Tuesday, 7 August 2018

SWALI KUHUDUMIA WAZAZI KAMA WANANDOA

*Swali*
Ivi ikitokea umeoa alafu mama yako mzazi akapata matatizo ya kiafya ambayo yanalazimu tu ukae nae umuuguze, tena hayo matatizo ya kiafya siyo ya kupona Leo au kesho, (ingawa anakuwa siyo serious sana)
Alafu mke wako akawa hataki kukaa na mama yako mzazi, utafanyaje?

Naombeni mchango katika hili ndugu zangu.
........
........
Anajibu,Psychologist & Counselor *Ev Elisha Kazimoto*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

....................................
*_Mada hii tuihitimishe kwa Mtazamo huu wa Kisaikolojia na Kiroho na Kibinadamu_*
👉Kwanza niizungumzie ndoa kama ndoa katika Context ya Kisaikolojia.... Ndoa ni muunganiko wa Hisia ambatano za watu wawili me na ke,ambao mioyo yao imeaminiana na kuridhiana kuficha mapungufu ya mwenzake na kutosheleza mahitaji ya kihisia ya mwenzake.
ukiijua ndoa kwa mfumo huu wa kisaikolojia,utawaza zaidi nje ya box,mwenzangu anaupungu wapi hautakimbilia kuufunua,ila utakimbilia Kuufunika ili abaki akiwa mwenye Sifa na siyo Aibu mtazamo wa kwanza ni kulinda Status ya mwenzako kwa jamii inayowazunguka na watoto wenu.
Pili, Kisaikolijia mpaka umeamua kuishi na mtu kama mmiliki wa Hisia zako milele, maana yake Umemuamini hawezi Kuangusha moyo wako,awezi Shusha Hisia zako bali kuzipandisha. Na Hisia ziko ndani ya mtu ila hisia Utibuliwa na Mazingira kwa sababu hiyo kazi ya mwana ndoa ni Kuhakikisha anatengeneza mazingira kwa mwenzake yakutibua hisia za furaha siyo kutibua hisia za Masikitiko na uzuni.( Kumbuka najibu swali la mwana ndoa huyu baba mwenye mzazi mgonjwa lakini mke kama anaweka ngumu kumuhudumia) unganisha doti za kisaikolojia hapo,mwisho utaona shida iko wapi na wajipange vipi.
👉Tatu, Ukiamua kuoana na mtu,ujipange kutosheleza hisia zake,mbali na hapo hukufaa kuwa naye(kosa kubwa la kiufundi wana ndoa wanafanyaga) aidha kwa kutojifunza au kwa kuya dharau mambo au kwa kulipa kisasi badala ya kuondoa sumu. *_Kumtosheleza mwenzako, Kisaikoljia ni kuhakikisha shahuku ya kitu aliyokuwa nayo inakamilika,aoni kupungua ila anaona kupata msaada kama umemtua Mzigo)_*  kumwacha mwenzako analalamikia kitu ambacho aliona unauwezo wa kukikamilisha ila umekitupilia mbali,kwa kutojali,kwa kuupuza,au kuona haikuhusu sana wewe NI KOSA LA KISAIKOLOJIA linaloweza gharimu ndoa yako
👉Kimtazamo wa Biblia Ndoa ni Agano la milele la watu wawili me na ke waliokusudiwa na Mungu kuwa mwili mmoja, kuishi maisha ya umoja na upendo ili *Wakamilishe Kusudi la Mungu kuwaunganisha wawili* Ndoa ina mtawala( Mwanaume) ambaye ndiye msimamizi na mtoa mwongozo wa maisha ya kila siku( angalizo alopewa) ni _Asitawale kwa mabavu ila kwa upendo na huruma_ (kwa lugha ya utawala kuna mtawaliwa anayepokea maelekezo na kuya tekeleza bila kunung'unika ambaye ni mke)
👉Dhana ya Msaidizi hii imetafsiriwa vibaya na wana ndoa au watu wengine kulingana na hisia zake na mwelekeo wa matakwa yake. *_Lakini dhana ya Usaidizi na kufanana naye_* inabeba Mtazamo wa Kuhakikisha aliyeletwa katika maisha yako *Anawezeshwa Kutimiza Kusudi la Mungu lililowekwa kwake(ndani yake)* hii ndo Dhana ya MSAIDIZI. (dhana hii haiangalii   kazi tu na majukumu) na kumtazama mtu mke tu ndo amekuja kusaidia huo ni mtazamo wa chini sana wa kimwili.(Ndoa ni Equal Sharing)
