Tuesday, 29 November 2016

MAANDALIZI YA KIROHO YA KUINGIA KATIKA NDOA(PART II)

💝💝 SEHEMU YA PILI; MAANDALIZI YA KIROHO KWA NDOA YAKO MPYA💝💝
By Ev. Elisha Kazimoto(Baba Eve)
                 0755444078
Mtu wa Mungu upendwaye sana na Mungu karibu katika sehemu hii ya pili, upate Maarifa ya kujiandaa kuingia katika ndoa takatifu kwa Ushindi, lakini siyo kwa vijana tu, hata wazazi mtakua namna ya kuwaombea watoto wenu katika kipindi hiki muhimu kwa maisha yao_  Tutaongozwa na Andiko la *2Wakorintho 2:11* Tupate nguvu ya kukaba Kona zote za adui tuanze na Bwana kwa Ushindi. 👇�👇�
*_2 Wakorintho 2 : 11 - Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake._*
💝  Kuna mazingira shetani amewashinda wana ndoa, kwa sababu wameshindwa mapema *Kuzijua Fikira za Adui* Kwa neema ya Mungu leo unafunuliwa siri hizi, ujue namna ya kusimama kwenye maombi yako.
👉� _Tuziangalie hizi sehemu 8,zilizo orodheshwa juu kwenye sehemu ya kwanza ya somo hili:_
1⃣  *Kipindi cha kujitambulisha kwa wazazi pande mbili za familia* Kipindi hiki ni muhimu kukiombea, mnapo kutana na mwenzako mkakubaliana ninyi kuoana, mkapendana, msishangilie kwamba sasa tayari nimeisha mpata, kuna safari ya kujitambulisha,(Kijana kumtambulisha binti kwa familia yake wamjue, vivyo hivyo kwa binti kumtambulisha kijana kwa familia yake wamjue.
👉� _Katika Kipindi hiki adui anaweza kukufungia kibali, Usikubalike, usipendwe kwenye Familia, ukampeleka *3/4* ya wana familia wakasema huyu Hapana *(NO)*❌❌❌❌ sasa ukakuta wanao kikubali ni 2,3 kati ya famikia na jamaa yote_ hii inaweza pelekea mkavunja uchumba, (mtazalisha majeraha ya mioyo na Regret kwenye ndoa nyingine utakayo ipata, pale itokeapo changamoto ya kindoa)
👉� Lakini mnaweza kukomaa mkaoana, mtaanza maisha na ukuta wa mahusiano mabaya katika familia(mtakuwa na kazi ya kupambana kujenga mahusiano ya kifamilia na kuishi maisha ya taadhari na kujihami sana)
👉� Lengo la adui la kubana furaha na amani katika ndoa linakuwa limefanikiwa, kwani atatumia mwanya huo wa kutokukubalika katika familia husika, kuleta migogoro kati yenu na familia kwa ujumla, _Lakini kupitia mlango huo wa kuto kukubalika anaweza kuwainua maadui kwenye familia wawapige mishale na kuwasumbua sana, ili mradi ndoa iyumbe._
👉�🙏�  *Sasa ukimpata mwenzi, katika mchakato wa kumtambulisha mwenzako, fanyeni maombi ya kuonba kibali mbele za Mungu na mbele za familia yote, mkubalike, mpendwe, mpewe support na baraka zote*  huo ndo umuhimu wa kuwa vizuri na Mungu.
2⃣  *Kipindi cha kupeleka Mahari(Sherehe za Mahari)* Kipindi hiki pia ni Kipindi muhimu cha kuombea, kipite salama, katika Kipindi hiki kuna kukosa kukamilisha mahari, mkabaki na deni, ukakopa mke, ikawashushia heshima, kibali, na ikaleta kero katika ndoa, lakini pia kuna kuambiwa maali kubwa kuliko uwezo na wakagoma kushusha, linakuwa jaribu kwenu, mnakopa, mnasogeza mbele sana harusi, au mnabebana kienyeji?
👉� Lakini pia kuna mambo yanayo ambatana na pesa mkichomekewa kitu msicho kijua vizuri kumbe ni kwaajili ya babu, bibi, shangazi aliye kufa, mnaunganishwa na maroho ya kifamilia(mapepo) juu kwa juu yanakuja kuwa mwiba kwenye ndoa, maana mlisha yavika, yaenzi nk.
