🛣 *SEMINA YA NENO LA MUNGU KUHUSU UTUMISHI WA MADHABAHUNI PA BWANA*🛣
_By Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp 0755444078)_
......................................
*_Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu_*
*SEHEMU YA 9*
*Tambua Nguvu Kuu 3 Zinazo Pambana na Huduma yako*
..........
..........
..........
_Shalom mwana wa Mungu,mtumishi wa Kristo uliyepewa Hazina kubwa ya katika Ufalme wa Mungu(Huduma yako),nikukaribishe katika sehemu hii muhimu ya 9,ambapo tunaziangalia *Silaha 3 hatari* kwa huduma yoyote duniani,ujue kwamba kila siku,kila saa na mahara popote huduma yako inawindwa na silaha hizi ili *Kukusambalatisha* katika Tasnia ya Utumishi wa Madhabahuni pa Bwana. Lakini tukizijua silaha hizi ni Nusu ya ushindi,na tukianza Harakati ya kuzipinga ndo ushindi wetu_
🔫 Labda niseme hivi kama wewe umeamua kumtumikia Mungu aliye hai, *Jipange kushindana* na hizi silaha hatari katika huduma yako, nataka ni kwambie utakuwa na *_Huduma safi,yenye kibali cha Mungu na kwa wanadamu_* na utaona huduma yako ikikua siku hadi siku.
🔫Lakini pia chunguza kwa makini watumishi mbali mbali wa Kada zote Ukiziona zinashida,huzielewi elewi vile,mtumishi ni kama ukimpima kwa Neno la Mungu bado unamashaka naye, basi *Usiende Mbali* Fatilia kwa ukaribu yeye vipi haya mambo matatu Ameyashinda ( *_Wengi wao Utakuta wanatumika CHINI ya Silaha hizi tatu_*) tayari wametekwa na wanaendeshwa na adui.
1⃣💣⚰ *Nguvu ya Kwanza na Silaha ya Kwanza ni KIBURI*
🔫Hii ni Silaha ya kwanza inayotolewa na Adui Ibirisi na shetani ikiwa ya kwanza kuziendea huduma zote duniani( Wachungaji,Mitume,Manabii,Wainjilisti,Walimu,Waimbaji na wooote watumikao madhabahuni pa Bwana) hii inatolewa mara baada ya huduma ya mtu kuanza *Kuchanua na kupata kibali* mbele za watu,ndipo Silaha hii uachiliwa haraka sana katika Moyo wa mtu.
🔫 *Kiburi* ni Tabia ya Shetani iliyo kuu iliyompelekea yeye kushushwa chini mpaka kuzimu na *Kupoteza* Sifa zote,nafasi zake zote alizokuwa nazo mbinguni(juu). ISAYA 14:13-15.
🔫Shetani anaifahamu sana Silaha hii na nguvu yake ikimwingia mtu katika Huduma, Adhabu yake kutoka kwa Mungu huwa ni *Kushushwa Chini* kutoka katika viwango vyako vya Awali na kibali na kuwa mtu wa kawaida na kudharauliwa. ESTER 1:10 hadi mwisho, na 2:1-4,jifunze kwa Vashti Malkia wa Mfalme Ausuelo,kiburi kilipoota tu akapigwa chini umalkia na akainuliwa mwingine Ester akachukua nafasi yake.
🔫Unapoingia katika huduma chunga sana *_Hali ya kujiinua,kupenda Sifa,Heshima,kuona we ni Special kuliko wengine wote,kuona we ni mkuu kuliko wengine wote,kujipa sifa za Kiungu si kwa utukufu wa Mungu bali kwa utukufu wako_* jua nyuma yako Linakuja ANGUKO la hatari sana. DANIELI 8:10, MATHAYO 11:23.
🔫Watumishi wengi uanza vizuri huduma( _Nakupa siri_),huduma zikianza kukubalika,kupanuka na kuwa kubwa ndipo Taratibuu shetani uanza kupenyeza mtazamo mpya ndani ya mtumishi wa *_Kujiona tofauti na wengine,special anakubalika sana kuliko wengine_* na kiuhalisia ni kweli ndivyo alivyo,ila shida Anapandikiziwa roho yakujifanyia Promo,Matangazo,na kufanya matendo ya kuonyesha yeye ni Mkuu,ndipo majina mengi Makuu yamebuniwa, ( mfano, _Kama wote ni wachungaji,yeye lazima aongeze Mchungaji Mkuu,kama wote ni waimbaji lazima aongeze Mwimbaji Mashuhuri sana,nk,nk *Hizo ni dalili za Kiburi*_) mtu akianza hivyo anaelekea kushushwa.
🔫Kushushwa kunakotokana na Kiburi alichopandikiza shetani ndani ya mtu kumegawanyika katika makundi 2(wengine wanaweza shangaa,mtumishi flani ANAKIBURI CHA UZIMA ila bado ni FIRE mbona hajashushwa) nisikilize nikufundishe kitu hapa. *1.Kuna kushushwa ukaondolewa katika kundi la watumishi wa Kristo wanaoupendeza moyo wa Mungu* ukabaki unatumika kwa nguvu kubwa lakini Wee ni Makapi katika ufalme wa Mungu,unatumika kama Ngazi, wapande wengine wafike ila wewe unaishia palepale. Mungu anaviacha vipawa vyake juu yako tu kwasababu ya watu wengi walio nyuma yako wanaohitaji msaada wako. *2.Pili, Kuna kushushwa kwa Kufungiwa kibali na Neema zote za Mungu zikaondolewa juu yako ukawa mtu wa kawaida sana. Ndipo utaona mtumishi flani aliwika miaka flani saizi KWISHA* utadhani siyo yeye, ndo chanzo cha watumishi wengine kwenda Kuzimu kutafuta Njia mbadala ili walinde heshima zao na nguvu zao,wanaamua kutumia Ushirikina katika kazi ya Mungu waendelee kuaminiwa,waendelee kutenda yale maajabu,au kuwa na kibali walichokuwa nacho mwanzo. ( _Unamkumbuka Sauli? Baada ya kukataliwa na Mungu akiamua kwenda kwa wenye pepo(mpiga Ramli) amsaidie kuongea na Mungu_ 1Samweli 28 soma yote.
🔫 Lakini katika utumishi wako wate chunga sana SIFA za watu,wengine wanatumiwa na adui wakupambe na kukupa heshima nyingine ambazo hukustahili kama mwanadamu,kuwa makini *TO NEUTRALIZE* (Zi punguzie nguvu)kwa KURUDISHA SIFA kwa Mungu wako,Roho Mtakatifu, Yesu Kristo mwenye kuyatenda hayo yote. 1PETRO 5:6....Nyenyekeeni chini ya mkono wa Bwana....Usikubali kupokea kila heshima na sifa.
⚰⚰Alama kuu ya mtumishi wa Shetani hata kama anamsema Yesu kwa nguvu, ni yule anayependa penda sifa,kuinuliwa, Anasujudiwa anafurahi, anapigiwa magoti anafurahi,wanamshukuru kwa kuwaponya,kuwafungua naye anakubali na kufurahi nakuongezea kuwa KWAKE *HAKUNA LINALOSHINDIKANA* Siyo kwa Yesu wangu hakuna linalo shindikana, No ni Kwake yeye. Huyo ni Marehemu katika huduma kama upo chini ya mtumishi huyo KIMBIA HARAKA toka chini yake utashushwa pamoja naye.
🔫Ni vizuri watumishi tujifunze kwa waliotangulia waliokuwa watumishi wenye nguvu kweli WALIJINYENYEKESHA pale watu walipo taka kuwachomekea sifa na upekee ili kiburi kiote,wao walikipinga kwa sentensi za wazi kuonyesha wao ni watu tu ila Yesu ndo juu
*Msikie Yohana Mbatizaji* ambaye Yesu anasema hakuna mkuu kuliko Yohana ila sikia watu walipo mchomekea sifa za kumpambanisha huduma yake na ya Yesu bosi wake alivyo wajibu.....
26 Wakamwendea Yohana, wakamwambia, Rabi, yeye aliyekuwa pamoja nawe ng'ambo ya Yordani, yeye uliyemshuhudia, tazama, huyo anabatiza na watu wote wanamwendea.
Yohana 3:26
27 Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni.
Yohana 3:27
28 Ninyi wenyewe mwanishuhudia ya kwamba nalisema, Mimi siye Kristo, bali nimetumwa mbele yake.
Yohana 3:28
29 Aliye naye bibi arusi ndiye bwana arusi; lakini rafiki yake bwana arusi, yeye anayesimama na kumsikia, aifurahia sana sauti yake bwana arusi.
Yohana 3:29
30 Basi hii furaha yangu imetimia. Yeye hana budi kuzidi, bali mimi kupungua.
Yohana 3:30
31 Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote.
Yohana 3:31
👉Napenda mstari wa 30,aloo huyu alikuwa mtumishi wa viwango vizuri vya unyenyekevu.
🔫Leo hii mitume,manabii, wachungaji,waimbaji wanajibizana kwenye Media na madhabahuni kuonyeshana Mimi ni Hatari,mkuu kuliko wote Tanzani,Afrika,Duniani wewee tayari we ni Gugu maji. Vipawa,karama umepewa kiburi cha nini,na ungevitengeneza mwenyewe.....ingekuwaje sasa?
👉Wee hatari kwa lipi?kufufua maiti?au *Kasingle kako kupigwa kila Media mpaka na kwenye baha?* Mshukuru Mungu na umpe sifa zake,sisi ni watumwa wasio na faida.
👉Mtumishi wa Mungu unayeingia kwenye hudumaa ikimbie Roho ya Kiburi,haraka sana unaposifiwa mrudishie Bwana sifa hizo na *_Msihi Mungu,omba,lia upewe moyo wa Kunyenyekea_* ili uwe mbali na Adhabu ya Kushushwa na Bwana na kukataliwa mbele zake.
🔫Kumbuka kiburi ni silaha ya kwanza inayozitangulia silaha zote,ikikushinda utapandikiziwa silaha zote 3,na yataibuka matabia mengi mengi mabaya ndani yako na katika huduma yako,utashangaa kila mtu hakukubali,basi tu wanakutumia kwakuwa ya Ka Kipawa uliko nako ila mioyo yao inakukataa na wengine kabisa Wanakufuta katika List ya watumishi wanaoweza kuwatumia.
🔫Lakini ukiishinda hii silaha aisee utaufurahia utumishi wako na utaona kila kona Kibali kinafunguka,watoto kwa watu wazima wanakukubali na kukupenda.
⚔ *Ila sasa jiandae kwa Silaha ya pili* inakuja kukujaribu kama nayo utairuka,kazi yako endeleza maombi,ongeza Maarifa nayo uishinde ili ubaki kileleni kwa Bwana.
_Fuatana nami katika Sehemu ya 10 ya somo hili maalumu la Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu,uijue silaha ya 2 inayo pambana na huduma yako_
*Ulikuwa nami mchambuzi wa mambo ya kiroho Ev Elisha Kazimoto*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto.
No comments:
Post a Comment