Thursday, 1 December 2016

MWANAMKE NA UCHUMI(PART I)

🍇🍇 *MWANAMKE NA UCHUMI*🍇🍇
  *_By Ev. Elisha Kazimoto_*
     *0755444078*
_Haleluyaa wanawake jeshi la Bwana, nakusalimia kwa jina la Bwana, leo nakuja kwako tena, na somo la uponyaji wa ndoa na familia yako kama Mwanamke mlinzi na mjenzi wa familia. Somo hili lina lenga kukufungua ufahamu wako, uweze kuiletea furaha familia yako, lakini pia kukupa nguvu ya kuwa mshauri mwenye nguvu_  *Sisemi kukupa nguvu ya kumtawala mume wako, au kukupunguzia unyenyekevu na wajibu kwa mmeo kwa sababu ya kuwa na kipato flani cha kuwezesha kuratibu masuala yalo binafsi na ya familia*
🍇 Hapa nazungumza nguvu ya kuleta radha ya ndoa tulivu na yenye dira ya kimaendeleo.
_Sasa tuongozwe na maandiko makuu mawili katika somo hili la Mwanamke na Uchumi, *Mhubiri 10:19, 9:16*,hivyo fuatana nami mchambuzi wa masuala ya mahusiano na ndoa Ev Elisha (Baba Eve)_
*_Mhubiri 10 : 19 - Karamu hufanywa kwa ajili ya kicheko, Na divai huyafurahisha maisha; Na fedha huleta jawabu la mambo yote._*
🍇 Kuna vitu hatupaswi kujifanya hatuvioni, hau havipo, wala tusizame kiroho sana tukasahau tupo duniani mwilini, panapo hitaji jitihada tuweke, panapo hitaji maombi tuombe, panapo hitaji akili tutumie ili tuziridhishe nafsi zetu na tumwabudu Mungu kwa uhuru.
🍇 Pesa ni muhimili wa mambo mengi katika ndoa, Pesa ina chochea upendo, furaha, amani, utulivu, na maendeleo. Pesa ikiwepo migogoro midogo midogo inapungua, kero ndogo ndogo za kimaisha zina pungua, mawazo yanatulia na mpaka hisia za tendo la ndoa zina jaa, maana akili imetulia.
🍇   *_Uchumi ukiyumba kwenye familia, muhanga wa kwanza ni mama, ndiye anaumia zaidi, wanafuata watoto, mume ni muhanga wa mwisho_*
🍇 Kwani, watoto wakishikwa na njaa wana mlilia baba? Kwani hali ikiwa ngumu anaye ikimbia familia ni mama,? Mwanaume anaweza kwenda kutafuta pesa miaka 3 hajarudi, mama huwa anaacha familia? Baba anaweza tembea huko na kule, akala libandani, lakini mama hawezi kula nje ya nyumba mpaka aletee watoto kwanza wale.  *_Sasa ndo unaweza kujua mama ulivyo na mzigo wa kuhakikisha familia yako ina tengamaa kiuchumi_*
🍇 Lakini wanawake wengine wamejisahau baada ya kuona mme ana kipato flani, ameridhika, hajishughilishi na chochote, *_Na hali hii imemfanya kupoteza nafasi yake ya ushauri kwa baba, na kumfanya kuziba kinywa muda wote😷😷😷, kwa sababu hana mchango wowote katika uendeshaji wa familia👇�👇�👇�👇�👇�
*_Mhubiri 9 : 16 - Ndipo niliposema, Bora hekima kuliko nguvu; walakini hekima ya maskini hudharauliwa, wala maneno yake hayasikilizwi._*
👉�👆�Wanawake wengi, wamekosa uhuru wamepoteza uwezo wa kusikilizwa kwa kutokuwa ma kipato hata kidogo.
🍇Kumbuka sizungumzii kutumia pesa kama fimbo kwa mwanaume, hapo utabomoa ndoa, na huwenda hata usifanikiwe kuwa na kipato,  *_Nafundisha Mwanamke na Uchumi Kwa maendeleo na ustawi wa Ndoa yako_*

  *UFANYE NINI KUWEKA MSINGI WA KIPATO?*
🍇 Jitambue wewe ni Mwanamke wa Aina Ipi? ( Wakuajiliwa, Kujiajili, Msomi au Hukusoma, Mlemavu au Nina viungo vyote?)
🍇 Heshimu mme wako, na Mthamini kwanza,  kumbuka hakuna mume anaye weza ruhusu ufanye mchakato wa kuimarisha uchumi wako na familia kama ndani tu, huna pesa we ni *Jeuri* ukiwa na pesa itakuwaje?
🍇Jenga mahusiano mazuri na watu,  huwezi kuwa huingjliani na watu, huelewani na watu ukajipanga kufanya biashara, utamuuzia nani? (  *Katika Uchumi watu ni mtaji wako)*
🍇Angalia mahitani ya mazingira uliyomo, yanahitaji nini, ujipange kuyapa mahitaji hayo.
🍇Jifunze, mambo kwa wengine upate ujuzi wa mambo mbali mbali huwezi jua la kukuokoa ni lipi?
🍇 Jiamini na jikubali kuwa unaweza kufanikiwa malengo yako.
🍇Usiogope Hasara, hasara ni sehemu ya faida

No comments:

Post a Comment