Thursday, 26 November 2020

MAVAZI KATIKA MAHUSIANO

*Miongoni mwa majukumu na wajibu wa kila mmoja kwa mwenzake ni kuangalia mwonekano wa mwenzako ukoje*
👉Ukiwa bachela unavaa kwa kadri uonavyo vema wewe ila ukiingia kwenye mahusiano Imara au ndoa utavaa kwa kadri ya mwenzako aonavyo vema kwake(unafanya kitu kinacho shika hisia zake siyo za wengine)
👉Sasa hapa mahusiano mengine yamevunjika mengine yamekuwa hatarini kwakutojua saimolojia ya mahusiano na mavazi au urembo.
👉Narudia pamoja na kwamba unavaa ili upendeze,kimbuka unapendeza kwaajili ya nani, kwaajili yako ili utafutwe au upendwe na wengine au kuufurahisha moyo wa mpenzi wako ajisikie Alichagua Cute au Hb na ajisifie kwa wengine?
👉Wao wanao sema mme wangu au mke wangu hawezi nipangia nivaeje nitokeje,aniache....Kweli atakuacha atawafuata wanaomwambia hivi ulivyo vaa umebamba au wanao vaa kama anavyotaka yeye, USIJE KULALAMIKA.( *Umekataa mwenyewe kuingia kwenye Hisia zake*)
By Ev Elisha Kazimoto(psychologist )0755444078

No comments:

Post a Comment