Saturday, 13 June 2020

DADA JITAMBUE(PART V)

*Sehemu ya Tano ya Somo, Ukijitambua Kama Dada wa Thamani, Utapata Mme Haraka*
_Mnenaji ni mimi Mtumishi wa Mungu *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist )*_
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail :babaeve755@gmail.com
......................
Karibu Tumalizie somo letu...
👉Ukisha jua siri mbalimbali zikupasazo kufanya ili kupandisha Status yako ya Kiroho na Kimwili,hapo sasa ndipo inakupasa kuingia Magotini kuomba,kushugulika na Ngome za Giza ambazo mara zote ushindana kuzuia kusudi lililo jema lisitimie kwenye maisha yako.
👉Muhusishe Bwana akutangulie mbele yako katika kukusafishia njia ya kumpata aliye chaguo la Mungu kwako(Mme mwema)
1 Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi wake,ambaye nimemshika mkono wake wa kuume,ili kutiisha mataifa mbele yake,name nitalegeza viuno vya wafalme;ili kufungua milango mbele yake,hata malango hayatafungwa. 
Isaya 45:1

2 Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma; 
Isaya 45:2

3 nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli. 
Isaya 45:3
....................
👉Sasa njoo uoate siri za namna gani na mambo ya kushugulikia katika maombi yako ili kumpata mmeo aliyekusudiwa na Mungu kwako.
🔥 *HATARI ZA KUSHUGHURIKIA KATIKA MAOMBI DHIDI YA UBINTI WAKO*🔥
🔥Shugurika na Roho/Madhabahu za kifamilia na ukoo wenu.
👉Kuna mambo huyajui kwenye familia,matabia yamefunga milango kwenye mafanikio yako,kuna rohobzinang'ang'nia mtu hata akiokoka hizo usizipe nafasi kil siku zishughurikie.
🔥Shugurika na Roho za kuchelewesha mambo. Unakuta mdada upo ni mzuri umekamilika kila kona ila *Unachelewa kuolewa mpaka unaingia 40s* piga roho hizo za jangwani za kukuzungusha 
🔥Shughurika na Roho za Kukataliwa. Kuna watu wanakataliwa live na wengine wanakataliwa kwenye ulimwengubwa roho, kimwili anaonekana anapendwa na watu ila kiroho anakataliwa na hawezi olewa kirahisi.
🔥Kataa roho za ndoa ya jinsia moja. Kuna wadada wanapendwa sana na wadada wenzao mpaka wanaambiwa yaani ningekuwa mwanaume ningekuoa wewe, ila wanaume HAWA MPENDI NA HAWAMKUBALI, hizo ni roho za Lesbian.
🔥Shughurikia Roho za Uchafu juu yako. Kuna wadada wazuri sana ila wanaonekana kwenye ulimwengu wa Roho wachafu na wana nuka, huwezi olewa kama umepakwa mavi kwenye ukimwengu wa Roho,utavaa nguo za gharama na  unyunyu lakini wapi wanaume wanapita kushoto.
🔥Shughurika na Ndoa za Majini(mapepo). Kuna wadada hawawezi olewa kwakuwa wao walisha funga ndoa na mapepo kwenye ulimwengu wa Roho. 
👉Mara nyingi wadada hao *Alama zao* ( _Wanaota wana sex,wanaingiliwa kimwili wakiwa wamelala na wanaune wanao wajua au wasiowajua, Wanaota wana nyonyesha watoto, wanaota wanafunga ndoa baharini, wanaota ndoto za baharini baharini, wanaota wanavalishwa pete, wanaota wanafunga ndoa, wanaota wako Beach na mwanaume, wanapenda sana kushikwa maziwa sana, wana penda sex sana hata kujichua, wanapenda wadada kimapenzi zaidi ya kupenda wakaka, Wana Hasira za Karibu na za haraka sana na wagumu kueaamehe mtu hasa jinsia ya kiume_) ukiona vijidalili hivyo kwako na hujaolewa,hujapata mchumba,au unamchumba ila mahusiano yanasua sua,au yameenda miaka 3,4,5 pambana kwenye maombi unaweza USIOLEWE.
*_Basi mimi niishie hapo najua dada umepata dozi ya kutosha katika Series ya Somo hili Refu kweli kweli lenye shemu karibu 5(Part 1 hadi Part 5) Mungu akupe Neema ya Kujifunza na kufunguka._*
Mwandaaji wa Somo hili ni Mtumishi wa Mungu
*Ev Elisha Kazimoto(Psychologist & Counselor*)
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
e-mail :babaeve755@gmail.com

