Friday, 26 May 2017

KIPIGO KILEKILE

*_NAKUPIGA KWA KIPIGO KILEKILE ULICHO NIKUSUDIA_*
     *_Ev Elisha Kazimoto(0755444078)_*
( *Katika Mkesha wa Shusha Kipigo Kilekile Ulichokusudiwa na Maadui zako*)
Shalom Mwana Maombi _Kila mtu katika maisha ana mimba ya mafanikio, kuna mimba ya uchumi wako mkuu,kuna mimba ya ndoa ya kicheko,kuna mimba ya Elimu,mimba ya Ajira, mimba ya huduma na utumishi nyumbani mwa Bwana, hizo zote zimebebwa kwa uchungu,zinalelewa kwa uchungu,mpaka kuzaliwa ni kazi imetumika_
*KUTOKA 21:22-25*
22 Watu waume wakiteta pamoja, wakamwumiza mwanamke mwenye mimba hata akaharibu mimba, tena yasiwe madhara zaidi; sharti atatozwa mali kama atakavyomwandikia mumewe huyo mwanamke; atalipa kama hao waamuzi watakavyosema. 

23 Lakini kwamba pana madhara zaidi, ndipo utatoza uhai kwa uhai, 

24 jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu, 

25 kuteketeza kwa kuteketeza, jeraha kwa jeraha, chubuko kwa ajili ya chubuko. 
_Lakini wapo wanaume(maadui, wachawi,wanadamu wenye hila) uteta kwa pamoja, ufanya vikao vya siri ili kupambana na mwanamke mwenye mimba(mtu mwenye maono) na kuharibu._
🏹Sikiliza ewe mwanamke(mtu uliye beba ndoto za maisha yako) hao hawalengi kukuumiza tu ila na kuharibu mimba yako.
🏹Sasa ni vizuri kujua lengo la adui umshugulikie mapema kabla ya kuharibu kwa *Kipigo kilekile* alicho lenga juu yako.
🏹Kama mwana harakati wa kiroho,mwombaji katika mkesha wa leo, *_Tunawapiga maadui zetu katika ulimwengu wa roho kwa kipigo kilekile walicho kusudia juu yetu, Bwana awapige kwa Mauti ile ile walioikusudia juu yako iwe juu yao, Wapigwe kwa migogoro ya ndoa,ya kazini,umaskini ule ule walio ulenga juu yako_*
🏹Hatuwaachii, tafakari ni mamvo gani yanakusonga katika safari yako ya maisha,?(wanaume wameteta kuharibu minba yako)washushie kipigo kile kile,wapige kwa Ajali hiyo hiyo walokuandalia,kwa Aibu hiyo hiyo walioikusudia,magonjwa yale yale wanayo kurushia. ( *_Huu ni Usiku wa Kuvua Vazi bovu nakuwavika walio kuvalisha_*) Nikuwarudishia hayo hayooo!
*_Yeremia 30 : 16 - Basi, watu wote wakulao wataliwa; na adui zako wote watakwenda kufungwa; kila mmoja wao; na hao waliokuteka nyara watatekwa; na wote waliokuwinda nitawafanya kuwa mawindo._*
Kataa kuliwa,kabla hawajala mimba yako Amuru watafunwe wao,Kabla hawajateka mambo yako Amuru watekwe wao kwa jina la Yesu.
*_Inuka,usiogope mimba yako itazaliwa ila kwenye maombi yako omba mimba yako isiharibiwe mpaka izaliwe,na mwambie Bwana Yesu ajuaye mwisho kabla ya mwanzo, mwambie Walio Teta gizani,makabulini,maofisini baharini na kwenye matambiko waharibu mimba yangu huko huko, Wageuziwe kwa kipigo kile kile walicho kilenga juu yangu kiwe juu yao wakati mimi na pita salama._*
🏹Nisikilize mtu wa Mungu, wabaya wako wataangukia mtegoni walioutega wenyewe,wakati wewe Unapita Salama waliko kutegea.
*ZABURI 141:9-10*
9 Unilinde na mtego walionitegea, Na matanzi yao watendao maovu. 

