Tuesday, 29 November 2016

HIVI NI KWELI MWANAMKE AKIVAA SURUALI NI DHAMBI?

💙💙 *HIVI MWANAMKE AKIVAA SURUALI TU, NI DHAMBI?*💙💙
   _By Ev. Elisha Kazimoto_
     *0755444078
_Shalom, shalom waenda mbinguni, leo nieona niseme, nitoe mtazamo wangu, baada ya kukutana na changamoto hii kwemye magroup ya whatsapp, Facebook, makanisani ni mijadala isiyo isha, miaka nenda Rudi, ni suruali, suruali, dhambi, siyo dhambi, sasa na mimi nimekuja na mtazamo wangu kwa kadri ya Neema hiyo niliyo pewa ya kumjua Mungu_ *Sikushawishi, si lazims uamini niaminivyo, ila ntalinena neno la Bwana*( _Karibu tuanze kwa kutafakari maswali haya_) 👇�👇👇�👇
*MASWALI YA MSINGI*
👉�Dhambi nini?
👉�Dhambi ni uniform kwa watu wote au inategemea na mazingira?
👉�Dhambi kwa mavazi, ipo kwa vazi lenyewe au kwa mtu anaye vaa?
👉�Mungu ana hukumu matunda au Mbegu(tendo au Nia ya ndani)?
👉�Kwa mujibu wa Kumbukumbu la torati 22:5,mavazi ya kike ni yapi na ya kiume ni yapi?
👉 Je, Kukwaza ni dhambi au siyo dhambi?
_Hayo maswali yakijibiwa vizuri, wanawake watavaa suruali, au hawata vaa suruali._
🍇 *_Ijulikane kabisa dhambi ni uasi, kwenda kinume na maagizo, na dhambi haina kabila, lugha wala taifa, ni moja duniani kote ndo maana tuna Neno la Mungu moja, ndiyo Uzani⚖ wa kupima Uovu(Dhambi) na Haki Dunia yote._
*HIVI MWANAMKE AKIVAA SURUALI NI DHAMBI?*
🍇 Wapendwa nianzie kwenye swali hili, kumekuwa na sintofahamu makanisani na kutofautiana katika mitazamo ya mavazi, wengine suruali kwa wanawake 👖👖 ruksa, hata kanisani, praise team, wengine hata, ukivaa safarini, chumbani, ni dhambi yaani kuinunua tu ni dhambi, sasa ukweli ni upi na kila mmoja anasimamia maandiko?
🍇Kwa hiyo, andiko hili, halithibitishi, vazi halisi la kiume ni lipi na la kike ni lipi, mfano, kuna nchi nyingi kama za scandnavia, ulaya, America, kuna baridi kali watu wote wanavaa suruali, Je, hawa watu wahukumiwe kwa andiko hili kuwa ni dhambi? Tutapata majibu katika uchambuzi huu....
👉�Ikiwa ni kwa andiko hili, tu hukumu mavazi, basi wanaume vazi lao ni Kanzu. Hata Yesu alivaa kanzu
_Nigusie hii dhana ya Andiko la Kumbukumbu 22:5,pale kila utamadumi utatafsiri kivyake, maana kuna jamii zingine suruali ndo vazi la heshima la kumsitiri Mwanamke na kanzu (gauni) vazi la kiume, kwa hiyo tusi weke dhambi kwa suruali, suruali kama suruali halina dhambi, ila mvaaji ndo mwenye nia ya dhambi_
Warumi 14 : 2 - Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.
👉� _Wewe ambaye unaitazama suruali kama dhambi kwako ukiivaa, usijaribu kuvaa kwako ni dhambi, umekwisha kujihukumu nafsi, na kila tendo lisilo tokana na imani ni dhambi_  Yule avaaye kwa nia ya vazi, la kujisitiri, kwa nia safi, nia yake haikuwaza uovu, amevaa yeye kama yeye, usimuhumukumu wewe usiye vaa, maana yeye anaimani na dhamiri yake yamshuhudia vema.
Mathayo 5 : 28 - lakini mimi nawaambia, Kila mtu atazamaye mwanamke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