DADA JITAMBUE(PART IV)

*Sehemu ya Nne ya Somo, Ukijitambua kama Dada wa Thamani, Utapata Mme Haraka*
_Mnenaji ni mimi *Ev Elisha Kazimoto*(Psychologist )_
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail :babaeve755@gmail.com
.........................
Karibu Tuendelee......
👉Hautaweza kupata Mme wa Viwango kama Unajiweka ovyo ovyo kimwili,huna maadili,huna staha,hujiheshimu, wewe umekazana na kuomba tu,hupati mme, Tengeneza status za kimwili zinazo vutia ili kila akuonaye kabla hajaanza kuona vitu vya kiroho vinavyo kutoka vya Kimungu basi aone Peesonality yako na Tabia zako za kimwili zinamfaa wewe kuwa mke wake
5. *Heshima na Adabu* Dada kaa ukijua pamoja na status ya kiroho,kuwa mwombaji,muimbaji,muhubiri nk,havikupi mme bila kuwa na combination ya status za kimwili,.
👉Miongini mwa status muhimu ni wewe dada kuwa na Heshima na Adabu kwa watu.
👉Heshima na adabu yako itakupa kibali kwa watu itakutangaza kwa watu,watu watatamani kuwa karibu nawe lakini kukumili.
👉Waweza kuwa na kopato,elimu,huduma kubwa ya kiroho ila ukiwa na jeuri,kiburi,dharau aisee utaishia kuitwa SHANGAZI WA KANISA,wadogo zako woote wataolewa ila wewe uta SUGUA BENCHI,hapo hakuna pepo, pepo ni Tabia yako.
👉Heshimu mwenye kipato kidogo,kikubwa,wazuri kwako na wabaya kwako,huwezi jua kwamba unaye mdharau ndo anaweza kuwa kiunganishi cha mmeo mtarajiwa au akakata muunganiko wako na mmeo mtarajiwa.
6. *Jenga jina Mahali ulipo zaliwa(Unako tokea)na Jenga jin Ugenini*
👉Kuna watu ujisahau sana, wengi wetu tuliko zaliwa na kukulia ni tofauti na tunakoishi sasa mpaka tunapata wenzi tunawapa mbali na tuliko kulia  na kulelewa.
👉Unajua nini, watu wengi wanajenga Jina waliko sasa wanaonekana watu wazuri sana *Ila kwao,aliko kulia wanamjua kama mtu ovyo,hafai,aambiliki,mvivu,mchafu,kahaba* kumbuka ukimpata mchumba LAZIMA MTARUDI KWENU, vipi familia na mdugu zako na majirani watakusemeaje wewe kwa mwenzako na ukweni kwako?
👉Na wengine nyumbani kwao na majirani wanamjua mtu mwema,mpole,mtakatifu,mtu wa watu,ila kumbe *Kule anakoishi sasa, watu wanajiuliza hivi huyu Alizaliwa na mwanamke au ni pepo flani limevaa mwili* haya mambo yatakuharibia hata ukijificha itakuumbua.

7 *Ishi Maisha yako Halisi, Acha Kukopi kopi(Artificial life)*
👉Wewe ni mdada wa aina flani,ishi kama wewe usiishi kama flani, tafuta uhalisia wako ndo utaishi maisha ya maana na ya furaha na watu watakupenda kwa namna ulivyo.
👉Ukiishi sawa sawa na wewe ulivyo NATURE YAKO,utafanya mambo kwa ubora na uzuri ila ukiwa unaishi kwa kukopi flani utakuwa unjitesa sana kulazimisha ufanane na flani, wewe siyo flani wewe ni wewe.
👉Yaani na maanisha, _Kuwa na tabia yako kama ulivyo lelewa,heshima ya kwako,ongea ya kwako,matumizi ya pesa ya kwako,vaa ya kwako, ukitaka kuwa kama flani utajikuta kila siku unakosea na kujutia,unatamani kuishi kama flani ambaye anauza mwili wake kila siku ana wanaume 7 kila mmoja anaonga, wewe huna halafu unahitaji uvae,ule,utoke out nk kama yeye utakosea na status yako itashuka_
👉Jikubali kama ulivyo, pambana kuongeza status yako,utaishi maisha yenye radha,yasiyo na majuto au mashariti magumu, au maumivu ya kutendwa.
👉Hakuna raha na ujasiri mkubwa kama mwana dada kuolewa na Heshima yako,hakuna anayekunyoshea vidole vya *Huyo hamna kitu* ina leta raha,inakufanya ujione Malkia kwa mmeo lakini utaheshimika.
*_Mpaka hapo ni seme Mungu akubariki,tukutane katika sehemu yetu ya Tano na ya mwisho katika Somo hili, mnenaji alikuwa mimi Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto(Psychologist )_*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail :babaeve755@gmail.com

DADA JITAMBUE(PART III)

*Sehemu ya Tatu ya Somo, Ukijitambua kama Dada wa Thamani, Utapata Mme Haraka*
_Mnenaji ni mimi Mtumishi wa Mungu *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)*_
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail babaeve755@gmail.com
....................
Sasa Karibu tuendelee....
👉Jambo lingine muhimu kwako Mdada wa Yesu Kristo ni Kutengeneza Status yako ya Kimwili.
👉Kumbuka Ndoa ni 50%Kiroho na 50% Kimwili, kwa hiyo unapojipanga kuingia katika ndoa,usiishie kuomba tu,lazima Ujipange na Kimwili, kumbuka tunaishi duniani, Vipo *Vigezo vya Kimwili* Vijana wana vitazama katika kuchagua mke bora wa kuishi naye.
👉Na labda ni kwambie, Wengi wa vijana wanaanza na Vigezo vya Kimwili ndo wanachungulia Rohoni, kwa nini Ndoa ni ya hapa hapa Duniani, usije ukasema mimi niko Rohoni sana mambo ya mwili sina haja nayo sana, HUTAOLEWA,utabaki kusubiri bila majibu.
..............
2⃣Tengeneza Status yako ya Kimwili.
👉Pamoja na kwamba kwenye ulimwengu wa Roho ndo vitu vinaanzia nakuja kwenye ulimwengu wa mwili,basi tunahitaji kutengeneza mazingira ya Kimwili ili kuwa na pawepo na uwiano kati ya thamani ya kiroho na thamani ya kimwili ndo unazalisha mtu UNIQUE  anayetafutwa kwa kasi na vijana.
👉Usije kaa Rohoni tu ukashindwa kushugulikia Status ya kimwili, kumbuka  *_Wengi wa watu wanatazama mwili kabla ya rohoni_* unaweza poteza muujiza wako, kwasababu STATUS YAKO YA KIMWILI iko chini.
👉Pambana kujenga status ya kimwili ili watu wakuonao waseme YES, you are Beautiful (CUTE GIRL)
👉 *Status za Kimwili* ambazo dada kama dada zinakupandisha chati na uonekane ni Wife Material na unafaa kuolewa haraka....
1. *Usafi* Binti muda wote jiweke nadhifu, uwe na nguo moja au nyingi *Jiweke Safi, Smart*
👉Unatoka kidogo,unaenda kwa mangi Toka ukiwa Vizuri, hujui utakutana na nani na atakuwa anakufanyia tathimini gani.( Mwonekano wako wa kwanza waweza kukuongezea Credits au kukupunguzia Credits).
2. *Ujasiliamali (Uchumi)* Unahitaji kuongeza thamani yako na kulinda thamani yako, Jitemgenezee mazingira ya *Kutokuwa Tegemezi kwenye Mahusiano na uchumba* wengi wamepoteza Thamani zao na kushindwa kuolewa haraka kwasababu WANA NJAA, UHITAJI WA PESA, wanayumbishwa na kutapeliwa na vijana matapeli wenye uchumi kidogo
👉Hasara za kuwa tegemezi ni kukosa *Msimamo binafsi na kauli ya NO or YES* Muda wote kila kitu utakuwa unasema YES kwa unyonge, unajua hapa ni makosa, napoteza utu wangu, nanyanyaswa ila utafanyaje, huna kitu unalazimika kusema YES,ili usikatiwe huduma ya vichenji.
3. *Lugha* unajua nini, wewe mwanadada ni mfanya biashara, unahitaji lugha tamu, lugha inayovutia wateja wako.
👉Lugha inaweza kukuweka mbali na wateja wako au karibu na wateja wako.
👉Ukari hauwi katika Lugha, kujilinda na kujiheshimu dada hakupo katika kuwatukana wakaka na kuwadharau.
👉Tumia lugha nzuri,kataa wahuni na matapeli kwa Lugha nzuri, siyo lazima Utukane na umdharirishe mtu.
4. *Taaluma* Miongoni mwa vitu ambavyo katika zama hizi sio vya kuchukulia rahisi ni TAALUMA( *Professional*) una ujuzi upi, wa nini, unaweza kukusaidiaje katika kuendesha maisha.
👉Wale ambao bado mpo katika mchakato wa kusoma, *Soma kwa bidii* ongeza vidato,jiweke katika level nzuri,usiache shule kisa umeambiwa na mchumba wako kwamba UTASOMA NIKISHA KUOA, au haina haja sana ya wewe kusoma MIMI MMEO NIPO, *Nyakati zinabadirika binti yangu* unaweza ukajutia maamuzi yako ya kuacha shule ili uolewe.
👉Wale ambao mambo ya shule vidato yameisha waacha kidogo, TAFUTA UJUZI (kwasasa ni kila kona ujuzi unapatikana) *Jiimarishe uwe mtaalamu haswa*