10 Wabaya na waanguke katika nyavu zao wenyewe, Pindi mimi ninapopita salama.
       *Ev Elisha Kazimoto*
       0755444078

Monday, 22 May 2017

UFUNGUO WA 7

🔑🔑🔑🔑🔑🔑🔑 *Ufunguo wa 7: MWENZANGU ANAHITAJI KUWA SALAMA(KULINDWA)*
_Salaam wana ndoa,kwa mara nyingine tunasogea katika meza ya Maarifa tupate ufunguo wa saba wa kufungulia chumba cha Amani na furaha cha ndoa zetu,na sasa tuangalie Nguvu ya kumlinda mwenzako inachochea vipi utulivu wa ndoa_ *Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto* katika uchambuzi wetu, karibu.
☔ Kuna vitu ukivitazama katika mwili wa mwanadamu waweza kuviona ni vidogo na havina maana saana kuvijali, kumbe ondoa uone balaa lake. ( _Umewahi kufikilia kope za macho yako ziki nyofolewa nini kitakutokea?ndani ya dk 1 unaweza usifumbue macho tena., au ulisha wahi kujiuliza kwa nini kope za macho yako zina cheza kila sekunde kama mshale wa saa? Zikitulia utakuwa kipofu kwa uchafu utakao vamia macho yako_) sasa kope za macho zina jua kitu kimoja *Jicho Lazima Lilindwe* muda wote ndo shuguli zingine ziende.
☔Mwana ndoa, mkeo/mmeo ni kama mboni ya jicho lako na wewe ni kope zake,unahitaji kuwa *Active Kumlinda* kumlinda kisaikolojia,kimwili na kiroho ndipo ndoa yenu itulie iwe ya furaha.
☔Kuna vitu mwana ndoa unahitaji kujua, moja kuna watu wakorofi, wapendao kujishugulisha na mambo ya wengine hata kujeruhi mioyo ya watu,iwe kazini au kanisani, hakikisha mwenzako anajua anaye mlinzi mtetezi katika maisha(Jenga mazingira ya kumwondolea mazingira ya Personal attacks za watu aidha kwa kupeana mbinu za kuishi,kufanya kazi,kuongea,ku interact na watu ili kupunguza mazingira ya mwenzako kujeruhiwa. *_Note. Mwenzako akijeruhiwa na watu nje,we ndo utaganga vidonda ndani  na wakati huo kuna vitu ndani vitavurugika_* Pili, Familia yako na ya mwenzako ziwekee mipaka ya kumnyoshea mkono,mdomo na macho mwenzako kufikia kumjeruhi(Wazazi, mawifi,mashemeji,ndugu zako)wajue mkeo/mmeo hawana *Mamlaka* yakumgeuza watakavyo, jua wewe *Ndo uliye na mkataba na mwenzako* hawa wengine ni wapita njia( Ukiruhusu mwenzako ashambuliwe, jua wao hawatakuwepo mchana wala usiku moto utakapo kuwa unawaka ndani mnaungua wawili.)
☔Tatu, Hakikisha katika maombi yako unamwombea mwenzako kila siku alindwe na maroho yavamiayo watu na kubadiri tabia zao. *_Si wote wenye migogoro ya ndoa zile tabia korifi ni nature yao, hapana walishambuliwa_* Ndo maana wenzao wanawashangaa na kuona hapana huyu mtu hafai kuishi naye wakati mwanzoni walioona wanafaa.
☔Kazi ya wachawi na mapepo ni kukupa tabia korofi itakayo mkera mwenzako mpaka muishi kinyume na matarajio na lengo lao la kuzalisha kizazi kibovu chenye malezi mabaya.
☔Uombapo mkinge mwenzako na maroho mabaya,kemea tabia mbaya zinazo kera, mauti, ulemavu,magonjwa sugu,mateso nk ili ndoa yenu ikae na furaha.
Nne, Mlinde mwenzako kisaikolojia hasa katika *_Utumiaji wa lugha nzuri katika mawasiliano,kumuhudumia huduma anazo stahili kama mme/mke asianze kuwaza huyu mtu vipi? Hakikisha tendo la ndoa kwako si mpaka ulazimishwe au ubembelezweee nk_* (huu ufunguo unajitegemea wa tendo la ndoa) tutauchambua peke yake.
NB: _Ndoa ni furaha ya wiwili,inayowafanya na wengine wavutiwe na ndoa na kumbariki Mungu,ila ndo ikiwa mbaya nijanga liumizalo kama mfiwa,na uzima furaha yakila kitu, kula vizuri,vaa vizuri lakini kisaikolojia unakuwa na maumivu makali zaidi ya utungu wa mwanamke mwenye mimba. Hayo yote tunayaepusha kwa Kulinda kona 4 hizo tulizoona, kumbuka maumivu ni yenu wawili ndani wengine wasababishaji life is going as usual. Usikubali kitu chochote,mtu yeyote awe kero,msumbufu kwa mkeo/mmeo_
    *Psychologist Ev Elisha Kazimoto*
          0755444078

