Thursday, 26 November 2020

NJIA YA KUVUNJA MAHUSIANO

Mwl. Naomba Ukija uje na Majibu  ya Ipi njia nzuri ambayo haiumizi  moyo wakt mnataka ku-break up mahusiano yenu...  kwa  njia ya SIMU  / SMS,   Au   Mnakutana sehemu  Mna-break kwa kuOnana.

Ipi? njia nzuri hapo😁

maana wengine utashaanga tu! mmeachana😂😂
*Anajibu Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto*
*NJIA YA KUVUNJA MAHUSIANO SIYO COMMON NI CONDITIONAL*
👉Unapo amua kuvunja mahusiano inategemea una mtu wa character.
👆Kuna watu una kaa naye mvunje mahusiano Reaction yake italeta hasara(Kubakwa,Kukupiga,Kukuaibisha au palepale kufanya tukio baya) huyo usikae naye tumia njia zingine.
👉Sababu ya kuvunja mahusiano ni kwasababu ya tabia, mmeshindwa kuelewana,au mnapendana ila mapenzi ya Mungu yamegoma
👆Angalia ipi njia ipi haitaleta athari kati yenu mbaya.
👉👆Mahusiano katika nyanja hizo wapo ambao mtakaa eneo la wazi site huru mtaambiana kwakweli hatuna budi kuend up mahusiano mta break na kuachana(kama wote saikolojia zenu ziko vizuri)
👉👆Wengine tumia simu mpe taarifa ya kusitisha mahusiano na sababu zako kwa upendo kabisa na sitisha.
👉👆Mwingine mpe ishara kimya kimya unamkatia mizizi chini kwa chini mti ukisha kauka ndoa unamalizia na taarifa ya nilisha futa mahusiano nawe kwa sababu hii na hii.
*Kuwa makini unapovunja mahusiano isiwe ni kwa sababu za tamaa zako, na kukurupuka usije ukaumia wewe mwenyewe ikakugarimu*
By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)0755444078

KULIPA MAHARI

Nina swal......

*Je ni sahihi kwa kijana kusaidiwa kutoa mahari, mfano kusaidiwa na ndugu zake au hata mwanamke anayetarajia kumuoa........na je akisaidiwa huyo mke hawi wa wote waliochangia mahari?*
*KULIPA MAHARI KIMANTIKI NI KAZI YA KIJANA MUOAJI*
*Anajibu Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto*
👉Kijana unapoanza kuhisi kichwani mwako unahitaji *Kuchumbia* jambo la kwanza anza kujipanga kutafuta mahari.
👉Ukianza kuchumbia uwe na uhakika wa kulipa mahari mwenyewe.
👉Usichumbie kwa imani na kuwatwisha mzigo ndugu, wazazi na kanisa wakulipie Mahari.
👉Mahari kwa tafsiri ya haraka ya kimantiki Ni Gharama inayoonyesha kiwango cha Utayari wako na Upendo wako kwa huyo unaye mtaka, Upo tayari kugharimika kiasi gani hata umpate? Sasa usipo Lipa mahari au ukisaidiwa mahari nani mwenye upendo wa umuoaye wewe Au ndugu zako au kanisa? Heshima ya mwanamke iende kwa nani?wewe mmeo au ndugu au kanisa lililolipa mahari?
👉Kabla ya kuanza kuchumbia jua wewe kijana(mwanaume) Biblia imekufananisha na Yesu Kristo(wewe ni kichwa cha mkeo) Yesu alilipa Gharama hata mauti ili atupate sisi,je wewe umelipa gharama ili umpate mkeo?
👉Wazazi,ndugu,kanisa wacha wapambane na maandalizi ya harusi,wewe *LIPA MAHARI* kwa namna vyovyote.
👉NB: Suala la wazazi kukusaidia,kukulipia mahari isiwe ni kwasababu Umeshindwa iwe ni kwasababu Mzazi anapendelea,ametaka kuhusika na hapo pia,ila kijana mwenye akili zaidi,lipa wewe mahari pesa ya wazazi na ndugu ielekeze kwa mambo mengine.
👉Kama uneshindwa kulipa mahari,wakakusaidia siyo dhambi ila haitakupa heshima na nguvu.
👉Mdada kukusaidia kulipa mahari siyo dhambi ila umevua kofia yako umempa yeye awe kichwa, yeye anachoweza kukusaidia *Nikuongea na familia wasikutoze mahari zaidi ya uwezo wako,mwambie mimi ninauwezo wa kulipa laki 5 tu😎😎 ikizidi hapo tutasogeza mbele harusi au sioi 😍😍 sasa kama anakupenda yeye aende apambane na hali ya familia yake mpaka washushe to laki 5.
👉Na si vizuri kukopa mke,eti muoane utamalizia mahari huko ni kujidharirisha na kujipa mzigo mkubwa baada ya kuoana,si wote uwa wanamaliza kwa wakati wengine mpaka wanazaa watoto miaka 5,10 ndo wanakuja kumalizia deni.
*ANGALIZO LANGU KWA VIJANA*
1.Kama unahisia za kuoa pia uwe na hisia za kutafuta pesa mapema.
2.Kama bado huna uhakika wa kupata pesa Usitongoze mdada yeyote, *Jifanye Uwaoni, au wote ni dada zako wa kuzaliwa* ila ukishaanza kupata kipesa fungulia speed za kutafuta.
3.Mahusiano ni gharama ukiamua kusema I LOVE YOU JUA KUNA NA I GIVE YOU.....
4.Vijana msikwepe kazi, au kupenda kazi za kukaa kwenye kiti, chimba hata mitaro,chota maji,buruta toroli tafuta pesa kila kona mahusiano na ndoa ni MATUMIZI.
5.Na ninyi wadada ukianza kuchumbiwa Soma na Angalia uwezo wa mchumba wako ulo mkubali, *Kipato chake cha 50elfu kwa mwezi,wewe unamtaka 50elfu kila wiki ya kusuka,unataka IPhone simu wakati yeye ana tekno ya batani, huu nikuwa CHUMA ULETE* umemkubali huyo taka vichache kwake,mkioanana pambaneni wawili kuinua kipato chenu.
6.Dada japo pesa ni muhimu katika mahisiano ila,kabla ujaingia kwenye mahusiano uliishije? Balance mazingira,usimpende au kutompenda mtu kwa sababu ya uwezo mdogo,maisha ni safari ya mabadiriko ujui kesho anaweza kuwa milionea.
*By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)0755444078*

NDUGU KUCHUMBIA BINTI MMOJA

*Swali:* Kuna wa kaka 2 mtu na mdgo wake yn wamekutana ba mkubwa na mdogo,,,yule kaka mkubwa alikua na mahusiano na bint lengo amuoe 🤗lkn ikafikia kipind yule bint gafla t akamwambia huyo kaka kuanzia leo ckutaki hata kukuona😫bac kaka wa watu akakubali matokee maisha yakaendelea,,,,,baada y muda flani mdg mtu akamwambia kaka ake kua nimepata bint wa kuoa lkn kaka naonba unisamehe mm ndo nmemshawish mchumba ako akukatae ili nimuo mm je kama n ww unafanyaje🤗na je ndugu yko akishaoa utaweza kwenda kwake maana hapo awali bint alikwambia htk hata kukuona inakuaje hapo🤔
*Anajibu Msaikolojia...Ev Elisha Kazimoto*
*UNAWEZA KULIPOKEA KIRIHO ILA KISAIKOLOJIA LITAKUTESA*
👉Suala la mahusiano ni gumu sana kisaikolojia tofauti na watu wanavyo dhani, likibebwa kirahisi linaweza kukufanya *Kichaa aliye timamu*(Mtu aliyepoteza uwezo wa mchakato wa akili katika utulivu japo haokoti makopo na kula uchafu)
👉Mahusiano yanahitaji ukiyaanza ujipange sawa, *Uingie kwa sababu za Msingi zitakazo shibisha akili na moyo wako amani, na Ukitoka ujue unatoka kwa sababu za Faida ya Usalama wako wa uzuri wa baadaye,siyo sababu ambazo zitakuuma ukikumbuka ukagundua ni uzembe au hila flani za watu*
👉Sasa hawa ndugu na mke wao mmoja wote wako kwenye Mtihani mkubwa kisaikolojia ambao unaweza kugharimu (Mahusiano ya kiundugu, kiroho,na kindoa) hapa kila mmoja ana mtego na maumivu yake.
1⃣Mdada mwolewaji(Yuko kwenye mioyo wa watu wawili ambao ni ndugu wa karibu) anaweza kutumika kama silaha ya kuua hao ndugu,familia zao au ndoa zao.
👉Mdada anakuja kwenye familia ila haji kukiwa amani anakuja kama CHANZO CHA MACHAFUKO kwa ndugu wawili na familia yote.
👉Namna ya kupunguza shari *Akubali kwa siri Awe mchepuko wa Kaka mtu(kaka wa mme wake) ampe penzi la kutosha naye kisiri siri ili kaka mtu atengeneze amani kati yake na mdogo wake na wazazi.
👉Ila itakuwa ni hatari kama mmewe atagundua moto na vita vitatokea.
*Huo ndo mtihani alio nao*
2⃣Kumbuka kaka mtu anampenda bado mke wa mdogo wake maana yeye aliachwa si kwamba aliacha.
👆👉Upendo huo unao fukuta ndani, vipi ukiibuka wote wakiwa wameoa lakini huyu akaendelea kumfatilia mke wa mdogo wake( Ndoa zao wote ziko hatarini) 
👉👆Kaka mtu akiamua ku REVANGE(kulipa kisasi )kwa ajili ya kutibu majeraha ya moyo kwasababu ya kumeshwa sega la asali mdomoni kwa hila?(hapo kuna hatari zaidi)
3⃣Mdogo mtu ameua undugu kwa tamaa,Alifanya kwa upumbavu, itakuwa ni vigumu kueleweka kwa kaka yake na familia, mpaka wawe na kiwango kikubwa cha Kiroho.
👉Jambo la msingi hapa *Refarii ni Mdada, AWAACHE WOTE wawili akaolewe kwingine, maana yeye na mdogo mtu wote Hawana Akili* wanapooana hawaendi kukaa mawinguni, wanakaa kwa jamii na ndugu zao ni hao,unakuja umeisha wagawanya mioyo,unadhani baba na mama na baadhi ya ndugu mawifi na mashemeji *watakufurahia kuona wewe ndo umewafanya mtu na kaka yake wasiingiliane,wasipendane,wasisaidiane nk, Utapendwa na wawili ila kumi watakuona mchawi wa Familia na wazazi Watakulaani milele* acha, acha kabisa mzazi yeyote anapenda kuona wanae wanapendana wanasaidiana sasa wewe umewagawanya,hata kama una pesa watakuona wee mchawi wa uzao wa tumbo lao.
👉👆Ushauri wa dada awaache wote. Ajue huyo mdogo mtu ni mbovu kuliko kaka yake.
By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)0755444078

ZAWADI ZA NGUO ZA NDANI

*MADA YA LEO 27  MAY 2020*

Katika Mahusiano yeyote zawadi kwa  ndugu zangu wa-maasai huita sawadi, ina nafasi gani katika kukuza penzi au mahusiano yenu? Je  Pia?  kuna  baadhi ya zawadi inapaswa isitolewe kwa watu walioko katika mahusiano     mfano: Wapo wapenzi   wana nunuliana hadi CHUPI  na BOXER, 

Hii  imekaaje? JE ZAWADI ZETU kwa watu tuwapendao ziwe na mipaka au full kujiachia.

*N:B:* Siku Mkiachana  roho yako  isikuume wala  kuzidaii kwa Ex  wako huyo.


