Friday, 20 January 2017

ZIBUA NJIA ZILIZO ZIBWA NA ADUI

*NI MAOMBI YA KUZIBUA NJIA ZILIZO ZIBWA NA ADUI*
_Shalom,shalom wewe mwana maombi,unayeitwa mtu wa vita,tukiwa katika usiku wa mkesha,ujumbe wetu wa leo,ni KUZIBUA NJIA Zilizo ZIBWA na maadui_
*_Ayubu 19 : 8 - Yeye ameiziba njia yangu nisipate kupita, Na kutia giza katika mapito yangu._*
✍Tukiwa katika mwaka wa Kwenda Mbali(KUTOKA 8:24-28)Neno la Mwaka 2017,wako maadui ambao kila siku hujipanga kwa hila Kuziba,njia zetu za mafanikio ya kiroho na kimwili.
✍Siku zote,Njia ndiyo mahali pa kupitia kuelekea pale uliko kusudia kwenda,njia ikiwepo safari ipo,njia ikizibwa,safari inakuwa na utata. *_Ndiyo maana kwasababu tunakusudia kwenda mbali mwaka huu,lazima pia tujipange KUZIBUA chanel(njia zetu)za mafanikio zinazo zibwa na maadui siku kwa siku._*
✍Kinacho fanywa maadui zako(wachawi na mapepo)nikuweka vikwazo katika njia zako, magonjwa,kufuta kibali chako,umasikini na uhitaji,mafarakano na migogoro,tabia ngumu na matukio yaumizayo ndiyo mawe yao ya kiziba njia yako ili wakupunguzie kasi ya safari(speed).
*_Maombolezo 3 : 9 - Ameziziba njia zangu kwa mawe yaliyochongwa; Ameyapotosha mapito yangu._*
✍Siku zote mtendee adui kile anacho kusudia kutenda,mtendee na zaidi ya kilee..sasa kwakuwa adui anaziba njia zetu kwa mawe yaliyo chongoka ili atuumize,sisi tunaziba njia yake kwa MIIBA,tunamzuia kupita kabisa kwa jina la Yesu.
*_Hosea 2 : 6 - Basi kwa ajili ya hayo, angalia, nitaiziba njia yako kwa miiba, nami nitafanya kitalu juu yake, asipate kuyaona mapito yake._*
Hatulegei,hatupunguzwi speed,ila kasi yetu ni ile ile tunaenda mbali,kiuchumi,kiroho,kindoa,kitaaluma na kiafya kwa jina la Yesu.
*_By Ev Elisha Kazimoto_*
         *@2017*
    *0755444078*

No comments:

Post a Comment