UFUNGUO WA 6

🔑🔑🔑🔑🔑🔑  *Ufunguo wa 6: NIKIYATAMBUA MAZURI YAKE(MKE/MME WANGU),NIKAYASIFIA NITAMFANYA AYATENDE ZAIDI*
_Kwa mara nyingine tunapanda ngazi ya Maarifa ili tufikie kilele cha Furaha,Amani na Upendo ulokusudiwa kuonekana katika ndoa za watu, leo tunaungalia ufunguo wa 6, *"the Issue of Acknowledging"* Tabia ya Kutambua jambo alilotenda mtu_ Karibu uoo nami mchambuzi  wako Psychologist Ev Elisha Kazimoto.
🏹Nianze kukupeleka katika Nature ya Binadamu na Saikolojia ya Binadamu ndo ujue wakati mwingine waweza fungua mlango kwa adui bila kujua au kwasababu ya maarifa kidogo na kupelekea msiba katika ndoa,leo upate maarifa usione gharama kuanza upya.
🏹Umewahi alikwa eneo kwenye sherehe au tukio flani muhimu, halafu wakasimamisha watu,au kuwatambulisha watu,wewe ukasahaulika unavyo jisikia? Umewahi ona umefanya kitu,kwenye jamii wanapo tambua michango ya watu halafu na wewe unechangia lakini waka mute,wasikutambue kwa mchango wako unavyo jisikia ?kuna namna ya kuumia na maswali ya kwa nini waniruke, wanipotezee, hawajaona kama nimefanya cha maana nk, *_Nature ya binadamu anatamani akifanya jambo atambuliwe,apongezwe, aambiwe Yes 👍 utaona kasi,furaha atakayo kuwa nayo_* Tabia hii tumeichota kwa Mungu, anahitaji asifiwe akutendeapo jambo.(Atambuliwe ndo maana huwa tunaoa ushuhuda, na bible inasema kila aliye na mwana anao ushuhuda.
🏹Kuna vitu vidigo sana ambavyo vinadharauliwa lakini kisaikolojia huwa ndo nguzo kubwa ya kichocheo cha hisia.
🏹Kama unapenda kuona mwenzako jinsi ambavyo hakuumbiwa kununa,au kuzira zira, na alivyo na sura nzuri,tabasamu zuri,lugha nzuri, nk, *_Anza kutambua matendo yake anayoyatenda_Mfano jizoeze kumwambia mwenzako, jambo hili umefanya vizuri, amevaa vizuri msifie mwambie umependeza sana, amepika chakula mwambie umepikia vizuri,kitamu, haba anefanya kitu katika familia kidogo au kikubwa mwambie umefanya vizuri sanaa.
🏹Neno Asantee,umefanya vizuri,umependeza, nashukuru, umejitahidi nk huonyesha jinsi mwenzako alivyo wathamani kwako, unavyo mkubali,alivyo wa pekee, na mpa mtu mzigo wa kuendelea kujitahidi kufanya bora zaidi kila siku. _Makosa mengine tuyaonayo yanafanywa na wenza wetu mpaka tunakereheka mpaka tuna hitirafiana, yaweza kuwa ni Matokeo *Yakuona makosa ya wenzetu na kuyazungumza mara kwa mara,kumlaumu kwa hayao, kisaikolojia umeendelea kumpa nguvu ya kukosea* kama vile ukiongea mazuri mara kwa mara kwa mwenza wako unampa nguvu ya kutenda hayo_ sasa ni wewe kuchagua kusifia moja,2,3....zuri alitendalo mwenza wako ili umpe nguvu ya kuyatenda hayo mengi? Au ulaumu madhaifu yake kila siku umpe nguvu ya kutenda hayo!
🏹 NB:  _Kuna vitu vina leta raha na kujisikia safe pale mwenzako anapokwambia nakupenda, polee kwa kazi, umefanya vizuri mpenzi wangu,umependeza, hivi kwani utata na kigugumizi kiko wapi?kama usipo mwambia mkeo au mmeo utamwambia nani? Mpaka unaingia kaburini hayupo mtu wa Karibu anayeweza chukua nafasi ya mwenza wako,auburudishe moyo wako wakati mwenza wako yupo hai,ukibana raha hiyo kuitengeneza pata pesa,utajiri but kisaikolojia utakuwa umevurugika na ndo hasara kubwa duniani utakuwa umepata._
    *Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve)*
        0755444078

