🔹🔹 _Swali: Nitumie vigezo vya kiroho au kimwili kuchagua mwenzi wa maisha?_🔹🔹
Anajibu mchambuzi wa masuala ya Kimahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)*
Whatsapp 0755444078
*NDOA NI 50%KIROHO NA 50%KIMWILI KUWA MACHO ONGEZA UWEZO WA MAARIFA*
👉Labda nifafanue dhana hii ili kuwasaidia vijana na wanandoa wote ili kulinda amani,furaha na upendo kati ya COUPLES za wapendanao.
👉Tunasema ndoa ni 50%kiroho kwa sababu Mungu ndo mwanzilishi wa Ndoa,hatuingii kwenye ndoa tuonavyo sisi,ila kwa mapenzi ya Mungu ili tulitimize kusudi la Mungu.
👉Kwa maana hiyo tunahitaji lumihusisha Mungu sana kila hatua *_Wakati wa kutafuta,baada ya kimpata,na wakati wa kuishi naye_* Mungu ahusike ili kuwahifadhi mkae katika amani,furaha na upendo kati yenu
👉Sababu nyingine ya kumuhusisha Mungu kila hatua ni ili kujenga ukuta wa kimdhibiti adui kuwavamia na kuharibu uchumba na ndoa yenu.
5 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote, Wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
Mithali 3:5
6 Katika njia zako zote mkiri yeye, Naye atayanyosha mapito yako.
Mithali 3:6
👉Pili nimesema ndoa ni 50% kimwili, kwasababu hatuishi Mbinguni,tunaishi duniani na tumepewa *_Akili na Utashi wa kujua mema,zuri,baya na kubaini vitu vipendezavyo na vichikizavyo_* kwakuwa tumepewa Ujuzi wa Kimungu wa kiutashi wa kubaini kinachotufurahisha hapa duniani nafsi zetu Mungu alitupa Fursa ya Kuchagua.Ili katika uchaguzi huo tuyatumikie matokeo ya uchaguzi wetu bila kulalamika.
*_Unajua kwa nini? Asilimia 100 za kuchaguliwa na Mungu ziliishia kwa Adamu,alipo chaguliwa na Mungu baadaye alimualaumu Mungu kwa alichompa_*
11 Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa u uchi? Je! Umekula wewe matunda ya mti niliyokuagiza usiyale?
Mwanzo 3:11
12 Adamu akasema, Huyo mwanamke uliyenipa awe pamoja nami ndiye aliyenipa matunda ya mti huo, nikala.
Mwanzo 3:12
👉Baada ya hapo Mungu akaweka Nafasi ya wewe mwanadamu(Kija au binti)Muulize Mungu akushauri katika uchaguzi wako,yeye awe na sehemu yake na wewe uwe na sehemu yake.
👉 *Kwa maana hiyo unapomwomba Mungu naye Mungu anajua unatamani vigezo gani vya Kimwili atakupa mtu unaye mtaka kama anaona anakufaa ila vigezo vinaweza visiwe vyote ulivyotaka lakini Mungu pia anaheshimu vigezo vyako kama UMEANZIA KWAKE*
Kwa hiyo omba,angalia kwa macho nani akupendezaye kwa macho na moyo wako.
👉Lakini kisaikolojia (kimwili) unaoana na mtu ambaye utapata confidence ya kutembea naye,kuwa huru naye,kumtambulisha kwa watu kwamba huyu ni mme wangu au mke wangu lakini ambaye utakuwa naye na hisia za kushiriki naye tendo la ndoa kwa raha.
👉👆Si unajua kuna mtu ambaye kwako binafsi *Hakuamshi hisia,hata ungemtazama asubuhi mpaka jioni,awe amevaa au naked* hiyo ni kisaikolojia ila mwingine hata ukimuwaza tu au kuona picha yake unasikia Mahaba kupanda.
QUOTE: *_Kuna dada mmoja miaka ya nyuma kama 2013 nilimsaidia juu mahusiano yake,kija alikuwa anamfatilia yuko well off yaani amekamilika,anakazi,pesa,usafiri,nyumba,si mbaya sura ila BINTI HAISI HISIA YOYOTE YA KUMPENDA,ila kijana amemsaidia mambo mengi,pesa,gharama za chuo anampa bila kumwomba,binti aliamua kumkubali kwasababu ametumia vitu vyake japo hamuombi,yaani amemkubali kwa huruma,ila binti aliniambia hivi,SIJISIKII KUMPENDA HATA KIDOGO NA HISI HATA TUKIOANA SITA HISI WALA KUSIKIA RAHA YA KUSHIRIKI NAYE TENDO LA NDOA,NTAMPA TU AFANYE YEYE ARIDHIKE MAANA YEYE KAFA KAOZA KWANGU ILA MIMI HATA 1%HAKUNA_* Hapo ndo nikasema unaandaa bomu la DIVORCE na kuishi kwa Stress milele na hiyo yaweza kukupelekea KUCHEPUKA wakati umeokoka kutafuta mtu anaye touch hisia zako.Ni heri ufanye COSTFUL BREAK UP lakini ujuandalie amani baadaye.
*KUWA MAKINI NA MUNGU NA VIGEZO VYA KIMWILI,TUPO DUNIANI*
By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)0755444078
No comments:
Post a Comment