*_Je, ni sahihi kuendeleza mawasiliano na Ex boyfriend/Ex girlfriend? Je, inawezekana watu walokuwa wapenzi wakaachana kuwa marafiki?_*
*Anajibu Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto*
*KUACHANA SI UADUI,ILA LENGO LA KUACHANA LISIPO ZINGATIWA INAWEZA KUWA TANZI KWAKO(UNAHITAJI KUJIULIZA KWA NINI MLIACHANA,SABABU HIYO ITOSHE KUKUWEKEA MIPAKA YA MAWASILIANO NA HUYO EX WAKO*)
👉Usipojua Dhana ya kuachana,utavuruga mahusiano yako mapya au ndoa yako.
👉Sababu iliyofanya muachane ndo inapaswa kukuongoza kukata mawasiliano ya karibu na ex wako,usipo kata mawasiliano naye ATAVURUGA MAISHA YAKO MAPYA ya ndoa au mahusiano wakati yeye anamtu wake au ana maisha yake au atakauwa na maisha yake bila wewe.
👉Unashauriwa ex wako muwekee mipaka ya mawasiliano,kusaidiana,kukutana nk....
👉Walio wahi kuwa kwenye mahusiano,pamoja na kuachana,kuna namna mioyo yao iliwahi kuungana,kuaminiana na kupendana, *kwa hiyo mawasiliano ya mara kwa mara,yanaweza TIBUA hisia za mwanzo na kuwafanya wa RUDIANE kihisia na kujikuta wanaanza mapenzi ya siri nje na ndoa zao au mahusiano yao*
By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)
No comments:
Post a Comment