Saturday, 20 May 2017

UFUNGUO WA 5

🔑🔑🔑🔑🔑 *Ufunguo wa tano:5⃣(Mke/Mme) ANANIHITAJI MIMI NA SIYO VITU VINGINE*
_Uheri wewe uliye katika site ya kupata Maarifa yatakayo kufanya usiinfiliwe na mdudu alaye ndoa chini kwa chini,kwa kutumia sumu ya ujinga, sasa karbu tuendelee na ufunguo wa 5 kati ya 12 za ndoa ya furaha na kicheko_ by Psychologist Ev Elisha Kazimoto.
🔰Kuna Mistakes huwa inafanywa na wana ndoa kimzaa,kwa kudharau au kutojua, nini *_Mkeo/Mmeo anakuhitaji wewe kuliko vitu vyote, si suala la pesa zipo,hazipo, magari umenunua,matumizi unaachilia, na chakula unapika vizuri, hivyo vyote ni ziada ya ndoa_* Ila msingi mkubwa wa ndoa ni kwamba mwenzio ANAKUHITAJI WEWE, kama pesa zilikuwepo angekuwa anazihitaji angezitafuta na akapiga chini kuoa au kuolewa,ila anakuhitaji wewe, mtoto yupo au hayupo huyo ni waziada kwa utukufu wa Mungu ila yeye alikupenda wewe ndo alikuona kwa sura, *_Usipo kuwa makini kutumia nafasi yako ya kuhitajika, Usipo hitajika tena kwa huyo moyoni mwake,ndipo utakuwa umeizika ndoa yako_* wewe unahitajika sana kwa mwenzako.
🔰Kuhitajika kwako kuna sura pana sana, maneno yako matamu,ya faraja,yakusifia,yakupongeza yanahitajika sana kwa mwenzako, kujua mwenzako anahisi nini,anajisikiaje,anataka nini,nini kinamtatiza,nini ufanye ajisikie furaha huo ndo umuhimu wako kwa mwenzako.
🔰Ndoa nyingine zimepata shida sababu ya kuacha Ombwe(gap/vacuum )katika moyo wa mwenzake, lakini wao wanakuwa busy na mambo mengine,watoto,biashara,ofisi,huduma,simu nk,ilimradi pesa ipo,hauumwi,unakula,unavaa nk, hii siyo sawa. _wewe kama wewe unathamani zaidi ya pesa na magari na watoto_
🔰Je, mwenzako yuko huru kwako muda wowote,unapatikana kisaikolojia na kimwili anapokuhitaji?au upatikanaji wako niwa masharti, niwakuvizia,kubembeleza? Unahitajika kuwa *Available* Usije ukaweka kitu chochote kwenye nafasi yako kikuwakilishe kwa mwenzako pale anapokuhitaji.
*_Kuwa Availbale_* _Ni pamoja na kumfanya mwenzako asihisi upweke kihisia,kimwili na kiroho, bali ahisi kukamilika.
NB: _Maamuzi yako kwa mwenzako yakila siku katika kutimiza majukumu na wajibu wako katika familia na ndoa yanaweza mfanya mwenzako kuona/kujua Humuhitaji ata kama hujamwambia sikuhitaji, au hata kama hamjaachana. Fanya Mambo yatakayo mfanya mwenzako ahisi Wewe Unamwitaji sana, na yeye anakuhitaji sana katika naisha yake_
    *Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto*
      0755444078

