Friday, 15 May 2020

UVULI WA MKONO WA BWANA

🏹🏹 *USIKU WA MAOMBI NA KUOMBA UVULI WA  MKONO WA BWANA UWE JUU YETU*🏹🏹
_Na Mnenaji :Ev Elisha Kazimoto_
Whatsapp 0755444078
.............................................
_Shalom mwana wa Mungu leo nitanena nawe siri ya Bwana kwa watu wake,walio lishika Agano lake_
👉Mungu ni Mungu wa kulishika Agano lake kwa uaminifu.
👉Bwana ana wivu siku zote kwa watu wake, hataki na hapendi kuona wanaonewa.
👉Uweza wa Bwana wa kuokoa ni mkuu sana pale Ghadhabu yake inaposhuka katika nchi, *_Anao uweza wa kupiga adui,wabaya katika eneo moja na Kuwahifadhi watu wake salama walio katika Eneo moja na waovu_*
SOMA MISTARI HII KWA UTULIVU.
43 Alivyoziweka ishara zake katika Misri, Na miujiza yake katika konde la Soani. 
Zaburi 78:43

44 Aligeuza damu mito yao, Na vijito wasipate kunywa. 
Zaburi 78:44

45 Aliwapelekea mainzi wakawala, Na vyura wakawaharibu. 
Zaburi 78:45

46 Akawapa tunutu mazao yao, Na nzige kazi yao. 
Zaburi 78:46

47 Aliiharibu mizabibu yao kwa mvua ya mawe, Na mikuyu yao kwa mawe ya barafu. 
Zaburi 78:47

48 Akaacha ng'ombe zao wapigwe kwa mvua ya mawe, Na makundi yao kwa umeme. 
Zaburi 78:48

49 Akawapelekea ukali wa hasira yake, Ghadhabu, na uchungu, na taabu, Kundi la malaika waletao mabaya. 
Zaburi 78:49

50 Akiifanyizia njia hasira yake; Wala hakuziepusha roho zao na mauti, Bali aliiachia tauni uhai wao; 
Zaburi 78:50

51 Akampiga kila mzaliwa wa kwanza wa Misri, Malimbuko ya nguvu katika hema za Hamu. 
Zaburi 78:51

52 Bali aliwaongoza watu wake kama kondoo, Akawachunga kama kundi jangwani. 
Zaburi 78:52

53 Hao akawachukua salama wala hawakuogopa, Bali bahari iliwafunikiza adui zao. 
Zaburi 78:53

54 Akawapeleka hadi mpaka wake mtakatifu, Mlima alioununua kwa mkono wake wa kuume. 
Zaburi 78:54

55 Akawafukuza mataifa mbele yao, Akawapimia urithi kwa kamba, Na kuwakalisha kabila za Israeli katika hema zao. 
Zaburi 78:55
👉Majanga,Tufani,Magonjwa hatari,Dhoruba katika dunia(nchi )havijaanza leo tangu zama za kale zilikuwepo.
👉Ila Mungu ana kanuni yake *Hapatilizi wabaya na wema* kwa pamoja.
👉Wabaya upatilizwa kwa ubaya wao na *Wema uhifadhiwa kwa Uvuli wa mkono wake*
🏹Unaweza jiuliza inakuwaje, soma mistari hapo juu, uliwahi kufikilia *Wakati Mito inageuzwa damu Misri Waisraeli Walipata wapi maji?* Kuna Mito Haikugeuzwa damu kwaajili tu ya Taifa la Bwana.
👉Mazao ya wa Misri yalipoliwa na nzige na tunutu, Mashamba ya waisraeli hayakuguswa hata kama yalikuwa yamepakana.
👆👉 *Kilichokuwa kikifanya kazi pale ni Uvuli wa mkono wa Bwana kwa Waisraeli*
👉Mkono wa Mauti,upepo wa mauti,maangamizi yalipo pita katika nchi, wana wa Mungu,waliokusudiwa na Mungu kwaajili ya Uaminifu wao,walipewa *Angalizo,Jambo la kufanya ili wawe salama kati ya mauti inayopita* Enzi za Yoshua,Ahabu kahaba kwa kuwaficha wapelelezi aliambiwa ili awe salama wakati upanga wa mauti unapita katika mji, *Afunge kamba Nyekundu katika Dirisha la Nyumba yake* Alama ya *Uvuli wa Kuhifadhiwa* mbali na mauti wakati wa maangamizi, akaongezewa mkazo Akae ndani asitoke nje ya nyumba, na watu wake wote wanaotaka usalama wakae ndani wasitoke nje ya nyumba hiyo, na atakaye toka damu yake ikimwagika hatia itakuwa juu yake mwenyewe.
18 Angalia, tutakapoingia katika nchi hii, funga kamba hii nyekundu katika dirisha hili ulilotutelemshia; nawe uwakusanye kwako nyumbani mwako, baba yako, na mama yako, na ndugu zako, na watu wote wa nyumba ya baba yako. 
Yoshua 2:18

19 Itakuwa mtu awaye yote atakayetoka katika mlango wa nyumba yako kwenda njiani, damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe, na sisi tutakuwa hatuna hatia; na mtu atakayekuwa ndani ya nyumba yako damu yake itakuwa juu ya vichwa vyetu, mkono wa mtu ukimpata. 
Yoshua 2:19
👉Unajua nini, hata sasa ziko *Kamba Nyekundu kwenye ulimwengu wa Roho* zinafungwa katika mioyo yetu, hizo ni ALAMA YA UVULI wa kutuepusha na Mabaya.
🔹Utakatifu ni kamba nyekundu
🔹Utumishi mwaminifu kwa Bwana ni kamba nyekundu
🔹Jina la Yesu ni kamba nyekundu
🔹Damu ya Yesu ni kamba nyekundu
🔹Maombi yatokayo katika moyo safi ni kamba nyekundu
🔹Imani katika Bwana na Neno lake halisi ni kamba nyekundu kwenye moyo wako.
👉Shida kubwa ya watu wa Mungu baadhi,ni *Kuruhusu Upepo wa Hofu na Vitisho kuzunguka mioyoni mwao na kuyeyusha Imani zao* Wanalia kama waio mjua Mungu waliavyo, wanasema kama wasiomjua Mungu wasemavyo..... *Kumbe nyakati za Dhaoruba wana wa Mungu wana Lugha yao tofauti na wana wa giza*
👉Sasa kazi ya wana wa Mungu ambao tumeambiwa tufunge Kamba nyekundu kwenye madirisha ya mioyo yetu,maombi yetu kwa Bwana ni kumwambia Bwana *_Tunaomba Uvuli wa mkono wako utufunike na utuhifadhi katika nyakati mbaya_* Mungu ni mwaminifu atatuhifadhi,atatuficha,nyakati za Tauni,dhoruba,vitana njaaTutapita katikati yake na Kuvuka salama, *Unachotakiwa ni Kulisikia na Kuliamini Neno la Bwana* Ukiliamini kuna uponyaji na ushindi.
39 Yesu akasema, Liondoeni jiwe. Martha, dada yake yule aliyefariki, akamwambia, Bwana, ananuka sasa; maana amekuwa maiti siku nne. 
Yohana 11:39

40 Yesu akamwambia, Mimi sikukuambia ya kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu? 
Yohana 11:40
👉👆Amini, Amini Ushindi Upo....Ingia kwenye maombi sasa sema na Mungu,haijalishi Kuna historia gani juu ya tatizo lako, wewe Amini tu.
*_Mungu akubariki,ulikuwa nami mnenaji wako Ev Elisha Kazimoto(0755444078)_*

No comments:

Post a Comment