Friday, 29 June 2018

AINA 5 ZA WANAUME

Habari ya uzima kaka,,,,,nipo na swali ,,,,,je kunao wanaume wanaopenda kulalamika kila wakati hta kama mabibi zao wamefanya mambo mazuri kiasi gani,,,,they can't appreciate at all,,,kila time ni complains tu,,,,hao wanaweza fanyiwa nini natunawaita akina nani?
...........................................
*Anajibu Mwanasaikolojia Ev Elisha Kazimoto( Whatsapp 0755444078)*

_Katika mahusiano ni vizuri unapoingia katika mahusiano ya uchumba au kwenye ndoa,jitahidi kusoma tabia na Hulka ya Mwenza wako na Uridhike nayo au Uiboreshe sawa na unavyopenda_.
👉Kwanza inabidi ujue aina ya mme wako(kulingana na muuliza swali):.
1.Wanaume wasiotaka kuonekana hawajui kitu flan.( *_Hawa bhana ni wanaume ambao kila kitu anakijua,hata kile asichokijua anajifanya anakijua, mara nyingi hawa uwa wanakawaida ya kupenda kujulikana na sifa_*) Tabia hii hutokana na kukaa kwenye mazingira yasiyompa changamoto au watu wasiompa changamoto ila yeye anajiona ndo yuko juu ya wote.
👉Watu wa aina hii awe mke au mme mara nyingi huwa kero hata kwenye familia au kwenye jamii maana HAWASHAURIKI ila yeye akushauri. Mara nyingi maamuzi yao ni ya KUSHUTUKIZA hayana mipango na mashauri kwakuwa wanapenda waendelee kuoekana wao ndo wanaweza na wanajua sana kuliko wengine ili waendelee kuogopwa(Hii ni aina ya kwanza ya watu(kwa muuliza swali, aina ya kwanza ya mme)
2. *Wanaume wasiotambua nafasi ya mwanamke* Hawa ni aina ya wanaume ambao saikolojia yao imeathiriwa na mazingira ya kimakuzi,kimalezi,na makundi, hawa mara nyingi wana kitu tunakiita *Poor Psychological Interpretation* (Udhaifu wa tafsiri katika akili zao)mara nyingi wanapenda kuona wenzao Hawawezi,hawajui..... *Hawa wana  Generalization Problem*  (tatizo la kujumuisha) kama waliona,walipitia,walisikia, kwa wazazi,ndugu, jamii udhaifu wa mwanamke mmoja au baadhi ya wanawake wanamapungufu kadhaa, *Uyahamisha na kuyafanya ni matatizo ya wanawake wote* uanza kujihami (defense mechanism ) hapa ndo tunapata wale *Wasiosifia wake zao,hata wafanye vizuri,wavae wapendeze,lolote niwagumu kusifia* kwa nini hawafanyi.... Saikolojia yao inawambia KUMSIFIA NIKUMPANDISHA NAFASI mlingane,au akudharau,kukuzoea.
3. *Aina nyingine ni wanaume wa Heshima*(tunawaita WANAUME MACHIFU ),hawa wanapenda tu kuwa juu,kuheshimiwa,wanapenda kuweka mipaka (daraja kubwa)kati yao na wake zao mpaka watoto wao. Hawapendi kuzoelewa na mke wala watoto.
4. *Kuna BABY HUSBAND(Wanaume watoto)* hawa ni wanaume wadekaji,lakini pia niwapolee,ila hawajishulishi kiakili,kila kitu mpaka aamuliwe na mtu mwingine aidha wazazi,ndugu au marafiki. Hawa ikitokea shida ndogo kwenye ndoa na familia kila eneo watajua,wanahaha na kuogopa sana.
5. *Friendly Husband*(Mwanaume Rafiki) hawa ni miongoni mwa wanaume AMAZING  & ROMANTIC (wanaume wa pekee na wamahaba)wanaheshimu hisia za wake zao,wanapenda ku Present wake zao vizuri kwa watu,wanapenda sana kuwa karibu na wake zao na watoto zao, ni Caring husband,ni walinzi wa familia na hisia za wenzao,wanapenda romantic play(kucheza na kutaniana na wenza wao)wanasifia,wanashaurika,wanasikiliza,wanadekeza nk. *_Hili ni kundi ukifanikiwa kulipata hakikisha unakuwa mnyenyekevu sana kwao utafanijiwa sana na ndoa yako itakuwa Tamu sana._*
🤝Kama una aina zingine nne hapo juu,jitahidi sana kufanya vizuri,usi React kwenye udhaifu wake,usishindane naye,TIMIZA WAJIBU WAKO hilo ndo litakusaidia kuepuka makali yake na kumwombea maana hiyo ndo HULKA YAKE.
  By Psychologist Ev Elisha Kazimoto(whatsapp  0755444078)

