*Sehemu ya Pili ya Somo, Kama Ukijitambua Kama Mdada wa Thamani, Utapata Mme Haraka*
_Uko naminenaji Ev Elisha Kazimoto(Psychologist )_
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
e-mail babaeve755@gmail.com
.................
Karibu tuendelee....
👉 *Kazi yako kama Dada Tengeneza na Ongeza Thamani yako*👈
1⃣Tengeneza Status yako ya *Kiroho* kama Dada uliyeokoka.
👉Unajua maisha ya Kiroho ndiyo yanayo vuta mambo ya kimwili.
*2 Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, kama vile roho yako ifanikiwavyo. 3 Yohana 1:2*
👉Ukiona unazembea kwa mambo ya kiroho,jua unachelewesha muujiza wako wa kimwili(mmeo)
👉Thamani yako ya kiroho inapopanda *Inavuta muujiza wako kimwili*
👉Unahitaji kila siku mwana dada ujue kwamba *Thamani yako inawindwa na shetani na mawakala wake* ili ishushwe,na upoteze NDOTO NA MATUMAINI ya kuingia katika ndoa ya baraka.
👉Kwa sababu hiyo hakikisha kila siku unaongeza uwezo na unalinda njia zako zote za ubinti wako.
*1 Yeye asetaye vipande vipande amepanda juu mbele ya uso wako; zishike silaha, ilinde njia, vitie nguvu viuno vyako, uongeze uwezo wako sana.Nahumu 2:1*
👉Wadada wengi wamejisahau katika kulinda THAMANI ZAO, wanaishi wanavyotaka, siyo kikanuni, jambo lililopelekea Kupoteza thamani zao kirahisi.
👉Kumbuka thamani ikishuka,na matumaini ya kupata mtu sahihi yanapotea, *na uwezo,nguvu ya kutafutwa na mtu sahihi inapotea*
👉Kazi yako ni Kuongeza Thamani yako, *Watafutaji wanatafuta vitu Unique vyenye Thamani*
👉Sasa kazi yako ni kuanza kutengeneza Status yako kiroho,uone jinsi ilivyo na nguvu ya kuvuta mambo inayo tamani maishani.
👉Twende pamoja katika kuangalia Status muhimu za kukazania kuwa nazo kiroho:
👏 *Status za Kiroho za kukuvuta karibu na mmeo*👏
🔹 *Tengeneza sifa ya kuwa Mwombaji* Miongoni mwa sifa kuu ya mdada(na mwanamke mtarajiwa mama wa familia )ni Kuwa mwombaji,hiyo ni kibiblia.
👉Maombi yatakufanya uwe karibu na Mungu lakini maombi yatakufanya uwe na uwezo wa kutambua wanaume feki na mwanaume sahihi wa kukuoa wewe.
👉Sikiliza wewe ni dada mtafutwaji, waweza kuja watu 20 wote wako vizuri kimwonekano,ila hawawezi kuwa waume zako wote 20,yupo mmoja utamjuaje? Ni namna unavyokaa magotini,penda kufunga,kuomba jiombee na mwombee mmeo mtarajiwa.
🔹 *Tengeneza Statu ya Kuishi Maisha Matakatifu yasiyo na michanganyo* Miongoni mwa vitu vinavyoweza kukupa kibali mbele za Mungu cha kupata mtu sahihi ni wewe kulinda maisha yako yasichafukiwe na dhambi au makosa na uchafu wowote.( *Hii inawashinda wengi*)ila wewe jipange kushinda.
👉Usiwe wa kujirahisisha kiasi kwamba *_Mwili wako unajulikana kwa kila kijana,maeneo yako yote muhimu ya mwili yanajulikana,hisia zako zinajulikana kwa kila mmoja_* Weka Distance ya Kusaidia Mwili wako Uheshimiwe.
👉Usifurahie sana kushikwa na kila mmoja,( *Kushikwa sehemu za mwili kuna Raha yake,unasikia kuburudika ila KUNA GHARAMA YAKE*)itakusumbua,itakuchelewesha baraka zako au kupoteza kabisa muujiza wako.
👉Sasa ni heri ukaweka msimamo usio badirishwa na mtu yeyote awe mchumba wako au rafiki,ni heri akakuchukia au urafiki n auchumba ukavunjika lakini umelinda STATUS YAKO na utakatifu wako ambavyo ni nyenzo ya kukuletea mme sahihi.
👉Ila ukiwa simple kwa kila mtu, *Huyu atashika,atachezea sehemu zote,mwingine hataishia kuchezea atazama ndani kabisa na kuvunja Agano lako na Mungu na Mmeo* hapo ndo Utatamani usiku uwe mchana na mchana uwe usiku.(Ujui gharama zake na bora usijue kama bado ujakutana na changamoto hizo omba zisikukute ongeza umakini).
🔹 *Tengeneza Status ya Huduma,utumishi kwa Bwana* Ni hatari na hasara kwako dada upo kanisani upo upo tu, ni mpiga makofi na kucheza sifa na kurudi nyumbani, aisee mume utamtafuta kama sindani katikati ya takataka.
👉Dada kanisani pawe kama nyumbani kwenu, hakikisha *Una Huduma ambayo mpaka kanisa hata watoto wa sunde school wanajua hii uwa ni Huduma ya Dada Joyce,Mary,Happy nk* na usipoonekana siku hiyo kanisa zima linajua kuna mtu hayupo leo.
👉Pambana na huduma zote bila kudharau kama kudeki vyoo, kanisa, kwa mchungaji,uimbaji,ushemasi nk fanya kwa jasho lako la mwisho na kwa kupenda na kujitoa, huduma kazi yake *Ni kukutangaza na kukufunua kwa watu na kukupa kibali* ukiifanya kwa moyo na kwa bidii aloo utaonekana haraka.
👉Hatufanyi huduma ili tuonekane,au tuolewe ila tunafanya kwamba tunampenda Bwana lakini huko huko ndo tunakutana na mahitaji yetu.
🔹 *Tengeneza Status ya Kujifunza Neno la Mungu, Kuhudhuria Ibada* Usifanye makosa ya kuwa Empty Vessel,dada huna hata mistari ya biblia 10, soma neno, nenda kanisani kwenye ibada,idara nk,usiwe mtu wa kuonekana mara moja kwa wiki, wewe utakuwa hujajipanga kupokea baraka zako za mme.
👉Ibda kwako iwe LAZIMA siyo ya Muhimu tu. Huko ndiko utakako kutana na majibu ya maombi yako na mtu wako.
👉Mpe Mungu kipaumbele na yeye atahusika kwenye mambo yako.
*_Mwisho wa sehemu ya pili ya somo letu, tukutane katika sehemu ya Tatu ambapo nako kuna siri nyingine nyingi za kukufanya uwe mdada wa Viwango_*
Mnenaji alikuwa Mtumiahi wa Mungu *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist )*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail babaeve755@gmail.com
No comments:
Post a Comment