Thursday, 26 November 2020

MUDA SAHIHI WA KUINGIA KWENYE NDOA

*🌷🌷MADA*🌷🌷🌷 *Je! Niwakati gani sahihi unafikiri kijana aoe au Kuolewa ??*
Karibu Sanaa🥰
*Anajibu Msaikolojia Ev Elisha Kazimoto*
*MUDA SAHIHI WA KUOA NA KUOLEWA*
👉Kikawaida jambo lolote ili lifanyike kwa ubora na uzuri na mtu alifurahie au limnufaishe lazima lizingatie mambo yafuatayo...
1⃣Uhitaji wako ni mkubwa kuliko kutolihitaji.
👉Kuna muda ambapo kuna jambo unalihitaji ila halina umuhimu sana kwa wakati huo,kuna wakati lina umuhimu,na kuna wakati lina ulazima.
*Muda wa umuhimu na ulazima* ndo muda sahihi wa kuoa au kuolewa.
_Viashiria vya Umuhimu na Ulazima_
1.Kusudi ulilo nalo moyoni mwako la Kimungu linahitaji mtu wa pili akusaidie?
2.Majukumu yako kuongezeka na kuanza kushindwa kuyamudu.
3.Vishawishi vya zinaa kuongezeka kila mara na kuelekea kukushinda.
2⃣Ukiwa Tayari kimaandalizi kumtumza mme au mke bila kuhisi umeongezewa mzigo mzito katika maisha.
3⃣Kumpata mtu sahihi wa kuanza naye safari ya maisha ya ndoa.
4⃣Kigezo cha umri miaka 20
_Hivi ni vitu vinavyo mwongoza mtu kuingia katika ndoa na akaishi maisha ya amani na raha na mwenzake._
By Ev Elisha Kazimoto(Psychologist)

No comments:

Post a Comment