Tuesday, 29 November 2016

MAANDALIZI YA KIROHO YA KUINGIA KATIKA NDOA(PART I)

💝💝  MAANDALIZI YA KIROHO KWA NDOA YAKO MPYA💝💝
  By Ev. Elisha Kazimoto(Baba Eve)
            0755444078
_Shalom, shalom vijana wote mnao mlio katika Mahusiano ya uchumba, wale mnaotaka kuanza uchumba, wale mnao tegemea kufanya send off, Harusi hivi karibuni, bado huja chelewa_ kwa Neema niliyo pewa, na kuelekezwa na Mungu hatua kwa hatu kabla sija oa, na kuzinusurisha ndoa nyingi... Leo nasema nawe nakupa siri hii ka Mungu alivyo nifundisha. Basi fuatana nami katika uchambuzi huu nami *_Ev. Elisha Kazimoto (Baba Eve)_* Karibu upate maarifa uinusuru ndoa yako. Tuataongozwa na andiko hili la Isaya 60:6.👇�👇�👇�👇�
*_Isaya 62 : 6 - Nimeweka walinzi juu ya kuta zako, Ee Yerusalemu; hawatanyamaza mchana wala usiku; ninyi wenye kumkumbusha Bwana._*
💍 Kwanza ni vizuri kujua Ndoa unayoindea ni Taasisi Nyeti, kubwa yenye baraka na yenye ushindani mkubwa katika ulimwengu wa roho kuliko unavyo fikiria, ndiyo maana  *_Kijana wa kike au wa kiume kwanza unahitaji kuwa vizuri na Mungu hasa, pili unahitaji Kupata mtu sahihi kutoka kwa Mungu ndipo utaweza kuvipiga vita vya kiroho na kushinda na kuishi ka Amani, furaha, uhuru na kuoenda na kupendwa(Psychological Needs)_
💍Kwa nini, uwe vizuri na Mungu, na upate mtu sahihi ndipo uingie kwenye ndoa? _Shetani kama adui mkuu anawinda ndoa sana, mawakala wa shetani lama wachawi na mapepo wanawinda ndoa sana kuliko maelezo_
💍👆�Kwa nini ndoa inawindwa hivyo?  *Ni kwa sababu, Ndoa ndo kisima cha mabaya au mema*
👉� _Ni ndoa pekee ndo inaweza toa watumishi wa Mungu wakali juu ya ufalme wa giza_
👉� _Ni ndoa pekee ndo inaweza toa watu wenye uwezo mkubwa wa kusimamia haki na katika Taifa_
👉� _Ni ndoa pekee inayo weza kufanya Kanisa liwe na nguvu za Mungu ikiwa na amani_
👉� _Ni ndoa pekee inayoweza andaa jamii yenye hofu na Mungu_
Lakini kwa upande wa pili....
👹 _Ni ndoa pekee inaweza andaa watoto wamitaani walio poteza mwelekeo wa maisha_
👹 _Ni ndoa pekee inayo weza zalisha makahaba na majambazi_
👹 _Ni ndoa pekee inayo weza zalisha waabudu shetani, watu wasiompenda Mungu_
👹 _Ni ndoa pekee inayo weza kuandaa wachawi wakubwa na waganga kwa kurithishwa mikoba_
💍  *Sasa unapo kwenda kuoa au kuolewa ujue una ushindani mkubwa adui anatamani aanze na wewe*
💝 Siku moja roho wa Mungu alini nong'oneza siri kubwa juu ya maandalizi ya ndoa, *_ Nikaambiwa kwamba, maadui wengi na ndo kanuni yao, wanapenda kushughurika na kila kitu kinapo anza wakiweza kupanda uharibifu, kuharibu mwanzo wa kitu watafaulubkatika Mwendelezo wa kitu, ila ukiwashinda katika mwanzo wa kitu, basi utakuwa na vita ya kawaida ya upinzani lakini si kama aliyepandiwa sumu mwanzo wa kitu*
👉 Ndipo nikapewa siri ya maeneo maadui, shetani na mawakala waliko elekeza nguvu kupambana na ndoa, na wakiweza hiyo ndoa itakuwa na changamoto kubwa. Sasa fuatana nami nikuletee siri hii.
*MAENEO YA KUWA MAKINI NAYO*
👉� _Unapo amua kuanza mchakato wa kuingia katika ndoa takatifu, weka ulinzi juu ya kuta zifuatazo kama Neno kwenye Isaya 60:6,alivyo sema juu ya walinzi, wasilale, wasinyamaze waendelee kumkumbusha Mungu daima_ mimi nilipo pewa siri hii nilishughulika haswa, siyo kidogo ni haswaa, na na kuwasaidia wengine tujaepusha mabomu mengi yaliyo kuwa yametegwa.
1⃣  *Wakati wa kujitambulisha kwa familia pande mbili zote*
2⃣  *Wakati wa Kupeleka Maali(sherehe za maali)*
3⃣  *Kitchen Party*
4⃣  *Sendoff*
5⃣  *Harusi*
6⃣  *Zawadi zote katika sherehe zote kwaajili ya wana ndoa wapya(ninyi)*
7⃣  *Salamu wakati wa sherehe zote kwa maharusi(handshaking & Hugs)*
8⃣  *Tendo la ndoa la siku ya kwanza na kwa mara ya kwanza na huyo mwenzako*
👉 _Hayo ni maeneo muhimu unapaswa kuyashughulikia kwenye maombi na kuwa macho sana, hiyo ndo milango🚪🚪🚪ya maadui kupanda uharibifu katika Ndoa.
( _Nita kuchambulia moja baada ya lingine kama riho alivyo nifundisha katika hili_) Usikose sehemu ya pili katika uchambuzi huo.
    By Ev. Elisha Kazimoto(Baba Eve)
                 0755444078

No comments:

Post a Comment