*MUDA WA KUTOA JIBU LA NDIYO AU HAPANA HAUKO FIXED,BALI UTATEGEMEA MTAZAMO,HISIA, ZA MWAMBIWA JUU YA ANAYE AMBIWA,PIA KAMA MTU NI MCHA MUNGU ITATEGEMEA CONNECTION ALIYO NAYO NA MUNGU ILI KUPATA JIBU LA NDIYO AU HAPANA*
NB: _Wengi katika kutoa majibu, wanazingatia mambo yafuatayo....._
1⃣Kukariri kwa mazoea ya watu kwamba mwanaume usimpe jibu haraka ataona kama ulikuwa umeisha sota kutafuta mme(Kwa hiyo hata kama anakupenda au siku nyingi anasubiri umwambie neno atajifanya hana muda na wewe mpaka umsumbuepo tena.( Angalizo: Unaweza kusubiri usumbuliwe tena jamaa akatafuta mwingine ukabaki na maumivu)
2️⃣Kuna watu wanachelewa kutoa jibu kwa kuanza kufanya utafiti wa *Uhalali wako wa Kumuoa,asije chukuliwa na Jambazi la kiroho au la kimaisha*(Hii imekaa sawa)
3⃣Kuna watu wanachelewa kutoa jibu la ndiyo au hapana kwa kusema Amauulize Mungu ila wengi wao *Wanauliza Mungu hali ya Hewa(ya mfukoni mwako)ikoje...Akigundua ATM inasoma maisha yako poa,hata Mungu hajasema chochote utasikia NIMEPATA AMANI KUBWAAAA SANA JUU YAKO baada ya kumuuliza Mungu, wengine kama *Wewe ni Kijana wa Kuishi kwa Imani(Wale wa Mbele ninaendelea...)Utaambiwa SIJAPATA KIBALI KWA MUNGU JUU YAKO,ila ukweli ni kwamba Ameona Mambo yako hayasomi.
*_Ushauri:Dada Toa jibu kulingana na Nia ya moyo wako,na kama ni Mungu basi muulize Mungu,kama unacheki hali ya hewa cheki vzr,na usimkawilishe mtu itakugharimu,Ukimpenda mpe jibu hata kama ni papo kwa papo,kama humpendi mwambie kwa ustaarabu Sijaona kama itawezekana_*
By Ev Elisha Kazimoto(Pychologist)0755444078
No comments:
Post a Comment