Monday, 6 August 2018

SEMINA YA SEHEMU YA 10

🛣 *SEMINA YA NENO LA MUNGU KUHUSU UTUMISHI WA MADHABAHUNI PA BWANA*🛣
   *_By Ev Elisha Kazimoto(Whatsapp  0755444078)_*
......................................
_Utumishi wa Kweli katika Kristo Yesu_
       *SEHEMU YA 10*
*Tambua Nguvu Kuu 3 Zinazo Pambana na Huduma yako*
..........
..........
..........
_Haleluyaa wana wa ufalme wa Mungu mnaotumika katika madhabahu Takatifu ya Mungu,nakuletea mwendelezo wa somo letu muhimu la Utumishi wa Madhabahuni pa Bwana sehemu ya 10,tuziangalie *Silaha 3 hatari* zinazo haribu Huduma nyingi za Kiroho duniani kote,na leo tunaingia Silaha ya 2._
2⃣ *TAMAA YA MALI NA PESA*
💰Hii ni Silaha ya pili kutumwa kwa mtumishi wa Mungu anayeingia katika Huduma,au aliye mkongwe katika huduma. Silaha hii inaachiliwa kwa mtu ili kuigeuza *_Nafsi yake badala ya Kumtumikia Mungu kwa Moyo wake wote, basi Nafsi yake Inaangalia Maslahi gani atapata katika kufanya kazi hiyo ya Mungu_* Anacho kitafuta shetani siyo kingine ni ili uende kinyume na Neno la Mungu kwanza,ukishatoka kwenye neno la Mungu utakuwa nje ya Mfumo wa Kimungu na utakuwa unaendeshwa na Ibirisi badala ya Roho wa Bwana.( MATHAYO 4:6-7)....Shetani hapa alimtengenezea Yesu Fauru moja ili amwendeshe ila Yesu alimshinda kwa kulinda Kusudi alilopewa na Kauli ya Neno la Mungu.
💰Unapoingia kwenye huduma ni muhimu kujua mambo ya fuatayo;
A)Huduma,Vipawa vya Roho mtakatifu Haviuzwi wala Havinunuliwi kwa bei yoyote.👇👇👇👇👇
18 Hata Simoni alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekewa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha akisema,
Matendo ya Mitume 8:18

19 Nipeni na mimi uwezo huu, ili kila mtu nitakayemweka mikono yangu, apokee Roho Mtakatifu.
Matendo ya Mitume 8:19

20 Lakini Petro akamwambia, Fedha yako na ipotelee mbali pamoja nawe, kwa kuwa umedhania ya kuwa karama ya Mungu yapatikana kwa mali.
Matendo ya Mitume 8:20