👉�🙏�  *_ Kwa hiyo mkishaamua kuanza mchakato, omba mpangiwe mahari iliyo katika uwezo wenu(kijana), omba na kubatilisha nguvu ya mila na tamaduni zenye viashiria vya matambiko visihusishwe na ndoa yenu.* kwa namna hiyo mtakuwa mmeufunga mlango wa adui. Mmepunguza speed yake kuwafuatia.
3⃣ *Kipindi cha kitchen Party* Shughuli hii inahusu kumwandaa binti kwaajili ya ndoa yake, Kipindi hiki ni muhimu sana, lakini bahati mbaya kanisa limekosa kitu hiki, watu sahihi wakutumia nafasi hii kuweka msingi mzuri wa ndoa,  badala yake Afla hii inashikwa watu wakawaida, wengine ni maadui(mawakala wa shetani), na wengine wanakuja wamejiandaa kwa kupenyeza silaha ya maneno juu ya ndoa, wengine wanakuja na zawadi zilizo setiwa kuleta madhara kwenye ndoa(kipengele cha zawadi ntafafanua kwa kina)
👉�🙏�  _Mnapo endelea na safari ya maandalizi ya harusi, omba kipindi hicho adui asikutumie kumpandia mwanamke wazo potofu juu ya wanaume, ndoa nk_( Maana wenginebwafundaji wa binti,ni wabovu kwa waume zao,wengine wameachika,niwakorofi,wanaweza mpanda roho ovu ndoa yenu ikayumba ndani ya mwaka 1,mke anakuja amejiandaa kwa Reactions)
4⃣  *Sendoff* Kipindi muhimu sana, kinachoambatana na mambo mengi, majira haya ya send off wakati binti anaagwa, kinajumuhisha watu wengi, wazuri na wabaya, *_Kwakadri mnavyo karibia kuhitimisha safari ndivyo mnavyo ongeza uwanja wa maadui_* 
👉�  Ikumbukwe kuwa kuna maadui walioko ndani ya familia yako binti, hawapendi uolewe au uwe na ndoa nzuri, hivyo hivyo kwa wageni waalikwa wote na vikundi vyote vilivyo jiandaa kutoa zawadi kukuaga, kukusindikiza, wote wanania hiyo, wengine wanakuja wameji koki kulipua ndoa yako kwa zawadi tu watakazo kupa, salamu watakazo kuaga nazo. Kuwa macho usijisahau... Wakiku *Send* na mateso, utasa, kukataliwa, magonjwa utaumia sana katika ndoa.
👉�🙏�  *_Omba uondoke vizuri nyumbani kwenu bila kubebeshwa mabomu ya hatari, yakaja kuripukia ndani ya ndoa yenu_*
5⃣  *Kipindi cha Harusi* Ni eneo na muda muhimu wenye ushindani, maana kwa maadui wengi ndo inakuwa hatua yao ya mwisho kutega mtego, iombeeni harusi kwa nguvu kubwa, muda huu ndo maadui wa pande mbili za familia na kundi la maadui wasio na undugu wanajipanga kushambulia.
👉� Harusi nyingi zimekumbana na vituko siku hiyi ya harusi, bibi harusi hoi, bwana harusi yuko hoi, na kama hakuna watu wenye macho ya kiroho ndo siku muhimu ya wachawi kuchoma ndoa hiyo au kuwa fedhehesha maarusi. Kuna vitu vinaambatana katika harusi kama zawadi na salamu, ni nyenzo muhimu za mashambulizi, mnapoomba kuweni makini sana na harusi, fuatana nami namba 6👇�👇�👇
6⃣  *Zawadi* Zawadi ni nyenzo muhimu inayo tumiwa na maadui kujerui, kutesa, kufunga na kuua, jipange kwanza kabla ya Sherehe zote zinazo husisha zawadi, mpaka siku ya harusi wakati wa kupokea zawadi, na kufungua zawadi na kutumia zawadi. *Sikiliza siri hizi*
👉� _Kwa nini uombee zawadi,? Wakati wa uletaji zawadi, zingine wanawafunika, zingine wana wapa sasa maadui wana nuizia zawadi hizo mkizutumia ndo mwanzo wa taabu, mambo yanayo ambatana na zawadi:_ *Kuachilia roho ya mafarakano, kuonana tofauti na mlivyo kuwa mkichumbiana, utasa, na umaskini*
👉� Kuna maharusi flani wali letewa pear ya viatu vyote vya mguu wa kushoto, nguo za ndani ambazo zimeisha tumika, Lakini Mungu akawafunulia, maana yake, viatu vya mguu mmoja, mpate watoto jinsia moja tu, nguo za ndani kuharibu tendo la ndoa nk. Maadui hawatuwazii mema.
👉�  *_Mnapoomba shughurikia, zawadi, haijalishi imetoka wapi, au ni kubwa au ndogo, futa manuizo yote yaliyoelekezwa kwenye ndoa kupitia zawadi, tumia damu ya Yesu kutakasa vitu vyote, na mtakavyo bitilia mashaka chomeni_🔥🔥🔥
👉� Ni muhimu kuset watu waombaji, na wenye ufahamu katika kupokea zawadi, zile za watu mnao wajua kabisa ni maadui, zitambukiwe, zitengwe, pigeni moto kama imani haiko juu sana.
7⃣  *Salamu wakati wa sharehe(hugs)* Miongoni mwa vitu nilivyo himizwa kuvifanya na mke wangu, ni kupangua kwenye ulimwengu wa roho, kabla wakati huo na baada ya tukio, ma kuzuiliwa hata watu wengine tusiwape hugs. _Kwa nini, kuna salamu, hugs zinaambatana na mishale ya mashambulizi, na wengine kukuvika maroho ya mateso._ kwa sababu hiyo kuwa makini moyo wako na akili yako isikae tu kusherekea, bali endelea kupangua, kupinga mashambulizi yanayo tumwa.
8⃣  Tendo ka ndoa ndo moyo wa Ndoa,ndo tendo linalokutofautisha kati yako na vijana wengine,ndo palipo fungwa Agano la Amani au Migogoro. Uchezee....Waweza oa au olewa unahisi Hamu na uhitaji mkubwa wa sex,ukaingia kwenye ndoa Ikakatika Ghafla,tafuta hisia hazipo,haziji...Jua kuna mtu anatafutwa na Adui kuangusha au kuiyumbisha ndoa. _Ukikatiwa umeme wa sex waweza kaka na mwenzako kitanda kimoja,shuka moja mwezi 1,2,5, bika sex,hujisikii hata kupapaswa_ Hilo ni shambulio kwenye ulimwengu wa roho.
👉Mambo 2 waweza fanya, moja onana na wanasaikolojia watakusaidia, pili onana na watumishi wa Mungu wakufungue kifungo hicho....Kama ni mwenzako fanya operation ya kiroho ya kumfu gua mwili wake.
👉Kuna watu wanaridhishwa na majini usiku na wanaachwa wameondolewa hamu ya kibinadamu kwa hiyo anashughurika na mapepo bila kujua au kwa kujua ila aibu kukwambia...Sasa umfungue kwa maombi urejeze hisia zake.
*Kipindi cha kwanza cha Tendo la ndoa*,  Hapa baadhi ya watu wameshambuliwa na maadui, kwa kuwatumia zawadi kuwadhohofisha katika tendo la ndoa, aidha kwa kumfanya mmoja wapo asitoshelezwe, apoteze hamu ya tendo, apoteze nguvu za tendo, amchukie mwenzake na kutomkubali kwenye nafsi kushiriki naye tendo( _Hii ni halisi ni miongoni mwa huduma ya maombezi nimefanyia wana ndoa wenye mwezi 1 wameoana_) walichezewa mchezo huu.  *Ni vizuri kuomba kabla, Mungu awape kuridhishana, kufurahiana katika tendo, na ni vizuri siku hiyo kabla ya kuanza mujikabidhi kwa Mungu (*siku ya kwanza)
_Ulikuwa nami mchambizi wa mahusiano na Ndoa Ev. Elisha Kazimoto(Baba Eve)_
      *0755444078*

No comments:

Post a Comment