Tuesday, 26 June 2018

MIPAKA YA HOUSE GIRL

Shalom. ‼
Swali kwa wote❓
🔆🔆🔆🔆🔆🔆🔆🔆🔆🔆
Jamani mke Na mume ni wafanyakazi,  Na wapo busy Na kazi kila moja,

Je ni vizuri house girl kupika chakula cha Mume endapo mke atakuwa busy kazini???

⭕Kama Jibu Ndio au Hapana, Je ni Kwa nini??

⭕Usiijibu tu haraka ❗❗fikiria kihekima.

👆👆👆👆👆
*Mwana Saikolojia wa Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto (0755444078 whatsapp )Anajibu kama ifuatavyo*
....................................*Tuhitimishe Mada hii Kisaikolojia na Kijamii*
_Kwanza Muuliza swali ameweka viangalizo(conditions)nikama swali amelirahisisha tayari,kwamba *Je,ni vizuri au Vibaya,house girl akipika chakula cha mme wake KAMA mama yuko busy kazini?* hapo ndo mzizi wa hoja upo_
👉Kwanza wana ndoa lazima mjipambanue ninyi ni ndoa ipi(ya wafanyakazi wote,mfanyakazi mmoja,au wote si wafanyakazi, na kazi zenu zinakula muda kiasi gani na muda wa nafuu ya kazi zenu ukoje,niwaajili au mmejiajili) kisha pambanua ndoa yenu ni ya aina ipi nirahisi mama kama MSIMAMIZI MKUU wabmambo ya familia ikiwemo budget za matumizi ya ndani,breakfast na lunch,na dinner (chai asubuhi, chakuja cha mchana na usiku)atajua namna ya kupangilia ambo ya familia kwa ustawi wa familia yake.
👉Pili lazima wana ndoa mjue familia yenu ni ya aina ipi(familia ndogo,familia kubwa)una watoto wadogoau wakubwa wawezao kufanya majukumu ya kifamilia au wote nitegemezi wanasubiria kika kitu wafanyiwe.
👉Mama,ujue mmeo ni mme wa aina ipi( *Chifu,Rafiki, Dis minder) ukisha jua aina ya mme ujipange kukabiliana na aina ya familia ulo nayo kutoa huduma kama mama ili uendane na saikolojia ya mmeo.
_Baada ya mambo haya sasa twende kujibu hoja ya muuliza swali_

