*USITEGEMEE MME/MKE SAHIHI KAMA WEWE SI MTU SAHIHI.*
*_By Ev. Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
💖Kumekuwa na maswali mengi ktk maisha ya vijana ya ntampataje mke au mme sahihii
💖Ukweli ni kwamba mtoa mme /mke ni Mungu mwenyewe tu na ndo mwasisi wa ndoa
💖Kwa hiyo kama wewe si mtu uliye na mahusiano mazuri na Mungu usitegemee Mungu kukupa mtu wa watofauti, mzuri, mkamilifu, au utaomba omba Mungu akujibu kwa kukufunulia mtu wako
💖Mungu hafanyagi makosa, Wewe ni tapeli wa kiroho, utakutanishwa na tapeli mwenzio wa kiroho (biblia inasema, nitakufanyia msaidizi wa kufanana na wewe)
💖Tangu uokoke hajawahi kuombea mambo ya Kimungu, kazi ya Mungu na Mungu akakujibu aidha kwa Neno lake, maono, njonzi, ndoto, kwa manabii nk, Leo hii unataka kuolewa/kuoa ndo unasema Mungu amenifunulia 😜, Mungu kasema nami 😝, aliwahi kusema na wewe nini mbali na mke /mme?
💖Unaishi maisha ya kutoaminiwa na Mungu wala wanadamu, halafu unahitaji ukiomba siku mbili Mungu aachilie mtu makini 🙅🏻
💖Unajua kabisa mimi nimeokoka ila dhambi mbele kwa mbele, unahisi ukiomba Mungu mke/mme utapewa wa aina gani
💖Umeharibu wadada wa watu kwa kufunua uchi wao, Umeharibu vijana wa watu kwa kuwazanisha ktk mapenzi kwa mwili wako, halafu unaomba Mungu akupe mke Bikra 😜😜🙅🏻au mme pure😜😜🙅🏻🙅🏻, unahisi hayo maombi yatajibiwa ❗❓
😡🙅🏻USITEGEMEE MAKUBWA USIPO JITUMA 😡🙅🏻
👥 *MUDA GANI UNAMUOMBA MUNGU NAYE AKAKUPA MWENZI*👥
❤Miongoni mwa makosa makubwa yanayo fanywa na vijana ni kujiachia ktk wokovu na kutulia bila kumuhusisha Mungu ktk maisha na mipango yao mpaka polee wanapo hisi kubanwa na uhitaji
❤Vijana wengi wanahisi kumpata mke au mme ni suala la kwenda na kuchagua au kuchaguliwa, kwa hiyo wanaanza kuomba kwa kasi pale wanapo hisi Umri umeenda huku hawapati mtu, ndo maombi makali yanaanza huku akijalibu kwa kila mmoja kuvizia
❤Mke/mme anaandaliwa katika maombi kwa muda mrefu, hata hujawa na presha, ukifika wakati akija tayari umeisha mhakikisha ktk ulimwengu wa roho hakuna utata
❤Lakini Mungu hatoi waume au wake wa kufua nguo na sex tu, Mungu anatoa msaidizi wa kukusaidia katika kazi zote za Kimungu na kibinadamu alokupa Mungu, baada ya wewe kuonyesha Uaminifu wa kuzifanya kwa bidii,.
❤Kwa hiyo kwa mtu alookoka muda wake wa kupata mwenzi ni ule muda ambao Mungu akimtazama anaona kazi yake, kazi zako vimekulemea /unavinya kwa Uaminifu ndo muda huo Mungu anamleta msaidizi wa kukusaidia
❤Kama uko vzr na Mungu, Usiumize kichwa cha mbona hawaji, simpati, wee piga kazi ieleweke ya Mungu na ya kwako, atavutwa hata kama yupo wapi hujawahi muona
(maneno haya ni roho tena uzima) nina ushuhuda mrefu sana kuhusu mahusiano, Nimefunguliwa ufahamu wangu kuomba kuhusu mke nikiwa darasa la(V), nimepata mke sahihii wangu wa kuoa 2014 kwa mkono wa Mungu mwenyewe si kwamba tulifahamiana kwa muda mrefu(ndo wengine wamejibana) ufahamu wao mpaka apate aliye somo naye shule
❤Jiachie kwa Bwana, mtumikie Mungu, mwamini Mungu utapata mke/mme sahihii kwa wakati.