*_Mf.Kama ni kupamba maharusi, Kupamba kumbi,keki,ufundi wa nguo nk, Somea chuo kabisa uwe mtaalamu haswa_*
Achana na mambo ya kwenda kujifunza cherehani kwa fundi wa mtaani kwenu, au kupamba kwa flani ambaye naye anatamani akae yeye ndo anajulikana, nenda chuoni upate vitu adimu na uongeze ubunifu wako,ili *Upunguze ushindani juu yako* ufanye vitu Unique and attractive.
👉Nataka ni kwambie wanaumebwatapanga foleni kwako,lakini hata ukiolewa utakuwa unathaminiwa na kupendwa sana.
_Unaonaje unaitiwa tenda ya kupamba kwenye harusi ya mil 2,3, au 5 siku moja unainuka na mil 5,wakati kuna mfanyakazi anafanya kazi mil 5 anaipata baada ya miaka 5?_
*Dada ongeza status yako bhana ndoa kupata ni rahisi*
_Kufikia hapo ni hitimishe sehemu ya Tatu ya somo letu,lakini nikukaribishe kwa sehemu ya nne ambapo tunaendelea na Status za Kimwili, 5,6 na 7..Barikiwa sana na Bwana_
Mnenaji alikuwa mimi Mtumishi wa Mungu *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail babaeve755@gmail.com

DADA JITAMBUE(PART II)

*Sehemu ya Pili ya Somo, Kama Ukijitambua Kama Mdada wa Thamani, Utapata Mme Haraka*
_Uko naminenaji Ev Elisha Kazimoto(Psychologist )_
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
e-mail babaeve755@gmail.com
.................
Karibu tuendelee....
👉 *Kazi yako kama Dada Tengeneza na Ongeza Thamani yako*👈
1⃣Tengeneza Status yako ya *Kiroho* kama Dada uliyeokoka.
👉Unajua maisha ya Kiroho ndiyo yanayo vuta mambo ya kimwili.
*2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. 3 Yohana 1:2*
👉Ukiona unazembea kwa mambo ya kiroho,jua unachelewesha muujiza wako wa kimwili(mmeo)
👉Thamani yako ya kiroho inapopanda *Inavuta muujiza wako kimwili*

👉Unahitaji kila siku mwana dada ujue kwamba *Thamani yako inawindwa na shetani na mawakala wake* ili ishushwe,na upoteze NDOTO NA MATUMAINI ya kuingia katika ndoa ya baraka.
👉Kwa sababu hiyo hakikisha kila siku unaongeza uwezo na unalinda njia zako zote za ubinti wako.
*1 Yeye asetaye vipande vipande amepanda juu mbele ya uso wako; zishike silaha, ilinde njia, vitie nguvu viuno vyako, uongeze uwezo wako sana.Nahumu 2:1*
👉Wadada wengi wamejisahau katika kulinda THAMANI ZAO, wanaishi wanavyotaka, siyo kikanuni, jambo lililopelekea Kupoteza thamani zao kirahisi.
👉Kumbuka thamani ikishuka,na matumaini ya kupata mtu sahihi yanapotea, *na uwezo,nguvu ya kutafutwa na mtu sahihi inapotea*
👉Kazi yako ni Kuongeza Thamani yako, *Watafutaji wanatafuta vitu Unique vyenye Thamani*
👉Sasa kazi yako ni kuanza kutengeneza Status yako kiroho,uone jinsi ilivyo na nguvu ya kuvuta mambo inayo tamani maishani.
👉Twende pamoja katika kuangalia Status muhimu za kukazania kuwa nazo kiroho:
👏 *Status za Kiroho za kukuvuta karibu na mmeo*👏
🔹 *Tengeneza sifa ya kuwa Mwombaji* Miongoni mwa sifa kuu ya mdada(na mwanamke mtarajiwa mama wa familia )ni Kuwa mwombaji,hiyo ni kibiblia.
👉Maombi yatakufanya uwe karibu na Mungu lakini maombi yatakufanya uwe na uwezo wa kutambua wanaume feki na mwanaume sahihi wa kukuoa wewe.
👉Sikiliza wewe ni dada mtafutwaji, waweza kuja watu 20 wote wako vizuri kimwonekano,ila hawawezi kuwa waume zako wote 20,yupo mmoja utamjuaje? Ni namna unavyokaa magotini,penda kufunga,kuomba jiombee na mwombee mmeo mtarajiwa.
🔹 *Tengeneza Statu ya Kuishi Maisha Matakatifu yasiyo na michanganyo* Miongoni mwa vitu vinavyoweza kukupa kibali mbele za Mungu cha kupata mtu sahihi ni wewe kulinda maisha yako yasichafukiwe na dhambi au makosa na uchafu wowote.( *Hii inawashinda wengi*)ila wewe jipange kushinda.
👉Usiwe wa kujirahisisha kiasi kwamba *_Mwili wako unajulikana kwa kila kijana,maeneo yako yote muhimu ya mwili yanajulikana,hisia zako zinajulikana kwa kila mmoja_* Weka Distance ya Kusaidia Mwili wako Uheshimiwe. 
👉Usifurahie sana kushikwa na kila mmoja,( *Kushikwa sehemu za mwili kuna Raha yake,unasikia kuburudika ila KUNA GHARAMA YAKE*)itakusumbua,itakuchelewesha baraka zako au kupoteza kabisa muujiza wako.
👉Sasa ni heri ukaweka msimamo usio badirishwa na mtu yeyote awe mchumba wako au rafiki,ni heri akakuchukia au urafiki n auchumba ukavunjika lakini umelinda STATUS YAKO na utakatifu wako ambavyo ni nyenzo ya kukuletea mme sahihi.
👉Ila ukiwa simple kwa kila mtu, *Huyu atashika,atachezea sehemu zote,mwingine hataishia kuchezea atazama ndani kabisa na kuvunja Agano lako na Mungu na Mmeo* hapo ndo Utatamani usiku uwe mchana na mchana uwe usiku.(Ujui gharama zake na bora usijue kama bado ujakutana na changamoto hizo omba zisikukute ongeza umakini).
🔹 *Tengeneza Status ya Huduma,utumishi kwa Bwana* Ni hatari na hasara kwako dada upo kanisani upo upo tu, ni mpiga makofi na kucheza sifa na kurudi nyumbani, aisee mume utamtafuta kama sindani katikati ya takataka.
👉Dada kanisani pawe kama nyumbani kwenu, hakikisha *Una Huduma ambayo mpaka kanisa hata watoto wa sunde school wanajua hii uwa ni Huduma ya Dada Joyce,Mary,Happy nk* na usipoonekana siku hiyo kanisa zima linajua kuna mtu hayupo leo.
👉Pambana na huduma zote bila kudharau kama kudeki vyoo, kanisa, kwa mchungaji,uimbaji,ushemasi nk fanya kwa jasho lako la mwisho na kwa kupenda na kujitoa, huduma kazi yake *Ni kukutangaza na kukufunua kwa watu na kukupa kibali* ukiifanya kwa moyo na kwa bidii aloo utaonekana haraka.
👉Hatufanyi huduma ili tuonekane,au tuolewe ila tunafanya kwamba tunampenda Bwana lakini huko huko ndo tunakutana na mahitaji yetu.
🔹 *Tengeneza Status ya Kujifunza Neno la Mungu, Kuhudhuria Ibada* Usifanye makosa ya kuwa Empty Vessel,dada huna hata mistari ya biblia 10, soma neno, nenda kanisani kwenye ibada,idara nk,usiwe mtu wa kuonekana mara moja kwa wiki, wewe utakuwa hujajipanga kupokea baraka zako za mme.
👉Ibda kwako iwe LAZIMA siyo ya Muhimu tu. Huko ndiko utakako kutana na majibu ya maombi yako na mtu wako.
👉Mpe Mungu kipaumbele na yeye atahusika kwenye mambo yako.
*_Mwisho wa sehemu ya pili ya somo letu, tukutane katika sehemu ya Tatu ambapo nako kuna siri nyingine nyingi za kukufanya uwe mdada wa Viwango_*
Mnenaji alikuwa Mtumiahi wa Mungu *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist )*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail babaeve755@gmail.com

DADA JITAMBUE(PART 1)

🧏🏻‍♀️🧏🏻‍♀️ *UKIJITAMBUA KAMA MDADA WA THAMANI,UTAPATA MME HARAKA*🧏🏻‍♀️🧏🏻‍♀️
_Shalom wadada wa Yesu Kristo,leo nizungumze na mdada mmoja baye leo anataka afumbuke macho yake aone kile ambacho nakiona kwake( *Umeumbwa kwaajili ya Mtu flani Special*) haukuja tu duniani, Una mwenzako special_
*By Ev Elisha Kazimoto(0755444078)*
...............................................
🧏🏻‍♀️Mara nyingi tunakosea katika Kujitazama si katika kutafuta vitu.
🧏🏻‍♀️Nguvu kubwa ya kutafuta,tungeiwekeza katika Kujitazama kama Mungu anavyo tutazama basi, ni rahisi sana kupata kile ambacho unakitamani( Ubavu wako).
🧏🏻‍♀️Unajua tangu ulipoumbwa na Mungu tumboni mwa mama yako, *_Ulikuwa unaumbwa kwaajili ya mwanaume wako_* wewe ukuumbwa ili uzunguke ukitafuta mtu,ila uliletwa Duniani kwaajili ya Mtu(mmeo).
*Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.Yeremia 31:22*
🧏🏻‍♀️Popote alipo Rais lazima Mlinzi awepo(na popote alipo mwanaume jua mwanamke anahitajika) *Huyo mwanamke anaye hitajika ni wewe(dada)*
🧏🏻‍Baada ya kuja duniani unacho hitaji kuwa nacho ili *Upelekwe,ukutanishwe na mmeo ni Wewe Kuishi kwa Thamani yako uliyoumbwa nayo*
🧏🏻‍♀️Kinacho weza kukuwaisha kwa mmeo au kukuchelewesha kukutana na mmeo ni LEVEL YA THAMANI YAKO.
🧏🏻‍♀️Kila anayeingia katika ndoa anaingia kwa kiwango cha thamani yake kupanda.
🧏🏻‍♀️Siri ni kubwa, *Watafutao hawatafuti sura au jinsia ya kike, Wanatafuta THAMANI ndani ya jinsia ya Kike inayoweza Kutunza VISION aliyo nayo mwnaume* 
🧏🏻‍♀️Na hata siku moja Hakuna ambaye utafuta kununua au kupata kitu cha Thamani ya CHINI, au kibovu,wanatafuta Kitu cha Thamani ya juu.
🧏🏻‍♀️Na ukiona mtu anatafuta kitu cha thamani ya chini jua na yeye ni wa Thanani ya chini zaidi ya wewe unaye tafutwa.
👉Unahitaji mtu wa Viwango katika maisha yako, hakikisha unaongeza viwango vyako vya thamani yako.
*_Hii ni sehemu ya kwanza ya somo hili kati ya sehemu 5 zilizobeba somo hili usikose sehemu ya pili, Ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa EV ELISHA KAZIMOTO (Psychologist )_*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail babaeve755@gmail.com