1⃣Mama mwenye familia ni muhimu kujua, kuoata house girl hakuondoi,au kupunguza wajibu wako kama mama wa familia na kwa mme wako.
2⃣Mama ni muhimu kujua,wewe ndo mlinzi wa mme wako katika mazingira yanayoweza onekana kumvutia sana mmeo,akahamisha attention yake kwako na kuhamishia kwa house girl au mdogo wako.
3⃣Hakikisha unasoma mazigira ya mmeo kujua vitu anavyo pendelea,na mazingira anayopendelea hakikisha hivyo unavifanya wewe kwa bidii na ubora zaidi kila siku.
4⃣Hakikisha unashuka na kuwa mnyenyekevu kwa mmeo,kumthamini na unapo muhudumia muhudumie haswaa kama mama.
_Baada ya Maangalizo hayo turudi kujua house girl katika familia_
👉Kupata house girl ni maamuzi ya watu 2 baada ya kuona wapi *Pana mapungufu* na nani aje kusaidia kazi(KUSAIDIA) je, ni house girl au house boy? Ni maamuzi ya watu 2 na wanajua kwa nini wamemleta, hivyo WAMERIDHIA tuna changamoto hapa huyu aje asaidie kulingana na ( *Aina za familia,na kazi mlizo nazo*) sasa anapo kuja kusaidia ndipo mama anaitazama ( *aina ya mume aliye naye*) ili kuruhusu kazi zinazofanywa na house girl au house boy ziwe na mipaka ipi.
👉 *SI KOSA KAMA HOUSE GIRL ATAPIKA CHAKULA CHA FAMILIA AU BABA(naanza kujibu swali sasa)* Kutegemea Mama yupo wapi,anafanya nini,muda wake wa kuwahi kupika na familia kula itakuwa muda gani.( *kama mnatoka kazini wote saa 10,11,12 hamja pata lunch lakini mama unauwezo wa kuagiza house girl akaandaa ili msishinde Njaa,fanya hivyo)( KULINGANA NAAINA 3 ZA MMEO)
👉Lakini NIMAKOSA MAKUBWA *Kutengeneza mazoea ya kila siku chakuka cha familia,kuandaliwa na house girl*) mwanamke mjanja.... _Muda alo busy anahimiza chakula cha familia kiandaliwe na anakihakikisha kabka hakija letwa mezani kama kitamfaa na mme wake, *Lakini anapo pata nafasi yoyote ya kuandaa chakula anahakikisha anatulia kumuandalia mmewe kitu kizuri zaidi ya anavyoandaa house girl* na ni makosa makubwa house girl kuwa mkali wa mapishi kukuzidi mama,tafuta hata walimu wa mapishi hata ingia online search namna ya kupika chakuka flani_
👉Pamoja na ubize wote wa kazi za huwezi kukosa siku 2,au 3 ukamwambia house girl kaa pembeni nimwandalie mme wangu na familia chakula bora zaidi
👉Na mme Rafiki,anaona,anajua how far mke wagu yupo na majukumu mengi.
👉Kama aina ya mme wako ni CHIFU,juavni mtu asiye tazama unafsnya nini,unamajukumu gani,uko busy kiasi gani...Yeye anachojali TIMIZA WAJIBU KWAKE WEWE KAMA WEWE KWAKE( not good this type) ndoa haiwezi kuwaya furaha na mambo yote hayata fanyika kwa upendo,furaha na ubunifu,bali kama WAJIBU. Hapo mama jitese zaidi hata kukubali vitu vingine viharibike visiende vema lakini utimize wajibu wako.
👉Kama mmeo ni RAFIKI, hakikisha unamshirikisha mambo yako kama rafiki,unapo pata nafasi na ujitahidi kuiata nafasi nyingi nyingi kumfurahisha mmeo kama rafiki,mwandalie vitu vizuri anavyopoenda,muhudumie kwa nguvu zote mpaka appreciate(akukubali kuwa naam) ili hata muda uke upo busy na kazi za serikali,au biashara ajue mke wangu akioata nafasi uwa ananifanyia kweli mambo mazuri.(USIMPOTEZE RAFIKI) hata house girl ajue ukiwepo mambo ni moto,unamjali mmeo haswaa.
👉Kama mmeo ni DIS MINDER (yaani yeye hajali) umefanfa wewe,au mtu mwingine,ilimmradi mambo yameenda...Chunga sana usijisahau ukamwachia house girl au boy,kazi hakikisha unaonyesha utofauti wa wewe na wasaidizi wako hao kwa mmeo.

NB: *Katika majukumu yote hakikisha unaweka mipaka ya mambo kadhaa,hata housegirl ajue kuwa hapa kwa namna yoyote,mama awe busy,au awe huru siruhisiwi kugusa ni mama tu* kika mtu ana mambo yake mi nakupa mfano ya general,ila kika mtu ana uzito wake....... Ya jumla *Usiruhusu house girl afanye haya,Kuingia chumbani kwako,kufua nguo za mmeo hasa za ndani,kutandika kitanda cha mmeo,kudeki chumbani kwako,kumpelekea mmeo maji bafuni* hayo baadhi......... Na mengine wewe binafsi utaona haya ni yangu tu....Fanya hivo
*Kwa ujumla wake, Ndoa aihitaji mazoea,inahitaji ujanja na maarifa ya juu,ili kulinda hisia za mwenzako,lakini kumfanya mwenzako akufurahie. Kwa hiyo ni mama tafuta njia nzuri za kumfurahisha mmeo na kumpendeza afurahie uwepo wako kwenye familia*
👉Wanaume tujifunze kuwa waume RAFIKI ili kuruhusu akili yako na moyo wako na macho yako kuona hali ya mkeo aliyo nayo na KUMUHURUMIA,kujua hajafanya hili si kwamba ni uzembe au hajali,ila ni kwasababu katingwa,kachoka,huwa akipata nafasi anafanya kwa asilimia za kutosha. Basi muhurumie,mpe pole,msifie,mfariji,mpongeze,MSAIDIE inapo bidi.
👉 Mme *Chifu Aheshimiwi,Anaogopwa* woga siyo kupendwa ni Kukwepa Shari, sasa usijivune kwakuwa unaogopwa,ila jua mkeo kakuzidi Akili Anakwepa Shari ili maisha yaende.
@Kubadirika ni Muhimu ili ulete radha ya ndoa iliyokusudiwa na Mungu na kisaikolojia.
👉Mwana mama kuhurumiwa na kusaidiwa,si kigezo cha kukwepa wajibu wako,ila umetengenezewa mazingira na mmeo mwenye maarifa ya juu ya *kupalilia upendo* katika ndoa yenu.

*_Uchambuzi wa mada hii umeandaliwa na Mwana Saikolojia wa Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp  0755444078)_*

Sunday, 10 June 2018

ASILI YA USHINDI WA MTU WA MUNGU

*ASILI YA USHINDI WA MTU WA MUNGU*
    _By Ev Elisha Kazinoto_(0755444078)
.......
.......
_Shalom mtu wa Mungu,katika ujumbe huu naomba watu wa aina 3 wanitegee sikio vizuri._
1⃣Mtu wa Mungu(Uliyeitwa kwa jina ka Bwana)nitegee sikio usikie ushindi wako ambavyo siyo wa kubabaisha una chimbuko imara.
2⃣Wachawi(mawakala wa Shetani)mnaotesa watu na kuwawinda kama mwindaji awindavyo ndege( mjue si rahisi kumnasa mtegoni mtu wa Mungu)
3⃣Shetani na baraza lake la mapepo(wanaoratibu matatizo katika maisha ya watu)wajue uwezo wao ulivyo wekewa mpaka na Bwana juu ya watu wa Mungu.
............................................

*(Warumi 8:31-37 )*
------------
31Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?
32Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote, atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye?
33Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki.
34Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
35Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo? Je! Ni dhiki au shida, au adha, au njaa, au uchi, au hatari, au upanga?
36Kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Kwa ajili yako tunauawa mchana kutwa, Tumehesabiwa kuwa kama kondoo wa kuchinjwa.
37Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda.
👉 *_Mambo muhimu yakujua hapa kwa kundi la kwanza 1⃣ Mtu wa Mungu_*
✍Tendo la Mungu kuwa upande wa maisha yako(kuitwa mwana wa Mungu/mtumishi wa Mungu)tayari vitu vyote *Haviruhusiwi tena kuwa juu yako* (yaani kuwa na nguvu ya kukushinda na kukukandamiza)
*(Waefeso 1:18-23 )*
------------
18macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;
19na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;
20aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho;
21juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, wala si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao pia;
*22akavitia vitu vyote chini ya miguu yake, akamweka awe kichwa juu ya vitu vyote kwa ajili ya kanisa; ambalo*
23ndilo mwili wake, ukamilifu wake anayekamilika kwa vyote katika vyote.
✍Yesu hakutolewa kwa wanadamu kwa hasara,yaani ujio wa Yesu duniani siyo tu kuokoa wanadamu,ila ni pamoja na *Kukomesha utawala wa adui ibirisi na mawakala wake juu ya kanisa* ili tusiishi kwa hofu ya mauti na mateso
*(Mathayo 16:15-18 )*
------------
15Akawaambia, Nanyi mwaninena mimi kuwa ni nani?
16Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
17Yesu akajibu, akamwambia, Heri wewe Simoni Bar-yona; kwa kuwa mwili na damu havikukufunulia hili, bali Baba yangu aliye mbinguni.
*18Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.*
✍Mahusiano tuliyo nayo na Bwana Yesu,kati yetu yameunganishwa na upendo mkuu usiotenganishwa kwa kitu chochote(Upendo wa mauti ni mkuu una wivu)
*(Waefeso 5:28-32)*
------------
28Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
*29Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.*
30Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake.
31Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.
*32Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa.*
(Palipo na upendo pana kisasi cha mauti kama utaigilia kuharibu upendo)

