiani,wengine wanapita kwenda kaa nyuma kabisa mbali nawe)
👉Jambo muhimu na la pekee ni muhimu kujua *Tumaini /lengo la wito wetu, halibadirishwi na mazingira,au kelele za watu tunaosafiri nao, bali tumaini letu linabatilika kwa maamuzi yetu wenyewe ya kukubali kukata tamaa na kurudi nyuma*
25 Usiogope hofu ya ghafula, Wala uharibifu wa waovu utakapofika.
Mithali 3:25

Kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako, Naye atakulinda mguu wako usinaswe.
Mithali 3:26

Maana bila shaka iko thawabu; Na tumaini lako halitabatilika.
Mithali 23:18
👉Uongoze moyo wako( *wewe mwenyewe*) usiruhusu mazingira au mtu mwingine nje na Bwana na neno lako wauongoze watakavyo wao utaishia njiani.
19 Sikia, mwanangu, uwe na hekima, Na kuuongoza moyo wako katika njia njema.
Mithali 23:19

Basi utaijua hekima kuwa tamu kwa nafsi yako; Ikiwa umekwisha kuiona; Ndipo itakapofuata thawabu; Wala tumaini lako halitabatilika.
Mithali 24:14.
*_Nimalize kwa kusema hivi, katika maisha ya kiroho au ya kimwili kuna vitu viwili au vitatu vikuu vyenye uwezo mkubwa wa Kuathiri Maisha yako yote mpaka unaondoka duniani_*
1⃣ *Adaptation*
2⃣ *Revolution*
3⃣ *Unique*
👉 *Adaptation* You lose your characters, Qualities then you absorb of other people( _Yaani unapoteza sifa zako na tabia zako unaanza kuishi za wengine_) Kuwa makini na adaptation inaweza kukugharimu pale itakapo hitajika uhalisia wako wewe kama wewe na si wa mazingira kutatua changamoto mbele yako.
👉 *Revolution*  Ambition,and struggle to change the existing system to follow your perception /desires ( _Yaani unafanya harakati na unatamani ugeuze mazingira au watu wawe kama wewe au upendavyo_) Hii ni nzuri sana ila hakikisha ulivyo unafaa mazingira yote na rika zote na hali zote na wewe una vitu muhimu vya kusaidia wengine. Ila utatumia nguvu kubwa sana na unaweza umia na kupiteza baadhi ya vitu vyako muhimu.
👉 *Unique* To be distinguished from other people, to possess your  own characters.( _Yaani maisha ya upekee sawa sawa na ulivyoumbwa,ulivyo chagua uwe sawa sawa na Nature yako_) Hii itakusaidia usigongane na watu,usiwe na stress utaenjoy maisha yako..
*_Imeandaliwa na Ev Elisha Kazimoto_*
         Whatsapp 0755444078