Friday, 19 May 2017

UFUNGUO WA 4

🔑🔑🔑🔑4⃣ *Ufunguo wa Nne: IMENIPASA KUBEBA MADHAIFU YAKE ILI AWE NA FURAHA*
_Karibu kwenye mwendelezo wa kujifunza juu ya funguo 12 za ndoa yenye kicheko, na leo tunaangazia ufunguo wa 4, unajua nini? *Kwa Namna yoyote hatutaachia nafasi Kisaikolojia wala kiroho mpaka Adui aingize Sumu na mpasuko katika ndoa zetu* Fuatana na Msaikolojia Ev Elisha na Mungu akubariki_
♦Nianze kwa Kuzibua ufahamu wako, Wewe uliye binadamu unayeishi duniani Unayo mapungufu,unao udhaifu,pamoja na kuokoka,kutumika unao udhaifu *Kama mwanadamu* sizungumzii udhaifu wa Kutenda dhambi(Nielewe vizuri), Nasema hivi kama mwanadamu unao udhaifu, na Ndiyo maana ukaumbiwa Msaidizi mke/mme.
♦Miongoni mwa mapungufu uliyokuwa nayo, ni pamoja na kutojizalisha, kutoweza kujifariji,kujipa furaha,kutimiza mahitaji yako yote *Kikamilifu* kuna kutimiza mahitaji yako ila si kikamilifu, Ndo maana ukapewa Mwenza ili azibe mapungufu yako.
♦Yako mapungufu mengine unayaona kwa mwenzako,baada ya kuyapunguza umeyakuza kwa kuyatangaza kwa watu, kumsimanga kwayo,kumdharau kwa sababu ya mapungufu hayo na *_Huo huwa ndo mwanzo wa migogoro ya ndoa,mpasuko na kuachana_* kumbe ilibidi umsaidie,umtie moyo,umfanye aone mapungufu yake hayana nguvu katika ndoa yenu, bari faraja ndo imetawala *_Na huo huwa msingi wa ndoa imara na yenye furaha_*
♦Miongoni mwa vitu vinavyo mfanya mtu ajisikie vizuri na kuongeza upendo juu yako ni kuona unabeba udhaifu wake,unamtia moyo katika udhaifu wake,unajitahidi kuyabadirisha madhaifu yake yawe uwezo wa kufanikiwa. *_Ukifanya hivyo utaona mwenzako anakupenda sanaa,na kukuheshimu na kukuthamini_* Hii ndo ladha ya ndoa tunaitafuta katika maisha yetu.
NB: _Nahitimisha kwa Falsafa ya Mungu alosema *Nitakufanyia msaidizi wa kufanana nawe, unaielewa?* Maana ya kufanana si kwamba mtafanana kila kitu,tabia,kama we mchoyo basi unapewa mchoyo mwenzako,kama mdhaifu wa kusoma neno unapewa mdhaifu mwenzako, mfanano aloukusudia Mungu ni mfanano wa Kumkamilisha mwenzako,yaani atakufanyia msaidizi wa kukukamilisha(kujufunika katika upungufu wako) mfano wake ni huu, mfuniko wa soda na chupa ya soda ufanano wake ni mfuniko uzibe chupa siyo vikingane na mdono wa chupa hapo utaegesha tu mfuniko siyo kuifunga chupa iwe imara_ Basi Funika madhaifu ya mwenzako mfurahie ndoa.
   *_Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve)_*
         0755444078