_"Nitie kama muhuri moyoni mwako, Kama muhuri juu ya mkono wako; *Kwa maana upendo una nguvu kama mauti,* Na wivu ni mkali kama ahera. Mwako wake ni mwako wa moto, Na miali yake ni miali ya Yahu."_
*(Wimbo Ulio Bora 8:6 )*
✍Dhoruba muda wote katika maisha ya mwili huu zipo kila siku,ila katika hizo zote *Lazima Kushinda* kwakuwa kinachotushindia ni Upendo wa Mauti wa Yesu Kristo tulio unganishwa naye ndiyo unao meza mishale ya maadui zetu.
*(1 Petro 1:5-6)*
------------
*5Nanyi mnalindwa na nguvu za Mungu kwa njia ya imani hata mpate wokovu ulio tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.*
6Mnafurahi sana wakati huo, ijapokuwa sasa kwa kitambo kidogo, ikiwa ni lazima, mmehuzunishwa kwa majaribu ya namna mbalimbali;
👉 *_Mambo ya kujua katika kundi hili la 2⃣la wachawi(mawakala wa shetani)_*
✍Ramli,madawa,uganga wa aina yoyote na umaarufu wa kufanya uchawi ambao mchawi aweza kuwa nao, *_Hauruhusu kumwondolea Neema,Ulinzi,Kibali_* alicho nacho mtu,alichopewa na Mungu.
*(Hesabu 23:16-25)*
------------
16Bwana akaonana na Balaamu akatia neno kinywani mwake, akasema, Umrudie Balaki, ukaseme hivi.
17Akafika kwake, na tazama, amesimama karibu na sadaka yake ya kuteketezwa, na wakuu wa Moabu pamoja naye. Balaki akamwambia, Bwana amenena nini?
18Naye akatunga mithali yake, akasema, Ondoka Balaki, ukasikilize; Nisikilize, Ee mwana wa Sipori;
19Mungu si mtu, aseme uongo; Wala si mwanadamu, ajute; Iwapo amesema, hatalitenda? Iwapo amenena, hatalifikiliza?
20Tazama, nimepewa amri kubariki, Yeye amebariki, nami siwezi kulitangua.
21Hakutazama uovu katika Yakobo, Wala hakuona ukaidi katika Israeli. Bwana, Mungu wake, yu pamoja naye, Na sauti kuu ya mfalme i katikati yao.
22Mungu amewaleta kutoka Misri, Naye ana nguvu kama nguvu za nyati.
*_23Hakika hapana uchawi juu ya Yakobo, Wala hapana uganga juu ya Israeli._*  Sasa habari za Yakobo na Israeli zitasemwa, Ni mambo gani aliyoyatenda Mungu!
...
*25Balaki akamwambia Balaamu, Basi usiwalaani kabisa, wala usiwabariki kabisa.*
👆👉 Mungu hamtoi mtu Misri(upaganini)kwenye mikatale ya dhambi,halafu aruhusu achezewe na shetani na vibaraka vyake.
👆👉Nguvu iliyo tumika kutuvuta kutoka Dhambini ni kubwa kuliko nguvu inayotuwinda kututesa muda huu wakati tupo katika neema ya Wokovu.