Friday, 12 June 2020

NDOA NI 50%KIROHO NA 50%KIMWILI

🔹🔹 _Swali: Nitumie vigezo vya kiroho au kimwili kuchagua mwenzi wa maisha?_🔹🔹

Anajibu mchambuzi wa masuala ya Kimahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)*
Whatsapp 0755444078
*NDOA NI 50%KIROHO NA 50%KIMWILI KUWA MACHO ONGEZA UWEZO WA MAARIFA*
👉Labda nifafanue dhana hii ili kuwasaidia vijana na wanandoa wote ili kulinda amani,furaha na upendo kati ya COUPLES za wapendanao.
👉Tunasema ndoa ni 50%kiroho kwa sababu Mungu ndo mwanzilishi wa Ndoa,hatuingii kwenye ndoa tuonavyo sisi,ila kwa mapenzi ya Mungu ili tulitimize kusudi la Mungu.
👉Kwa maana hiyo tunahitaji lumihusisha Mungu sana kila hatua *_Wakati wa kutafuta,baada ya kimpata,na wakati wa kuishi naye_* Mungu ahusike ili kuwahifadhi mkae katika amani,furaha na upendo kati yenu 
👉Sababu nyingine ya kumuhusisha Mungu kila hatua ni ili kujenga ukuta wa kimdhibiti adui kuwavamia na kuharibu uchumba na ndoa yenu.
5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; 
Mithali 3:5

6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. 
Mithali 3:6

👉Pili nimesema ndoa ni 50% kimwili, kwasababu hatuishi Mbinguni,tunaishi duniani na tumepewa *_Akili na Utashi wa kujua mema,zuri,baya na kubaini vitu vipendezavyo na vichikizavyo_* kwakuwa tumepewa Ujuzi wa Kimungu wa kiutashi wa kubaini kinachotufurahisha hapa duniani nafsi zetu Mungu alitupa Fursa ya Kuchagua.Ili katika uchaguzi huo tuyatumikie matokeo ya uchaguzi wetu bila kulalamika.
*_Unajua kwa nini? Asilimia 100 za kuchaguliwa na Mungu ziliishia kwa Adamu,alipo chaguliwa na Mungu baadaye alimualaumu Mungu kwa alichompa_*
11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? 
Mwanzo 3:11

12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. 
Mwanzo 3:12

👉Baada ya hapo Mungu akaweka Nafasi ya wewe mwanadamu(Kija au binti)Muulize Mungu akushauri katika uchaguzi wako,yeye awe na sehemu yake na wewe uwe na sehemu yake.
👉 *Kwa maana hiyo unapomwomba Mungu naye Mungu anajua unatamani vigezo gani vya Kimwili atakupa mtu unaye mtaka kama anaona anakufaa ila vigezo vinaweza visiwe vyote ulivyotaka lakini Mungu pia anaheshimu vigezo vyako kama UMEANZIA KWAKE*
Kwa hiyo omba,angalia kwa macho nani akupendezaye kwa macho na moyo wako.
👉Lakini kisaikolojia (kimwili) unaoana na mtu ambaye utapata confidence ya kutembea naye,kuwa huru naye,kumtambulisha kwa watu kwamba huyu ni mme wangu au mke wangu lakini ambaye utakuwa naye na hisia za kushiriki naye tendo la ndoa kwa raha.
👉👆Si unajua kuna mtu ambaye kwako binafsi *Hakuamshi hisia,hata ungemtazama asubuhi mpaka jioni,awe amevaa au naked* hiyo ni kisaikolojia ila mwingine hata ukimuwaza tu au kuona picha yake unasikia Mahaba kupanda.
QUOTE: *_Kuna dada mmoja miaka ya nyuma kama 2013 nilimsaidia juu mahusiano yake,kija alikuwa anamfatilia yuko well off yaani amekamilika,anakazi,pesa,usafiri,nyumba,si mbaya sura ila BINTI HAISI HISIA YOYOTE YA KUMPENDA,ila kijana amemsaidia mambo mengi,pesa,gharama za chuo anampa bila kumwomba,binti aliamua kumkubali kwasababu ametumia vitu vyake japo hamuombi,yaani amemkubali kwa huruma,ila binti aliniambia hivi,SIJISIKII KUMPENDA HATA KIDOGO NA HISI HATA TUKIOANA SITA HISI WALA KUSIKIA RAHA YA KUSHIRIKI NAYE TENDO LA NDOA,NTAMPA TU AFANYE YEYE ARIDHIKE MAANA YEYE KAFA KAOZA KWANGU ILA MIMI HATA 1%HAKUNA_* Hapo ndo nikasema unaandaa bomu la DIVORCE na kuishi kwa Stress milele na hiyo yaweza kukupelekea KUCHEPUKA wakati umeokoka kutafuta mtu anaye touch hisia zako.Ni heri ufanye COSTFUL BREAK UP lakini ujuandalie amani baadaye.
*KUWA MAKINI NA MUNGU NA VIGEZO VYA KIMWILI,TUPO DUNIANI*
By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)0755444078