👉�👆�Agano la kale dhambi ilikuwa ni matendo, na yalihumumiwa matendo, lakini agano jipya Yesu anahukumu kuanzia nia, yaani mpaka umezini, siku ulo zini, siyo siku uloanguka, ulizini na kuanguka tangu ulipo anza mchakato wa nitalala na huyu binti, au ulipo kubali kwamba ntakupa👉�👙, sasa wewe unaye vaa suruali 👖ndani yako umekusudia nini, ndo hukumu inako anzia.
Warumi 8 : 27 - Na yeye aichunguzaye mioyo aijua nia ya Roho ilivyo, kwa kuwa huwaombea watakatifu kama apendavyo Mungu.
👉�👆�Mungu anatujua vizuri, kwa kuichunguza Nia ya moyo na kujua, huyu amevaa suruali lakini lengo, ka msukumo awatege watu, aonyeshe umbo lake, nk, nk... Huyu amevaa walaaa hana lolote ndani, kavaa kujisitiri na safari, na kazi hii, sheria ya ofisini nk, na Ameamua kuvaa ya heshima
🍇   *_Lakini wapendwa tusiwe na ufahamu mdogo, wewe waihukumu suruali kama dhambi, hujui gauni, blause, sketi nayo ni dhambi, ila tu umevaaje, ikoje? Kwani vimini ni suruali? Vitop ni suruali? Magauni na sketi za mpasuo hatari ni suruali? Je, ni vizuri kwa sababu ni nguo za kike? Kata K, suruali siyo dhambi kwa sababu imevaliwa na mvulana ni vazi lake? Tusiwe na ufahamu finyu panua fikira_
👉�Kwa maana hiyi, basi dhambi iwe ni mfumo wa uvaaji na aina ya uvaaji, hapo ndo haki itatendeka.
🍇 Lakini, tunapo soma maandiko tuyaelewe na Context yake, tusijenge fundisho kwa scripture moja, waloambiwa wana wa Israel kwa lengo maalumu la Kimungu kwa walati ule, wewe uhukumuye suruali 👖 kwa wadada, pia Usile kiti moto🐖🐖🐖🐖🐖 nguruwe, Mungu alisha sema Ni najisi, sasa vitu vitamu siyi dhambi, ila visivyo vitamu, havikuvutii ni dhambi? Tafakari, Mungu huyo huyo alowavika mavazi Adamu na Hawa, aliwekawapi ili la Adamu suruali, Hawa sketi? Mimi nakutafakarisha mwisho wa uchambuzi wangu ntatoa msimamo wangu mimi kama mimi, ila na mimi nina roho wa Bwana
*_Mwanzo 3 : 21 - Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika_* Haya mavazi ilikuwa suruali, kanga, gauni, pedo, mini, kanzu, vitenge, suti, na kipi alipewa nani? Usibane ufahamu wako sehemu moja, unapo tafuta mti kumuua 🐍nyoka na kumtupa shimo, refu mchina binadamu mwenzako, anamshukuru Mungu kwa kupata Kitoweo🍗🍤.
👉�Sasa tunapo angalia andiko moja na kujenga fundisho la dhambi ya kitu, tutajikuta kila kitu dhambi, dhambi, na tataanzishwa makanisa ya dhambi, dhambi, tutaacha kuihubiri kweli ya Kristo.
*Kwa kuwa mada hii imekuwa tata na imeleta kigugumizi kanisani, mimi sitaifumbia macho, na inena kama nitakavyo pewa neema ya kuinena, na nakuomba panua mawazo, Usibaki na ulivyo pandijiziwa na Imani ya Dhehebu lako, angalia Neno linasemaje? Naomba utafakari haya chini, mifano hii*👇�👇
🍇 Nimesema, tukitumia andiko moja kuweka fundisho la dhambi, dhambi.... Kwanza tutafungua madhehebu mengi ya dhambi,  dhambi, na tutakuwa na makanisa ya dhambi, dhambi lakini hatuihubiri kwrli ya Mungu, na makusudi ya kuanzisha hiyo dhambi, dhambi siyo kuwafanya watu wawe watakatifu ila kuwavuruga vichwa na kuwafanya watakatifu wa mwili lakini rohoni yooote yanafanyika yale yale tulo sema, dhambi, dhambi