👉 *_Mambo muhimu kuyajua katika kundi la 3⃣ Shetani na balaza lake_*
✍Adui akipewa(kuruhusiwa)nafasi ya kukugusa kwa namna yoyote anawekewa mipaka *asifanye anavyotaka* juu ya mtu wa Mungu
(Yobu 1:8-12)
------------
8Kisha Bwana akamwuliza Shetani, Je! Umemwangalia huyo mtumishi wangu Ayubu? Kwa kuwa hapana mmoja aliye kama yeye duniani, mtu mkamilifu na mwelekevu, mwenye kumcha Mungu na kuepukana na uovu.
9Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Je! Huyo Ayubu yuamcha Bwana bure?
10Wewe hukumzingira kwa ukigo pande zote, pamoja na nyumba yake, na vitu vyote alivyo navyo? Kazi za mikono yake umezibarikia, nayo mali yake imeongezeka katika nchi.
11Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako.
*12Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana.*
✍Mpaka anaowekewa shetani katika kukugusa  popote pale *unaendana na kiwango cha imani yako* kwa hiyo usitegemee mtu wa Mungu kushindwa na jaribu lolote.
_"Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili."_
*(1 Wakorintho 10:13 )*
👉Kwa makundi hayo matatu,yote yanapaswa kujua kuwa vita yoyote inayo muhusisha *Mtu wa Mungu,Wachawi(mawakaka wa ibirisi,au ibirisi na baraza lake la mapepo* vita hiyo haimuhusu mtu ni Bwana ndiye anapigana nayo kwakutangaza ushindi kwa mtu wake.
*(1 Samueli 17:47-50 )*
------------
46Siku hii ya leo Bwana atakuua mkononi mwangu, nami nitakupiga, na kukuondolea kichwa chako, nami leo nitawapa ndege wa angani na wanyama wa nchi mizoga ya majeshi ya Wafilisti, ili kwamba dunia nzima wajue ya kuwa yuko Mungu katika Israeli.
*47Nao jamii ya watu wote pia wajue ya kwamba Bwana haokoi kwa upanga wala kwa mkuki; maana vita ni vya Bwana, naye atawatia ninyi mikononi mwetu.*
...
49Daudi akatia mkono wake mfukoni, akatwaa humo jiwe moja, akalitupa kwa kombeo lake, akampiga Mfilisti katika kipaji cha uso; jiwe hilo likamwingilia kipajini, akaanguka chini kifudifudi.
50Hivyo Daudi akamshinda yule Mfilisti kwa kombeo na jiwe, akampiga Mfilisti, akamwua; walakini Daudi hakuwa na upanga mkononi mwake.
*_Mungu akubariki kwa ujumbe huu alonipa Bwana,kwaajili yatu wote wanaompenda Bwana lakini wanapitia vita kali ya kiroho katika maish yao_*
     By Ev Elisha Kazimoto
     Whatsapp 0755444078

