Saturday, 24 June 2017

MJENZI UTUMIA AKILI SANA

🌈 *MJENZI LAZIMA AWE MTU ANAYETUMIA AKILI SANA*🌈
   *_Semina Ya Wamama_*
       ( *Ev Elisha Kazimoto*)
     WhatsApp      0755444078
_Shalom wamama Watumishi wa Kristo,mliopewa vyeo vingi na na Mungu katika Biblia kuonyesha uhakisia wenu. Mnaitwa Jeshi kubwa *Zaburi 68:11* Mnaitwa Wajenzi wa Nyumba/Ndoa *Mithali 14:1*, Mnaitwa Mke Mwema *Mithali 31:10*, Mnaitwa Msaidizi, *Mwanzo 2:18* Mnaitwa Walinzi, *Yeremia 32:21*, Mnaitwa Waombolezaji *Yeremia 9:17-21* hizo zote na nyingine ni lugha za Kimungu zinazo tambulisha uhalisia,uwezo na sifa ya Mwanamke Aliye kusudiwa na Mungu katika *Familia, Ndoa na Kanisani* kama akikaa katika Nafasi yake Kwa Akili_
🌈🌈 *Andiko Kuu La Somo*🌈🌈
     *LUKA 14:25-32*
25 Makutano mengi walipokuwa wakifuatana naye, aligeuka, akawaambia, 

26 Kama mtu akija kwangu naye hamchukii baba yake, na mama yake, na mke wake, na wanawe, na ndugu zake waume na wake; naam, na hata nafsi yake mwenyewe, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 

27 Mtu ye yote asiyeuchukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu. 

28 Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? 

29 Asije akashindwa kuumaliza baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, 

30 wakisema, Mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumaliza. 

31 Au kuna mfalme gani, akitaka kwenda kupigana na mfalme mwingine, asiyeketi kwanza na kufanya shauri, kwamba yeye pamoja na watu elfu kumi ataweza kukutana na yule anayekuja juu yake na watu elfu ishirini? 

32 Na kama akiona hawezi, hutuma ujumbe kutaka sharti za amani, mtu yule akali mbali. 
_Katika Andiko kuu kuna vipengele kama 7 tutakavyo simamia katika Uchambuzi wa Somo letu la *Mjenzi (Mwanamke)Anahitaji kutumia Akili sana* ili tuweze kunusurisha Kanisa la Mungu, Familia zetu, Ndoa zetu,Uhai wetu na Maisha yetu ya kiroho_
1⃣ *Maamuzi yako kwa yale unayo yafuata kuyatimiza* ( mstr 26)
2⃣ *Mzigo ni wa maisha niwa kwako tu*(mstr 27)
3⃣ *Muda wa Kutafakari Hatima yako kama kuna faida katika maamuzi yako* (mstr 28)
4⃣ *Wanaokuzunguka wanakutafsiri vipi kwa maisha hayo ulochagua*( mstr 29)
5⃣ *Udhaifu wako utakapo julikana na watu, utakuwa na nguvu za kuendelea mbele?*(mstr 30)
6⃣ *Una ufahamu juu ya Adui yako unayepambana naye asiharibu hatima yako?*(mstr 31)
7⃣ *Jipime uwezo wako kabla ya maamuzi*(mstr 32)
🎸 Kuna mambo unahitaji ufunuliwe au ufundishwe na watu waliofunuliwa siri hiyo ndo ufanikiwe katila hayo, zaidi ya hapo utajiona ni mtu usiye na faida duniani( *Zaburi 32:8*)
🎸 Wanawake adui amewaondoa kwenye Msingi wa uhalisia wao, baada ya kugundua ni Wadhaifu wa Kutumia Akili Ipasavyo katika kujenga maisha yao ya kiroho,ndoa na familia
*_1 Wakorintho 15 : 34 - Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi; kwa maana wengine hawamjui Mungu. Ninanena hayo niwafedheheshe._*
🎸Maadui(wachawi na shetani na mapepo yake) ili waharibu kiroho chako,familia yako au ndoa yako (kwako wewe mwanamke)ni kuchezea akili zako(kukudanganya)
*_2 Wakorintho 11 : 3 - Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo._*
🎸 *Sifa kubwa* ya mwanamke mwenye Akili(Maarifa)Kibiblia Ni mwanamke mwenye _uwezo wa Kujenga Nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe_( Akili +Juhudi binafsi)kusababisa raha katika Nyumba( yaani Mkusanyiko wa watu, tangu *Ndoa yake, familia-watoto na Kanisa*)
*_Mithali 14 : 1 - Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe._*
🎸AKILI; Ni uwezo wa kufanya Maamuzi Sahihi yenye faida kwako(kukunufaisha) kwa lugha nyingine *_Mwanamke yeyote anaye fanya maamuzi yenye kumletea Hasara kiroho, kihuduma na katika ndoa, huyo Hana Akili Kabisa_* ni sawa na mtu Aziniye (mwanaume aziniye na mwanamke)
*_Mithali 6 : 32 - Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; Afanya jambo litakalomwangamiza nafsi yake._*
🎸🎸 *Mwanamke mwenye Akili ya kujenga hatia yake* Ni Yule anaye jua kuwa Maisha Safi,au ya Shida, Dhiki, Raha ni yake na familia yake tu, wala haya muhusu rafiki yakeau adui yake.
🎸🎸🎸 *Mwanamke mwenye Akiliyakujenga hatina yake* Ni yule anaye jiuliza maswali ya kiroho,kimwili na kisaikolojia,kuwa kama mambo yakiniharibikia anayeumia ni nani, au ya kinyooka anaye faidika ni nani.(Ndipo anachukua maamuzi yakutenda au kuacha)
🎸4⃣ *Mwanamke mwenye akili ya kujenga hatima yake* Ni yule anaye tafsiri nguvu ya maamuzi yake itakavyo athiri nyumba yake,kanisa la Mungu na kupitia hiyo Mungu atainuliwa au atashushwa.
🎸5⃣ *Mwanamke mwenye Akili ya kujenga hatima yake* anauwezo wa kuzuia madhaifu yake,ya familia yake na ndoa yake yasijulikane na mtu wa nje mpaka ayamalize mwenyewe.
🎸6⃣ *Mwanamke mwenye Akili ya kujenga hatima yake* Ni yule mwenye Uwezo wa Kubainisha Maadui zake kutoka katika marafiki zake na kuwadhibiti.
🎸7⃣ *Mwanamke mwenye Akili ya kujenga hatima yake* Ni yule anaye tambua udhaifu wake na uwezo wake, na akadhibiti udhaifu wake usiathiri maisha yake
❌❌ *ALAMA ZA WANAWAKE WACHAWI WACHANGIAO KUBOMOA NDOA YAKO NA TABIA YAKO NA KIROHO CHAKO*❌❌
1⃣ _Wanapenda kukuaminisha kuwa wao ni marafiki wazuri kuliko waleulokuwa unawaona ni rafiki zako_
2⃣ _Wanapenda Kusimulia udhaifu wa mchungaji na mama mchungaji na viongoziwa kanisa_
3⃣ _Wanahitaji mambo ya siri siri, hawatendi mambo yao uhuru, mpaka wajifichefiche_
5⃣ _Wanapenda Kusimulia madhaifu tu ya waume zao na kuyahusianisha na ya mme wako_
6⃣ _Ni washauri na wahimizaji wa kumfanyia mmeo vitendo vya ukomoaji kama kumnyima tendo la ndoa_
7⃣ _Wanapenda kutengeneza vikosi makanisani kwa lengo la kuwaumiza wengine wanao wachukia_
8⃣ _Wanapenda kujadiri kila ujumbe na matangazo kanisani kwa lugha ya Leo alikuwa anamuongelea mtu flani_
9⃣ _Wanapenda kumteka mtu kwa zawadi tata(za ovyo)_
🔟 _Wakitafuta kukuingiza katika kundi la kichawi kanisani ukagoma wanatengeneza genge la kukuchukia milele.
*_Ukiwa mwanamke mwenye ndoto za kwenda mbinguni,kumtumikia Mungu,kuwa na ndoa nzuri, jipange kuamua kutumia Akili vizuri katika maisha yako. Ulikuwa nami mchambuzi wa masuala ya Kisaikolojia,Mahusiano na Ndoa, Ev Elisha Kazimoto(Baba Eve) WhatsApp 0755444078_*

No comments:

Post a Comment