‼️‼️ KARIBUNI
*Nianze na hii ya zawadi*
_ZAWADI NI MIONGONI MWA VICHOCHEO VYA MAPENZI KATI YA WANA MAHUSIANO_
👉Zawadi ina kazi kubwa kwa anaye toa na anaye pokea kwa hiyo wote mnahitaji kuwa makini sana Kiroho na Kisaikolojia.
1⃣Kwake atoaye zawadi anawekeza( *Anatafuta nafasi chumba cha kukaa katika moyo wa anayepokea zawadi*)Hii ni kibiblia👇👇👇👇
21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako. 
Mathayo 6:21

👉Kazi ya zawadi ni kuhifadhi moyo wa atoaye zawadi ndani ya moyo wa aliyepokea zawadi.
👉Kwa hiyo hapo jua pindi utumiapo au uishipo na zawadi ya mtu jua *Unaishi na moyo wake* 
👉Sasa kama ni zawadi njema jua upendo utakuwa mkubwa kati yenu na mioyo yenu itaambatana sana.
👉Kwa sababu hiyo, Zawadi ni mpeano kila mtu tafuta nafasi ya kukaa moyo wako ndani ya mwenzako.
👉Kama unataka upokee tu zawadi jua mwenzako *Yupo moyoni mwako,ila wewe haupo moyoni mwake* ndo maana mkiachama wewe utaumia sana ila yeye hataumia sana,atapona haraka wewe utachekewa kupona machungu.
2⃣Kazi ya zawadi kwa apokeaye, inakufanya wewe kuwa *Mtumwa wa Nafsi, Hisia,Maamuzi kwa aliyekupa zawadi* ndiyo maana unapaswa kuwa makini na zawadi na aina ya zawadi....Hii ni kibiblia pia👇👇👇👇
Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi.

Mithali 15:27
👉Zawadi inakuondolea Ujasiri binafsi mbele ya aliyekupa zawadi.
👉Zawadi inakawaida ya kununua Hisia zako,na maamuzi yako.... _Ndiyo maana wengi wanaopoteza Usichana wao au uvulana wao,wokovu wao nk Zawadi zilitangulia kununua maamuzi yao,akija kuambia Sex,au hitaji lolote anaona ni gumu lakini akifikilia zawadi alizopewa,alizokula anaona mwenyewe *Atakuwa si muungwana kumkatalia* atakuwa mkatili kumgomea, anaona aibu kukataa lolote._
👉Ni watu wachache ambao Zawadi hata ziwe za gharama *Haziwezi nunua Maamuzi na Nafsi yake* hao ni WACHACHE NA WAWE WAMEIVA KIROHO NA KISAIKOLOJIA ila wenye wokovu wakawaida wa wengi wetu HUCHOMOKI( a.k.a HUTOBOI).
👉Kiwango cha zawadi ndo kiwango cha nguvu ya Kulainisha moyo wa mpokeaji na kununua nafsi yake na maamuzi yake.
👉 *NB: _Zawadi ni muhimu kuzichunguza na kuwa nazo makini, Zawadi ni Sadaka katika Madhabahu ya moyo,ikinenewa maneno ya kiroho au ya kipepo inauwezo wa kutekeleza matakwa,ndo maana unapaswa kujua zawadi hii inatoka kwa nani,viwango vyake vya wokovu,au utu wake na inahusiana na nini_* Kuna zawadi ukiipokea kwa mtu,ukiitumia
1.Hutokuja kuzaa
2.Hutaolewa au kuoa
3.Magonjwa yanaanza hapo
4.Laaana na mimosi juu ya mafanikio yako.
NIMALIZIE KWA KUSEMA KATIKA POINTI YA SWALI:
👉Zawadi ya nguo ya ndani katika Uchumba *Usipokee* Narudia Usipokee labda wale bao wefikia kiwango ambacho zile nguo zinapelekwa kwenye sendoff kwaajili ya bibi harusi kwaajili ya harusi kesho yake.
👉Umekosa zawadi zote mpaka ununue nguo za ndani kwa mwenzako.
👉Sehemu za Siri ni maeneo maalumu ya AGANO,so na kinachofunika pale lazima kiwe safi kina enda na nguvu ya kuhifadhi agano.
👉Umewahi kujiuliza kwa nini wachawi uwa wanaiba *Nguo za ndani za wamama na wadada wengi,wanakuta imeibiwa haionekani tena au anakuja kuipata baadaye ila matokeo baada ya kuipata au kupotea waulize wanajua shida zake,ni somo maalumu hilo si la humu VERY DANGER* NDO MAANA HATA WADADA NA WAMAMA MSIZOEE KUFUA NGUO ZA NDANI NA KUANIKA NJE ZIKALALA,ITAKUGHARIMU SIKU ADUI YAKO AKIFANIKIWA KUISHIKA.
By *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)*
0755444078

MAHUSIANO NI GHARAMA

NAULIZA HIVI,
          Baadhi ya watu  wanasema wanaogopa kuanzisha penz kwa sababu wanaogopa gharama ya penzi lakn pia wengina wanasema,
  Penzi la kweli halina gharama je ni kweli au wapendwa hiyo imekaaje hapo? Majb na maon tafadhali🙏🙏🙏
*Anajibu Msaikolojia Ev  Elisha Kazimoto*
*KILA KITU KINACHOLETA MATOKEO CHANYA,RAHA,FURAHA MCHAKATO WAKE LAZIMA UHUSISHE GHARAMA*
👉Ni muhimu kujua kuwa gharama ni mchakato ambao unakulazimisha kufanya jambo husika ili utoe matokeo chanya, kwa lugha nyepezi *Inakulazimu kufanya jambo hata kama unahisi ugumu au uwezo ni mchache,inakulazimu ufanye* ili kutimiza Azma ya furaha yako.
👉Sasa mahusiano ni sekta ambayo mwenye akili timamu unapoingia mchakato wa kuanzisha na kulinda mahusiano LAZIMA UINGIE GHARAMA KUBWA ili utoe matokeo unayoyahitaji na usipo ingia gharama basi utapokea matokeo au majibu tofauti na shauku yako.
*Baadhi ya Gharama ambazo unaziingia kwenye mahusiano*
1⃣MUDA: Ukianzisha mahusiano,uwe tayari kutoa muda wako kwaajili ya mwenzako,muda wowote ili kulinda furaha na upendo.
👉Wengi walioanzisha mahusiano na KUJIFANYA BUSY,mahusiano yao Yalivunjika,au walienda bila furaha.
👉Kuna wakati umebanwa,lakini inakulazimu uwe na muda wa kuwasiliana na kumsikiliza,kumwambia kitu mpenzi wako.
2⃣GHARAMA YA PESA. Ukianzisha mahusiano uwe mkaka au mdada USIWE MBAHIRI AU KUHURUMIA PESA, jua tu utaingia gharama ya kuhudumia mwenzako kwa PESA.
👉Usipo taka pesa ikitoke ukakwepa gharama mahusiano yata yumba au kuvunjika.
NB:Uwe makini hapa kuna watu wanaingia kwenye mahusiano wanalengo la kutengeneza KITEGA UCHUMI,wengine kwa sababu ya malezi au hali zao wana uhitaji mkubwa wa kutunzwa kipesa. Sasa usipo jipanga kwa gharama ya pesa UTAYAKIMBIA MAHUSIANO.( Ila ushauri usiwe mchwa kwenye mahusiano unatafuna tu, kuwa ng'ombe unalishwa nawe unanywesha maziwa)(yaani hudumiwa nawe hudumia kwa pesa)
3⃣Gharama ya KUUMIZA NA KUUMIZWA, kwenye safari ya mahusiano kuna wakati UTAMUHUMIZA MTU AU ATAKUUMIZA kwa makusudi au kwa bahati mbaya,ujipange kwa gharama hiyo kubeba maumivu ya muda na kuyatua kwa amani na mahusiano yanendelee.
4⃣Gharama ya WEWE KUTUMIA AKILI KUISHI MJINGA/KICHAA MZURI.
👉Wengi hawajui kwenye ndoa au mahusiano *Mmoja wapo ni Mjinga au Kichaa mrembo/handsome* ambaye ukiamua ujibizana naye au ku ACT kwa matendo yake juu yako NDOA AU MAHUSIANO yatavunjika au itakuwa kelele kila mara.
👉Dawa ya kukwepa kero na migogoro wewe ongeza uwezo wa akili timamu,ila mwenzako umuhesabu kama *Kichaa mrembo au handsome* kama haleti madhara makubwa hasa katika uchumba ila kwneye ndoa WEKA MUHURI kwamba ninaishi na mgonjwa,mimi ni mzima hapo mtazeeka pamoja.
👉Msiwe vichaa wote ndani,mmoja awe mwenye akili,APUUZIE Shari hizi,hapo mnaenda, sasa KUPUUZA KILICHOKUUMA NDO GHARAMA HIYO KUBWA EVER HAPPENED.
Niishie hapo zipo nyingi.
*By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)*

MAHUSIANO AYLIYO KUFA

*Hapa Kuna sababu kadhaa Hatari*
1⃣Mlianzisha mahusiano BILA MALENGO HALISI, inafikia hatua uhalisia ukikosa watu wanapoteza hamu kati yao.(maana kinacho BOND watu ni Malengo)
2⃣Umeanzisha mahusiano ukiwa na Mbadala moyoni au njiani katika safari ya mahusiano kuna Abiria mwingine umempa lift ameshusha upendo wa mtu wa kwanza.(uwezi kubeba watu 2 kwa upendo sawa ndani yako, mmoja atapotea)
3⃣Mmekosa Maarifa ya Kisaikolojia ya kuendesha mahusiano ili mtie bidii kuyalinda na kuchochea upendo.
4⃣Mkisha juana kimwili(sex) kunazaliwa mazoea na dharau unzuri(kuna dharau mbaya) ambayo mtu anakudharau kwa kukuchukia, ila dharau mzuri ni mtu *Anakuona kawaida,huna jipya kwake,mvuto wa kumuangaisha akae akikiutafuta tafuta* ila kwa uhalisia HAKUCHUKII.
*By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)*

USALITI WA WAZI KWA NINI?

Kuna Dada mmja ameolewa sasa wana mtoto mmoja na mwingine tumbon ,,,,lkn mume cku y Jana amefanya kituko yn amerudi nyumban akiwa na mwanamke mwingine na nyumbani mke wake yupo,,,,,iv wanaume mnakwama wp kitu kama hiko unategemea kitokee nn labda 🤔
*Anajibu Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto*
*Hapa inabidi turudi nyuma sana,katika INTIMACY YAO, tusianze kuangalia kituko alichokifanya mume, kila kitu kina Catalyst*
👉Kuna mambo yanapelekea maamuzi mabaya au ya adhabu ya kisaikolojia kufanyika.
1⃣Kama watu wana mahusiano mazuri ya kindoa,mwanaume awezi fanya kitu kama hicho,na kama anatabia ya unzinzi atafanya kwa siri huko ila si kiivi alivyo fanya.
2⃣Kama wana mgogoro ambao umepelekea mwanaume kukosa baadhi ya haki zake kama SEX,HESHIMA nk, ataamua kukuonyesha anaweza kupata mahitaji hayo nje na wewe.
👉Sasa hapo hatuhukumu mtu mmoja lazima tuwangalie wote,chanzo cha shida kiko wapi,nani anapaswa kubadirika ili mwenzake abadirike.
Ila kisaikolojia hapa *Mwanamke kuna mahali amejisahau*
👉Wanaume wengine si wepesi wa kupiga,kutukana,au kukufukuza ila ATAKUJIBU KWA KUKUUMIZA KISAIKOLOJIA, inaitwa *Psychological Punishment*