Wednesday, 6 June 2018

SEX NA HUDUMA NA MFUNGO

*TENDO LA NDOA NA MFUNGO*
Swali: Je, Ni Sahii kushiriki tendo la ndoa mkiwa kwenye mfungo wa maombi, au unajiandaa kwenda ibadani kuhudumu.?

*Anajibu Ev Elisha Kazimoto*
WhatsApp 0755444078
_Kwanza niweke sawa dhana na tafsiri ya tendo la ndoa kwa wana ndoa. *Tendo la ndoa kwa wana ndoa ni Safi, na Takatifu, na huru kwa wana ndoa muda wowote ili mradi wamekubaliana na kwa utaratibu*_  na hiyo ni kwa mujibu wa neno la Mungu.👇👇👇👇👇
*1Wakorintho 7:1-5*


1 Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke. 

2 Lakini kwa sababu ya zinaa kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke na awe na mume wake mwenyewe. 

3 Mume na ampe mkewe haki yake, na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake. 

4 Mke hana amri juu ya mwili wake, bali mumewe; vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake, bali mkewe. 

5 Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda, ili mpate faragha kwa kusali; mkajiane tena, Shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu. 
✍ Inabidi tujue jambo moja, hakuna unajisi wowote,ubaya wowote katika tendo la ndoa, hizo ni imani potofu na misimamo binafsi si ya Neno la Mungu. *Uharamu wa tendo la ndoa,na Muda wake ni kwa watu wasiyo wana ndoa, ila kwa wana ndoa ni Safi,Ruksa muda wowote* Dhana za Huruhusiwi kushiriki tendo la ndoa siku ya ibada, au kama unaenda kufanya huduma, kusimama madhabahuni, huu ni ushetani, ni upotofu, ni huujumu wa ndoa, ni kuwafunga watu kongwa lisilo la haki. *_Alicho kibariki Mungu,utakihitaje kimelaaniwa? Mwanzo 1:28_* Mungu alilibariki tendo la ndoa na hakuliwekea majira wala nyakati za kuli attend,iwe asubuhi, mchana,usiku, usiku wa manane, free enjoy wana ndoa, unaenda kuimbisha saa 9 mchana, unahitaji kuburudika na kutuliza saikolojia yako hata saa 7 zimua, it's your property, zingatia tu utaratibu,muda wako na Mungu na muda wako na mpendwa wako. Ni muhubiri unaenda kuhubiri mkutano wa nje,una wife wako umemuhitaji mchana, Enjoy your blessings, wee ndo unajua muda uloutenga na Mungu na wako na mke wako. *Tendo la ndoa halina Limitation ya Kibiblia kwa wana ndoa* labda ushauri na mawazo tu ya mtazamo na mapendekezo kulingana na hali ya mazingira,kitu ambacho siyo kanuni wala sheria.
*Tendo la Ndoa na Kufunga* _Nahisi wana ndoa wanajua nitakacho eleza hapa, kwa vijana wanaweza wasijue, Tendo la ndoa si kama kunywa chai,kuchovya mkate kwenye chai, *Ile ni Kazi Ngumu japo ni Enjoyment* ila inahitaji nguvu za ugali, muscular. *Ogopa kazi inayo toa jasho mtu* hiyo siyo mchezo mchezo.
✍Tendo la ndoa kulifanya linahitaji nguvu,uwe umeshiba,uwe na joto la mwili ndo utaisimamisha misuli ya *Fimbo ya ufalme*,au mama ndo utahimili mapigo.
✍Tendo la ndoa linahitaji akili safi iliyo tulia,yenye oxygen ya kutosha ili kuibua hisia za sex, *_Sasa mtu aliye funga, ana njaa,akili inachoka,oxygen imepungua,lakini joto la mwili limeshuka, nguvu hana za kusimamisha fimbo muda mrefu kwa sababu ya chakula mwilini hakuna_* kwa sababu hiyo tendo la ndoa litakuwa gumu. Tena afadhali kidogo kwa Mwanamke anapokea,ila mwanaume anaye toa, one goal uchovu wake ni kama mwendo wa alotembea more than 5 km kwa miguu.
✍ *_Kama umefunga una nguvu za kusukuma mzigo na isikupe shida kuchoka, hakuna unajisi ingia kazini. Hivi ni vitu vilivyo barikiwa,sasa ukiokoka kupita maelezo kila kitu unakiita dhambi, kumbusu mkeo siku ya j2 dhambi, ku sex siku ya ibada dhambi, acheni kutengeneza dhambi, Tendo la ndoa kwa mwana ndoa halina unajisi kwa siku wala muda._* Alivyo vitakasa Bwana wewe usiviite najisi, vitu vyote ni safi kwa walio safi,ila ni najisi kwa walio najisi.👇👇👇👇
*Tito 1 : 15 - Vitu vyote ni safi kwa hao walio safi; lakini hakuna kilicho safi kwao walio wanajisi, wasioamini; bali akili zao zimekuwa najisi, na nia zao pia.*
✍Mwisho ushauri wangu na taadhari yangu, tusitumie utashi wetu usio na fact za kibiblia kuonyesha kosa au dhambi, tutumie ujuzi,experience na neno la Mungu kuwaonyesha watu ukweli wa mambo.
NB: Tendo la ndoa linahitaji utulivu, maandalizi, nguvu na muda mzuri na kuridhishana, lisifanyike kwa kukimbia kimbia au kumridhisha mtu mmoja,mnapo lifanya,muwe mmefunga,mnaenda ibadani,au mmetoka ibadani hakikisheni ni kwa furaha yenu wote na kufurahi wote pamoja.
*_Ulikuwa na mchambuzi wa masuala ya kisaikolojia na kiroho katika mahusiano na ndoa, Ev Elisha Kazimoto(Baba Evan)_*
WhatsApp 0755444078