Thursday, 26 November 2020

NDUGU KUCHUMBIA BINTI MMOJA

*Swali:* Kuna wa kaka 2 mtu na mdgo wake yn wamekutana ba mkubwa na mdogo,,,yule kaka mkubwa alikua na mahusiano na bint lengo amuoe 🤗lkn ikafikia kipind yule bint gafla t akamwambia huyo kaka kuanzia leo ckutaki hata kukuona😫bac kaka wa watu akakubali matokee maisha yakaendelea,,,,,baada y muda flani mdg mtu akamwambia kaka ake kua nimepata bint wa kuoa lkn kaka naonba unisamehe mm ndo nmemshawish mchumba ako akukatae ili nimuo mm je kama n ww unafanyaje🤗na je ndugu yko akishaoa utaweza kwenda kwake maana hapo awali bint alikwambia htk hata kukuona inakuaje hapo🤔
*Anajibu Msaikolojia...Ev Elisha Kazimoto*
*UNAWEZA KULIPOKEA KIRIHO ILA KISAIKOLOJIA LITAKUTESA*
👉Suala la mahusiano ni gumu sana kisaikolojia tofauti na watu wanavyo dhani, likibebwa kirahisi linaweza kukufanya *Kichaa aliye timamu*(Mtu aliyepoteza uwezo wa mchakato wa akili katika utulivu japo haokoti makopo na kula uchafu)
👉Mahusiano yanahitaji ukiyaanza ujipange sawa, *Uingie kwa sababu za Msingi zitakazo shibisha akili na moyo wako amani, na Ukitoka ujue unatoka kwa sababu za Faida ya Usalama wako wa uzuri wa baadaye,siyo sababu ambazo zitakuuma ukikumbuka ukagundua ni uzembe au hila flani za watu*
👉Sasa hawa ndugu na mke wao mmoja wote wako kwenye Mtihani mkubwa kisaikolojia ambao unaweza kugharimu (Mahusiano ya kiundugu, kiroho,na kindoa) hapa kila mmoja ana mtego na maumivu yake.
1⃣Mdada mwolewaji(Yuko kwenye mioyo wa watu wawili ambao ni ndugu wa karibu) anaweza kutumika kama silaha ya kuua hao ndugu,familia zao au ndoa zao.
👉Mdada anakuja kwenye familia ila haji kukiwa amani anakuja kama CHANZO CHA MACHAFUKO kwa ndugu wawili na familia yote.
👉Namna ya kupunguza shari *Akubali kwa siri Awe mchepuko wa Kaka mtu(kaka wa mme wake) ampe penzi la kutosha naye kisiri siri ili kaka mtu atengeneze amani kati yake na mdogo wake na wazazi.
👉Ila itakuwa ni hatari kama mmewe atagundua moto na vita vitatokea.
*Huo ndo mtihani alio nao*
2⃣Kumbuka kaka mtu anampenda bado mke wa mdogo wake maana yeye aliachwa si kwamba aliacha.
👆👉Upendo huo unao fukuta ndani, vipi ukiibuka wote wakiwa wameoa lakini huyu akaendelea kumfatilia mke wa mdogo wake( Ndoa zao wote ziko hatarini) 
👉👆Kaka mtu akiamua ku REVANGE(kulipa kisasi )kwa ajili ya kutibu majeraha ya moyo kwasababu ya kumeshwa sega la asali mdomoni kwa hila?(hapo kuna hatari zaidi)
3⃣Mdogo mtu ameua undugu kwa tamaa,Alifanya kwa upumbavu, itakuwa ni vigumu kueleweka kwa kaka yake na familia, mpaka wawe na kiwango kikubwa cha Kiroho.
👉Jambo la msingi hapa *Refarii ni Mdada, AWAACHE WOTE wawili akaolewe kwingine, maana yeye na mdogo mtu wote Hawana Akili* wanapooana hawaendi kukaa mawinguni, wanakaa kwa jamii na ndugu zao ni hao,unakuja umeisha wagawanya mioyo,unadhani baba na mama na baadhi ya ndugu mawifi na mashemeji *watakufurahia kuona wewe ndo umewafanya mtu na kaka yake wasiingiliane,wasipendane,wasisaidiane nk, Utapendwa na wawili ila kumi watakuona mchawi wa Familia na wazazi Watakulaani milele* acha, acha kabisa mzazi yeyote anapenda kuona wanae wanapendana wanasaidiana sasa wewe umewagawanya,hata kama una pesa watakuona wee mchawi wa uzao wa tumbo lao.
👉👆Ushauri wa dada awaache wote. Ajue huyo mdogo mtu ni mbovu kuliko kaka yake.
By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)0755444078

No comments:

Post a Comment