Thursday, 18 May 2017

UFUNGUO WA 3

🔑🔑🔑3⃣ *Ufunguo wa tatu: MFANYE MWENZAKO WA PEKEE*
_Karibu tena katika ngazi ya tatu,tunapo tumia 🔑 kufungua chumba cha tatu kati ya 12 vya ndoa ya kicheko na furaha_
✍Ladha ya ndoa kwa mwanandoa yeyote ipo katika Kutofautisha kati ya watu wengine,vitu vingine na Mpenzi wako( Huu ndo ufauru wa kukinda penzi lenye furaha)
✍Nikupe siri moja ambayo wanandoa wengi wanaitupa njiani mara baada ya kuoana na kusogea mbele miaka 2,3,6..... Unajua tendo ulilolifanya (baba kumchagua huyo mkeo) au wewe mama tendo la kusema YES kwa huyo uliye naye sasa *_Ulifanya tendo la kuonyesha Upekee kati yake na wengine wote,ndo maana mkapendana sanaaa sababu ya kuonyeshana utofauti kwa uchaguzi_* Nini sasa kinawafanya watu wawe chini ya migogoro? Inaweza kuwa nguvu ya kumtofautisha mwenzako na wengine,vitu vingine impotea au imepungua.
✍ *Kwa nini nimfanye mwenzangu wa pekee?* Ukilielewa swali hiki vizuri hutokuja kuruhusu vitu vidogo vizime vicheko vya ndoa yenu. *Swali ni Kwa nini*
🔑 Anavyo nifaa,hayupo mwingine wakunifaa vile( kumbuka watu wote wanamipaka mikubwa katika kukuhudumia,kukufurahisha na kukutunza, *Ila mmeo/mkeo hana mipaka* hivyo Una sababu yakumfanya mwenzako aonekane wa pekee.
🔑Sababu nyingine, Niliwaacha wengine,kwaakili yangu timamu na kuona huyu anafaa kuliko wengine, Tendo la kufanya maamuzi ya kuoana na huyo ni kumfanya pekee, basi fanya tendo lingine la kuteleleza mambo ya matendo yabkila siku ya kumuonyesha mwenzako ni wapekee.
✍Je, unahitaji usimchoke mwenzako?  Jitahidi kumfanyia mambo atakayoona kweli ni mimi ni watofauti. *_Ili uonyeshe upekee kwa mwenzako, chunguza vitamanio vyake,anapenda nini, anahitaji nini, vitu gani vina kamata hisia zake, vifanye hivyo utaifanya ndoa yako iwe na burudani_*
✍Mama, ndani onyesha upekee wa mmeo,kwa mapishi,vyakula,kumuhudumia kwa kipaumbele, hayo mambo yanaonyesha upekee kwake,na nguvu ya upendo inaongezeka.
✍Baba, mfanye mkeo aone kati ya wanawake wengi na yeye anapendwa,anafanyiwa vitu vya kipekee, surprise, outing ndogo ndogo,simple gift nk, upendo unakua, ujue si wote wanayafanya,sasa ukiyafanya ndo unamfanya wa pekee.
🔑🔑🔑 NB: _Jambo moja unahitaji kulihifadhi Akilini,Ndoa ni Gharama ukikwepa gharama hata kama mlianza kwa vicheko, mtaendelea kwa kununiana, ingia gharama ya Kumfanya mwenzako wa pekee tofauti na wanawake wengine na Wanaume wengine, Pili ujue, kumuona wakawaida na kumshusha thamani haikusaidii ila inakugharimu,maana hutatafuta mwingine,hatatoka wa mwingine aje kukuzibia pungu lake, pambana mwenyewe kumfanya Ang'are kuliko wote_
   *Mwanasaikoloji Ev Elisha Kazimoto*
       0755444078

UFUNGUO WA 2

🔑🔑2⃣ *Ufunguo wa Pili: MIMI NDIYE FURAHA YA MWENZANGU(MKE/MME WANGU*)
_Karibu katika mwendelezo wa uchambuzi wa funguo 12 za Ndoa ya Furaha na Amani,na leo ni ufunguo wa pili *Mimi ndiye Furaha yake* Karibu_
✍Katika maisha hakuna jambo zuri kama kumfanya mwenzako(hasa kwetu wana ndoa)Afurahi,ajisikie utulivu wa wewe kuwepo, na wewe kuwa sehemu ya maisha yake.
✍Kosa kubwa la Kisaikolojia kwa wana ndoa,ni kususia hisia za mwenzako, kutojali hisia za mwenzako. Jambo unalopaswa kujua ni Hakuna mtu aliye Katika Agano la ndoa anayeweza kujifurahisha mwenyewe,au kufurahishwa na mtu mwingine, isipo kuwa yule aliyeungwa naye. Ndiyo maana maumivu yakuumizwa na mwenzako katika ndoa ni makali kuliko yale unayoweza kuumizwa na mtu yeyote, na ndiyo maana mtu akiumizwa na watu,kazini,ofisini nk,akija ndani akakuta furaha saikolojia yake ya maumivu inapoa haraka kuliko aloumizwa kwenye ndoa aende nje,hata angepata exposure ngapi maumivu hayakomi, mpaka mwenzake atakapo Amua kumfurahisha.
✍Usidharau Furaha katija maisha ya ndoa, furaha *_Inafungua mioyo ya wana ndoa,inatoa mwanga mpya wa mawazo mapya kwa mtu_* hakuna aliyefanikiwa kifamilia kiroho au kimaendeleo kama hamja fikia hatua kupeana,kutunziana furaha.
✍Miongoni mwa vitu wana ndoa ni vya kujali sana ni kutengeneza mazingira ya mwenzako kufurahi, *_Usitegemee katika maisha yako kufurahi, kama mwenzako hajafurahi_* Furaha ya mwenzako ndo inayo zalisha furaha yako.
✍Nini kinafanya mwenzako awe na furaha? Ni swali muhimu, lakini ni swali lililo wazi na lakisaikolojia, (hakuna aliyeoa auvolewa bila kufurahishwa na mwenzake) mambo yaliyo kufurahisha tangu unampata huyo mpaka ukasema YES,vitu hivyo nivyakulinda. _Ndoa zimeingia katika migogoro hata kuvunjika baada ya wanandoa kuruhusu mmoja kuumia,kuzalisha uchungu,na kudharau hisia za mwenzako hata kupelea uchungu wake kukuambukiza na ndipo Amani upotea._
✍Vitu gani vinamfurahisha mmeo/mkeo( *Caring yako,Lugha yako, huduma yako,kumpenda Mungu kwako, Uaminifu wako etc*)?
Ukihitaji ndoa yenye kudumu katika Amani, na Vicheko, hakikisha unalinda furaha ya mwenzako,buni vitu vinavyo mfanya afurahi , *_Ni nature, Furaha kuzalisha vitu vizuri, umewahi kusoma andiko linalosema Furaha ya Bwana ni Nguvu zetu?_* hiyo ndo nafasi ya furaha. Hakikisha mke/mme wako anafurahi kwa uwepo wako.
✍ Usichanganye, pesa,mali nk (Vitu )siyo chemichemi ya furaha ya mwenzako, ni maisha yako mwenyewe ya kila siku mbele ya mwenzako.
NB: Kumfanya mwenzako afurahi ni kutengeneza network ya maisha yasiyo na stress na kujuta.
     *_Ev Elisha Kazimoto_*
       0755444078

