Wednesday, 29 August 2018

MAHUSIANO NI INTIMACY II

❤❤ *RELATIONSHIPS IS ALL ABOUT INTIMACY/MAHUSIANO UJUMLA WAKE NI UKARIBU*❤❤
     *Sehemu ya II*
_Whatsapp 0755444078_
Facebook Elisha Kazimoto
.......
.......
_Karibu katika mwendelezo wa somo letu la Mahusiano ujumla wake ni Ukaribu wenu,bado mchambuzi ni mimi Mwanasaikolojia na mchambuzi wa mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto_
❣Uchumba mwingi,na ndoa za wana wa Mungu zinaendelea kuchechemea na zingine kuvujia ndani kwa ndani, changamoto kubwa ni ya Kisaikolojia wala siyo ya Kiroho(kwamba kuna pepo) kama ni pepo utalikarisha mwenyewe kwakukosa kwako maaraifa,na kudharau mambo madogo, ya kishamba, kipuuzi, ya kitoto yaliyo uhai wa kisaikolojia na kujizamisha sana kiroho  kisicho kusaidia katika mahusiano yako wala ndoa yako,utaendelea kuimba,kuhubiri na kufanya yote ya Kimungu ila kwenye mahusiano unachechemea na unahisi mwiba mkuu,kumbe ungeuchomoa kwa kuongeza Maarifa ya Kisaikolojia baada ya kujiweka vizuri kiroho.( _Kwenye Biblia hutakuta mpige busu mkeo au mmeo,hutakuta mfanyie mkeo au mmeo surprise haya utayapata kwa wanasaikolojia_).
❣ *Intimacy ina Kazi zake na Raha yake katika Maisha ya Mahusiano* Mahusiano yaliyo Hai yanafurahia  Amani na furaha katika ndoa na ndicho Mungu alikikusudia katika ndoa.
❣Mahusiano yaliyo hai Kuna Kuaminiana na kulinda kuamiana.
❣Mahusiano yaliyo hai kuna mawasiliano ya Caring.(kujali)
❣Mahusiano yaliyo hai kuna Kuthaminiana(kumwona mwenzako ni pekee na kulinda nafasi yake)
❣Mahusiano yaliyo hai kuna Kumsikiliza mwenzako na kujua nini cha kufanya.
*ALAMA ZA MAHUSIANO YALIYO POA/KUFA*
👉 *Hakuna kuaminiana* hata kidogo,kila mmoja anasiri zake(hapa wala hakuna kitu kinacho lindwa chochote,kiwe cha kiroho au kimwili hapa ni matokeo ya harufu ya Mauti katika mahusiano)unahitaji kuanza harakati mpya za kumwamini mwenzako kwa sehemu kubwa maana huyo ndo wa moyo wako na maisha yako,mjenge,mtengeneze kwa upendo Aaminike.
👉Kuna *Dharau/Kudharauliana* hapa kila mmoja anafanya bidii kushusha uwezo,nafasi na utu wa mwenzake. Hapa ndo mtu humuona mwenzake hafai kwa chochote cha maana.
👉 *Kutoa Siri za ndani za mwenzako nje kwa watu* Kwakuwa moyo umejaa uchungu na kutoridhika na kukubaliana na mwenzake hapa mtu upunguza uchungu kwa *Kumsema mwenzake katika udhaifu na mapungufu yake tu* jambo ambalo uendelea kupanua Distance (umbali)wa mahusiano.
👉 *Kutimiza baadhi ya wajibu ila Siyo Hisia kwa mwenzake* Mahusiano yaliyo poa,au kufa utasikia lugha hizi, *_Unakosa nini?Hauli?Huvai? Unataka nini sasa.._*kila kitu na kupa au najufanyia, yaweza kuwa kweli ila *Unatoa Material support siyo Emotional support* wana mahusiano wengi wanajificha nyuma ya wajibu kumbe kihisia hawapo, Hisia zikitangulia ndizo zinazaa Wajibu. Ndani ya Kutimiza hisia za mwenzako ndo kuna wajibu, ila ndani ya wajibu hakuna Hisia.(Unaweza mpya mwenzako vyote,Usipo mpa Hisia zako anaoana zero)
👉 *Kujihesabia haki katika makosa* mahusiano yaliyopoa au kufa Kila mmoja hupenda kujiona yeye ndo mwenye haki na mwenzake ndo mwenye makosa, ndiyo maana kwenye mahusiano yaliyopoa au kufa hakunaga neno Samahani mwenzangu,ila kila mtu anapambana ashinde atakama anajua anamakosa.
💈💈 *Aina za Watu wagumu wasio weza Kutengeneza Intimacy katika Mahusiano yao na ndoa zao*💈💈
1⃣ *Watu wenye Asili ya Ubishi* yaani watu wabishi kisaikolojia niwagumu wa kutengeneza mazingira ya Ukaribu, kwa sifa yao ya Ubishi uwasogeza mbali na wenzao,uwafanya wawe wakali na wakorofi kwa wenzao.
2⃣ *Watu wajuaji* Aina hii ya watu ambao huona Kila Kitu anakijua,niwagumu sana kutengeneza Ukaribu na wenzi wao,uona wenzao hawajui ila wao wanajua kwa maana hiyo Ufuata mawazo yao tu,jambo ambalo upanua umbali wa mahusiano na wenzi wao.
3⃣ *Watu wenye Dharau ya Jinsia* Kati ya Kundi ambalo wanaishi kwenye mahusiano kiugumu ni kuwa na Mke au Mme anayedharau jinsia yako na kutukuza jinsia yake. Mara nyingi watu wa kundi hili hawafurahii mahusiano yao,maana utegemea kupokea,kuona mwenzake anafanana naye(jambo ambalo kisaikolojia wala kirohi haliwezekani)Mungu aliweka utofauti kubalance maisha.
4⃣ *Watu wasio amini katika Positive* Kundi hili kila kitu Ukisemea,Uamini katika Negative kwanza,lolote kwao ni baya hata kama ni zuri,wanajua ndani ya moyo ni zuri ila hawapendi kuonyesha uzuri huo kwa kukiri kwa kinywa. Hali hii haiwaruhusu kutengeneza Intimacy na wenzi wao..
5⃣ *Watu wasiopenda Kutambua Kazi za wenzao na Kuzikubali* Kundi hili Uamini katika ayatendayo yeye ndiyo sahii,ndiyo bora na ndiyo yakufuatwa ila ya wengine yana makosa na mapungufu( *Failure of Appreciation*) kwa tabia yao hawawezi kujenga Intimacy na wenzi wao lazima wawe mbali kimahusiano kwa maana hawatazami jema kwa wenzao na kulipalilia ila makosa na kuyalalamikia.
6⃣ *Watu wenye Itikadi Binafsi zisizo badirika*(STATIC PEOPLE) Kundi hili ni gumu kujenga ukaribu na wenzi wao kwakuwa *_Utafuta watu wengine/wenzi wao wajiingize kwenye imani zao siyo Kubadirishana matamanio ya pamoja(Sharing of common Interests)_* huwa hawaoni kama wanaweza kupata kitu cha ziada kwa mwenzake. Hawaingizi kipya,hawasomi mazingira na nyakati za wenzi wao na kuji Tune katika mwelekeo wa kuboresha,kulinda Mahusiano.
_Makundi haya na baadhi kati ya mengi yaliyo na shida ya kujenga Intimacy/ukaribu na wenzi wao,jambo ambalo upelekea migogoro baina yao ya mara kwa mara,na kuishi maisha ya Ukame katika ndoa au mahusiano na wengine hali ikizidi kuwa ngumu,Distance ikipanuka zaidi na kufikia mwisho uamua Ku Break Mahusiano yao katika uchumba na katika ndoa Divorce/Kuachana hutokea_
👉Ushauri wa Kisaikolojia ambao waweza kuutumia ukakusaidia ambao unaenda sambamba na Neno la Mungu,ni huu *_Chagua mahusiano ya Urafiki,na Utoto_* Yesu anasema Siwaiti tena Watumwa ila *Rafiki zangu* Mahusiano ya kirafiki katika ndoa yanajenga Amani ya uchumba au ndoa,Mtatofautiana ila mtasamehana na kuendeleza urafiki,Kumfanya mwenzako afurahie uwepo wako kwenye maisha yake,hutaki kumkwaza,kumuumiza,kumdharau,kumsogeza mbali ila karibu,unaona ni bora kama wewe,unathamini umoja wenu.( *Kutendeana vitu vya kihisia na kutafuta kufurahishana* kasome Bible hizi ni falsafa za Kisaikolojia ila zipo kwenye Bible,ukizipinga Hujui neno la Mungu ni Ugumu wako tu.)
👉Chagua Mahusiano ya Kitoto( _Yesu akasema Msipo kuwa kama watoto wachanga kamwe hamtaingia katika ufalme wa Mungu_) Sifa ya mtoto Hatunzi Makosa moyoni ni mtu wa Kuachilia(Ndoa na uchumba)vina haribika kwa kosa la Kutunza makosa ya mwenzako moyoni,unasamehe mdomoni ila moyoni unasubiria kuhesabu kosa lingine.
👉Sifa ya mtoto nibKumwamini mwenzake,watoto hawajawahi kutoaminiana,mdo maana wanacheza wote,wanamegeana chakula wote na vyovyote moyo wake umefunguka kwa mwenzake muda wote,hata wagombane kesho wanacheza wote kwa vicheko.
👉Sifa ya mtoto ni kutafuta michezo ya furaha ya kucheza na mwenzake. *_Wana ndoa wengi utani,michezo,iliishia honeymoon wengine kwenye wiki la kwanza la ndoa yao_* hamuwezi kwenda mbali kimahusiano mtaishi kiugumu ugumu.
NAFUNGA UCHAMBUZI KWA SENTENSI NA FALSAFA YA KISAIKOLOJIA.
_Kila mtu ana mtazamo wake juu ya kitu,uzuri wa kitu haupo juu ya kitu ila juu ya macho ya mtu akitazamaye,na Ishi unavyo amini wewe na si watu wengine wanavyoamini, Penda kuongeza maarifa mapya maana si kila unacho kiamini ni sahihi na kinaendana na wakati huo, Maana Ukikosea katika unacho kiamini utajirekebisha na utakuwa umejifunza,ila Ukikosea kwa ulichoaminishwa Utaumia na Kuwalaumu watu._"
    *Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na ndoa Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

No comments:

Post a Comment