Thursday, 26 November 2020

KIJANA KUMUWEKA NJIA PANDA MDADA

*SWALI KUTOKA KWA MDADA*
Jamaniiiiiiii wanaume munapotoka from one relationship to another be very careful,unapomwabia binti nitakuoa,anakaa na matumaini akikusubiri, lakini unavyo muache dhuuuuuuuuu,amekusubili miaka amejitunza juu yako,all over sudden una break his heart, lazima mutaigia kwenye ndoa na laana tu, wanaume kuweni makini musitamani mwanamke alie sababu yako,
*_Anajibu Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto_*
*Message hii ni nzuri ila inge COVER jinsia zote boys and girls, kwakuwa watu wengi wanatumia mahusiano kama site ya kutimiza short terms plans,(Malengo yao ya muda mfupi) mbali na lengo la muda mrefu la ndoa.*
Wengi wanapoingia kwenye mahusiano....
1.Hawana uhakika kama wako tayari wao kuongia kwenye ndoa.
2.Hawana uhakika kama walioingia nao kwenye mahusiano ya kuelekea ndoa ni watu sahihi wa kuoana
3.Hawajawa na dhamira ya dhati ya kuipenda ndoa.
4.Wanateswa na historia za waliyopitia nyuma
5.Wanateswa na taarifa za mazingira yanayowazunguka
_Mambo hayo ndo yanawafanya watu wote wote vijana kwa mabinti kuwa wasaliti au kuvunja mahusiano bila sababu za msingi._

No comments:

Post a Comment