Tuesday, 16 May 2017

FUNGUO WA 1 KATI YA 12

🔑🔑 *FUNGUO 12 ZA NDOA YENYE KICHEKO*🔑🔑
_Haleluyaa, ni haki yako kuifurahia ndoa na nimapenzi ya Mungu kila umwonapo mwenzako uhisi Mungu alikupendelea na kukuzawadia huyo. Njia nyepesi na muhimu ya kujenga dhana hizi mbili na zikawa katika uhalisia ni Kujifunza,kupata maarifa ili usikosee katika kutunza mwono wako wa kwanza_
*Leo naanza kukupakulia siri ya ufunguo mmoja mmoja npaka zitakapo isha 12*
1⃣ *NILIYE MCHAGUA(HUYU) NI MZURI NA NDIVYO ALIVYO*
🔑Ufunguo wa kwanza unajikita na saikolojia yako, mtazamo wa hisia zako na tafsiri za ndani za hisia zako, kabla ya kuangalia mazingira ya nje na madhaifu. _Kwa kawaida huwa hakuna mtu anachagua mtu mbaya kwake, huyo ulo mchagua ni sahii na ni mzuri, huwezi kumpenda kwa viwango,kabla saikolojia yako haimtazami kuwa ni mzuri(si suala uzuri wa sura tu,yaani ni mtu sahihii anaye tosha kukamilisha furaha yako) kwanza umfikirie na kumuona ni mzuri._
Sasa mapungufu mengine aliyo nayo yanaweza futwa,badirishwa,kwa mtazamo wako wa unamuonaje mwenzako?
Kuna kosa kubwa wana ndoa wanalifanya linaleteleza kupoteza ladha ya penzi lenu. *_Pindi ikitokea mwenzako akakosea kwako, mara moja,2,3 unafuta Uzuri wake kichwani mwako aliokuwa nao kwako hata ukamchagua_* hili ni kosa la kisaikolojia linaloweza kuifanya ndoa yako iyumbe.
Unajua wana ndoa,unapaswa kujua uwe mke au mme, kosa au kutofautiana, hakubadirishi utu na uzuri wa asili ulioona anao huyo mwenzako hata ukaamua kumfanya ni mtu wa pekee wa maisha yako. Hasa tuliookoka, unajua ndoa *Selection of a Single Best Pertner to Move with* si jambo linaloweza futwa na simple mistakes ndo maana Bible inasema alichounganisha Mungu mwanadamu hatenganishi mpaka kifo. _Jenga saikolojia ya makosa,itirafu ni sehemu ya kudhihirisha uhalisia wa binadamu yeyote,ila Uzuri wake ulio ndani yake ni bora zaidi ya makosa haya,sasa niweke mazingira ya kumsaidia kufuta makosa na kulinda uzuri wake kwangu_
NB: ya ufunguo wetu wa 1🔑leo, *_Usikubali Makosa ya kimazingira yafunike uzuri wako au wake kwa mwenza wako, pambana kuuona uzuri wake ndani yake na umsaidie auishi uzuri uliokufanya useme YES KWAKE_*
   MWANASAIKOLOJI EV ELISHA KAZIMOTO.
       *0755444078*
   _PARADISE UNIVERSITY(MARRIAGE CORNER )_

Friday, 12 May 2017

SABABISHA HASARA KWA ADUI

*KUISHI KWANGU NI HASARA KWA ADUI*
       *_Ev Elisha Kazimoto_*
      *0755444078*
_Shalom leo usiku wa maombi ya mkesha,nikuletee message fupi ya kusimamia katika vita yako ya kiroho na kimwili_
👉Mara nyingi tunawindwa,hatujui au tunajua ila ujue unawindwa na wachawi,watu wenye wivu na maisha yako,lakini sikiliza neno moja kabla ya mambo yote( Kuokoka ni kupakwa mafuta ya ushindi,mafuta hayo huwezi kuyafuta juu ya mtu kabla hajatimiza kusudi la kupakwa mafuta yale)
1 Samweli 20 : 31 - Maana wakati mwana wa Yese akiwa hai juu ya nchi, wewe hutafanikiwa, wala ufalme wako. Basi, sasa peleka, ukamlete kwangu, maana hakika yake atakufa huyu.
*_Kumbe kuendelea kuishi kwangu kama mpakwa mafuta,kunawafanya maadui kutofanikisha madili yao. Nasema Sitakufaaa kwa jina la Yesu madili ya maadui yaendelee kukwama_*
👉Ni sikilize,kinaposemwa kifo na kutofanikiwa panua akili yako na ufahamu wako wa kiroho( maadui wanajua kuendelea kwako kusimama kiroho,kuwa moto kiroho hawatafanikisha kukunasa wewe na familia yako, mpaka kwanza waue kiroho chako) *Sema hafi mtu*
👉Wachawi wanajua,kanisa likiendelea kuwa na maombi,umoja,mikesha ya nguvu,naombi ya kufunga hawataweza kuliua,kulivuruga,kuteka watu,kwa hiyo wanahitaji waue kwanza hizo program zinazoleta mchemko wa kiroho ndo waweze fanikisha biashara yao( *Sema Halipozwi kanisa hili*)
👉Wanadamu,maadui wanajua kama ndoa yako itaendelea kuwa ya furaha na amani,hawatafanikisha kuvuruga uzao wenu na uchumi wenu na maendeleo yenu, kwa hiyo mpaka wawagonganishe vichwa kwanza( *Sema hatugongani katika ndoa hii*)
_Hivi sentensi ambayo iko pale kwenye msitari umeielewa,Sauli(adui wa Daudi) anamwambia Yonathani, "Mwana wa Yese awapo hai katika nchi wewe hautafanikiwa,mlete kwanza auwawe" umeitafakari?_ Adui hawezi kufanikiwa mbele ya mwenye haki,aliyepakwa mafuta ya ushindi,mpaka kwanza akuue,akuondoe mbele yake. *_Sasa hasara kwa maadui,bahati mbaya,mafuta ya wokovu na utumishi tukiyo pakwa hayaruhusu mtu kuuwawa kabla ya kukamilisha kusudi alilopewa_*
👉Sasa nizamu ya kuomba,kupangua mauti zote zilizoandaliwa juu yako, *Mauti za ndoa, za uchumi ,za kazi,za afya za kiroho,nazibatilisha kwa jina la Yesu,naita upako wa maguta ya Kristo ya wokovu tuliyo pakwa ya uhishe kila kitu ili maadui wasifanikiwe mikakati yao*
_Isaya 61 : 10 - Nitafurahi sana katika Bwana, nafsi yangu itashangilia katika Mungu wangu; maana amenivika mavazi ya wokovu, amenifunika vazi la haki, kama bwana arusi ajipambavyo kwa kilemba cha maua, na kama bibi arusi ajipambavyo kwa vyombo vya dhahabu._
*_Huu ni mwaka @2017 wa Kwenda mbali hazimishwi mtu,hakwamishwi mtu,harudishi nyuma mtu,hafi mtu mpaka tumefika tuendapo kwa utukufu wa Mungu baba_*
     Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve)
    @Anointedman
*0755444078*