🍎🍎 NAMNA YA KUMPATA MWENZI WAKO WA MAISHA🍎🍎
By Ev. Elisha Kazimoto
0755444078
kwanza lazima ujue mambo ya msingi kabla yakuanza kumtafuta mke au mme wako wa maishani mwako.
I) Usimjaribu mtu kama atakubali au atakataa, nenda ukiwa umedhamilia kuwa huyo ndo umpendaye. Ukijaribu hutapata kitu sahihi.
II) Hakikisha unajua ni mtu wa aina ipi unamuhitaji maishani mwako, itakupunguzia, kugusa gusa kila mtu.
III) Jitathimini kama unaweza kuumizwa na ukahesabu ni changamoto, ukasonga mbele na maisha yako kwa amani.
IV) jiulize wewe ni mzembe katika mambo ya Mungu au unajuhudi? Maana Mungu hatafanya kosa kukupa kitu tofauti na wewe ulivyo.
V) Jitathimini unauwezo wa kusamehe, Maana mahusiano yanahitaji kusameana.
*MAMBO YAKUZINGATIA UNAPO ENDA KUANZISHA MAHUSIANO BINTI/KIJANA.*
i) Jiamini, kuwa wewe unafaa sana kumuoa uliye mwendea, au unafaa sana na unaviwango vya kuolewa na huyo alo kufuata endapo mmependana. Ukijiona mnyonge kwa sababu ya familia yao, au pesa zake au elimu yake, basi utakuwa mtumwa katika mahusiano.
ii) Jijali, kuwa smart, hakuna mtu awe msichana au mvulana anayependa mtu asiye jitambua ki Personality, kuwa mtanashati au mrembo, Personality ina nguvu ktk mahusiano. Unaweza kuwa unanena kwalugha ili shagala bagala, utazeeka bila kuoa au kuolewa, siyo jaribu ni wewe.
iii) Usiende kwa mbwembwe kuanzisha mahusiano, be natural, sema hisia zako, usitunge maono, ndoto usizoota, sema unavyojisikia kuhusu huyo.
iv) Hakikisha umemsoma mtu unaye mpenda uone kamnalandana ktk Interests,
V) Usimchukue mtu, kisa pesa, elimu, au cheo, pima kina cha moyo wako kina upendo wa dhati kwake?, ndoa si pesa, wala elimu, ni upendo amani na furaha, unapo muona mwenzako.
*SWALI MUHIMU :NDOA NI SUALA LA KIBINADAMU NA KUBAHATISHA AU NI HALISI NA LA KIBIBLIA?*
Vijana wengi wameingia katika ndoa feki kwa Kuto jua misingi wa ndoa..
Mke au mme, hapatikani kwa kubahatisha, anapatikana kwa kanuni za Kimungu.
Wengi wanajiuliza swali hili, njia gani nimpate mme au mke? Zifuatazo ni kanuni za KIBIBLIA za kumpata mwenzi
I) Lazima uwe mtu wa kuwajibika, kujishughulisha na mambo ya Mungu kwa moyo wa bidii, na nia ya kumtumikia Mungu si ili upate mke au mme.
Mungu hakupi mtu wa kuzaa, kukutunza, kufua na kupika, bali anakupa msaidizi kwa kazi yake alo kupa zikiwemo zako na uhitaji wako wa mwili.
Tatizo la kupata mtu huku wewe ni mzembe, ni kupata mtu mtakaye shindana daima na si msaidizi. *MWANZO 2:18-25* Adamu alipiga kazi ndo anapewa msaidizi.(kuwaita majina wanyama na ndege ilikuwa kazi ngumu sana,na unaipiga pekeako bila mwingine. Hii ilimpa Credits za kutafutiwa mwenza.
II) Unahitaji kuwa mtu wa maombi ya bidii, kuombea mwenzako, Mungu amfinyange akufae na amfae Mungu, kila mtu anamapungufu, kama huombi utampata akiwa na nature yake bila kupuruniwa, mtazozana daima. Jifunze kuombea mwenzako na kazi ya Mungu.
Pia kazi ya maombi ni kumthibitisha mwenzako kuwa yeye ndiye au umtazamie mwingine,kumfunua mwenzako aliko ajulikane kwako. *YAKOBO 5:16* Kuna point mbili, maombi ya mwenye haki(sasa vijana wanaomba huku wameisha onja,huyu,yule)usitegemee majibu ya Mungu, lakini pili Maombi ya mwenye haki akiomba KWA BIDII, sasa ukifubga siku 3,hapo unaona ndo bidii, bidii haina mwisho,kukata tamaa,lakini unafanya kitu beyond normal.
*_By Ev. Elisha Kazimoto(Baba Eve)_*
*0755444078
Tuesday, 29 November 2016
NAMNA YA KUMPATA MWENZI WAKO WA MAISHA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment