Tuesday, 29 November 2016

MWANAMKE USIACHE NYUMBA YAKO WAZI(PART I)

🏡🏡 WANAMKE USIACHE NYUMBA YAKO WAZI🏡🏡
   By Ev. Elisha Kazimoto
    0755444078
🌲 _Haleluyaa mwana mama uliye katika ndoa takatifu, na binti unaye jiandaa kuingia katika ndoa takatifu, leo nina uponyaji mkubwa wa ndoa yako kama Mungu alivyo nipa neema yake ya kuzijenga Ndoa, naamini kufikia mwisho wa somo hili, utajisikia vizuri, utajiona mwanamke shujaa, anaye weza fanya mabadiriko makubwa katika ndoa yako na familia yako kwa ujumla_ somo letu hili lina bebwa na Maandiko makuu 2. *YEREMIA 31:22* na *MITHALI 14:1* karibu sasa upate maarifa.👇�👇�👇�👇�

*_Yeremia 31 : 22 - Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume._*
🌲 Kwenye andiko hili tunapewa sifa ya mama kama *Mlinzi*, hongera sana mama,  Sifa ya mlinzi ni kuwa *Hodari, Anasilaa, Halali usingizi* yuko macho muda wote akiangalia adui ni sehemu gani anaweza pitia apambane naye.
🌲Lakini mama umepewa sifa ya kuitwa *Jambo Jipya,* kitu kipya kina sifa zake, *Kina vutia kwa kila mmoja, na hasa aliye kinunua kukimiliki, kinathamiwa, kinatunzwa vizuri, kibaangaliwa kwa upekee,* _Hizo zote sifa zinakufanya uitwe mlinzi kwa mume wako_.  Ukijitambua kwa picha hiyo huwezi kusikia ndoa ina shida, maana mlinzi anadhibiti mianya ya uharibifu, kwa lugha nyingine, *Kuanguka kwa Ndoa, Migogoro ya Ndoa kwa Asilimia kubwa ni matokeo ya mwanamke kuto simama kwenye nafasi yake kama mlinzi* Ndiyo maana katika somo langu la  *_Nafasi yako Mwanamke Inahitaji Akili sana Kuliko Nguvu_* Nimeongea namna mwanamke waweza tumia akili yako ukaepusha dhoruba katika ndoa yako.
🌲Andiko letu lingine linaonyesha mwanamke kama mjenzi wa nyumba👇�👇�🏡
*_Mithali 14 : 1 - Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe._*
🌲Unaweza kuona wewe mama ulivyo na nafasi kubwa katika familia,  Nyumba unayoambiwa hapa kujenga imegawanyika sehemu mbili,  Sehemu ya Ndoa yako(Wewe na Mmeo), na Sehemu ya watu unaoishi nao kwenye nyumba yako(wewe, mmeo, watoto wenu, kama kuna mfanyakazi, au jamaa yenu nk) _Saaa mwanamke mwenye Hekima(Akili) Huijenga nyumba yake(Husababisha familia yake kustawi, kubarikiwa, kuendelea,_) Bali mwanamke mpumbavu *Huibomoa kwa mikono yake mwenyewe*(Mpumbavu ni mtu anaye fanya kosa huku akijua ni kosa, yaani anaamua kukosea) umeelekezwa, umefundishwa namna ya kuifanya ndoa yako iwe na utulivu, hufanyi wewe ni mpumbavu.
🌲Kumbe mama wewe ni mjenzi wa nyumba yako, tukiona ina matobo, Crack (kuta za upendo na malezi) zimepasuka tunasema mama hakujenga vizuri nyumba yake, tukikuta mume anatembea kwa watu nguo hazijanyooshwa pasi, kufuliwa, mama hajajenga nyumva vizuri, tukikuta nyumba ndani mpangilio wa vitu viko ovyo, mama hajajenga vizuri, tukikuta mnalala na mmeo mmepeana migongo hata Tendo la ndoa hakuna, mama hajajenga vizuri.
🌲 _Lakini tukikuta nyumba imetulia, hakuna magomvi, upo upendo, amani, furaha maelewano tutajua mama huyu kakaba vizuri eneo lake kwa kutumia akili ya juu mno_
🌲 Sasa mama, hongera kwanza kwa kuwa *MJENZI WA NYUMBA* najua baada ya somo hili hutakuwa *MBOMOAJI*, Chukua Siri hii alonifundisha Roho wa Bwana ikusaidie, *_Ukisikia Nyumba yoyote, jua Inavyumba na Milango_* Kwa sababu hiyo Mithali 14:1 ametwambia nyumba inayojengwa au kubomolewa na mwakamele, sasa hii *Nyumba yako huwa ina Vyumba 6* kama ifuatavyo
1⃣  *Chumba cha Mawasiliano*
2⃣  *Chumba cha Utawala*
3⃣  *Chumba cha Maombi*
4⃣  *Chumba cha Hisia*
5⃣  *Chumba cha Uchumi*
6⃣  *Chumba cha Marafiki na Washauri*
🌲 _Mama hivi ndo Vyumba vya nyumba yako, kila chuma kina mlango wake 🚪na kufuri lake🔐, jukumu lako tu ni kuhakikisha kila chumba kimefungwa na ufunguo unao, huto kuja kujuta kwa nini uliolewa, ila chumba kimoja kikivamiwa na wezi Vyumba vyote vinavunjwa na nyumba inabomolewa_ Tuanze kuangalia chumba kimoja, kimoja.
*_Masomo haya, na mengine mengi yanapatikana katika Pages zangu za Facebook, account hizi,  Hazina ya Maarifa na Elisha Anointedman, Prophet Elisha Anointed person, Bado Liko Tumaini Ministry_* Huko utakuta masomo mengi yatakayo kujenga kiroho na kimwili.
*_Sehemu ya Kwanza ya Somo letu la Mwanamke Usiache Nyumba yako wazi lina ishia hapa, usikose sehemu ya pili ya somo_*
    _By Ev. Elisha Kazimoto(Baba Eve)_
    *0755444078*

No comments:

Post a Comment