🍇 Wewe unaye tumia, andiko hili Kumbukumbu la torati 22 :5, usiishie kutovaa suruali 👖, pia usisuke, kwani Andiko la mtume Paulo hujaliona analo kataza kusuka? (Si kuna dhehebu flani hawarusiwi kusuka) na wao wametumia andiko kutafuta utakatifu, sasa wewe usiye vaa suruali lakini unasuka, tena rasta, wigi, kawaida, ziko mbingu ngapi?
👉 Lakini pia, wewe usiye vaa suruali 👖, au husuki pia Funga Kitambaa kichwani muda wote, kwani hujasoma andiko linalo sema mwanamke asikae kichwa wazi? Funika maramoja nyumban mwa Bwana utimize haki yote(Si kuna dhehebu wote Wanawake ni vitambaa kichwani, hata ukienda mgeni kichwa wazi utapewa mlangoni na shemasi? (si nao wanaenda mbinguni)? Sasa ziko mbingu ngapi?
🍇Lakini kuna dhehebu ambao nguo ya Mwanamke yoyote, iwe suti, au gauni, sketi, sharti iwe na Malinda, hawa nao wana tafuta utakatifu na kuwalinda watu na matamanio ya mwili wa mwanamje, hao ni baadhi kwa madhehebu ya Kikristo, tena ta kipentekoste, saaa wapendwa tunatafuta utakatifu wa mavazi tu, hatufundishi watu wamjue Mungu Roho wa Bwana awafundishe kuvaa, kujipamba, kula, kuongea, tumejikita ma suruali kwa wanawake, wigi, rasta, rangi, kujipamba nooooo❌❌❌❌ tuwe natural, Sawa mbona *_Zinaaa ipo ya kutisha kuanzia washirika mpaka madhabahuni, Wapiga vyombo na Praise team ni zinaa tu?
_Wachawi wamejaa makanisani? Wezi wa mafungu ya kumi? Mbona wazushi na wanao chonganisha watu wamejaa_ watu roho chafu kweli kweli, ila wamefunga vitambaa vichwani, wamevaa malinda, wamenyoa nywele wanawake, wamevaa magauni wadada na sketi mpaka kisiginoni ila mchumba wake Mpagani, Ametoa mimba, hajaolewa ila analala kwa kijana jioni, ni wachumba ila wanaendelea kushiriki ngono, ila ni vipngozi wa kanisa, wana kwaya. *_Hainingii akilini_*
*_Luka 11 : 42 - Lakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili._*
👉�👆�Tusiwe nafarisayo, kuyaacha mambo ya Adili na kupambana na mambo ya mwili, eti mavazi( *_Unielewe, sishabikii Uvaaji Mbovu hata siku moja_*)  *Ila sishabikii Uanzishwaji wa Madhehebu ya Hii dhambi, hii dhambi,*na pendezwa na _Ufundishaji wa kweli ya Mungu, watu wa njue Mungu, Roho wa Bwana aliye Aba, yaani baba, anaye tujua aseme, mwanangu, usivae suruali hapa, hapa vaa, usisuke, omba, toa, shuhudia nk_
*_Mathayo 23 : 24 - Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia._*
👉�Hii ni aibu kwa watu wa rohoni, mijadala ya mawazi, kujipamba, mpaka na Viongozi wanaweka na sheria ya mwili lazima ujipambe hivi, uvae hivi, *_Jamani hatuwezi ongozwa na Roho? Neno la kuwa na Kiasi kwa mambo yote hatuwezi letendea kazi ili tumpendeze Mungu na wanadamu?_*
*MSIMAMO WANGU KUHUSU MAVAZI*
✍ _Jambo la kwanza, kila mtu naangalie alivyo itwa na Mungu  je, anayo kasi ya kiroho mbele za Mungu? Ili Roho wa kweli amwongoze_ Biblia inasema *Wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndiyo wana wa Mungu :Warumi 8:14*, Tafuta kuongozwa na Roho wa Bwana na si sheria ya kanisa wala dhehebu.
✍ _Itazame nia yako ya kile inachoenda kuvaa inalenga nini, msukumo wake ni upi, maana Mungu anaichunguza nia ya moyo_  *Warumi 8:27* Kama unavaa kwa nia ya kujichoresha, kuteka, kuibua hisia za watu, nk, umekwisha jihukumu, lakini kama wavaa kwa kujisitiri vema vaa, Mungu anaona.