MUDA SAHIHI WA KUINGIA KWENYE NDOA

*🌷🌷MADA*🌷🌷🌷 *Je! Niwakati gani sahihi unafikiri kijana aoe au Kuolewa ??*
Karibu Sanaa🥰
*Anajibu Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto*
*MUDA SAHIHI WA KUOA NA KUOLEWA*
👉Kikawaida jambo lolote ili lifanyike kwa ubora na uzuri na mtu alifurahie au limnufaishe lazima lizingatie mambo yafuatayo...
1⃣Uhitaji wako ni mkubwa kuliko kutolihitaji.
👉Kuna muda ambapo kuna jambo unalihitaji ila halina umuhimu sana kwa wakati huo,kuna wakati lina umuhimu,na kuna wakati lina ulazima.
*Muda wa umuhimu na ulazima* ndo muda sahihi wa kuoa au kuolewa.
_Viashiria vya Umuhimu na Ulazima_
1.Kusudi ulilo nalo moyoni mwako la Kimungu linahitaji mtu wa pili akusaidie?
2.Majukumu yako kuongezeka na kuanza kushindwa kuyamudu.
3.Vishawishi vya zinaa kuongezeka kila mara na kuelekea kukushinda.
2⃣Ukiwa Tayari kimaandalizi kumtumza mme au mke bila kuhisi umeongezewa mzigo mzito katika maisha.
3⃣Kumpata mtu sahihi wa kuanza naye safari ya maisha ya ndoa.
4⃣Kigezo cha umri miaka 20
_Hivi ni vitu vinavyo mwongoza mtu kuingia katika ndoa na akaishi maisha ya amani na raha na mwenzake._
By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)

MAWASILIANO NA EX -WAKO

Swali:
*_Je, ni sahihi kuendeleza mawasiliano na Ex boyfriend/Ex girlfriend? Je, inawezekana watu walokuwa wapenzi wakaachana kuwa marafiki?_*
*Anajibu Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto*
*KUACHANA SI UADUI,ILA LENGO LA KUACHANA LISIPO ZINGATIWA INAWEZA KUWA TANZI KWAKO(UNAHITAJI KUJIULIZA KWA NINI MLIACHANA,SABABU HIYO ITOSHE KUKUWEKEA MIPAKA YA MAWASILIANO NA HUYO EX WAKO*)
👉Usipojua Dhana ya kuachana,utavuruga mahusiano yako mapya au ndoa yako.
👉Sababu iliyofanya muachane ndo inapaswa kukuongoza kukata mawasiliano ya karibu na ex wako,usipo kata mawasiliano naye ATAVURUGA MAISHA YAKO MAPYA ya ndoa au mahusiano wakati yeye anamtu wake au ana maisha yake au atakauwa na maisha yake bila wewe.
👉Unashauriwa ex wako muwekee mipaka ya mawasiliano,kusaidiana,kukutana nk....
👉Walio wahi kuwa kwenye mahusiano,pamoja na kuachana,kuna namna mioyo yao iliwahi kuungana,kuaminiana na kupendana, *kwa hiyo mawasiliano ya mara kwa mara,yanaweza TIBUA hisia za mwanzo na kuwafanya wa RUDIANE kihisia na kujikuta wanaanza mapenzi ya siri nje na ndoa zao au mahusiano yao*

By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)

SUALA LA NDOA NI SUALA LA WAKATI

🪁🪁 *SUALA LA NDOA NI SUALA LA WAKATI*🪁🪁
_Kila jambo muhimu katika maisha ya mwanadamu,uwa tamu na zuri kama likitokea kwa wakati wake unaofaa_
🪁Wakati wa ndoa siyo umri, wala wkati wa ndoa siyo uwe umepata kazi, wala siyo uwe uko well off,suala la Ndoa *_Nila wakati ambao Mungu anamleta mtu sahihi, awezaye kusimama nawe kwa wakati ulio nao_*
🪁Siyo kila mtu anaweza kusimama nawe kwa wakati flani(hata kama amaeokoka au anauwezo kiuchumi)
🪁Kuna Majira ukimpata mtu kwa wakati wa Mungu, anafuta *Historia za Maumivu ulizo pitia,anaondoa Distance ya muda mrefu ukiokaa bila kuoa au kuolewa*
🪁Kwa upande mwingine waweza pata mtu katika muda wa haraka sana,mwenye uwezo sana,ila *Akauumiza Moyo wako na Ukachukia Mahusiano* Shida siyo yeye,shida ni Muda mliokutana haukuwa Muda sahihi kwako kukutana naye.
*_Jifunze Kuutafuta na Kuungoja na kuuombea Wakati wa Bwana kwako ambao utakuletea Furaha ya maisha katika ndoa na si majuto. Unapaswa kujua Mungu aliumba watu PAIRE, kila mtu anawake,usiwe na hofu ya kutokuolewa au kuoa_*
              ©2020 
*Ev Elisha Kazimoto*(Psychologist)
Whatsapp 0755444078

MAUMIVU YA MAHUSIANO

💊💊 *KATIKA MAUMIVU YA MAHUSIANO KUNA FAIDA YA KUTIBU MOYO WAKO*💊💊
_Mara nyingi watu wanaotuumiza katika mahusiano hawajui kuwa wanatujengea uwezo mkubwa wa kuendesha mahusiano mengine au ndoa yako bora zaidi kuliko jinsi wangetufurahisha. Kwa mwenye uwezo wa kuingia katika mahusiano kwa nia ya kuandaa FUTURE yake, kila maumivu ya kwenye mahusiano ni Darasa la Ushindi kwa Kesho yako,na ukishindwa kujifunza kwa yale yaliyokuumiza uwezi kujifunza kuboresha au kustawisha mahusiano yako au ndoa yako.Kwa hiyo Usimchukie aliyekuumiza kwenye mahusiano,bali amekujengea uwezo wa kutokosea tena ukaumia zaidi._
*Falsafa ya Kisaikolojia na Ev Elisha Kazimoto*(Psychologist )0755444078
         ©2020

MAAMUZI YA KUPENDA NA KUPENDWA

😘😘 *MAAMUZI YA KUPENDA AU KUPENDWA*😘😘
_Maamuzi ni Chaguo analolifikiria mtu ili kulifanikisha. Wengi wetu katika safari ya Kuanzisha maamuzi hatuanzishi mahusiano kwa Matokeo ya *Fikira za Kudumu* juu ya Maamuzi, wengi wetu tunasukumwa na *Mazingira Shawishi* juu ya kuanzisha mahusiano, ndiyo maana mahusiano mengi hayafiki kwenye *Ndoa* Break up zinakuwa nyingi. Shida ni Fikira ya Kupenda au Kupendwa ilitoka kwenye Mazingira au Kwenye Nia ya Dhati iliyolenga kutimiza Shahuku la Ndoa katika Muda Husika_
*Falsa ya Mahusiano na Ev Elisha Kazimoto*(Psychologist ) 0755444078
            ©2020

KIJANA KUMUWEKA NJIA PANDA MDADA

*SWALI KUTOKA KWA MDADA*
Jamaniiiiiiii wanaume munapotoka from one relationship to another be very careful,unapomwabia binti nitakuoa,anakaa na matumaini akikusubiri, lakini unavyo muache dhuuuuuuuuu,amekusubili miaka amejitunza juu yako,all over sudden una break his heart, lazima mutaigia kwenye ndoa na laana tu, wanaume kuweni makini musitamani mwanamke alie sababu yako,
*_Anajibu Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto_*
*Message hii ni nzuri ila inge COVER jinsia zote boys and girls, kwakuwa watu wengi wanatumia mahusiano kama site ya kutimiza short terms plans,(Malengo yao ya muda mfupi) mbali na lengo la muda mrefu la ndoa.*
Wengi wanapoingia kwenye mahusiano....
1.Hawana uhakika kama wako tayari wao kuongia kwenye ndoa.
2.Hawana uhakika kama walioingia nao kwenye mahusiano ya kuelekea ndoa ni watu sahihi wa kuoana
3.Hawajawa na dhamira ya dhati ya kuipenda ndoa.
4.Wanateswa na historia za waliyopitia nyuma
5.Wanateswa na taarifa za mazingira yanayowazunguka
_Mambo hayo ndo yanawafanya watu wote wote vijana kwa mabinti kuwa wasaliti au kuvunja mahusiano bila sababu za msingi._

MAVAZI KATIKA MAHUSIANO

*Miongoni mwa majukumu na wajibu wa kila mmoja kwa mwenzake ni kuangalia mwonekano wa mwenzako ukoje*
👉Ukiwa bachela unavaa kwa kadri uonavyo vema wewe ila ukiingia kwenye mahusiano Imara au ndoa utavaa kwa kadri ya mwenzako aonavyo vema kwake(unafanya kitu kinacho shika hisia zake siyo za wengine)
👉Sasa hapa mahusiano mengine yamevunjika mengine yamekuwa hatarini kwakutojua saimolojia ya mahusiano na mavazi au urembo.
👉Narudia pamoja na kwamba unavaa ili upendeze,kimbuka unapendeza kwaajili ya nani, kwaajili yako ili utafutwe au upendwe na wengine au kuufurahisha moyo wa mpenzi wako ajisikie Alichagua Cute au Hb na ajisifie kwa wengine?
👉Wao wanao sema mme wangu au mke wangu hawezi nipangia nivaeje nitokeje,aniache....Kweli atakuacha atawafuata wanaomwambia hivi ulivyo vaa umebamba au wanao vaa kama anavyotaka yeye, USIJE KULALAMIKA.( *Umekataa mwenyewe kuingia kwenye Hisia zake*)
By Ev Elisha Kazimoto(psychologist )0755444078

MSHAWISHI MKUU WA KUFANYA MAPEMZI

*KWA MSAADA WAKO NA WENGINE HAPA TUWEKE KUKBUKUMBU VIZURI ZA KIROHO NA KISAOLOJIA*
👉Kwanza kabisa,hali yoyote unayoweza kuiona huifurahii au ni changamoto kwako juu ya mchumba,mkeo,mpenzi wako huyo..... *Inamahusiano ya moja kwa moja ya kiroho na Kisaikolojia Umeisababisha wewe Mwenyewe Kijana na SI BINTI* ( Hivyo katika lawama unazoweza kutoa,zitoe kwa NAFSI YAKO halafu utafute msaada wa kutoka katika mzigo huu)nasi na darasa hili lipo kwaajili ya kukusaidia.
NB: *_Tunakila sababu ya kusema ukweli,kuchanganua kwa kina ili TUKUSAIDIE,tukikupa polee na ushauri mwepesi,Tutakupoteza na kuwaua wengine wajao ila hatutakupa ufumbuzi_*  (Sasa Fuatana nami)
1⃣Alama ya kwanza kwa mwanaume au mwanamke mwenye mapenzi ya Dhati kwako na anayeweza kukupenda daima hata kwenye ndoa,ila ambaye HAWEZI KUKUSALITI na kuwa na mahusiano ya siri mengine ni yule *Anayeweza Kuwa mwaminifu Kutokutaka MFANYE NGONO kabla ya Ndoa*
👉Sasa kwa maelezo yako, binti alijitahidi kwa mara ya kwanza kutimiza kanuni hii ya kukukwepa Msishiriki Ngono(SIYO TENDO LA NDOA KAMA ULIVYOLIITA MAANA NINYI SI WANA NDOA) ALIKATAA KUSHIRIKI NGONO NA WEWE,lakini ukatafuta ushauri pengine,ukaja na mbinu nyingine UKAMSHINDA mkashiriki NGONO kinyume na kanuni za kiroho,kinyume na kanuni za Kisaikolojia( *Hapo ndo uliharibu kila kitu*)
👆👉Upendo wa dhati na furaha yake juu yako,na uaminifu wake kwako ulikuwa umefungwa kwenye Siri ya kutojuana kimwili,baadaya ya kujuana....
1.Heshima,Upendo,Uaminifu Vikapotea(Maana mlivifungua kabla ya Kiapo ch Uaminifu)
👉Sasa unataka Akupede kama nani? Akuheshimu kama nani?Akuamini na kukulindia uaminifu kama nani? *_Wakati anakuona wewe ni muhuni,mlaghai,mtu asiye mvumilivu,na mwaminifu?_* Kwasababu tendo la mpakanafanya ngono Lugha ya udanganyifu ilitumika,lakini mlifanya wote mkijua hii SI HALALI.
👉Kwa maneno mengine kiroho mmeuondoa mkono wa Mungu juu yenu uletao amani,furaha na upendo kwenu,mkabaki WAKIWA.(Laana hiyo ya Zinaa kibiblia)
👉Lakini kisaikolojia mkavuruga system ya Siri ya uminifu na hamu ya kujua siri(mkabaki WAKAWAIDA)
2️⃣Ulifanya jambo la kuumiza moyo wa binti kwa wakati ambao alikuwa hajawa tayari kuumizwa ndo maana AKAKUCHUKIA.
1.Umemlazimisha kufanya ngono,Ukambebesha Mzigo wa Majukumu ya malezi....Nje na wakati.
A)Mfano kama alikuwa bikira wewe umemdhalilisha na kuondoa heshima yake kabla ya kiapo...Unataka akupendeje,akuheshimu na kukuamini kwa Lipi?
B)Kama alikuwa si bikira, alijilinda asipate mimba muda mrefu ila wewe UMEMLAZIMISHA APATE MIMBA BILA KUTAKA(Unataka akupende kwa lipi hapo,au akuheshimu,ajivunie uwepo wako kwake kwa lipi?)wakati umemuanzishia safari ya miaka yakutokuwa huru?
3⃣Umemvuruga kisaikojia wakati alikuwa hajajipanga kiwa mama mwenye mtoto,changanya na maudhi ya mimba(mlio olewa na kuoa mnajua kipindi cha mimba kilivyo)sasa huyu mdada anateseka wakati jamaa aliye mtesa HANA MUDA WA KUMUHUDUMIA 24HRS/7DAYS? Asikuchukie wee nani?.
👉Kwanza kama alikuwa na wapenzi wengine means alikuwa bado hajadhibitisha nani wakumuoa,we ukamuwahi ukampamzigo wa mimba,kwa hiyo anaingia katika hofu na wasiwasi wa nani atamuoa na kukpa furaha..Je niwewe uliyempa mzigo?,ni yule aliyempenda kwanza je ataendelea kumpenda na mzigo wa mwingine?
NB:Vijana kwa mabinti fahamuni hili, *_Upendo wa uchumba au mahusianobya urafiki,Haulindwi au kuimarishwa na NGONO kabla ya ndoa,Inalindwa na Uaminifu wa wewe KUKATAA NGONO kabla ya ndoa,Kijana au binti atakaye kuacha kwa kigezo cha humpendi kwakuwa imemnyima ngono, Jua huyo ALIKUWA TAPELI,KIBAKA NA MUHUNI na Hafai kuwa mke au Mme_*
👉Sasa kijana nikushauri sasa. _Jambo la kufanya hapa baada ya kuharibu, Kwanza nenda katubu,uokoke upya,uongozwe sala ya toba upya,halafu ongea na mzazi mwenzio kuhusu hatima yenu,muulize atakuwa tayari muoane au muachane Utunze damu yako tu? Jibu atakalokupa yeye NDO ULIFUATE,Ukishakosea huna namna,tumikia kosa lako kwa amani ili usizalishe Matatizo makubwa bya baadaye_
*Imechambuliwa na Mchambuzi wa masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto(psychologist)*
   WHATSAPP 0755444078
        ©2020

MUDA WA KUTOA JIBU UKITONGOZWA

*MUDA WA KUTOA JIBU LA NDIYO AU HAPANA HAUKO FIXED,BALI UTATEGEMEA MTAZAMO,HISIA, ZA MWAMBIWA JUU YA ANAYE AMBIWA,PIA KAMA MTU NI MCHA MUNGU ITATEGEMEA CONNECTION ALIYO NAYO NA MUNGU ILI KUPATA JIBU LA NDIYO AU HAPANA*
NB: _Wengi katika kutoa majibu, wanazingatia mambo yafuatayo....._
1⃣Kukariri kwa mazoea ya watu kwamba mwanaume usimpe jibu haraka ataona kama ulikuwa umeisha sota kutafuta mme(Kwa hiyo hata kama anakupenda au siku nyingi anasubiri umwambie neno atajifanya hana muda na wewe mpaka umsumbuepo tena.( Angalizo: Unaweza kusubiri usumbuliwe tena jamaa akatafuta mwingine ukabaki na maumivu)
2️⃣Kuna watu wanachelewa kutoa jibu kwa kuanza kufanya utafiti wa *Uhalali wako wa Kumuoa,asije chukuliwa na Jambazi la kiroho au la kimaisha*(Hii imekaa sawa)
3⃣Kuna watu wanachelewa kutoa jibu la ndiyo au hapana kwa kusema Amauulize Mungu ila wengi wao *Wanauliza Mungu hali ya Hewa(ya mfukoni mwako)ikoje...Akigundua ATM inasoma maisha yako poa,hata Mungu hajasema chochote utasikia NIMEPATA AMANI KUBWAAAA SANA JUU YAKO baada ya kumuuliza Mungu, wengine kama *Wewe ni Kijana wa Kuishi kwa Imani(Wale wa Mbele ninaendelea...)Utaambiwa SIJAPATA KIBALI KWA MUNGU JUU YAKO,ila ukweli ni kwamba Ameona Mambo yako hayasomi.
*_Ushauri:Dada Toa jibu kulingana na Nia ya moyo wako,na kama ni Mungu basi muulize Mungu,kama unacheki hali ya hewa cheki vzr,na usimkawilishe mtu itakugharimu,Ukimpenda mpe jibu hata kama ni papo kwa papo,kama humpendi mwambie kwa ustaarabu Sijaona kama itawezekana_*
By Ev Elisha Kazimoto(Pychologist)0755444078

SAIKOLOJIA YA KULINDA MAHUSIANO

❤️❤️ *SAIKOLOJIA YA MAHUSIANO NI NGUMU SANA*❤️❤️
_Watu wengi ushangaa hivi imekuwaje na huyu tume break!!tume divorce!! Hivi huyu mtu amekuwaje tulianza kwa upendoooo wa motooo leo dah kama tunalazimisha vile!!_
👉Iko hivi, ili mahusiano yako yadumu, jambo la kwanza:
*_Unajua udhaifu wako na mapungufu yako, udhibiti mapungufu yako kwanza kabla ya kuyapigia kelele ya mwenzako,utafanya muda wa break up kusogea mbele,muda wa kuchokana usogee mbele( Yaani kama ilibidi (mbreak ndani ya miezi 6 muda utasogea mpaka mwaka 1)_*(Hiyo ni Faida kubwa)
👉Pili, _Akikisha unapomsifia mwenzako na Kumuona anakufaa sana (Katika Muda huo Yachungulie Madhaifu yake uyabaini) usikae unamsifia tu na Kujifanya Huoni madhaifu yake kisa upendo wenu mbichi na upo fire.(Muda wa upendo ukiwa juu ndo muda wa kumshauri na kumkosoa mwenzako na akaendelea kukupenda zaidi,ukisubiri upendo ushuke ukimkosoa ataona hufai na atakuchukia na itakuwa lango la break up au divorce_)
👉Tatu, Usisubiri ufanyiwe jambo ndo umfanyie mwenzako,wewe fanya kwake utalinda upendo na mahusiano( *Usisubiri upigiwe simu,usalimiwe,utafutwe,usifiwe,upewe zawadi, fanya wewe kwanza*) hayo mahusiano yata dumu imara.
*_Kutoka Meza ya Mwanasaikolojia Ev Elisha Kazimoto_*
       ©2020

Saturday, 13 June 2020

DADA JITAMBUE(PART V)

*Sehemu ya Tano ya Somo, Ukijitambua Kama Dada wa Thamani, Utapata Mme Haraka*
_Mnenaji ni mimi Mtumishi wa Mungu *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist )*_
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail :babaeve755@gmail.com
......................
Karibu Tumalizie somo letu...
👉Ukisha jua siri mbalimbali zikupasazo kufanya ili kupandisha Status yako ya Kiroho na Kimwili,hapo sasa ndipo inakupasa kuingia Magotini kuomba,kushugulika na Ngome za Giza ambazo mara zote ushindana kuzuia kusudi lililo jema lisitimie kwenye maisha yako.
👉Muhusishe Bwana akutangulie mbele yako katika kukusafishia njia ya kumpata aliye chaguo la Mungu kwako(Mme mwema)
1 Haya ndiyo Bwana amwambiayo Koreshi, masihi wake,ambaye nimemshika mkono wake wa kuume,ili kutiisha mataifa mbele yake,name nitalegeza viuno vya wafalme;ili kufungua milango mbele yake,hata malango hayatafungwa. 
Isaya 45:1

2 Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma; 
Isaya 45:2

3 nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni Bwana, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli. 
Isaya 45:3
....................
👉Sasa njoo uoate siri za namna gani na mambo ya kushugulikia katika maombi yako ili kumpata mmeo aliyekusudiwa na Mungu kwako.
🔥 *HATARI ZA KUSHUGHURIKIA KATIKA MAOMBI DHIDI YA UBINTI WAKO*🔥
🔥Shugurika na Roho/Madhabahu za kifamilia na ukoo wenu.
👉Kuna mambo huyajui kwenye familia,matabia yamefunga milango kwenye mafanikio yako,kuna rohobzinang'ang'nia mtu hata akiokoka hizo usizipe nafasi kil siku zishughurikie.
🔥Shugurika na Roho za kuchelewesha mambo. Unakuta mdada upo ni mzuri umekamilika kila kona ila *Unachelewa kuolewa mpaka unaingia 40s* piga roho hizo za jangwani za kukuzungusha 
🔥Shughurika na Roho za Kukataliwa. Kuna watu wanakataliwa live na wengine wanakataliwa kwenye ulimwengubwa roho, kimwili anaonekana anapendwa na watu ila kiroho anakataliwa na hawezi olewa kirahisi.
🔥Kataa roho za ndoa ya jinsia moja. Kuna wadada wanapendwa sana na wadada wenzao mpaka wanaambiwa yaani ningekuwa mwanaume ningekuoa wewe, ila wanaume HAWA MPENDI NA HAWAMKUBALI, hizo ni roho za Lesbian.
🔥Shughurikia Roho za Uchafu juu yako. Kuna wadada wazuri sana ila wanaonekana kwenye ulimwengu wa Roho wachafu na wana nuka, huwezi olewa kama umepakwa mavi kwenye ukimwengu wa Roho,utavaa nguo za gharama na  unyunyu lakini wapi wanaume wanapita kushoto.
🔥Shughurika na Ndoa za Majini(mapepo). Kuna wadada hawawezi olewa kwakuwa wao walisha funga ndoa na mapepo kwenye ulimwengu wa Roho. 
👉Mara nyingi wadada hao *Alama zao* ( _Wanaota wana sex,wanaingiliwa kimwili wakiwa wamelala na wanaune wanao wajua au wasiowajua, Wanaota wana nyonyesha watoto, wanaota wanafunga ndoa baharini, wanaota ndoto za baharini baharini, wanaota wanavalishwa pete, wanaota wanafunga ndoa, wanaota wako Beach na mwanaume, wanapenda sana kushikwa maziwa sana, wana penda sex sana hata kujichua, wanapenda wadada kimapenzi zaidi ya kupenda wakaka, Wana Hasira za Karibu na za haraka sana na wagumu kueaamehe mtu hasa jinsia ya kiume_) ukiona vijidalili hivyo kwako na hujaolewa,hujapata mchumba,au unamchumba ila mahusiano yanasua sua,au yameenda miaka 3,4,5 pambana kwenye maombi unaweza USIOLEWE.
*_Basi mimi niishie hapo najua dada umepata dozi ya kutosha katika Series ya Somo hili Refu kweli kweli lenye shemu karibu 5(Part 1 hadi Part 5) Mungu akupe Neema ya Kujifunza na kufunguka._*
Mwandaaji wa Somo hili ni Mtumishi wa Mungu
*Ev Elisha Kazimoto(Psychologist & Counselor*)
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
e-mail :babaeve755@gmail.com

DADA JITAMBUE(PART IV)

*Sehemu ya Nne ya Somo, Ukijitambua kama Dada wa Thamani, Utapata Mme Haraka*
_Mnenaji ni mimi *Ev Elisha Kazimoto*(Psychologist )_
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail :babaeve755@gmail.com
.........................
Karibu Tuendelee......
👉Hautaweza kupata Mme wa Viwango kama Unajiweka ovyo ovyo kimwili,huna maadili,huna staha,hujiheshimu, wewe umekazana na kuomba tu,hupati mme, Tengeneza status za kimwili zinazo vutia ili kila akuonaye kabla hajaanza kuona vitu vya kiroho vinavyo kutoka vya Kimungu basi aone Peesonality yako na Tabia zako za kimwili zinamfaa wewe kuwa mke wake
5. *Heshima na Adabu* Dada kaa ukijua pamoja na status ya kiroho,kuwa mwombaji,muimbaji,muhubiri nk,havikupi mme bila kuwa na combination ya status za kimwili,.
👉Miongini mwa status muhimu ni wewe dada kuwa na Heshima na Adabu kwa watu.
👉Heshima na adabu yako itakupa kibali kwa watu itakutangaza kwa watu,watu watatamani kuwa karibu nawe lakini kukumili.
👉Waweza kuwa na kopato,elimu,huduma kubwa ya kiroho ila ukiwa na jeuri,kiburi,dharau aisee utaishia kuitwa SHANGAZI WA KANISA,wadogo zako woote wataolewa ila wewe uta SUGUA BENCHI,hapo hakuna pepo, pepo ni Tabia yako.
👉Heshimu mwenye kipato kidogo,kikubwa,wazuri kwako na wabaya kwako,huwezi jua kwamba unaye mdharau ndo anaweza kuwa kiunganishi cha mmeo mtarajiwa au akakata muunganiko wako na mmeo mtarajiwa.
6. *Jenga jina Mahali ulipo zaliwa(Unako tokea)na Jenga jin Ugenini*
👉Kuna watu ujisahau sana, wengi wetu tuliko zaliwa na kukulia ni tofauti na tunakoishi sasa mpaka tunapata wenzi tunawapa mbali na tuliko kulia  na kulelewa.
👉Unajua nini, watu wengi wanajenga Jina waliko sasa wanaonekana watu wazuri sana *Ila kwao,aliko kulia wanamjua kama mtu ovyo,hafai,aambiliki,mvivu,mchafu,kahaba* kumbuka ukimpata mchumba LAZIMA MTARUDI KWENU, vipi familia na mdugu zako na majirani watakusemeaje wewe kwa mwenzako na ukweni kwako?
👉Na wengine nyumbani kwao na majirani wanamjua mtu mwema,mpole,mtakatifu,mtu wa watu,ila kumbe *Kule anakoishi sasa, watu wanajiuliza hivi huyu Alizaliwa na mwanamke au ni pepo flani limevaa mwili* haya mambo yatakuharibia hata ukijificha itakuumbua.

7 *Ishi Maisha yako Halisi, Acha Kukopi kopi(Artificial life)*
👉Wewe ni mdada wa aina flani,ishi kama wewe usiishi kama flani, tafuta uhalisia wako ndo utaishi maisha ya maana na ya furaha na watu watakupenda kwa namna ulivyo.
👉Ukiishi sawa sawa na wewe ulivyo NATURE YAKO,utafanya mambo kwa ubora na uzuri ila ukiwa unaishi kwa kukopi flani utakuwa unjitesa sana kulazimisha ufanane na flani, wewe siyo flani wewe ni wewe.
👉Yaani na maanisha, _Kuwa na tabia yako kama ulivyo lelewa,heshima ya kwako,ongea ya kwako,matumizi ya pesa ya kwako,vaa ya kwako, ukitaka kuwa kama flani utajikuta kila siku unakosea na kujutia,unatamani kuishi kama flani ambaye anauza mwili wake kila siku ana wanaume 7 kila mmoja anaonga, wewe huna halafu unahitaji uvae,ule,utoke out nk kama yeye utakosea na status yako itashuka_
👉Jikubali kama ulivyo, pambana kuongeza status yako,utaishi maisha yenye radha,yasiyo na majuto au mashariti magumu, au maumivu ya kutendwa.
👉Hakuna raha na ujasiri mkubwa kama mwana dada kuolewa na Heshima yako,hakuna anayekunyoshea vidole vya *Huyo hamna kitu* ina leta raha,inakufanya ujione Malkia kwa mmeo lakini utaheshimika.
*_Mpaka hapo ni seme Mungu akubariki,tukutane katika sehemu yetu ya Tano na ya mwisho katika Somo hili, mnenaji alikuwa mimi Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto(Psychologist )_*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail :babaeve755@gmail.com

DADA JITAMBUE(PART III)

*Sehemu ya Tatu ya Somo, Ukijitambua kama Dada wa Thamani, Utapata Mme Haraka*
_Mnenaji ni mimi Mtumishi wa Mungu *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)*_
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail babaeve755@gmail.com
....................
Sasa Karibu tuendelee....
👉Jambo lingine muhimu kwako Mdada wa Yesu Kristo ni Kutengeneza Status yako ya Kimwili.
👉Kumbuka Ndoa ni 50%Kiroho na 50% Kimwili, kwa hiyo unapojipanga kuingia katika ndoa,usiishie kuomba tu,lazima Ujipange na Kimwili, kumbuka tunaishi duniani, Vipo *Vigezo vya Kimwili* Vijana wana vitazama katika kuchagua mke bora wa kuishi naye.
👉Na labda ni kwambie, Wengi wa vijana wanaanza na Vigezo vya Kimwili ndo wanachungulia Rohoni, kwa nini Ndoa ni ya hapa hapa Duniani, usije ukasema mimi niko Rohoni sana mambo ya mwili sina haja nayo sana, HUTAOLEWA,utabaki kusubiri bila majibu.
..............
2⃣Tengeneza Status yako ya Kimwili.
👉Pamoja na kwamba kwenye ulimwengu wa Roho ndo vitu vinaanzia nakuja kwenye ulimwengu wa mwili,basi tunahitaji kutengeneza mazingira ya Kimwili ili kuwa na pawepo na uwiano kati ya thamani ya kiroho na thamani ya kimwili ndo unazalisha mtu UNIQUE  anayetafutwa kwa kasi na vijana.
👉Usije kaa Rohoni tu ukashindwa kushugulikia Status ya kimwili, kumbuka  *_Wengi wa watu wanatazama mwili kabla ya rohoni_* unaweza poteza muujiza wako, kwasababu STATUS YAKO YA KIMWILI iko chini.
👉Pambana kujenga status ya kimwili ili watu wakuonao waseme YES, you are Beautiful (CUTE GIRL)
👉 *Status za Kimwili* ambazo dada kama dada zinakupandisha chati na uonekane ni Wife Material na unafaa kuolewa haraka....
1. *Usafi* Binti muda wote jiweke nadhifu, uwe na nguo moja au nyingi *Jiweke Safi, Smart*
👉Unatoka kidogo,unaenda kwa mangi Toka ukiwa Vizuri, hujui utakutana na nani na atakuwa anakufanyia tathimini gani.( Mwonekano wako wa kwanza waweza kukuongezea Credits au kukupunguzia Credits).
2. *Ujasiliamali (Uchumi)* Unahitaji kuongeza thamani yako na kulinda thamani yako, Jitemgenezee mazingira ya *Kutokuwa Tegemezi kwenye Mahusiano na uchumba* wengi wamepoteza Thamani zao na kushindwa kuolewa haraka kwasababu WANA NJAA, UHITAJI WA PESA, wanayumbishwa na kutapeliwa na vijana matapeli wenye uchumi kidogo
👉Hasara za kuwa tegemezi ni kukosa *Msimamo binafsi na kauli ya NO or YES* Muda wote kila kitu utakuwa unasema YES kwa unyonge, unajua hapa ni makosa, napoteza utu wangu, nanyanyaswa ila utafanyaje, huna kitu unalazimika kusema YES,ili usikatiwe huduma ya vichenji.
3. *Lugha* unajua nini, wewe mwanadada ni mfanya biashara, unahitaji lugha tamu, lugha inayovutia wateja wako.
👉Lugha inaweza kukuweka mbali na wateja wako au karibu na wateja wako.
👉Ukari hauwi katika Lugha, kujilinda na kujiheshimu dada hakupo katika kuwatukana wakaka na kuwadharau.
👉Tumia lugha nzuri,kataa wahuni na matapeli kwa Lugha nzuri, siyo lazima Utukane na umdharirishe mtu.
4. *Taaluma* Miongoni mwa vitu ambavyo katika zama hizi sio vya kuchukulia rahisi ni TAALUMA( *Professional*) una ujuzi upi, wa nini, unaweza kukusaidiaje katika kuendesha maisha.
👉Wale ambao bado mpo katika mchakato wa kusoma, *Soma kwa bidii* ongeza vidato,jiweke katika level nzuri,usiache shule kisa umeambiwa na mchumba wako kwamba UTASOMA NIKISHA KUOA, au haina haja sana ya wewe kusoma MIMI MMEO NIPO, *Nyakati zinabadirika binti yangu* unaweza ukajutia maamuzi yako ya kuacha shule ili uolewe.
👉Wale ambao mambo ya shule vidato yameisha waacha kidogo, TAFUTA UJUZI (kwasasa ni kila kona ujuzi unapatikana) *Jiimarishe uwe mtaalamu haswa*

*_Mf.Kama ni kupamba maharusi, Kupamba kumbi,keki,ufundi wa nguo nk, Somea chuo kabisa uwe mtaalamu haswa_*
Achana na mambo ya kwenda kujifunza cherehani kwa fundi wa mtaani kwenu, au kupamba kwa flani ambaye naye anatamani akae yeye ndo anajulikana, nenda chuoni upate vitu adimu na uongeze ubunifu wako,ili *Upunguze ushindani juu yako* ufanye vitu Unique and attractive.
👉Nataka ni kwambie wanaumebwatapanga foleni kwako,lakini hata ukiolewa utakuwa unathaminiwa na kupendwa sana.
_Unaonaje unaitiwa tenda ya kupamba kwenye harusi ya mil 2,3, au 5 siku moja unainuka na mil 5,wakati kuna mfanyakazi anafanya kazi mil 5 anaipata baada ya miaka 5?_
*Dada ongeza status yako bhana ndoa kupata ni rahisi*
_Kufikia hapo ni hitimishe sehemu ya Tatu ya somo letu,lakini nikukaribishe kwa sehemu ya nne ambapo tunaendelea na Status za Kimwili, 5,6 na 7..Barikiwa sana na Bwana_
Mnenaji alikuwa mimi Mtumishi wa Mungu *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail babaeve755@gmail.com

DADA JITAMBUE(PART II)

*Sehemu ya Pili ya Somo, Kama Ukijitambua Kama Mdada wa Thamani, Utapata Mme Haraka*
_Uko naminenaji Ev Elisha Kazimoto(Psychologist )_
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
e-mail babaeve755@gmail.com
.................
Karibu tuendelee....
👉 *Kazi yako kama Dada Tengeneza na Ongeza Thamani yako*👈
1⃣Tengeneza Status yako ya *Kiroho* kama Dada uliyeokoka.
👉Unajua maisha ya Kiroho ndiyo yanayo vuta mambo ya kimwili.
*2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. 3 Yohana 1:2*
👉Ukiona unazembea kwa mambo ya kiroho,jua unachelewesha muujiza wako wa kimwili(mmeo)
👉Thamani yako ya kiroho inapopanda *Inavuta muujiza wako kimwili*

