Saturday, 13 June 2020

DADA JITAMBUE(PART 1)

🧏🏻‍♀️🧏🏻‍♀️ *UKIJITAMBUA KAMA MDADA WA THAMANI,UTAPATA MME HARAKA*🧏🏻‍♀️🧏🏻‍♀️
_Shalom wadada wa Yesu Kristo,leo nizungumze na mdada mmoja baye leo anataka afumbuke macho yake aone kile ambacho nakiona kwake( *Umeumbwa kwaajili ya Mtu flani Special*) haukuja tu duniani, Una mwenzako special_
*By Ev Elisha Kazimoto(0755444078)*
...............................................
🧏🏻‍♀️Mara nyingi tunakosea katika Kujitazama si katika kutafuta vitu.
🧏🏻‍♀️Nguvu kubwa ya kutafuta,tungeiwekeza katika Kujitazama kama Mungu anavyo tutazama basi, ni rahisi sana kupata kile ambacho unakitamani( Ubavu wako).
🧏🏻‍♀️Unajua tangu ulipoumbwa na Mungu tumboni mwa mama yako, *_Ulikuwa unaumbwa kwaajili ya mwanaume wako_* wewe ukuumbwa ili uzunguke ukitafuta mtu,ila uliletwa Duniani kwaajili ya Mtu(mmeo).
*Hata lini utatanga-tanga, Ee binti mwenye kuasi? Kwa maana Bwana ameumba jambo jipya duniani; mwanamke atamlinda mwanamume.Yeremia 31:22*
🧏🏻‍♀️Popote alipo Rais lazima Mlinzi awepo(na popote alipo mwanaume jua mwanamke anahitajika) *Huyo mwanamke anaye hitajika ni wewe(dada)*
🧏🏻‍Baada ya kuja duniani unacho hitaji kuwa nacho ili *Upelekwe,ukutanishwe na mmeo ni Wewe Kuishi kwa Thamani yako uliyoumbwa nayo*
🧏🏻‍♀️Kinacho weza kukuwaisha kwa mmeo au kukuchelewesha kukutana na mmeo ni LEVEL YA THAMANI YAKO.
🧏🏻‍♀️Kila anayeingia katika ndoa anaingia kwa kiwango cha thamani yake kupanda.
🧏🏻‍♀️Siri ni kubwa, *Watafutao hawatafuti sura au jinsia ya kike, Wanatafuta THAMANI ndani ya jinsia ya Kike inayoweza Kutunza VISION aliyo nayo mwnaume* 
🧏🏻‍♀️Na hata siku moja Hakuna ambaye utafuta kununua au kupata kitu cha Thamani ya CHINI, au kibovu,wanatafuta Kitu cha Thamani ya juu.
🧏🏻‍♀️Na ukiona mtu anatafuta kitu cha thamani ya chini jua na yeye ni wa Thanani ya chini zaidi ya wewe unaye tafutwa.
πŸ‘‰Unahitaji mtu wa Viwango katika maisha yako, hakikisha unaongeza viwango vyako vya thamani yako.
*_Hii ni sehemu ya kwanza ya somo hili kati ya sehemu 5 zilizobeba somo hili usikose sehemu ya pili, Ulikuwa nami Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa EV ELISHA KAZIMOTO (Psychologist )_*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail babaeve755@gmail.com

No comments:

Post a Comment