Thursday, 26 November 2020

KULIPA MAHARI

Nina swal......

*Je ni sahihi kwa kijana kusaidiwa kutoa mahari, mfano kusaidiwa na ndugu zake au hata mwanamke anayetarajia kumuoa........na je akisaidiwa huyo mke hawi wa wote waliochangia mahari?*
*KULIPA MAHARI KIMANTIKI NI KAZI YA KIJANA MUOAJI*
*Anajibu Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto*
👉Kijana unapoanza kuhisi kichwani mwako unahitaji *Kuchumbia* jambo la kwanza anza kujipanga kutafuta mahari.
👉Ukianza kuchumbia uwe na uhakika wa kulipa mahari mwenyewe.
👉Usichumbie kwa imani na kuwatwisha mzigo ndugu, wazazi na kanisa wakulipie Mahari.
👉Mahari kwa tafsiri ya haraka ya kimantiki Ni Gharama inayoonyesha kiwango cha Utayari wako na Upendo wako kwa huyo unaye mtaka, Upo tayari kugharimika kiasi gani hata umpate? Sasa usipo Lipa mahari au ukisaidiwa mahari nani mwenye upendo wa umuoaye wewe Au ndugu zako au kanisa? Heshima ya mwanamke iende kwa nani?wewe mmeo au ndugu au kanisa lililolipa mahari?
👉Kabla ya kuanza kuchumbia jua wewe kijana(mwanaume) Biblia imekufananisha na Yesu Kristo(wewe ni kichwa cha mkeo) Yesu alilipa Gharama hata mauti ili atupate sisi,je wewe umelipa gharama ili umpate mkeo?
👉Wazazi,ndugu,kanisa wacha wapambane na maandalizi ya harusi,wewe *LIPA MAHARI* kwa namna vyovyote.
👉NB: Suala la wazazi kukusaidia,kukulipia mahari isiwe ni kwasababu Umeshindwa iwe ni kwasababu Mzazi anapendelea,ametaka kuhusika na hapo pia,ila kijana mwenye akili zaidi,lipa wewe mahari pesa ya wazazi na ndugu ielekeze kwa mambo mengine.
👉Kama uneshindwa kulipa mahari,wakakusaidia siyo dhambi ila haitakupa heshima na nguvu.
👉Mdada kukusaidia kulipa mahari siyo dhambi ila umevua kofia yako umempa yeye awe kichwa, yeye anachoweza kukusaidia *Nikuongea na familia wasikutoze mahari zaidi ya uwezo wako,mwambie mimi ninauwezo wa kulipa laki 5 tu😎😎 ikizidi hapo tutasogeza mbele harusi au sioi 😍😍 sasa kama anakupenda yeye aende apambane na hali ya familia yake mpaka washushe to laki 5.
👉Na si vizuri kukopa mke,eti muoane utamalizia mahari huko ni kujidharirisha na kujipa mzigo mkubwa baada ya kuoana,si wote uwa wanamaliza kwa wakati wengine mpaka wanazaa watoto miaka 5,10 ndo wanakuja kumalizia deni.
*ANGALIZO LANGU KWA VIJANA*
1.Kama unahisia za kuoa pia uwe na hisia za kutafuta pesa mapema.
2.Kama bado huna uhakika wa kupata pesa Usitongoze mdada yeyote, *Jifanye Uwaoni, au wote ni dada zako wa kuzaliwa* ila ukishaanza kupata kipesa fungulia speed za kutafuta.
3.Mahusiano ni gharama ukiamua kusema I LOVE YOU JUA KUNA NA I GIVE YOU.....
4.Vijana msikwepe kazi, au kupenda kazi za kukaa kwenye kiti, chimba hata mitaro,chota maji,buruta toroli tafuta pesa kila kona mahusiano na ndoa ni MATUMIZI.
5.Na ninyi wadada ukianza kuchumbiwa Soma na Angalia uwezo wa mchumba wako ulo mkubali, *Kipato chake cha 50elfu kwa mwezi,wewe unamtaka 50elfu kila wiki ya kusuka,unataka IPhone simu wakati yeye ana tekno ya batani, huu nikuwa CHUMA ULETE* umemkubali huyo taka vichache kwake,mkioanana pambaneni wawili kuinua kipato chenu.
6.Dada japo pesa ni muhimu katika mahisiano ila,kabla ujaingia kwenye mahusiano uliishije? Balance mazingira,usimpende au kutompenda mtu kwa sababu ya uwezo mdogo,maisha ni safari ya mabadiriko ujui kesho anaweza kuwa milionea.
*By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)0755444078*

No comments:

Post a Comment