Tuesday, 29 November 2016

MWANAMKE USIACHE NYUMBA YAKO WAZI(PART III)

🌷 🌷Sehemu ya Tatu ya somo, Mama Usiache Nyumba Yako Wazi*🌷🌷
   By Ev. Elisha Kazimoto
               0755444078
4⃣🚪 Chumba cha Hisia🚪
👉� _Katika vyumba muhimu katika nyumba yako, hii ni bedroom_  Chumba cha hisia ni chumba hatari, maama ndicho kilisababisha useme No, kwa vijana kibao walo kuchumbia na ukasema Yes kwa huyo, na yeye ndo kilimfanya warembo wote apige chini akaku pick wewe katikati ya maelfu,  *sasa usipo linda hisia zilizo fanya hayo, mtaishi kama kaka na dada* na mpaka hapo ndoa hakuna, heshima hakuna, upendo hakuna, utii hakuna, maana kinacholeta hayo yote ni Chumba cha hisia. (Unahitaji kujua Saikolojia ya mwanaume ndo uishi naye, Mwanaume yeyote Anahitaji Sex(Big demand,Big issue ni Sex,siyo kupikiwa na kufuliwa nguo ni Sex) wewe unahaja na Care ili utulie Kisaikolojia, Ila yeye anahitaji Sex ili atulie na hapa ndo waba ndoa upishana. Anayepaswa kutoa Care ili mke atulie kisaikolojia,  na mke hatoi Sex ili mme atulie. Siri kwako mke Mbali na mapepo kuvamia ndoa yako ambayo inabidi uoambane nayo kwa maombi, gia kuu ya kumtuliza mmeo na kuuburudisha moyo wake Mpe Sex atakapo muda wowote,utamfanya aangaike kukupendeza wewe na kuku Care.
👉� Kwa nini magomvi ni mengi kwenye ndoa, angalia Wana ndoa wamepotezea Hisia zileee za mwanzo juu ya mwenzake,  *Unamuona mwenzako wa Kawaida* _Uchawi mkuu kwa wana ndoa ni kumzoea mwenzako na kumuona wa kawaida_ Mtaanza kuishi basi tu kwakuwa nina watoto wake, tumetiwa pingu💍💍za maisha ila si kama neno linavyo sema Umfurahie👇�👇�
*_Mithali 5 : 18 - Chemchemi yako ibarikiwe; Nawe umfurahie mke wa ujana wako._*
👉�👆Hivyo mama unahitaji kulinda chumba cha hisia kisiingiliwe na adui. *Unakilindaje?* _Hakikisha haufanyi mambo yatakayo umiza moyo, akili ya mme wako au yako(kwa Lugha nyingine epuka kuwa chanzo cha migogoro) migogoro ikianza ina ondoa amani na furaha, na hayo yakiondoka chemi chemi za Hisia zina ziba, basi kila kitu utakiona kawaida, unaweza ukakaa hata miezi 6,mwaka huna Hamu ya kushiriki tendo la ndoa, jibu ni kwamba Hisia juu yake huyo zimekufa,_ na hiyo ndo hatari kubwa.
👉� Katika kulinda chumba cha Hisia cha ndoa yako, zingatia mambo haya yaonekano  kuwa madooogo sana mbele za watu lakini sisi wana saikolojia ndo tunaita corner stones (kama mawe ya pembeni kwenye msingi wa nyimba),
🌷 *Usikosane na mwenzako ukapitisha muda mwingi, siku, wiki bila kupata suluhu, sameana* Umirundika makosa moyoni unaua hisia taratibu, taratibu mpaka utamuona mmeo hakufaa kukuoa. Kitu ambacho si kweli
🌷 *Utatue migogoro, hitirafu kibabe, kwa kelele, sebuleni, mbele ya watoto house girl nk* Mahakama ya wana ndoa, maneno yote magumu hutatuliwa Chumbani mkiwa wawili na Mungu katikati tena kwa sauti ya chini hata watoto Chumba cha pili hawasikii. (hapo utalinda hisia zenu)
🌷 *Usibishane, mkosoa mmeo live, live, kubali lipite hilo, mahakamani utamuonyesha mtazamo wako na ushauri wako ulivyokuwa ni muhimu, hata kama jambo limeisha fanyika, unajenga msingi wa mawazo yako kuheshika baaday.
🌷 *Usirudie, au kung'a g'ana na ulicho katazwa na mmeo,* unaua hisia zake kuona hum heshimu na yeye aanze kumudharau, hisia zinapotea
🌷 *Jitahidi kumuita jina zuri analo penda* unachochea hisia zake.
🌷 *Fanya mambo yako kwa wakati yanayo muhusu mmeo, chakula, kumwandaa kwenda kazini, muda wa kulala* Unamjengea hisia za mukuona mke makini.
🌷 *Andaa vyakula anavyo pendelea* Unaufanya moyo wake ukufurahie muda wote.
🌷 *Usipende kuwa mgumu, kujizungusha, kusema uongo, kukwepa unapoombwa kushiriki tendo la ndoa* Kuwa shapu, mwenye  furaha na tayari kama hauna tatizo la kiafya.. Hii itaifanya akili ya mmeo ikiwaze wewe daima. Kama haujisikii vizuri tafuta mbinu nzuri umweleweshe akuelewe, awe na Amani.
🌷🌷🌷Hisia zikifa Ndo imekufa, na zikipona ndoa imepona🌷🌷🌷
*_Masomo haya, na mengine mengi yanapatikana katika Pages zangu za Facebook, account hizi,  Hazina ya Maarifa na Elisha Anointedman, Prophet Elisha Anointed person, Bado Liko Tumaini Ministry_* Huko utakuta masomo mengi yatakayo kujenga kiroho na kimwili.
5⃣🚪 *Chumba cha Uchumi*🚪
🌷 Mama kama mtendaji mkuu wa familia unahitaji sana kujua namna ya kulinda pesa inayoingia ndani ya nyumba, ili kuweza kufanikisha mipango ta familia yenu ili miwe na maendeleo mazuri.
🌷 Unahitaji kutumia akili kama mjenzi na mlinzi, kwa pesa unayopewa ya shopping, kujia namna gani naweza kupata senti 1,kila ninapopewa pesa, ili angalau ikifika 10,ninunue vitambaa vya makochi, ambavyo naona mme wangu haja viweka kwenye bujeti, lakini.
🌷 Lakini mama kama wewe si mfanyakazi wa serikali, hakikisha unajishughulisha na kitu hata kidogo, kiingize pesa, ili ufanye vitu vidogo vidogo ndani ya nyumba yenu ipendeze, hata mkipata mgeni, akute nyumba yenu, muwe mnapanga, au mmejenga pana vutia.
Ngoja nikwambie mama uliyeolewa, *_Wanaume mawazo yao na macho yao huona mambo makubwa, mfano.. Kununua usafiri, viwanja kujenga nyumba, nk, hawonagi vitu sijui mambo ya sebuleni, vitambaa vya makochi, nk, hivyo Mwanamke chemsha akili, watu wakija ndani wakajuta nyumba haieleweki, hawansemi mumeo, ni Mwanamke ndo watamdharau._* unahitaji kulinda chumba cha Uchumi sana, sifa ya mume ni kutumia pesa, sasa na wewe wa kutumia pesa  umaskini, unawajia, tumia Hekima kumsaidia mmeo pesa ikae ndani.
🌷 Wale wamama mnao aminiwa na kukabidhiwa mshahara wote na mmeo, hongera wewe una nafasi kubwa ya kuifanya familia yako kuoiga hatua za maendeleo sana. Wanawake wengine siyo waaminifu ndiyo maana waume zao hawawakabidhi pesa nyingi. Wakipiwa pesa mara, kujiremba tu, kula vizuri mwanzo mwisho mpaka pesa inaisha kabla ya mwezi. Utalazimisha mmeo awe mwenyekiti na mwazini, ambapo mwazini katika familia ni mama, mmeo ni mwenyekiti, kazi ni kuidhinisha matumizi.
_Ukiweza kulinda chumba cha Uchumi, utaifanya ndoa yako kuwa na Amani._
6⃣🚪 *Chumba cha Marafiki na washauri*🚪
🌷 _Ndoa nyingi zipo kwenye moto, zina crack ya amani, upendo na furaha, asilimia kubwa ya majanga hayo, ni matokeo ya marafiki, na washauri waliojiweka karibu kwako mama_
Kuna marafiki ambao ni sumu kwenye ndoa, Marafiki na washauri wanao ambatana na wewe lakini ndoa yako inayumba, hao achana nao. Hakuna kitu cha thamani katika maisha kama ndoa ya amani, kwa sababu hiyo linda kwa gharama yoyote, unapoona rafiki, au mwana familia, ma sheshemeji, wifi, kaka, dada, wazazi wanataka kuleta shida kwenye ndoa yako, huo ndiyo muda wa kuongeza akili kuwa kabili👇�👇
*_Mithali 13 : 20 - Enenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima; Bali rafiki wa wapumbavu ataumia._*
👉� mama ukiambatana na marafiki wasio faa, wanao kushauri vibaya, huko saloon, huko kwenye vyama vya wanawake, _eti mimi mwanaume hawezi niendesha, alileta za kuleta usiku ntamkomesha simpi te do la ndoa, akini vuruga narudi kwetu_ *Haloo mama utaumia sana, wakati wenzako wako wana kula nyama na lutoka out na waume zao wewe una sota*
🌷 Hapa na sema na wote mama na baba, ila mama utengeneze mazingira ya mmeo kukupenda zaidi, ili akulinde na nguvu ya watu wa karibu kama familia.
🌷 *Ikifikia hatua ya kulinda mke, au mme haloo jifunge mkanda wa ujasiri, kwa akili sana pambana na wahuni waletao chokochoko, maneno iki mkosane, wadhibiti*
🌷 Mama, usikubali watu wengine wawe na kauli juu ya mmeo, sijui wazazi, ndugu, mara wanakwambia mmeo hiki, mara lile, ooho mmeo hatumuelewi, wanaleta shida sana, *WAPIGE STOP* huyo ni mmeo, mkisha kosana, moto ukawaka ndani, wao watakaa mbali.
🌷 *_Hivyo, hivyo na kwa wanaume na waasa, niliye mwanaume mwenzenu, Achana na udhaifu wa kukubali kila kitu, leo ndugu wanasema hili kwa mkeo, wazazi, yaani mkeo anakuwa kiwanja cha mazoezi cha kila mtu kujifunzia kuonya au kusema, kusuta, kila wakikutembelea wakondoka ndoa moto, PIGA MARUFUKU KUKANYAGA HAPO NYUMBANI KAMA HAWANA AJENDA NJEMA* ndoa siyo biashara kwamba ntafanya nyingine, Mlinde mkeo, kama kuonya, kufundisha, kuelekeza, wewe mwanaume ndo mwalimu wa kwanza na wa mwisho na Mungu wenu, wengine tu mashabiki. 👇�👇�👇�
*_Zaburi 38 : 11 - Wanipendao na rafiki zangu wanasimama mbali na pigo langu; Naam, karibu zangu wamesimama mbali._*
👉 Mkiruhusu kila mmoja anakuwa msemaji wa ndoa yenu, mtapoteana ndani, na wao watasimama mbali, wakati mnalala mzungu wa nne, tendo la ndoa halifanyiki, haji rafiki, wala ndugu, wala mzazi kukusaidia mfanye tendo la ndoa na mpige story. Watasimama mbaliii wataishia kushauri, kukuanika nje, kukunyoshea vidole, ndoa yenu inaangamia.
🌷 *Narudia Tena, Kama mmeo, mkeo halubadirishwa na wazazi akiwa mdogo, dunia haikumbadirisha, wewe hutambadirisha kwa nguvu*
_Niwashauri wana ndoa, kuhusu kubadirisha tabia ya mwenzio, usitumie ubabe, ukali, adhabu, huyo si mtoto, hasa sisi tuliookoka, nenda kwa Mungu mlilie Mungu, halafu tumia akili sana kuliko nguvu, kusema naye, kumpenda ndo ubadirishe tabia yake, Dhambi ikatae, na simama kwa kusema No. Ila vitu hivyi vya Interests, tumia akili na ukiona watu wanapenda sana Kudeal na Mmeo, au Mkeo kana kwamba yeye ni mjane, au mgane, wanamnyima raha wakati wewe upo, Deal nao kwa hakima, tetea ndoa, linda ndoa, usipo furahia ndoa unaweza usiende mbinguni hii ni utafiti na ni kwa 75% UNAACHWA KWASABABU NDOA INA SHIDA._
🌷🌷 Mungu awabariki tukutane katika somo lingine. _Ni mwalimu wa mahusiano na Ndoa, Ev. Elisha Kazimoto (Baba Eve)_🌷🌷
            0755444078

No comments:

Post a Comment