*SEHEMU YA I: TAALUMA YA TENDO LA NDOA*
*_Ev. Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
_Shalom, Shalom wana ndoa, leo nakuja na somo linalo sena, *Taaluma Ya Tendo la Ndoa*, somo hili ni refu maana ndani ya somo hili kuna majibu ya maswali mengi, yanayo tesa wana ndoa,_
Lakini pia tendo la ndoa limechukuliwa kama kitu cha kawaida, kama kunawa na kula jambo ambalo halihitaji utaalamu wowote ule, hivyo kupelekea watu kuchoka ndoa haraka, kuchoka tendo la ndoa haraka, kupoteza hamu ya tendo la ndoa. *_Sasa akilini mwako jua neno moja, kila kazi inapendeza kama itafanywa kwa viwango vya ubora, chakula chochote kinakuwa kitamu pale kinapo pikwa vizuri, ila kitakuwa kibaya mpishi akivurunda ma viungo, hivo TENDO LA NDOA LINAHITAJI TAALUMA YAKE_*
_Na mimi leo nitaanza kwa kukuchambulia kitu kimoja, hadi kingine, ujue Saikolojia ya tendo la ndoa, Sayansi ya tendo la ndoa, ujue na Sanaa ya tendo la ndoa, haloo utampenda mwenzako_
*Ambatana nami mwana saikolojia, Ev. Elisha Kazimoto*
📖Ndoa inakamilishwa kwa wana ndoa kushiriki Tendo la ndoa (sex)
♠Kumekuwa na mitazamo mbali mbali juu ya tendo la ndoa ambayo imefanya watu walitazame tendo hili kama Ni wakati kupata mateso, kuridhisha hisia zako, kupata watoto nk.
♠Mbaya zaidi kila mmoja anahisi ni kitu simpoooooo ambacho hakihitaji akili, mtu yeyote, muda wowote akikurupuka anaweza kushughulika.
♠Ukweli ni kwamba watu wengi hasa wana ndoa, hawafanyi tendo la ndoa ktk ubora wake, wengi wana baka na kubakwa, wanafanya kama wajibu, wanafanya ili mradi ameweza penyeza sehemu zake za siri ndani ya za mwenzake, ili mradi amemwaga mbegu kwa mwenzake, ili mradi amesuguliwa suguliwa sehemu zake za ndani
😩😩Kuna vilio vingi ndani ya ndoa kuhusu tendo la ndoa
😲😲Kuna malalamiko mengi ndani ya ndoa kuhusu tendo la ndoa, mara hanitoshelezi, anamaliza mapema, hajitumi, anataka nje ya ndoa, ananiumiza, ananichubua nk
😁😁Kwa hali hiyo, hujui kufanya tendo la ndoa, ila unafahamu kuingiza uume na kumwaga mbegu kwa mke wako, na mke unajua tu kumsaidia mmeo kumwaga mbegu ndani ya uke wako, hakuna ziada.
🏃🏻🏃🏻💃💃kwa sababu hiyo Kuna watu wana ndoa wanakimbia tendo la ndoa, muda ukifika anatamani itokee dharula ya kuahirisha game 😉😉
🌟🌟Tendo la Ndoa lina TAALUMA yake pana sana, kwa lugha nyingine tunasema tendo la ndoa nikawa Kiwanda chenye mitambo mbali mbali ambayo inahitaji wataalamu wa kuiendesha ili kuzalisha bidhaa. Na mtambo mmoja ukikwama bidhaa hazizalishwi.
❤Tendo la ndoa ni SAYANSI ✈
❤Tendo la ndoa ni SANAA 👯👯
❤Tendo la ndoa ni SAIKOLOJIA 🙇🏽🙇🏽🙇🏽
Ukitaka kufurahia kuenjoy tendo la ndoa, usiwe mvivu wa kujifunza na kuwa mbunifu kila siku.
..
🔴🔴🔴🔴 *TENDO LA NDOA NI SHIRIKISHI*
🌟Taaluma ya tendo la ndoa inaanza kwa kutambua tendo la ndoa ni la watu wa ngapi, au ni haki ya nani.
🏆Tendo la ndoa ni shirikishi, SI uhitaji wa mtu mmoja, ni shirikishi, yaani mmoja akiwa na uhitaji amshirikishe mwenzake kwa mbinu kubwa ya kiufundi ili na yeye network ya sex, hamu isome ili waanze mchezo.
