Thursday, 26 November 2020

ZAWADI ZA NGUO ZA NDANI

*MADA YA LEO 27  MAY 2020*

Katika Mahusiano yeyote zawadi kwa  ndugu zangu wa-maasai huita sawadi, ina nafasi gani katika kukuza penzi au mahusiano yenu? Je  Pia?  kuna  baadhi ya zawadi inapaswa isitolewe kwa watu walioko katika mahusiano     mfano: Wapo wapenzi   wana nunuliana hadi CHUPI  na BOXER, 

Hii  imekaaje? JE ZAWADI ZETU kwa watu tuwapendao ziwe na mipaka au full kujiachia.

*N:B:* Siku Mkiachana  roho yako  isikuume wala  kuzidaii kwa Ex  wako huyo.


‼️‼️ KARIBUNI
*Nianze na hii ya zawadi*
_ZAWADI NI MIONGONI MWA VICHOCHEO VYA MAPENZI KATI YA WANA MAHUSIANO_
👉Zawadi ina kazi kubwa kwa anaye toa na anaye pokea kwa hiyo wote mnahitaji kuwa makini sana Kiroho na Kisaikolojia.
1⃣Kwake atoaye zawadi anawekeza( *Anatafuta nafasi chumba cha kukaa katika moyo wa anayepokea zawadi*)Hii ni kibiblia👇👇👇👇
21 kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako. 
Mathayo 6:21

👉Kazi ya zawadi ni kuhifadhi moyo wa atoaye zawadi ndani ya moyo wa aliyepokea zawadi.
👉Kwa hiyo hapo jua pindi utumiapo au uishipo na zawadi ya mtu jua *Unaishi na moyo wake* 
👉Sasa kama ni zawadi njema jua upendo utakuwa mkubwa kati yenu na mioyo yenu itaambatana sana.
👉Kwa sababu hiyo, Zawadi ni mpeano kila mtu tafuta nafasi ya kukaa moyo wako ndani ya mwenzako.
👉Kama unataka upokee tu zawadi jua mwenzako *Yupo moyoni mwako,ila wewe haupo moyoni mwake* ndo maana mkiachama wewe utaumia sana ila yeye hataumia sana,atapona haraka wewe utachekewa kupona machungu.
2⃣Kazi ya zawadi kwa apokeaye, inakufanya wewe kuwa *Mtumwa wa Nafsi, Hisia,Maamuzi kwa aliyekupa zawadi* ndiyo maana unapaswa kuwa makini na zawadi na aina ya zawadi....Hii ni kibiblia pia👇👇👇👇
Atamaniye faida huifadhaisha nyumba yake mwenyewe; Bali achukiaye zawadi ataishi.

Mithali 15:27
👉Zawadi inakuondolea Ujasiri binafsi mbele ya aliyekupa zawadi.
👉Zawadi inakawaida ya kununua Hisia zako,na maamuzi yako.... _Ndiyo maana wengi wanaopoteza Usichana wao au uvulana wao,wokovu wao nk Zawadi zilitangulia kununua maamuzi yao,akija kuambia Sex,au hitaji lolote anaona ni gumu lakini akifikilia zawadi alizopewa,alizokula anaona mwenyewe *Atakuwa si muungwana kumkatalia* atakuwa mkatili kumgomea, anaona aibu kukataa lolote._
👉Ni watu wachache ambao Zawadi hata ziwe za gharama *Haziwezi nunua Maamuzi na Nafsi yake* hao ni WACHACHE NA WAWE WAMEIVA KIROHO NA KISAIKOLOJIA ila wenye wokovu wakawaida wa wengi wetu HUCHOMOKI( a.k.a HUTOBOI).
👉Kiwango cha zawadi ndo kiwango cha nguvu ya Kulainisha moyo wa mpokeaji na kununua nafsi yake na maamuzi yake.
👉 *NB: _Zawadi ni muhimu kuzichunguza na kuwa nazo makini, Zawadi ni Sadaka katika Madhabahu ya moyo,ikinenewa maneno ya kiroho au ya kipepo inauwezo wa kutekeleza matakwa,ndo maana unapaswa kujua zawadi hii inatoka kwa nani,viwango vyake vya wokovu,au utu wake na inahusiana na nini_* Kuna zawadi ukiipokea kwa mtu,ukiitumia
1.Hutokuja kuzaa
2.Hutaolewa au kuoa
3.Magonjwa yanaanza hapo
4.Laaana na mimosi juu ya mafanikio yako.
NIMALIZIE KWA KUSEMA KATIKA POINTI YA SWALI:
👉Zawadi ya nguo ya ndani katika Uchumba *Usipokee* Narudia Usipokee labda wale bao wefikia kiwango ambacho zile nguo zinapelekwa kwenye sendoff kwaajili ya bibi harusi kwaajili ya harusi kesho yake.
👉Umekosa zawadi zote mpaka ununue nguo za ndani kwa mwenzako.
👉Sehemu za Siri ni maeneo maalumu ya AGANO,so na kinachofunika pale lazima kiwe safi kina enda na nguvu ya kuhifadhi agano.
👉Umewahi kujiuliza kwa nini wachawi uwa wanaiba *Nguo za ndani za wamama na wadada wengi,wanakuta imeibiwa haionekani tena au anakuja kuipata baadaye ila matokeo baada ya kuipata au kupotea waulize wanajua shida zake,ni somo maalumu hilo si la humu VERY DANGER* NDO MAANA HATA WADADA NA WAMAMA MSIZOEE KUFUA NGUO ZA NDANI NA KUANIKA NJE ZIKALALA,ITAKUGHARIMU SIKU ADUI YAKO AKIFANIKIWA KUISHIKA.
By *Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)*
0755444078

No comments:

Post a Comment