👉Lakini kusudi la Mungu ni *Uwe mwezeshaji wa Mwenzako Kutimiza Kusudi la Mungu* na hii ni kwa watu wote Mke na Mme wote ni Msaidizi kwa mwenzake,ila Mungu alitumia Lugha kwa Adamu ya *Nitakufanyia Msaidizi* kwa kuwa Adamu ndo aliye kuwepo kwanza bila uwepo wa mwana mke yeyote na binadamu yeyeote,na alipewa maelekezo kwanza yeye na kwa kofia yake ya utawala alikuwa akipewa taarifa anakuja mwezeshaji mwenzako wa kufanana na wewe. Ila ukienda ndani zaidi unaona Uwezeshaji huu si wa mwanamke tu kwa mwanume,ila ni kila mmoja anamwezesha mwenzake,utaona pale MUNGU anaposema *Si wawili Tena bali ni Mwili Mmoja* hapa ndo anaunda kitu kinachoitwa Marriage Two way Traffic (ndoa ni maisha mpeanao toa-pokea)kwa kuwa mwili mmoja inakufanya uwe sawa na mwenzako (Similar but not the same) kwahiyo Mnasaidiana kutimiza lengo kila mmoja alilowekewa maishani mwake
👉Na ndiyo maana Aliposema Msaidizi hakuishia hapo aliongeza *Wa Kufanana Nawe* dhana ya kufanana hailengi tabia,kimo na uzuri,inalenga SOME ONE TO FIT IN YOUR LIFE(mtu wa kujaza kwenye mapungufu yako,siyo mwenye mapungufu kama wewe) anayeweza kuziba bonde lako,na kushusha kilima chako(na yeye ana bonde na kilima) ili mwende mbele sambamba (mke au mme)
👉Hapa kuna mfano mmoja muhimu sana ningekuwa ubaoni ningechora ila pata image hii, *_Kuna chain ya baiskeli au pikipiki,(wengine wanaita mnyororo kiswahili kisicho sanifu) na kuna ring ya meno ambayo chain inazumgukia kusababisha mwendo(inaitwa Freewheel )nimetafuta kiswahili chaki sijapata. Sasa chain  ni mwanamke,na freewheel ni mwanaume,kawaida ya chain ina matundu matundu na freewheel ina meno na nafasi)nenda kachunguze kutembea kwa baiskeli au pikipiki ni matokeo ya Jino moja kukanyaga kwenye tundu_*(gap  au mapungufu)ndo dhana ya kufanana.(kwa mantiki hiyo chain inafanana na na ringi la meno(freewheel ) ila kama yote ni chain,au yote ni maringi yenye meno huko sio kufanana huko ni KUENDANA kwa mtazamo si kwa matumizi
👉Katika mtazamo wa kibinadamu ndoa ni watu waliopendana kusaidiana katika shida na Raha na kujenga maisha yao.
*_Ukiiangalia mitazamo yote 3 inagusia kitu cha Kubebana pale panapotokea changamoto yoyote kwa mwenzako,ili kumfanya mwenzako naye afurahie ujio wako kwenye maisha yake_*
⚔ Sasa nizungumzie *Dhana ya wana ndoa na kuhudumia familia zao* kuna jambo ambalo ni la kiufundi ukilikosea linakugharimu ila ukitulia na kutumia hekima mnaliweka vizuri maisha yanaenda kwa amani.
👉1⃣ Kwanza ifahamike ndoa ni Taasisi inayo jitegemea na kujiendesha bila msukumo wa mtu yeyote kutoka nje au upande wowote wa familia iwe kwa mme au kwa mke,awe aliyeoa au kuolewa ni mdogo wa mwisho au wa kwanza katika familia, akisha Ingia kwenye ndoa hiyo Ni *Serikali kuu inayojitegemea* isiyo guswa/amrishwa kutoka nje isipokuwa wana ndoa wao wawili na Mungu wao, wengine Niwashauri,na Mnatumia maombi Siyo kauli ya Lazima/au Maagizo  kupata msaada kutoka kwa serikali hiyo.