🏆Tatizo kubwa ni Mmoja akiwa na uhitaji, anacommand mwenzake, au na mwenzake anatia mgomo au anakubali shingo upande, hapo amfanyi tendo la ndoa, mnaenda Kibaruani cha tendo la ndoa 😠😠
🏆 *_TENDO LA NDOA NI LA KISAIKOLOJIA_* 🏆
🌟Walio furahia tendo la ndoa na kuhisi wapo katika Bustani ya mapumziko na furaha, niwale walotumia saikolojia ktk tendo la ndoa
🌟Tendo la ndoa kiutaalamu tunasema lina anzia akilini kabla ya kushirikishwa mwilini
🌟Kwa maana hiyo unahitaji kutengeneza mazingira ya kisaikolojia, kulijaza kwa mwenzako akilini mwake mpaka alitamani, alewe kwa hisia nzito kabla hamjaanza game
🌟Mkianza kufanya tendo la ndoa, mmoja wapo kilindi chake cha hisia kilikuwa hakija jaa mpaka kupagawishwa na emotions, na kuona muda wa kuanza game kana kwamba unachelewa, basi mjue hamtafika kilele cha furaha pamoja, lazima mmoja aishie njiani.
*_MAANDALIZI YA TENDO LA NDOA KISAIKOLOJIA_*
♦Kisaikolojia inashauriwa tendo la ndoa liwe na ratiba maalumu ktk wiki, mbali na ratiba za DHARULA zisizo weza zuiliwa, hizo zitatokea ila hazina athari.
♦Makusudi ya ratiba, ni ili wana ndoa waweze kujiandaa vzr kisaikolojia ili wale chakula kitamu kilicho andaliwa aswaa
♦Kwanza kama mnatamani kushiriki Tendo la ndoa lenye viwango vya mahaba mazito ya kuwafanya muoane ni wana ndoa Adimu wenye kutengeneza Raha ya pekee kwa mwenzio, *_HAKIKISHA MNAJIEPUSHA NA MIGOGORO KTK NDOA YENU_* 🙅🏻🙅🏻
♦Migogoro inabana saikolojia, inaziba mifereji ya hisia kali za kufurahia tendo la ndoa kwa mwenzako.
♦Mkiruhusu migogoro, kila mkifanya tendo la ndoa yafuatayo yatatokea ;
😡Hamtafurahia tendo la ndoa
😩Mtafanya tendo la ndoa kama wajibu na si kupeana zawadi ya mahaba mazito
😲Hamtafika kileleni, hasa Mwanamke
♦Hakikisha ktk siku ya ratiba ya tendo la ndoa, pamoja na amani ya kila siku, lakini itengeneze siku hiyo iwe ya pekee kwa mwenzio kwa kufanya yafuatayo ;
💌Tumianeni sms zinazo express feelings zako (kama kila mmoja yupo kazini kwake)
💏Fanyianeni utani wa kimapenzi, jaman ninyi ni wana ndoa msiseme Dhambi.
🌹🍗🍖mfanyie mwenzio suprize ya zawadi simple simple anazozipendelea mwenzako, bites, chockolet, pipi nk.
❤ *_TENDO LA NDOA NI SAYANSI._*❤
🌹Kabla ya kufanya tendo la ndoa, ni muhimu kujua Sayansi ya miili yenu usawa wake na utofauti wake.
🌹Kisayansi mwili wa Mwanamke ni tofauti kabisa na mwili wa Mwanaume, japo wanafanana katika kufurahia tendo la ndoa ikiwa watalifanya kwa Ubora.
🌹SEX, inaenda sambamba na Hisia kali za mwili.
🌹Vyanzo vya hisia za Mwanaume ni tofauti na vyanzo vya hisia za Mwanamke. Na hapa ndo wengi wamechemka ktk kufanya tendo la ndoa
🌹Mwanaume, yeye analipuliwa hisia zake kwa KUONA, akiona sehemu Adimu, kama mapaja, maziwa, tumbo, uke, hips, macho yaliyo tekwa na hisia(macho ya kimapenzi) ndani ya 60sec, uume utakuwa umesimama na yuko hoi, anatamani akurukie aanze kazi.
🌹Mwanamke hisia zake zinatengenezwa, zinachochewa taratibu, taratibu kwa kuchezewa mwili wake, maeneo Muhimu, kama nywele, kiss nzito (romance), maziwa, tumbo (kitovu), mapaja, uke na kinembe(clitoris) zoezi hilo laweza kukuchukua 30dakika, lakini kwa kutazama tu hata uwe uchi saa 1,utamuathiri kihisia 10 %tu. Ila yeye akivua tu Mwanaume utaathirika kihisia 100%ktk sekunde 30
*_ATHARI ZA KUTOJUA SAYANSI YA TENDO LA NDOA NA MWILI WAKO._*
🔴Wana ndoa wengi wanalaumiana sana na wengine kuthubutu kutoka nje ya ndoa kwa sisingizio cha mambo yafuatayo ambayo ni matokeo ya kutojua Sayansi ya tendo la ndoa.
⚫Mume kuwa na Uume mfupi
⚫Uume mwembamba na mfupi
⚫Mwanaume kumaliza mapema
⚫Mwanaume kumchubua mke sehemu za ndani za uke
⚫Mwanamke kutokuwa na ute( mucus) wa kutosha
⚫Mwanamke kumnyima Mume tendo la ndoa
🔴Hayo yote ni matokeo ya kutojua Sayansi ya tendo la ndoa na miili yenu. *_MAJIBU YA SAYANSI YA TENDO LA NDOA KATIKA MASWALI HAYO_* 👆🏻👆🏻
🔵Sayansi inasema hivi, mke hatoshelezwi kwa kuwa na Uume mnene au mrefuu, anatosherezwa na kuchezea hisia zake kiwango cha juu, raha yake haipo ndani tu, ipo sehemu za nje na ndani (Issue ni maandalizi ya kutosha) chezea mwili wake hasa
🔵Mwanaume kumaliza mapema ni tatizo la wanaume wengi wasiojua Sayansi ya tendo la ndoa, na wanaokurupuka kufanya tendo la ndoa, lakini ni uzembe wa Mwanamke kusubiri kila kitu ufanyiwe kitandan,
🔷kwa kawaida kama vile Mwanaume anawahi ku Erect ndivyo anavyo wahi kumaliza game, ila mke mjanja anaweza mbakiza uwanjani mpaka wote wafike mwisho kwa kuchezea hisia zake pale tu mme Akimwaga mbegu. (utafafanuliwa kwa part ya Sanaa)
🔵Mwanamke kutokuwa na ute fluid ya kutosha, pia ni maandalizi hafifu ya tendo la ndoa, na aina ya vyakula unakula
🔵Mwanamke kumnyima Mume tendo la ndoa, ni matokeo makuu 2,kwanza, luendekeza migogoro kati yenu, pili Taaluma ndogo ya Mwanaume kumuandaa mkewe kabla ya tendo la ndoa, so limekuwa kero.
❤ *_MAMBO YA KUYAFAYA MFIKAPO UWANJA WA GAME LA TENDO LA NDOA._*❤
♻Tendo la ndoa lina sterling 2,mmoja ni kabla ya Kuanza sex (in & out rythym) na mwingine ni mara baada ya Kuanza sex (in & out)
♻Sterling kabla kukutanisha vioungo vyenu Uume na uke, ni Mwanaume (Huyu ndo mwandaaji mkuu wa tendo la ndoa) ukichemka kuliandaa mkianza tu hamfiki mwisho kwa pamoja na litamboa hasa mkeo
♻Sterling baada ya Kuanza sex, majukumu yanabadirika, yana kuwa ya Mwanamke, (ukijilaza kama gogo tu bila kujituma, utaachwa katikati ya safari dk 15 ambapo mungeenda mpaka 2hrs)
_Niishie hapo katika sehemu ya kwanza ya Taaluma ya Tendo la Ndoa, tutaendelea na sehemu ya pili na ya tatu upate full package kuhusu tendo la ndoa, hakika utampenda mke/mme wako, utatamani mkae chakulani_
( *_Uchambuzi uliletwa kwako na Mtaalamu wa Mahusiano na Ndoa_*)
_PSYCHOLOGIST & COUNSELOR_
*EV. ELISHA KAZIMOTO (BABA EVE)*
*0755444078*
Tuesday, 29 November 2016
TAALUMA YA TENDO LA NDOA(PART I)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mungu akuinue ktk huduma by Brian Kazimoto
ReplyDelete