21 Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele za Mungu.
Matendo ya Mitume 8:21
👉Kuna watumishi ambao ugundua mapema Hila ya shetani na kuikwepa nao huduma zao ushika kasi na kumalizika kwa utukufu mkuu.
B)Heshima,sifa na kibali vinaambatana na huduma yoyote,hivyo Shahuku ya kuwa na maisha yanayoendana na sifa unazopewa,heshima uumbika kwenye moyo hapo ndipo watu uanza kutengeneza *Mbinu zao feki za namna gani ya kupa Mali,Pesa ili aendane na sifa yake* hapa ndipo watu uanza kubadirishana *Exchange* Kati ya Huduma ya Kiroho na Fedha/Mali.
💰👉 Hapa unielewe, kuna tofauti ya Njia za Mungu za kukufanikisha katika Huduma yako kwa Kukubariki, kuinua watu wakakubariki baraka za mwilini,mali na pesa baada ya wewe kutumika kwa unyenyekevu na moyo mmoja kwa Bwana kama mtumwa asiye na Faida.👇👇👇
_Vivyo hivyo nanyi, mtakapokwisha kuyafanya yote mliyoagizwa, semeni, Sisi tu watumwa wasio na faida; tumefanya tu yaliyotupasa kufanya._
*Luka 17:10* na kuna Mtumishi anayetumia Neema alopewa kubuni mbinu za Kuchuma pesa na mali.
C)Katika huduma kuna Neema ya Pekee unapewa na vitu (vipawa )vya kuwahudumia watu nao wanakuhitaji mno kwa Gharama yoyote ili mradi wapate wanachokihitaji.
💰👉Hapa ndo utakuta watu Wanauza Uponyaji, *Ili uombewe Sharti ulipe Pesa,au mali,ili Uonane na mtumishi wa Mungu akuhudumie kwa karama alizo pewa na Mungu sharti Ulipe* Japo mbinu hizi zinapakwa rangi flani ya maandiko,au lugha laini *Eti Sadaka Maalumu, Mbegu,Sadaka ya ukombozi* nk... hapa kuna tatizo la kiroho na Uvamizi katika huduma jua kwa mtumishi huyu kama hajashtuka kuna *_Roho ya Tamaa ya Mali na Pesa_* inawinda roho yake na Huduma yake, ili Kumwondoa katika List ya Watumishi wa Kweli wa Yesu Kristo( MATHAYO 10:8)
👉Wengine wanaitwa kufanya huduma anapanga Kiwango,cha kuachia familia, kiwango chake mwenyewe na mavumbuzi mengi(unielewe vizuri, _Sizungumzii nauli ya kukusafirisha katika huduma, nazungumzia kiwango umachopanga cha wewe ili wakupate uwape huduma lazima iwe mil2,3,5 yakuacha nyumbani na matumizi yako_) hapa kuna shambulio.
💰Pesa ni nzuri,na imetupasa tuitafute kwa nguvu kubwa katika njia sahihi ya za Mungu,ila *Pesa isilipue mioyo yetu na kuacha Kulitumikia Kusudi la Mungu* tukaanza kulitumikia kusudi la Pesa. (1PETRO 5:2)....Adui wa wa Huduma ni Kupenda Pesa,kutanguliza pesa badala ya Huduma.
💰Kuna watu wanashahuku ya kuingia kwenye Huduma si wamtumikie Mungu ila wajitajirishe,wapate Maslahi yao( *Hao ndo mbweha*) unajua kwa wanao Tumika chini ya Upako wa Kishetani ni haki yao Kuuza Huduma,kwakuwa nao upako wameupata kwa gharama kubwa ya Kafara,damu za watu,waumini wao wamekabidhiwa kuzimu(wako rehani), kwa kuuza nafsi zao kwa shetani,akitoka huko anatoka na uchungu mkubwa lazima kila kitu kitauzwa ili afidie gharama ya nafsi yake au damu za watu alotoa kafara.
💰👉Na wengine kwa kutumika na Shahuku ya kutaka watoke kimaisha kwa kutumia Huduma,wamejikuta huduma zao haziendi,zinakosa kibali mbele za Mungu na mbele za wanadamu,wanaingia kwenye tuhuma nzito za kuwachafua kiutumishi,kwakuwa huduma zao haziongozwi kwa Msukumo wa Roho mtakatifu wakutaka Mungu ainuliwe bali wanatafuta wao wajulikane na kufanikiwa. Wengi wao wametumbukia kwenye nguvu za Giza ili mambo yao yaende.
👉Wewe uliyejipanga kumtumikia Mungu aliye hai tulia kwa mkono wa Bwana,jiulize je Wampenda Yesu na Kazi zake kuliko Mali na Pesa?( YPHANA 21:15-17) Mpende Yesu,mtumikie kwa moyo wako wote,mwombe Mungu akufanikishe akupe baraka zote za kiroho na za kimwili kwa kadri apendavyo yeye.
*_Nikupe siri moja mtumishi,Mafanikio katika Utumishi wa Kweli wa Yesu Kristo yanahitaji Uvumilivu mkubwa sana,na kumwamini Mungu unaye mtumikia kuwa upo wakati wa Bwana wa kukufanikisha_* wengi wa watumishi wanatumika kwa kuangalia watumishi wenzao walivyo fanikiwa nao wanaanzisha harakati waingie katika ushindani na wao wakimbizane na Mafanikio  nao wawe na heshima kubwa, ndugu utapotea. *Waweza vipata Ila ukaishia Duniani hapa* usiuone uzima wa Milele.Sasa hapo kunafaida gani ya kutumika?maisha ya duniani ni miaka 120,maisha ya mbinguni na jehanamu ni Mile na milele chagua mwenyewe. Endelea kukimbizana na Mali na Pesa ukibadirishana huduma na pesa lakini kumbuka unakimbizana na Mauti ya pili Jehanamu,wengine tunausubiri wakati wa Bwana wa kufanikiwa,tunaziombea roho zetu *Zisiwaze pesa na mali kwanza kupitia huduma* bali ziwaze kwanza *Watu wa Mungu wanawezaje kufunguliwa na Kristo kuinuliwa* na sisi Mungu atukumbuke kutubariki.
_Niishie hapa nikukaribishe katika sehemu ya 11 tutakapo iangalia silaha ya 3 na ya mwisho kwa Kadri alivyo nifunulia Mungu,alipokuwa akiniandaa kwa utumishi wake_
*Ulikuwa nami Mwl, Ev Elisha Kazimoto*
WhatsApp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

No comments:

Post a Comment