Tuesday, 15 May 2018

UNIOE HARAKA NISIKOSE MTOTO

*MADA YENYE UTATA KISAIKOLOJIA NA KIROHO*
_Soma chini ya mada ufafanuzi wa Msaikolojia Mtaalamu wa Mahusiano na ndoa Ev Elisha Kazimoto_
Whatsapp 0755444078
*MADA*

Wote tumeokoka Mimi na huyu mdada, tumekuwa kwenye mahusiano muda mrefu sana almost miaka mi2 bila matatizo.

Juzi mdada kaenda hospitali kupima kaambiwa ana matatizo kwenye mfumo wa uzazi ambayo kama hatozaa hivi karibuni basi anaweza asipate mtoto kabisa. Kaja kaniambia nimuoe haraka sana ili azae asije kufa bila mtoto na Mimi nikiangalia mambo yangu mambo sijajipanga kuoa mwaka huu. Amekuwa mwaminifu sana kwangu Nani nimekuwa mwaminifu kwake muda wote  ila kasema kama nikikataa kumuoa atatafuta MTU yeyote amuoe ili wazae nae mtoto na Mimi aniache. Wazazi wake wamemkubakia kufanya chochote ikiwa hata kuacha na Mimi na nikiangalia naona kweli kadhamiria kuolewa. Mimi nna miaka 29 yeye ana miaka 26.

Nifanyeje doctor Nioe ivoivo bila kujipanga au nimwache aende tuu.?
.................................................
*Hii mada Inahitaji utulivu mkubwa maana ina HOLD Effects za pande mbili kiroho na kisaikolojia.*
👉Kwanza niweke sawa mambo kadhaa kuhusu mahusiano ya kiuchumba kuelekea ndoa ili pasiwepo mtu wa kulamiwa katika pande hizi zote mbili ya msichana na mvulana.
👉Kwanza,Mahusiano ya uchumba ni jambo la makubaliano baina ya pande mbili,nini kifanyike na kifanyikeje na kwa muda gani,ni suala la makubaliano ya watu wawili kulingana na malengo yao.(Kwa mantiki hiyo,hawa watu nigekuwa nawafanyia Pdychological Counseling ofisini swali langu la msingi lingekuwa, Je,Mpango wa uchumba wenu mlikusudia myoane lini?baada ya mazingira gani kuwepo?).
*_Kwa maana kama mliweka makubaliano ya kuoana baada ya muda flani na vigezo vya muda huo mliona vina faa,basi kisaikolojia Kubadirisha muda inategemeana na jambo lililowafanya mbadiri muda lina nguvu kiasi gani KULIKO mambo yale yaliyowafanya mpange muda huo_*)
👉PiliSuala la kiroho Kama watu hawa wameanza mahusiano na Bwana,wamkabidhi Bwana suala hili na waingie katika ndoa muda wowote kiutakatifu,si lazima sherehe kubwa,ili mradi taratibu zimefuatwa ili kulinda maadili ya wokovu na kulinda uwepo wa Mungu katika ndoa yao.
*Ila niwatazamishe vitu kama 2 hapa vya kutulia kuwashauri watu hawa kulingana na lugha zao walizozitumia katika kuomba ushauri,kisaikolojia nazichambua hivi:*
🌈Lugha ya binti, *Nioe Haraka nipate Kuzaa,na kama hutofanya hivyo nitatafuta mtu yeyote mwingine wa kuzaa naye ili nisife bila kuzaa* Lugha hii ni dhaifu,kisaikolojia katika ndoa huyu mtu hafai kuwa mke,upendo wake upo kwa mtoto siyo mume( _Kumbuka tunapendana wawili bila watoto,tunafunga Agano la kuishi pamoja mpaka kaburini sisi wawili bila watot_ ila watoto ni zawadi ya Mungu,ndo maana wengine wanazaa walemavu,vipofu,viziwi,na wengine wanakufa,hatuachani na wengine wanakuwa wagumba mpaka uzee,inabaki ndoa ya waliopendana). Sasa mtu anapokuja na Hoja ya Kubadiri Utaratibu,mipango,ya namna yakuingia katika ndoa kwa utaratibu mzuri tuliokubaliana kisa eti,nimichelewa hatozaa na yuko tayari kutafuta mtu mwingine wa kuzaa naye,ninampa majibu yafuatayo.
1.Hakunipenda,anatafuta kigezo cha kuniacha,maana anajua sijajipanga na siwezi kuoa muda huu,hivyo anatafuta nafasi ya kunitoroka.
2.Huyu mtu kunakitu anahofu nacho,aodha anahitaji kunibambikizia mimba aseme niya kwangu kumbe kuna sehemu alipuyanga sasa anabumbabumba taarifa za daktari ili nimuoe haraka,au nifanye ngono naye haraka,kuficha uovu wake.
3.Huyu mtu anayeona mbadara wa mwanume mwingine mimi aliyenipenda bafo nipo, Ni hatari,hana mapenzi ya dhati na mimi.(Kama mtu anaweza kusema nitatafuta mtu mwingine wa kuzaa naye, that means *Anaye mtu,atampataj haraka hivo,watachumbiana muda gani,mpaka waoane,kwa lugha nyine atafanya Ngono na mtu mwingine,nani sasa,na wee ni binti siyo kijana kusema utongoze tongoze,kwa lugha nyepesi anauzoefu wa kutongoza wakaka na akawanasa kiulaini na hraka sana*)
*_Kwa mimi,huyu mtu NI HATARI SANA KUINGIA NAYE KWENYE NDOA_*.

.........................
Niseme kwa upande wa kijana. 🌈Ni jambo gani gumu kwake kimaandalizi hata asiweze kuoa mwaka huu?
_Lakini kwakuwa yeye ndo kichwa,na ukioa unatazamwa wewe kama kichwa kuendesha familia kiroho,kimwili na kijamii,hakikisha UNAOA KWA MUDA ULIOKUSUDIA KUWA HAPA NITAKUWA NIMEWEKA MAMBO SAWA,ili hata ukikutana na changamoto,usijilaumu kwa kuwahi kuoa,bali upambane kama kawida ya changamoto zote za maisha. *Kama unahisi hauko tayari kuoa mwaka huu,usilazimishe itakugharimu kisaikolojia mbeleni,mwache aende atafute mtu asiyeishi kwa mipango na malengo,wee tulia ufanye mambo kwa mipango na malengo utapata mtu wako kwa wakati._
*By Ev Elisha Kazimoto: 0755444078*

No comments:

Post a Comment