🔥🔥 *MAPITO YA MAHUSIANO* 🔥🔥
💎Ukurasa huu wa mahusiano, umekuwa 💉💉💉kwa wengi, umejeruhi wengi, ume 😭😭wengi, ume 🔪💏wengi, lakini pia Imetia wengi Nguvu 💪🏻💪🏻na maarifa mengi
💎Asilimia kubwa karibu 95%wameingia katika ndoa na watu ambao siyo walio anza mahusiano kwa mara ya kwanza (yaani alo oana naye ni mtu wa 2,3,4....9)katika maisha yake kuwa na mahusiano.
💎Wengine kwa kupitia katika mahusiano hayo mengi, wameunizwa na kujeruhika, wanaogopa mahusiano kama 🐅🐅🐉🐉, wengine wameanguka na kurudi nyuma kiimani, wengi wamepewa maumivu ya maisha kama kuzakishwa mtoto na kuachwa, kuachiwa magonjwa, kuondolewa sifa ya ubinti (Bikra) na kuachwa
💎Sasa unapo tafuta mtu wa kuoana naye na unapo mwomba Mungu ujue Kuna watu wa aina hiyo, ukipewa alo umizwa, Unauwezo wa kuganga moyo wake? Ni watu wachache 5%anaanza na mtu huyo wa kwanza ndo wanaona. (Ni wachache mno)
💏 *SABABU ZA KUPITIA MAHUSIANO MENGI PASIPO KUJUA*💏
💞Kufuata Mkumbo wa marafiki, maana yake hukumuuliza Mungu akakuruhusu uanzishe mahusiano hayo
💞Kutimiza au kuziba Gap la kisaikolojia la hisia na upendo, SI kibali cha Mungu
💞Tamaa ya macho na mwili, ukiingia siyo ulipata amani ya Kristo ndani yako
💞Ulihitaji msaada kwa mtu, akakusaidia akamiliki na hisia zako, siyo ulipewa na Mungu
💞Ulishinikizwa na wazazi, ndugu au marafiki, na si mpango wa Mungu
💞Ulihisi umechelewa Kuingia ktk Tasnia ya mahusiano ya kimapenzi, ukaamua ujiwahi, SI muda wa Mungu
💞Mungu alisema nawe uingie ktk mahusiano hayo ili akufundishe mambo ya msingi, unyoshwe usije ukawa mzigo kwa mtu wako sahihii ajaye
🚫Katika sababu hizo unaweza kukuta umepitia mahusiano hata 10 usipo kuwa makini.
*SABABU ZA UCHUMBA KUVUNJIKA*
💔Kukosa Uaminifu, endapo utaonekana hauna hauna msimamo wa kutulia na mchumba wako, ukatangatanga na wengine utavunja uchumba
💔Kugundulika kwa tabia isiyo weza kuvumilika, endapo mwenzako ataona tabia mbaya isiyo vumilika anaweza kuvunja uchumba,
💔Kuwa na misimamo mikali isiyo vumilika,
💔Ukiwa msiri, mtu usiye wazi kwa mwenzako Unafanya mambo kimya kimya
💔Kutegemea makubwa kwa mwenzako, ulihisi mwenzako atakuwa matawi ya juu kumbe wa kawaida
💔Marafiki wenye wivu, ukiendekeza kushauriwa shauriwa na marafiki watavunja uchumba wako
💔Kukosa mawasiliano ya karibu na mchumba wako, unapo anza mahusiano chunga mawasiliano yawe ya uhakika
💔Kutojali hisia za mwenzako, unaweza kumjibu unavyo taka, unaweza kumpotozea kimawasiliano hata wiki, au siku 2/3
💔Kuanza ngono kabla ya Kuingia katika ndoa, fasta mtavunja uchumba
💔Kukosa mipango ya maisha, kuendesha mahusiano ya kitoto yasiyo na mipango
💞 *NJIA ZA KULINDA UCHUMBA* 💞
💘Mpende mwenzako kwa viwango vya kutosha
💘Mwamini mwenzako, na wewe jiamini, kuwa chaguo lako liko sahihii
💘Usiruhusu mazoea ya karibu sana na watu wa jinsia tofauti na wewe, watakuletea kutoaminika kwa mwenzako, au migogoro katika uchumba wako
💘Jenga tabia ya kusikilizana, kama Kuna jambo lijadilini na mlitatue kwa pamoja
💘Jenga tabia ya Kusaidiana katika mambo mbali mbali, endapo mwenzako anashida, ibebe kwa mzigo uitatue
💘Ombea sana uchumba wenu, na muwe na ratiba maalumu ya maombi ya kulinda mipango yenu
*_By Ev Elisha Kazimoto_*
*0755444078*
Thursday, 1 December 2016
KUPATA MKE/MME SIYO BAHATI NI KANUNI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment