Saturday, 13 June 2020

DADA JITAMBUE(PART IV)

*Sehemu ya Nne ya Somo, Ukijitambua kama Dada wa Thamani, Utapata Mme Haraka*
_Mnenaji ni mimi *Ev Elisha Kazimoto*(Psychologist )_
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail :babaeve755@gmail.com
.........................
Karibu Tuendelee......
👉Hautaweza kupata Mme wa Viwango kama Unajiweka ovyo ovyo kimwili,huna maadili,huna staha,hujiheshimu, wewe umekazana na kuomba tu,hupati mme, Tengeneza status za kimwili zinazo vutia ili kila akuonaye kabla hajaanza kuona vitu vya kiroho vinavyo kutoka vya Kimungu basi aone Peesonality yako na Tabia zako za kimwili zinamfaa wewe kuwa mke wake
5. *Heshima na Adabu* Dada kaa ukijua pamoja na status ya kiroho,kuwa mwombaji,muimbaji,muhubiri nk,havikupi mme bila kuwa na combination ya status za kimwili,.
👉Miongini mwa status muhimu ni wewe dada kuwa na Heshima na Adabu kwa watu.
👉Heshima na adabu yako itakupa kibali kwa watu itakutangaza kwa watu,watu watatamani kuwa karibu nawe lakini kukumili.
👉Waweza kuwa na kopato,elimu,huduma kubwa ya kiroho ila ukiwa na jeuri,kiburi,dharau aisee utaishia kuitwa SHANGAZI WA KANISA,wadogo zako woote wataolewa ila wewe uta SUGUA BENCHI,hapo hakuna pepo, pepo ni Tabia yako.
👉Heshimu mwenye kipato kidogo,kikubwa,wazuri kwako na wabaya kwako,huwezi jua kwamba unaye mdharau ndo anaweza kuwa kiunganishi cha mmeo mtarajiwa au akakata muunganiko wako na mmeo mtarajiwa.
6. *Jenga jina Mahali ulipo zaliwa(Unako tokea)na Jenga jin Ugenini*
👉Kuna watu ujisahau sana, wengi wetu tuliko zaliwa na kukulia ni tofauti na tunakoishi sasa mpaka tunapata wenzi tunawapa mbali na tuliko kulia  na kulelewa.
👉Unajua nini, watu wengi wanajenga Jina waliko sasa wanaonekana watu wazuri sana *Ila kwao,aliko kulia wanamjua kama mtu ovyo,hafai,aambiliki,mvivu,mchafu,kahaba* kumbuka ukimpata mchumba LAZIMA MTARUDI KWENU, vipi familia na mdugu zako na majirani watakusemeaje wewe kwa mwenzako na ukweni kwako?
👉Na wengine nyumbani kwao na majirani wanamjua mtu mwema,mpole,mtakatifu,mtu wa watu,ila kumbe *Kule anakoishi sasa, watu wanajiuliza hivi huyu Alizaliwa na mwanamke au ni pepo flani limevaa mwili* haya mambo yatakuharibia hata ukijificha itakuumbua.

7 *Ishi Maisha yako Halisi, Acha Kukopi kopi(Artificial life)*
👉Wewe ni mdada wa aina flani,ishi kama wewe usiishi kama flani, tafuta uhalisia wako ndo utaishi maisha ya maana na ya furaha na watu watakupenda kwa namna ulivyo.
👉Ukiishi sawa sawa na wewe ulivyo NATURE YAKO,utafanya mambo kwa ubora na uzuri ila ukiwa unaishi kwa kukopi flani utakuwa unjitesa sana kulazimisha ufanane na flani, wewe siyo flani wewe ni wewe.
👉Yaani na maanisha, _Kuwa na tabia yako kama ulivyo lelewa,heshima ya kwako,ongea ya kwako,matumizi ya pesa ya kwako,vaa ya kwako, ukitaka kuwa kama flani utajikuta kila siku unakosea na kujutia,unatamani kuishi kama flani ambaye anauza mwili wake kila siku ana wanaume 7 kila mmoja anaonga, wewe huna halafu unahitaji uvae,ule,utoke out nk kama yeye utakosea na status yako itashuka_
👉Jikubali kama ulivyo, pambana kuongeza status yako,utaishi maisha yenye radha,yasiyo na majuto au mashariti magumu, au maumivu ya kutendwa.
👉Hakuna raha na ujasiri mkubwa kama mwana dada kuolewa na Heshima yako,hakuna anayekunyoshea vidole vya *Huyo hamna kitu* ina leta raha,inakufanya ujione Malkia kwa mmeo lakini utaheshimika.
*_Mpaka hapo ni seme Mungu akubariki,tukutane katika sehemu yetu ya Tano na ya mwisho katika Somo hili, mnenaji alikuwa mimi Mtumishi wa Mungu Ev Elisha Kazimoto(Psychologist )_*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail :babaeve755@gmail.com

No comments:

Post a Comment