✍ _Wewe uvaaye, ukijue neno, Kama katika mazingira yako, ukivaa hivyo unawakwaza watu, jiepushe na makwazo *Usivae*, maana Kuna Ole wa yule aletaye Makwazo_  *Luka 17:1-3* Lakini ukiwa kwenye mazingira yasiyo kwazwa na huo ivaaji, maadamu dhamili yako haikuhukumu Vaa.
✍ _Wewe usiye vaa kwakuwa unaona ni dhambi, siyo safi, Kwa waraka huu, au wengine wafanyavyo usivae, maana umekwisha jihukumu mwenyewe, usifanye tendo lisilo toka katika imani(kile ukiaminicho)_  *Warumi 14:23* ,tayari wewe unashaka moyoni mwako, ukifanya utafanya kwa kujiibia ibia na hiyo ndo dhambi.
✍ _Na wewe usiye vaa usimuhukumu avaaye, wewe katika hilo huna imani, hauli vyote, huyu ana imani anakula vyote kila mmoja athibitike katika nafsi yake mwenyewe kwa kile anacho kiamini kwa Neno la Mungu_ *Warumi 14:4,20*
✍ _Kwa Habari ya Imani ya Kipentekoste, wokovu sahihi, imetupasa Kuvaa kwa Heshima, na Kujisitiri miili yetu_  (  *_Sasa kinacho kusitiri mwanamke siyo sketi, gauni, hivyo unaweza vaa na bado ukawa tunakuona ni kama kahaba_*) Vaa vizuri, nguo yako yoyote iwe inakuweka vizuri👇�👇�
*_1 Timotheo 2 : 9 - Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;_*
✍ _Mwisho, ni vizuri kumuhofu Mungu, kuangalia ni mpendeze Mungu ila siyo wanadamu, itamuwa haina maana huvai suruali, husuki, nk lakini moyo yako unalia kila siku na unatamani kuvifanya hivyo, na siku zote haupingi kusuka wala kuvaa suruali kwa sababu toka ndani ya moyo wako unaichukia, ila ni basi tu kanisa limepiga marufuku,_  *_Yaani kwa lugha nyingine siyo kwamba Hatuzini kwa sababu ya watanionaje, nitapata ukimwi, hatupati mwaya wa siri wa kuzini, bali Hatuzini kw sababu Tunaichukia Zinaa toka moyoni_*
_Katika maisha ya kiroho usifanye jambo kufurahisha watub, msikilize Mungu_
*_Matendo ya Mitume 4 : 19 - Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kwamba ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe;_*
_Mungu awabariki, ulikuwa na mimi mchambuzi, kwa kutafakari na kupima, na hayo ndiyo ni onayo Mimi, na wewe una unavyoona, ila nami nina Roho wa Mungu ndani yangu_
*_1 Wakorintho 7 : 40 - Lakini heri yeye zaidi akikaa kama alivyo; ndivyo nionavyo mimi, nami nadhani ya kuwa mimi nami nina Roho wa Mungu._*
         *Ev. Elisha Kazimoto*
         *0755444078

6 comments:

  1. KUVAA SURUARI KWA MWANAMKE MCHA MUNGU NI TATIZO Maana mungu ndiye aliyetuumba, biblia inaposema mwanamke asivae vazi limpasalo mwanaume maana yake anazungumzia tofauti ya maumbile ya hawa wawili, mwanamke akivaa suruari kama ya mwanaume maumbile yake ni kichocheo cha wanaume, hisia za wanaume ni tofauti na mwanamke hata kama yy atavaa kwa maana ya kujisitiri

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huko mbinguni tutapata hitimisho. Wanaume mnajitetea oooh maumbile hamna popote kama dhambi unayo unayo Tu hata mtu akivaa bwanga.

      Delete
  2. Roho mtakatifu atuongoze juu ya hili na amani ya Kristo iamue ndani yetu

    ReplyDelete
  3. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete