*Sehemu ya Tatu ya Somo, Ukijitambua kama Dada wa Thamani, Utapata Mme Haraka*
_Mnenaji ni mimi Mtumishi wa Mungu *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)*_
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail babaeve755@gmail.com
....................
Sasa Karibu tuendelee....
👉Jambo lingine muhimu kwako Mdada wa Yesu Kristo ni Kutengeneza Status yako ya Kimwili.
👉Kumbuka Ndoa ni 50%Kiroho na 50% Kimwili, kwa hiyo unapojipanga kuingia katika ndoa,usiishie kuomba tu,lazima Ujipange na Kimwili, kumbuka tunaishi duniani, Vipo *Vigezo vya Kimwili* Vijana wana vitazama katika kuchagua mke bora wa kuishi naye.
👉Na labda ni kwambie, Wengi wa vijana wanaanza na Vigezo vya Kimwili ndo wanachungulia Rohoni, kwa nini Ndoa ni ya hapa hapa Duniani, usije ukasema mimi niko Rohoni sana mambo ya mwili sina haja nayo sana, HUTAOLEWA,utabaki kusubiri bila majibu.
..............
2⃣Tengeneza Status yako ya Kimwili.
👉Pamoja na kwamba kwenye ulimwengu wa Roho ndo vitu vinaanzia nakuja kwenye ulimwengu wa mwili,basi tunahitaji kutengeneza mazingira ya Kimwili ili kuwa na pawepo na uwiano kati ya thamani ya kiroho na thamani ya kimwili ndo unazalisha mtu UNIQUE anayetafutwa kwa kasi na vijana.
👉Usije kaa Rohoni tu ukashindwa kushugulikia Status ya kimwili, kumbuka *_Wengi wa watu wanatazama mwili kabla ya rohoni_* unaweza poteza muujiza wako, kwasababu STATUS YAKO YA KIMWILI iko chini.
👉Pambana kujenga status ya kimwili ili watu wakuonao waseme YES, you are Beautiful (CUTE GIRL)
👉 *Status za Kimwili* ambazo dada kama dada zinakupandisha chati na uonekane ni Wife Material na unafaa kuolewa haraka....
1. *Usafi* Binti muda wote jiweke nadhifu, uwe na nguo moja au nyingi *Jiweke Safi, Smart*
👉Unatoka kidogo,unaenda kwa mangi Toka ukiwa Vizuri, hujui utakutana na nani na atakuwa anakufanyia tathimini gani.( Mwonekano wako wa kwanza waweza kukuongezea Credits au kukupunguzia Credits).
2. *Ujasiliamali (Uchumi)* Unahitaji kuongeza thamani yako na kulinda thamani yako, Jitemgenezee mazingira ya *Kutokuwa Tegemezi kwenye Mahusiano na uchumba* wengi wamepoteza Thamani zao na kushindwa kuolewa haraka kwasababu WANA NJAA, UHITAJI WA PESA, wanayumbishwa na kutapeliwa na vijana matapeli wenye uchumi kidogo
👉Hasara za kuwa tegemezi ni kukosa *Msimamo binafsi na kauli ya NO or YES* Muda wote kila kitu utakuwa unasema YES kwa unyonge, unajua hapa ni makosa, napoteza utu wangu, nanyanyaswa ila utafanyaje, huna kitu unalazimika kusema YES,ili usikatiwe huduma ya vichenji.
3. *Lugha* unajua nini, wewe mwanadada ni mfanya biashara, unahitaji lugha tamu, lugha inayovutia wateja wako.
👉Lugha inaweza kukuweka mbali na wateja wako au karibu na wateja wako.
👉Ukari hauwi katika Lugha, kujilinda na kujiheshimu dada hakupo katika kuwatukana wakaka na kuwadharau.
👉Tumia lugha nzuri,kataa wahuni na matapeli kwa Lugha nzuri, siyo lazima Utukane na umdharirishe mtu.
4. *Taaluma* Miongoni mwa vitu ambavyo katika zama hizi sio vya kuchukulia rahisi ni TAALUMA( *Professional*) una ujuzi upi, wa nini, unaweza kukusaidiaje katika kuendesha maisha.
👉Wale ambao bado mpo katika mchakato wa kusoma, *Soma kwa bidii* ongeza vidato,jiweke katika level nzuri,usiache shule kisa umeambiwa na mchumba wako kwamba UTASOMA NIKISHA KUOA, au haina haja sana ya wewe kusoma MIMI MMEO NIPO, *Nyakati zinabadirika binti yangu* unaweza ukajutia maamuzi yako ya kuacha shule ili uolewe.
👉Wale ambao mambo ya shule vidato yameisha waacha kidogo, TAFUTA UJUZI (kwasasa ni kila kona ujuzi unapatikana) *Jiimarishe uwe mtaalamu haswa*
*_Mf.Kama ni kupamba maharusi, Kupamba kumbi,keki,ufundi wa nguo nk, Somea chuo kabisa uwe mtaalamu haswa_*
Achana na mambo ya kwenda kujifunza cherehani kwa fundi wa mtaani kwenu, au kupamba kwa flani ambaye naye anatamani akae yeye ndo anajulikana, nenda chuoni upate vitu adimu na uongeze ubunifu wako,ili *Upunguze ushindani juu yako* ufanye vitu Unique and attractive.
👉Nataka ni kwambie wanaumebwatapanga foleni kwako,lakini hata ukiolewa utakuwa unathaminiwa na kupendwa sana.
_Unaonaje unaitiwa tenda ya kupamba kwenye harusi ya mil 2,3, au 5 siku moja unainuka na mil 5,wakati kuna mfanyakazi anafanya kazi mil 5 anaipata baada ya miaka 5?_
*Dada ongeza status yako bhana ndoa kupata ni rahisi*
_Kufikia hapo ni hitimishe sehemu ya Tatu ya somo letu,lakini nikukaribishe kwa sehemu ya nne ambapo tunaendelea na Status za Kimwili, 5,6 na 7..Barikiwa sana na Bwana_
Mnenaji alikuwa mimi Mtumishi wa Mungu *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto
E-mail babaeve755@gmail.com
No comments:
Post a Comment