👖🥻 *MAVAZI KWA WALOOKOKA LIMEKAAJE?*🥻👖
*_Mtu ameuliza swali katika group la whatsapp hili hapa,.....Wapendwa mie Nina swali kidogo kuhusu mavazi kwa mtu aliyeokoka, Avaeje,Mavazi yapi yanaruhusiwa kuvaliwa kwa mlokole?_*
..................................................
Anajibu Mtumishi wa Mungu *_Ev Elisha Kazimoto_*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
_Shalom wapendwa wote mnaoamini katika Neno la Mungu na katika Wokovu,huu mjadala wa Mavazi na Mapambo si waleo,unasumbua wengi sana vichwa,ila leo Sitatumia Andiko la Biblia ila nitakupa HEKIMA ZA ROHO MTAKATIFU kama msimamizi wa Mioyo yetu wanadamu hasa Tuliookoka_ Karibu tujifunze:
*MAVAZI,MAVAZI,MAVAZI*
👉Suala hili linawapa shida Wakristo wengi,ila ni walio wachanga kiroho,au ambao hawajaonja Utamu wa juu wa Mungu baba,lakini hili ni jambo Jepesi sana kwa mtu aliyeokoka ila kwa ambaye hajaokoka ni chamgamoto kubwa au kwa mchanga kiroho au kwa mtu ambaye amekoka sawa ila bado anakiwango cha kawaida sana.
*Nitawapa Siri moja na Wala usije ingia katika mijadala ya Mavazi ikakuumiza kichwa, wasaidie watu Wamjue Mungu kwa Viwango vya juu*
Utakuwa umemaliza ubishi na mijadala ya Mavazi na Mapambo.
👉Kwanza hakuna Vazi Maalumu lililoanishwa kwenye Biblia kuwa la Mtu aliyeokoka(kama ilivyo Kanzu kwa Waislamu au buibui)
👉Pili Tunatofautiana tamaduni kutoka jamii moja na nyingine kwa hiyo ni vigumu kuhukumu vazi husika.
*HIVYO BASI, UKWELI NI HUU*
👉Mungu anafanya kazi na watu NADHIFU(hiyo utaikuta kwenye Biblia)ndoa maana kufua mavazi,lugha za mavazi safi ziko nyingi kwenye Biblia.
👉Lakini pili, Mungu (Bwana Yesu)amejitambulisha ni Bwana wa Mabwana, Mfale wa Wafalme, Mtakatifu, Mungu wetu, Baba yetu kwa sifa hizo tu *Zinakupa Akili ya kujua mimi kama mtoto wake,mtumishi wake, NITOKE vipi kimwonekano ili KUMWAKILISHA katika sifa zake*
👉Mfano mdogo tu, *_Tutashangaa na kubaki kujiuliza,na kulaani endapo tutamkuta mtoto wa Rais yuko rafu,amevaa ovyo ovyo,kwa nini itazua gumzo NI MTOTO WA NANI,ila akivaa mtoto wa mkulima au wa mtaani tutaona kawaida,ni mazingira yake_* Kwa hiyo sisi tukiookoka Tunaongozwa kimavazi na STATUS YA MUNGU WETU katika kuvaa.
👉Sasa itashangaza mtu Anahoji NIVAE VIPI WAKATI ANAJUA ANATOKEA FAMILIA IPI,NA WATU WANAITAZAMA NA KUITAFSIRI VIPI HIYO FAMILIA,tutakacho jua kwa mtu huyo ni HAJUI STATUS YA FAMILIA YAKE KWAKE NA MBELE ZA WATU. Kosa hajui status ya baba yake na cheo chake kwa watu na huyo ni MTOTO(Because hata mtoto wa rais wa mwaka 1,2 kukaa na Tope na mkojo ikulu au kwa watu aliko baba yake hataona shida maana hajui,mpaka walezi wamkamate na kumbadirisha mavazi ili afananie ufalme) na ndicho kinacho fanyika makanisani *Kukemea mavazi ya aina flani ni Kumshika mtoto mchanga mwenye mikojo atoke sebuleni arudi chumbani avae kulingana na hadhi ya baba yake ndo aje sebuleni(kanisani)*
👉Sasa Iko hivi,Ukisha okoka unapewa Roho mtakatifu,huyo *Atakufundisha kuvaa,kuongea,kufanya maamuzi yote* kuna mambo atakwambia hili HAPANA ulilifanya sawa ila kwa sasa NO haliendani na Hadhi ya Ufalme uliomo.
👉Mengine siyo dhambi ila atakwambia USIFANYE, Shida ya waliookoka UNA KIWANGO HICHO CHA KUMSIKILIZA ROHO MTAKATIFU NA KUMFUATA ANAVYO KUELEKEZA? Hapo ndo kuna shida.
👉 *Shida siyo kuambiwa Suruali kwa mwanamke ni ruksa au siyo ruksa,kusuka,kuvaa wigi au kuto vaa ni dhambi au siyo dhambi na mambo mengine yanayowachanganya watu makanisani na kuzua mijadala, Shida ni Hivi Umemjua Mungu wako aliyekuokoa kwa Kiasi gani* na Kiongozi uliyepewa Roho Mtakatifu unamtunza na kumsikiliza anavyokushauri?
👉Si kila jambo utakikuta kwenye Biblia unaambiwa Fanya au Usifanye, ndio maana tuliookaka tunasema Kumcha Bwana ni ZAIDI YA KUSHIKA AMRI 10,wokovu ni zaidi ya amri 10.Ukitembea na Amri 10 tu utakuwa mchanga kiroho mpaka unaingia kaburini na mbingu utaikosa ila shetani atakushinda.
NB: *_Ni hitimishe kwa kusema suala la mavazi na mapambo ukitaka kuliweka sawa iwe kanisani au maishani mwako,Fundisha watu au wewe jifunze, Ongeza Viwango vya Kumjua Mungu na Kumweshimu Mungu na Kumsikiliza Roho mtakatifu, Utavaa,utajipamba sawa sawa na Heshima ya ufalme wa Mungu na Hutahukumiwa na Mwanadamu wala Mungu na kwenye foleni ya kuhesabu namba kuingia mbinguni utakuwa front line_*
NI USHAURI WA KIUTUNISHI NA EV ELISHA KAZIMOTO
Whatsapp 0755444078
No comments:
Post a Comment