👉Unahitaji kila siku mwana dada ujue kwamba *Thamani yako inawindwa na shetani na mawakala wake* ili ishushwe,na upoteze NDOTO NA MATUMAINI ya kuingia katika ndoa ya baraka.
👉Kwa sababu hiyo hakikisha kila siku unaongeza uwezo na unalinda njia zako zote za ubinti wako.
*1 Yeye asetaye vipande vipande amepanda juu mbele ya uso wako; zishike silaha, ilinde njia, vitie nguvu viuno vyako, uongeze uwezo wako sana.Nahumu 2:1*
👉Wadada wengi wamejisahau katika kulinda THAMANI ZAO, wanaishi wanavyotaka, siyo kikanuni, jambo lililopelekea Kupoteza thamani zao kirahisi.
👉Kumbuka thamani ikishuka,na matumaini ya kupata mtu sahihi yanapotea, *na uwezo,nguvu ya kutafutwa na mtu sahihi inapotea*
👉Kazi yako ni Kuongeza Thamani yako, *Watafutaji wanatafuta vitu Unique vyenye Thamani*
👉Sasa kazi yako ni kuanza kutengeneza Status yako kiroho,uone jinsi ilivyo na nguvu ya kuvuta mambo inayo tamani maishani.
👉Twende pamoja katika kuangalia Status muhimu za kukazania kuwa nazo kiroho:
👏 *Status za Kiroho za kukuvuta karibu na mmeo*👏
🔹 *Tengeneza sifa ya kuwa Mwombaji* Miongoni mwa sifa kuu ya mdada(na mwanamke mtarajiwa mama wa familia )ni Kuwa mwombaji,hiyo ni kibiblia.
👉Maombi yatakufanya uwe karibu na Mungu lakini maombi yatakufanya uwe na uwezo wa kutambua wanaume feki na mwanaume sahihi wa kukuoa wewe.
👉Sikiliza wewe ni dada mtafutwaji, waweza kuja watu 20 wote wako vizuri kimwonekano,ila hawawezi kuwa waume zako wote 20,yupo mmoja utamjuaje? Ni namna unavyokaa magotini,penda kufunga,kuomba jiombee na mwombee mmeo mtarajiwa.
🔹 *Tengeneza Statu ya Kuishi Maisha Matakatifu yasiyo na michanganyo* Miongoni mwa vitu vinavyoweza kukupa kibali mbele za Mungu cha kupata mtu sahihi ni wewe kulinda maisha yako yasichafukiwe na dhambi au makosa na uchafu wowote.( *Hii inawashinda wengi*)ila wewe jipange kushinda.
👉Usiwe wa kujirahisisha kiasi kwamba *_Mwili wako unajulikana kwa kila kijana,maeneo yako yote muhimu ya mwili yanajulikana,hisia zako zinajulikana kwa kila mmoja_* Weka Distance ya Kusaidia Mwili wako Uheshimiwe. 
👉Usifurahie sana kushikwa na kila mmoja,( *Kushikwa sehemu za mwili kuna Raha yake,unasikia kuburudika ila KUNA GHARAMA YAKE*)itakusumbua,itakuchelewesha baraka zako au kupoteza kabisa muujiza wako.
👉Sasa ni heri ukaweka msimamo usio badirishwa na mtu yeyote awe mchumba wako au rafiki,ni heri akakuchukia au urafiki n auchumba ukavunjika lakini umelinda STATUS YAKO na utakatifu wako ambavyo ni nyenzo ya kukuletea mme sahihi.
👉Ila ukiwa simple kwa kila mtu, *Huyu atashika,atachezea sehemu zote,mwingine hataishia kuchezea atazama ndani kabisa na kuvunja Agano lako na Mungu na Mmeo* hapo ndo Utatamani usiku uwe mchana na mchana uwe usiku.(Ujui gharama zake na bora usijue kama bado ujakutana na changamoto hizo omba zisikukute ongeza umakini).
🔹 *Tengeneza Status ya Huduma,utumishi kwa Bwana* Ni hatari na hasara kwako dada upo kanisani upo upo tu, ni mpiga makofi na kucheza sifa na kurudi nyumbani, aisee mume utamtafuta kama sindani katikati ya takataka.
👉Dada kanisani pawe kama nyumbani kwenu, hakikisha *Una Huduma ambayo mpaka kanisa hata watoto wa sunde school wanajua hii uwa ni Huduma ya Dada Joyce,Mary,Happy nk* na usipoonekana siku hiyo kanisa zima linajua kuna mtu hayupo leo.
👉Pambana na huduma zote bila kudharau kama kudeki vyoo, kanisa, kwa mchungaji,uimbaji,ushemasi nk fanya kwa jasho lako la mwisho na kwa kupenda na kujitoa, huduma kazi yake *Ni kukutangaza na kukufunua kwa watu na kukupa kibali* ukiifanya kwa moyo na kwa bidii aloo utaonekana haraka.
👉Hatufanyi huduma ili tuonekane,au tuolewe ila tunafanya kwamba tunampenda Bwana lakini huko huko ndo tunakutana na mahitaji yetu.
🔹 *Tengeneza Status ya Kujifunza Neno la Mungu, Kuhudhuria Ibada* Usifanye makosa ya kuwa Empty Vessel,dada huna hata mistari ya biblia 10, soma neno, nenda kanisani kwenye ibada,idara nk,usiwe mtu wa kuonekana mara moja kwa wiki, wewe utakuwa hujajipanga kupokea baraka zako za mme.
👉Ibda kwako iwe LAZIMA siyo ya Muhimu tu. Huko ndiko utakako kutana na majibu ya maombi yako na mtu wako.
👉Mpe Mungu kipaumbele na yeye atahusika kwenye mambo yako.
*_Mwisho wa sehemu ya pili ya somo letu, tukutane katika sehemu ya Tatu ambapo nako kuna siri nyingine nyingi za kukufanya uwe mdada wa Viwango_*
Mnenaji alikuwa Mtumiahi wa Mungu *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist )*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail babaeve755@gmail.com

DADA JITAMBUE(PART 1)

🧏🏻‍♀️🧏🏻‍♀️ *UKIJITAMBUA KAMA MDADA WA THAMANI,UTAPATA MME HARAKA*🧏🏻‍♀️🧏🏻‍♀️
_Shalom wadada wa Yesu Kristo,leo nizungumze na mdada mmoja baye leo anataka afumbuke macho yake aone kile ambacho nakiona kwake( *Umeumbwa kwaajili ya Mtu flani Special*) haukuja tu duniani, Una mwenzako special_
*By Ev Elisha Kazimoto(0755444078)*
...............................................
🧏🏻‍♀️Mara nyingi tunakosea katika Kujitazama si katika kutafuta vitu.
🧏🏻‍♀️Nguvu kubwa ya kutafuta,tungeiwekeza katika Kujitazama kama Mungu anavyo tutazama basi, ni rahisi sana kupata kile ambacho unakitamani( Ubavu wako).
🧏🏻‍♀️Unajua tangu ulipoumbwa na Mungu tumboni mwa mama yako, *_Ulikuwa unaumbwa kwaajili ya mwanaume wako_* wewe ukuumbwa ili uzunguke ukitafuta mtu,ila uliletwa Duniani kwaajili ya Mtu(mmeo).
*Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.Yeremia 31:22*
🧏🏻‍♀️Popote alipo Rais lazima Mlinzi awepo(na popote alipo mwanaume jua mwanamke anahitajika) *Huyo mwanamke anaye hitajika ni wewe(dada)*
🧏🏻‍Baada ya kuja duniani unacho hitaji kuwa nacho ili *Upelekwe,ukutanishwe na mmeo ni Wewe Kuishi kwa Thamani yako uliyoumbwa nayo*
🧏🏻‍♀️Kinacho weza kukuwaisha kwa mmeo au kukuchelewesha kukutana na mmeo ni LEVEL YA THAMANI YAKO.
🧏🏻‍♀️Kila anayeingia katika ndoa anaingia kwa kiwango cha thamani yake kupanda.
🧏🏻‍♀️Siri ni kubwa, *Watafutao hawatafuti sura au jinsia ya kike, Wanatafuta THAMANI ndani ya jinsia ya Kike inayoweza Kutunza VISION aliyo nayo mwnaume* 
🧏🏻‍♀️Na hata siku moja Hakuna ambaye utafuta kununua au kupata kitu cha Thamani ya CHINI, au kibovu,wanatafuta Kitu cha Thamani ya juu.
🧏🏻‍♀️Na ukiona mtu anatafuta kitu cha thamani ya chini jua na yeye ni wa Thanani ya chini zaidi ya wewe unaye tafutwa.
👉Unahitaji mtu wa Viwango katika maisha yako, hakikisha unaongeza viwango vyako vya thamani yako.
*_Hii ni sehemu ya kwanza ya somo hili kati ya sehemu 5 zilizobeba somo hili usikose sehemu ya pili, Ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa EV ELISHA KAZIMOTO (Psychologist )_*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail babaeve755@gmail.com

Friday, 12 June 2020

NDOA NI 50%KIROHO NA 50%KIMWILI

🔹🔹 _Swali: Nitumie vigezo vya kiroho au kimwili kuchagua mwenzi wa maisha?_🔹🔹

Anajibu mchambuzi wa masuala ya Kimahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)*
Whatsapp 0755444078
*NDOA NI 50%KIROHO NA 50%KIMWILI KUWA MACHO ONGEZA UWEZO WA MAARIFA*
👉Labda nifafanue dhana hii ili kuwasaidia vijana na wanandoa wote ili kulinda amani,furaha na upendo kati ya COUPLES za wapendanao.
👉Tunasema ndoa ni 50%kiroho kwa sababu Mungu ndo mwanzilishi wa Ndoa,hatuingii kwenye ndoa tuonavyo sisi,ila kwa mapenzi ya Mungu ili tulitimize kusudi la Mungu.
👉Kwa maana hiyo tunahitaji lumihusisha Mungu sana kila hatua *_Wakati wa kutafuta,baada ya kimpata,na wakati wa kuishi naye_* Mungu ahusike ili kuwahifadhi mkae katika amani,furaha na upendo kati yenu 
👉Sababu nyingine ya kumuhusisha Mungu kila hatua ni ili kujenga ukuta wa kimdhibiti adui kuwavamia na kuharibu uchumba na ndoa yenu.
5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe; 
Mithali 3:5

6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako. 
Mithali 3:6

👉Pili nimesema ndoa ni 50% kimwili, kwasababu hatuishi Mbinguni,tunaishi duniani na tumepewa *_Akili na Utashi wa kujua mema,zuri,baya na kubaini vitu vipendezavyo na vichikizavyo_* kwakuwa tumepewa Ujuzi wa Kimungu wa kiutashi wa kubaini kinachotufurahisha hapa duniani nafsi zetu Mungu alitupa Fursa ya Kuchagua.Ili katika uchaguzi huo tuyatumikie matokeo ya uchaguzi wetu bila kulalamika.
*_Unajua kwa nini? Asilimia 100 za kuchaguliwa na Mungu ziliishia kwa Adamu,alipo chaguliwa na Mungu baadaye alimualaumu Mungu kwa alichompa_*
11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale? 
Mwanzo 3:11

12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala. 
Mwanzo 3:12

👉Baada ya hapo Mungu akaweka Nafasi ya wewe mwanadamu(Kija au binti)Muulize Mungu akushauri katika uchaguzi wako,yeye awe na sehemu yake na wewe uwe na sehemu yake.
👉 *Kwa maana hiyo unapomwomba Mungu naye Mungu anajua unatamani vigezo gani vya Kimwili atakupa mtu unaye mtaka kama anaona anakufaa ila vigezo vinaweza visiwe vyote ulivyotaka lakini Mungu pia anaheshimu vigezo vyako kama UMEANZIA KWAKE*
Kwa hiyo omba,angalia kwa macho nani akupendezaye kwa macho na moyo wako.
👉Lakini kisaikolojia (kimwili) unaoana na mtu ambaye utapata confidence ya kutembea naye,kuwa huru naye,kumtambulisha kwa watu kwamba huyu ni mme wangu au mke wangu lakini ambaye utakuwa naye na hisia za kushiriki naye tendo la ndoa kwa raha.
👉👆Si unajua kuna mtu ambaye kwako binafsi *Hakuamshi hisia,hata ungemtazama asubuhi mpaka jioni,awe amevaa au naked* hiyo ni kisaikolojia ila mwingine hata ukimuwaza tu au kuona picha yake unasikia Mahaba kupanda.
QUOTE: *_Kuna dada mmoja miaka ya nyuma kama 2013 nilimsaidia juu mahusiano yake,kija alikuwa anamfatilia yuko well off yaani amekamilika,anakazi,pesa,usafiri,nyumba,si mbaya sura ila BINTI HAISI HISIA YOYOTE YA KUMPENDA,ila kijana amemsaidia mambo mengi,pesa,gharama za chuo anampa bila kumwomba,binti aliamua kumkubali kwasababu ametumia vitu vyake japo hamuombi,yaani amemkubali kwa huruma,ila binti aliniambia hivi,SIJISIKII KUMPENDA HATA KIDOGO NA HISI HATA TUKIOANA SITA HISI WALA KUSIKIA RAHA YA KUSHIRIKI NAYE TENDO LA NDOA,NTAMPA TU AFANYE YEYE ARIDHIKE MAANA YEYE KAFA KAOZA KWANGU ILA MIMI HATA 1%HAKUNA_* Hapo ndo nikasema unaandaa bomu la DIVORCE na kuishi kwa Stress milele na hiyo yaweza kukupelekea KUCHEPUKA wakati umeokoka kutafuta mtu anaye touch hisia zako.Ni heri ufanye COSTFUL BREAK UP lakini ujuandalie amani baadaye.
*KUWA MAKINI NA MUNGU NA VIGEZO VYA KIMWILI,TUPO DUNIANI*
By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)0755444078

Friday, 15 May 2020

UVULI WA MKONO WA BWANA

🏹🏹 *USIKU WA MAOMBI NA KUOMBA UVULI WA  MKONO WA BWANA UWE JUU YETU*🏹🏹
_Na Mnenaji :Ev Elisha Kazimoto_
Whatsapp 0755444078
.............................................
_Shalom mwana wa Mungu leo nitanena nawe siri ya Bwana kwa watu wake,walio lishika Agano lake_
👉Mungu ni Mungu wa kulishika Agano lake kwa uaminifu.
👉Bwana ana wivu siku zote kwa watu wake, hataki na hapendi kuona wanaonewa.
👉Uweza wa Bwana wa kuokoa ni mkuu sana pale Ghadhabu yake inaposhuka katika nchi, *_Anao uweza wa kupiga adui,wabaya katika eneo moja na Kuwahifadhi watu wake salama walio katika Eneo moja na waovu_*
SOMA MISTARI HII KWA UTULIVU.
43 Alivyoziweka ishara zake katika Misri, Na miujiza yake katika konde la Soani. 
Zaburi 78:43

44 Aligeuza damu mito yao, Na vijito wasipate kunywa. 
Zaburi 78:44

45 Aliwapelekea mainzi wakawala, Na vyura wakawaharibu. 
Zaburi 78:45

46 Akawapa tunutu mazao yao, Na nzige kazi yao. 
Zaburi 78:46

47 Aliiharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe, Na mikuyu yao kwa mawe ya barafu. 
Zaburi 78:47

48 Akaacha ng'ombe zao wapigwe kwa mvua ya mawe, Na makundi yao kwa umeme. 
Zaburi 78:48

49 Akawapelekea ukali wa hasira yake, Ghadhabu, na uchungu, na taabu, Kundi la malaika waletao mabaya. 
Zaburi 78:49

50 Akiifanyizia njia hasira yake; Wala hakuziepusha roho zao na mauti, Bali aliiachia tauni uhai wao; 
Zaburi 78:50

51 Akampiga kila mzaliwa wa kwanza wa Misri, Malimbuko ya nguvu katika hema za Hamu. 
Zaburi 78:51

52 Bali aliwaongoza watu wake kama kondoo, Akawachunga kama kundi jangwani. 
Zaburi 78:52

53 Hao akawachukua salama wala hawakuogopa, Bali bahari iliwafunikiza adui zao. 
Zaburi 78:53

54 Akawapeleka hadi mpaka wake mtakatifu, Mlima alioununua kwa mkono wake wa kuume. 
Zaburi 78:54

55 Akawafukuza mataifa mbele yao, Akawapimia urithi kwa kamba, Na kuwakalisha kabila za Israeli katika hema zao. 
Zaburi 78:55
👉Majanga,Tufani,Magonjwa hatari,Dhoruba katika dunia(nchi )havijaanza leo tangu zama za kale zilikuwepo.
👉Ila Mungu ana kanuni yake *Hapatilizi wabaya na wema* kwa pamoja.
👉Wabaya upatilizwa kwa ubaya wao na *Wema uhifadhiwa kwa Uvuli wa mkono wake*
🏹Unaweza jiuliza inakuwaje, soma mistari hapo juu, uliwahi kufikilia *Wakati Mito inageuzwa damu Misri Waisraeli Walipata wapi maji?* Kuna Mito Haikugeuzwa damu kwaajili tu ya Taifa la Bwana.
👉Mazao ya wa Misri yalipoliwa na nzige na tunutu, Mashamba ya waisraeli hayakuguswa hata kama yalikuwa yamepakana.
👆👉 *Kilichokuwa kikifanya kazi pale ni Uvuli wa mkono wa Bwana kwa Waisraeli*
👉Mkono wa Mauti,upepo wa mauti,maangamizi yalipo pita katika nchi, wana wa Mungu,waliokusudiwa na Mungu kwaajili ya Uaminifu wao,walipewa *Angalizo,Jambo la kufanya ili wawe salama kati ya mauti inayopita* Enzi za Yoshua,Ahabu kahaba kwa kuwaficha wapelelezi aliambiwa ili awe salama wakati upanga wa mauti unapita katika mji, *Afunge kamba Nyekundu katika Dirisha la Nyumba yake* Alama ya *Uvuli wa Kuhifadhiwa* mbali na mauti wakati wa maangamizi, akaongezewa mkazo Akae ndani asitoke nje ya nyumba, na watu wake wote wanaotaka usalama wakae ndani wasitoke nje ya nyumba hiyo, na atakaye toka damu yake ikimwagika hatia itakuwa juu yake mwenyewe.
18 Angalia, tutakapoingia katika nchi hii, funga kamba hii nyekundu katika dirisha hili ulilotutelemshia; nawe uwakusanye kwako nyumbani mwako, baba yako, na mama yako, na ndugu zako, na watu wote wa nyumba ya baba yako. 
Yoshua 2:18

19 Itakuwa mtu awaye yote atakayetoka katika mlango wa nyumba yako kwenda njiani, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe, na sisi tutakuwa hatuna hatia; na mtu atakayekuwa ndani ya nyumba yako damu yake itakuwa juu ya vichwa vyetu, mkono wa mtu ukimpata. 
Yoshua 2:19
👉Unajua nini, hata sasa ziko *Kamba Nyekundu kwenye ulimwengu wa Roho* zinafungwa katika mioyo yetu, hizo ni ALAMA YA UVULI wa kutuepusha na Mabaya.
🔹Utakatifu ni kamba nyekundu
🔹Utumishi mwaminifu kwa Bwana ni kamba nyekundu
🔹Jina la Yesu ni kamba nyekundu
🔹Damu ya Yesu ni kamba nyekundu
🔹Maombi yatokayo katika moyo safi ni kamba nyekundu
🔹Imani katika Bwana na Neno lake halisi ni kamba nyekundu kwenye moyo wako.
👉Shida kubwa ya watu wa Mungu baadhi,ni *Kuruhusu Upepo wa Hofu na Vitisho kuzunguka mioyoni mwao na kuyeyusha Imani zao* Wanalia kama waio mjua Mungu waliavyo, wanasema kama wasiomjua Mungu wasemavyo..... *Kumbe nyakati za Dhaoruba wana wa Mungu wana Lugha yao tofauti na wana wa giza*
👉Sasa kazi ya wana wa Mungu ambao tumeambiwa tufunge Kamba nyekundu kwenye madirisha ya mioyo yetu,maombi yetu kwa Bwana ni kumwambia Bwana *_Tunaomba Uvuli wa mkono wako utufunike na utuhifadhi katika nyakati mbaya_* Mungu ni mwaminifu atatuhifadhi,atatuficha,nyakati za Tauni,dhoruba,vitana njaaTutapita katikati yake na Kuvuka salama, *Unachotakiwa ni Kulisikia na Kuliamini Neno la Bwana* Ukiliamini kuna uponyaji na ushindi.
39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. 
Yohana 11:39

40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? 
Yohana 11:40
👉👆Amini, Amini Ushindi Upo....Ingia kwenye maombi sasa sema na Mungu,haijalishi Kuna historia gani juu ya tatizo lako, wewe Amini tu.
*_Mungu akubariki,ulikuwa nami mnenaji wako Ev Elisha Kazimoto(0755444078)_*

Wednesday, 13 May 2020

MAVAZI NA MAPAMBO

👖🥻 *MAVAZI KWA WALOOKOKA LIMEKAAJE?*🥻👖
*_Mtu ameuliza swali katika group la whatsapp hili hapa,.....Wapendwa mie Nina swali kidogo kuhusu mavazi kwa mtu aliyeokoka, Avaeje,Mavazi yapi yanaruhusiwa kuvaliwa kwa mlokole?_*
..................................................
Anajibu Mtumishi wa Mungu *_Ev Elisha Kazimoto_* 
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
_Shalom wapendwa wote mnaoamini katika Neno la Mungu na katika Wokovu,huu mjadala wa Mavazi na Mapambo si waleo,unasumbua wengi sana vichwa,ila leo Sitatumia Andiko la Biblia ila nitakupa HEKIMA ZA ROHO MTAKATIFU kama msimamizi wa Mioyo yetu wanadamu hasa Tuliookoka_ Karibu tujifunze:
*MAVAZI,MAVAZI,MAVAZI*
👉Suala hili linawapa shida Wakristo wengi,ila ni walio wachanga kiroho,au ambao hawajaonja Utamu wa juu wa Mungu baba,lakini hili ni jambo Jepesi sana kwa mtu aliyeokoka ila kwa ambaye hajaokoka ni chamgamoto kubwa au kwa mchanga kiroho au kwa mtu ambaye amekoka sawa ila bado anakiwango cha kawaida sana.
*Nitawapa Siri moja na Wala usije ingia katika mijadala ya Mavazi ikakuumiza kichwa, wasaidie watu Wamjue Mungu kwa Viwango vya juu*
Utakuwa umemaliza ubishi na mijadala ya Mavazi na Mapambo.
👉Kwanza hakuna Vazi Maalumu lililoanishwa kwenye Biblia kuwa la Mtu aliyeokoka(kama ilivyo Kanzu kwa Waislamu au buibui)
👉Pili Tunatofautiana tamaduni kutoka jamii moja na nyingine kwa hiyo ni vigumu kuhukumu vazi husika.
*HIVYO BASI, UKWELI NI HUU*
👉Mungu anafanya kazi na watu NADHIFU(hiyo utaikuta kwenye Biblia)ndoa maana kufua mavazi,lugha za mavazi safi ziko nyingi kwenye Biblia.
👉Lakini pili, Mungu (Bwana Yesu)amejitambulisha ni Bwana wa Mabwana, Mfale wa Wafalme, Mtakatifu, Mungu wetu, Baba yetu kwa sifa hizo tu *Zinakupa Akili ya kujua mimi kama mtoto wake,mtumishi wake, NITOKE vipi kimwonekano ili KUMWAKILISHA katika sifa zake* 
👉Mfano mdogo tu, *_Tutashangaa na kubaki kujiuliza,na kulaani endapo tutamkuta mtoto wa Rais yuko rafu,amevaa ovyo ovyo,kwa nini itazua gumzo NI MTOTO WA NANI,ila akivaa mtoto wa mkulima au wa mtaani tutaona kawaida,ni mazingira yake_* Kwa hiyo sisi tukiookoka Tunaongozwa kimavazi na STATUS YA MUNGU WETU katika kuvaa.
👉Sasa itashangaza mtu Anahoji NIVAE VIPI WAKATI ANAJUA ANATOKEA FAMILIA IPI,NA WATU WANAITAZAMA NA KUITAFSIRI VIPI HIYO FAMILIA,tutakacho jua kwa mtu huyo ni HAJUI STATUS YA FAMILIA YAKE KWAKE NA MBELE ZA WATU. Kosa hajui status ya baba yake na cheo chake kwa watu na huyo ni MTOTO(Because hata mtoto wa rais wa mwaka 1,2 kukaa na Tope na mkojo ikulu au kwa watu aliko baba yake hataona shida maana hajui,mpaka walezi wamkamate na kumbadirisha mavazi ili afananie ufalme) na ndicho kinacho fanyika makanisani *Kukemea mavazi ya aina flani ni Kumshika mtoto mchanga mwenye mikojo atoke sebuleni arudi chumbani avae kulingana na hadhi ya baba yake ndo aje sebuleni(kanisani)*
👉Sasa Iko hivi,Ukisha okoka unapewa Roho mtakatifu,huyo *Atakufundisha kuvaa,kuongea,kufanya maamuzi yote* kuna mambo atakwambia hili HAPANA ulilifanya sawa ila kwa sasa NO haliendani na Hadhi ya Ufalme uliomo.
👉Mengine siyo dhambi ila atakwambia USIFANYE, Shida ya waliookoka UNA KIWANGO HICHO CHA KUMSIKILIZA ROHO MTAKATIFU NA KUMFUATA ANAVYO KUELEKEZA? Hapo ndo kuna shida.
👉 *Shida siyo kuambiwa Suruali kwa mwanamke ni ruksa au siyo ruksa,kusuka,kuvaa wigi au kuto vaa ni dhambi au siyo dhambi na mambo mengine yanayowachanganya watu makanisani na kuzua mijadala, Shida ni Hivi Umemjua Mungu wako aliyekuokoa kwa Kiasi gani* na Kiongozi uliyepewa Roho Mtakatifu unamtunza na kumsikiliza anavyokushauri?
👉Si kila jambo utakikuta kwenye Biblia unaambiwa Fanya au Usifanye, ndio maana tuliookaka tunasema Kumcha Bwana ni ZAIDI YA KUSHIKA AMRI 10,wokovu ni zaidi ya amri 10.Ukitembea na Amri 10 tu utakuwa mchanga kiroho mpaka unaingia kaburini na mbingu utaikosa ila shetani atakushinda.
NB: *_Ni hitimishe kwa kusema suala la mavazi na mapambo ukitaka kuliweka sawa iwe kanisani au maishani mwako,Fundisha watu au wewe jifunze, Ongeza Viwango vya Kumjua Mungu na Kumweshimu Mungu na Kumsikiliza Roho mtakatifu, Utavaa,utajipamba sawa sawa na Heshima ya ufalme wa Mungu na Hutahukumiwa na Mwanadamu wala Mungu na kwenye foleni ya kuhesabu namba kuingia mbinguni utakuwa front line_*
NI USHAURI WA KIUTUNISHI NA EV ELISHA KAZIMOTO
Whatsapp 0755444078

Thursday, 19 March 2020

PESA (MSHAHARA KATIKA NDOA)

💎💎 *PESA (MSHAHARA KATIKA NDOA) NI SUMU NA NI UPONYAJI*💎💎
_Anachambua mwanasaikolojia na Mshauri na Mtumishi wa Mungu *Ev Elisha Kazimoto* fuatana naye ujiongezee ulinzi wa ndoa yako_
................
................
*MFUMO WA KIUCHUMI KATIKA NDOA UNAOWEZA KULETA AMANI YA NDOA NA MAENDELEO YA FAMILIA*
_Uchumi(pesa )katika familia kwa wana ndoa imekuwa changamotl ya wengi,kiasi kwamba watu wanaishi kana kwamba ni *Watu waliokutana forb Part time* siyo wanandoa,na kana kwamba ni washirika wa muda katika ndoa na si wana ndoa wa kudumu_
👉Hii changamoto imekuwa kubwa sana hasa *Kwa Wafanyakazi na wafanya biashara ambao wote mke na mme wana kipato binafsi* hawa ndo wana maisha mabaya ya kindoa na kiroho.
👉Pesa kwa wana ndoa imekuwa Sumu ya kuwagawa na kuwafanya wawe  watu wawili ndani ya mmoja.
👉Shida kubwa hapa Siyo Pesa, *Shida ni Akili ya Kindoa* ndiyo imekosekana.
👉Kuna watu wanaingia kwenye ndoa wakiwa :
🏹Hawajakomaa kisaikolojia na Kiakili kwaajili ya ndoa(kuna kukomaa kiumri ila usikomae kiakili)
🏹Wanaingia kwenye ndoa bila kujua *Falsafa ya Mungu kuhusu ndoa*(Si wawili tena bali mwili mmoja), hiyo ya kwanza......Kwa hiyo watu wanaingia kwenye ndoa *Anaendelea kujiona yeye mwenyewe baada ya kumuona mwenzake* kwa hiyo wanaishi Kama watu wawili tofauti wenye agano la kuwa mmoja.
🏹Falsafa ya pili, Mungu amesema *Mtu ataacha baba yake na mama yake,naye ataambatana na mmewe*(Wengi wakiingia kwenye ndoa Hawaachi wazazi wao au ndugu zao kisaikolojia,kimwili wanakuja nao)ndiyo maana wanaendeleza ubinafsi wa kuwaza juu ya familia yake yeye kama yeye na si wawaze pamoja (mke na mme)juu ya familia zao.
🏹 *Sasa nisikilize kidogo hapa shida ya wana ndoa wenye vipato wote kwa nini ndoa zao ni changamoto, zaidi ya ndoa za maskini au za mtu mmoja mwenye kipato....*
1⃣Ukishindwa kujua *Ukishaoa au olewa unaanzisha Taasisi mpya* inayokuhusu wewe na mwenzako TU( ikiwa nzuri ni heshima kwako,na ikiwa mbaya ni dharau kwako) jua ya kwamba Utakuwa miongoni mwa walioolewa au oa bila kukomaa Akili na lazima ndoa yako italeta shida.
🏹Kwa hiyo basi Kama umeoa na kuolewa jua ya kwamba *KIPATO CHAKO, LENGO LA KWANZA NI KUJENGA TAASISI YAKO MPYA NDOA* wengine wazazi,ndugu, kazi ya Mungu vinafuata hapo.(Ukikosea hapo ukahisi KIPATO CHAKO ni kwaajili ya kusaidia wazazi,ndugu,na kujipamba,jua wewe ni Miongoni mwa watu ambao ulikuwa bado mchanga kuingia kwenye ndoa,au Hukujaliwa akili ya Kimaisha na uwezi kuwa na future ya maendeleo na baraka za Mungu)
*Note:Ukioa au Ukiolewa, kipato chako ni kwaajili ya Kujenga Heshima ya Taasisi mpya uliyoiingia* na Taasisi ya ndoa Haijengwi na mtu mmoja,inajengwa na wawili,mmoja akijichomoa na kuona mmoja(mme au mke)ndo atumie kipato chake kujenga Taasisi ya ndoa,jua *Ulioa au uliolewa na Mlemavu wa Akili* asiyeweza ku make future nawe, kwa hiyo suluhisho siyo kumwacha, ni kwenda na mzigo huo mpaka Mungu akusaidie au atakapofundishika,au Uamue kumfundisha kwa vitendo.(hilo ni somo lingine)
2⃣ *Ukishindwa kujua kuwa kwenye ndoa ( Ya watu wenye Akili) vipato na vitu vyote ni vya kwenu siyo vyako(uwe ni mshahara au biashara) jua kuwa Wewe bado ulifaa kuishi peke yako au na ndugu zako siyo mme au mke*
🏹Kuna maajabu ya wana ndoa kila mtu na mshahara wake,na matumizi yake,kiasi kwamba hakuna anaye ruhusiwa kuingilia kioato cha mwenzake, hata mmoja akiishiwa *Ataomba kukopeshwa na Mwenzake*(wana ndoa hao) Hii ni ndoa ambayo ni marehemu anaye tembea,lakini hawawezi kuenjoy maisha ya Raha ya ndoa,wataishi kwasababu wanaweza kuishi kwa nguvu ya pesa siyo nguvu ya Mahaba.
🏹 Wana ndoa yenye wafanyakazi wawili wenye vipato au wafanya biashara wote wana kipato, wanafursa ya kufanya mambo makubwa kwa mafanikio na amani zaidi.
🤝 *Kuwa wazi kwa kipato chako kwa mwenzako,muwe na asilimia mlizokubaliana za jumuisho la pesa za kufanya mambo ya familia,na asilimia zingine mtu anaweza fanyia private issues au kwa kumsurprise mwenzake* 
🏹Ni upagani na utoto wa akili, kuficha kipato chako kwa mwenzako kwa kisingizio cha *Kipato chako ni cha mambo yako mwenyewe na familia yako* wewe hukufaa kuoa au kuolewa, (NDOA NI COMMUNAL OWNERSHIP SIYO CAPITALIST SYSTEM (PRIVATE OWNERSHIP )
🏹Kinachoondoa amani kwa ndoa nyingi ni UMIMI KATIKA UCHUMI, suala la kusaidia wazazi na ndugu zenu ni suala la mipango ya pamoja kuangalia kipato chenu kwa ujumla na ni kiasi gani mwaweza tenga kusaidia familia zenu.
*NB: Wadada mnaofanya kazi na biashara hamjaolewa kuweni makini sana na dhana ya mme ndo anawajibu kutunza familia,na kipato chako ni kwaajili ya kujiremba na wazazi wako na ndugu zako,huo ni utoto na ushetani wa kuipundua kanuni ya Mungu ya kuwa kitu kimoja na kushindwa kuleta maendeleo*
🏹Lakini wavulana kabla ya kuoa au kuolewa *Dadisi sana kujua mtazamo wa mchumba wako kuhusu matumizi ya kipato chake,ukihisi dalili za ubinafsi wa kipato Huyo siye mke ni Mshirika wa mapenzi PIGA CHINI,bora uoe mpika vitumbua na chapati*
🏹Kuna mabinti uwa wana lugha ya Unaoa mimi *Huoi mshahara wangu* mshahara wangu utatunza wazazi walionisomesha, Hawa mara nyingi uwa wanachelewaga kuolewa kisaikolojia na Kimungu,uangukia mikononi mwa wanaume jeuri kimakusudi,ili wanyooshwe.
🏹Ni hakika mwanaume ndiye Anawajibu wa Kuhakikisha familia inasonga, je wewe mwanamke kama mratibu mkuu na msaidizi wa mfumo mpya kazi yako nini? Ni kuhakikisha mmeo Halemewi lakini unaweka mazingira ya kuchochea Maendeleo na mafanikio ya familia yenu.(Kumbuka nanyi mtazeeka,mtakuwa na watoto na wajukuu) mnavyochelewa kuunganisha nguvu pamoja ili mkimbie kimafanikio,ndivyo mtakavyo lemewa kubeba familia.
*MWISHO OA AU OLEWA NA MTU MWENYE AKILI JUMUISHI SI AKILI BINAFSI NDO MTATOBOA KIUCHUMI,KIROHO NA KISAIKOLOJIA*
By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist and Counselor )