2⃣Kuwa Taasisi inayojitegemea(wana ndoa) Haiwaondolei Sifa ya kuwa watoto kwa wazazi au ndugu wa ndugu zetu,haiwaondolei wajibu wenu kwa wazazi wenu na ndugu zetu kuwahudumia au kuwasaidia.
3⃣Mnahitaji kuwa na mfumo wenu wa makubaliano kama Taasisi inyojitengemea namna ya Kuzihudumia Familia zenu kwa kadri ya uwezo wenu huku mkiangalia namna ambavyo hamuwezi Athiri Uhuru wenu au Taasisi yenu.( hapa kunahitaji kupeana taarifa,kuelekezana,kushauriana kwa pamoja mpaka kufikia muafaka)
👉Shida kubwa katika kipengele hiki cha 3,kuna shida ya *Double standard* (Kupendelea familia yako kuliko ya mwenzako) hapa hamuwezi kufikia muhafaka mpaka muwe mmejenga msingi wa kuzibeba familia zote kwa usawa pale inapotokea shida au raha.
👉Chamgamoto ya pili ni Udhibiti wenu wa mwanzo tangu mnaoana wa ndugu,wazazi kutokuwa na usumbufu,kero kwa moja wenu( *Namna unavyo mlinda mwenzako asishambuliwe na familia yako*) inamfanya kuwa na imani nawe na familia yako,atakuwa huru kuwahumia kwa hali zote..
👉Changamoto nyingine ni kupeana taarifa halisi za familia yako,siyo kushtukiza ila kila mtu awe anajua kinachoendelea mana ho wote ni wazazi wenu au ndugu zenu.
_kwa pointi hizo hapo kijina mwenye shida katika swali hili la kifamilia anaweza ona wapi kulitokea shida_.
NINI KIFANYIKE.?
👉Uwenda mke hataki kumuhudumia mama wa kijana kwa kumleta hapa kwake kulingana na mazingira ya familia yako,nafasi,uhuru kama wana ndoa, au uwenda anaogopa kuingia kwenye mgongano na familia ya mke maana katika kutoa huduma huwezi toa 100% je,anaouwezo wa kubeba lawama?hivyo vinaweza kuwa baadhi ya sababu.
👉Lakini kulingana na uwezo wao wa kiuchumi na kimaisha(kama wana panga au wamejenga) kijana ampe somo mkewe kuhusu umuhimu wa wazazi wao katika maisha ya baraka na laana,na leo kwa kijana kesho kwa mwanamke aonyeshe wajibu wao kwa wazazi,pili wakubaliane njia ipi anahitaji mke itumike kumuhudumia mama? ( *Wa mwache kijijini watume pesa,huduma itatosha? Waajili mtu wa kumuhudumia kijijini? Au waajili mtu wa kumuhudumia hapa nyumbani, amsikilize mke anachagua njia ipi lakini MAMA APATE HUDUMA INAYO KIDHI.
👉Na kijana atumie saikolojia ya kuongea na mama yake na baba kama yupo,njia wanayoona inafaa kumuhumia mama,asionyeshe ugumu wa mke wake ila amlinde ionekane ni makubalianao yao wote au maamuzi ya mme. Mama ahudumiwe.
👉Lakini kama mke anaonyesha kutokuwa na dhamira njema ya mama wa kijana kuhudumiwa kwa namna yoyote, hapo ndipo MAAMUZI YA KIUME KAMA KICHWA CHA FAMILIA YACHUKUKIWE yenye busara,mama asiumie na yeye mme asiumie,hapo asimlete mama maana anaweza pewa hata sumu au asipate huduma inayohitajika mama akaacha laana kabla ya kufa. Ahakikishe anatumia njia yoyote kwa gharama yoyote Mama ahudumiwe.
👉Njia ya mwisho,naamini huyo kijana hakuzaliwa peke yake,kama kuna ndugu anayeweza kumchukua mama aongee na ndugubzake ili yeye akaiwezeshe familia hiyo na kusaidia gharama za matibabu basi wafanye hivyo kwa makubaluano.
*_Niishie hapo ukikuwa nami mchambuzi wa masuala ya mahusiano na ndoa Msaikolojia na mshauri Ev Elisha Kazimoto_*
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto.

No comments:

Post a Comment