Wednesday, 8 August 2018

MAHUSIANO YASIYO NA MAWASILIANO

💞 *USIMUUMIZE MWENZAKO KAMA UMUHITAJI,UMEMCHOKA*💞
   *_Anaandika Mwanasaikolojia na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa_*
       Ev Elisha Kazimoto(WhatsApp 0755444078)
Facebook Elisha Kazimoto
Call 0657557570
.........
.........
_Karibu katika kona ya Saikolojia ya mahusiano na mchambuzi wako Ev Elisha Kazimoto_
❣Kumekuwa na *Changamoto kubwa* ya watu walio katika mahusiano ya uchumba,au urafiki wenye lengo la kuelekea kwenye uchumba,uchumba uzae ndoa changamoto ya *_Kusua sua,kuyumba,kushuka kwa Mawasiliano yao_* ikiwa na kisingizio cha mmoja wapo yuko busy, au basi tu hana Mood ya kuwasiliana na Mpenzi wake. ( _Usiumize moyo wa mwenzako, kama umuhitaji au umemchoka_)Mwambie ukweli aendelee na misha yake atapata mtu wa kumpetipeti.
❣Kwanza niwasaidie kitu kimoja wana mahusiano(wachumba), *_Uhai wa Mahusiano(Uchumba) yoyote ni Mawasiliano_* nguvu ya na kiwango cha mawasiliano baina ya wapenzi ndicho kiwango cha *Upendo* kati yenu,au alicho nacho mwenzako juu yako.
❣Angaiko la mwenzako kukutafuta(kukuona au kukusikia kwanjia ya simu kwa siku,ndicho kiwango cha Hisia alicho nacho juu yako)
❣Ikumbukwe,upendo ni Hisia,na hisia hazionekani kwa macho zinaonekana kwa vitendo( *Reaction*) na Njia kuu ya Reaction ni Mawasiliano..
❣Mahusiano hayakui,mahusiano hayawi imara kwa zawadi,kwa maneno ya Nakupenda,yanakua, na yanaimarika kwa ninyi kuwasiliana mara kwa mara.
❣Utajuaje yakuwa umejaa moyoni mwa mwenzako au mwenzako amejaaje moyoni mwako, ni pale ambapo *unapita muda flani bila kuwasiliana na mwenzako,masaa 6,12siku 1 pengine kwa sababu maalumu kubwa* nini unasikia moyoni,angaiko la kumtafuta? Unahisi upweke? Unahisi kuwa down,au unasikia Kawaida tu muda wowote utamtafuta tu haina shida?( _Hapo ndo utajua Mahusiano haya yana Afya,haya yapo ICU haya ndo yameisha ingizwa kwenye jeneza ni muda wa Kumuaga marehemu_)
❣Mtu yeyote aliyekwenye mahusiano Hai,yasiyo na migogoro,ambayo watu bado wanahitajiana,mawasiliano yao ni *Hot(ya joto kubwa)* muda wote.
❣Angalizo, hakuna *_Kigezo chochote ambacho mtu anaweza shikilia kuwa Yuko Busy kiasi cha kumaliza siku 1,2 wiki bila kuwasiliana na mwenzake na ikawa ni Tabia_* kama si kwa dharula kubwa.
❣Najua ziko kazi flani mazingira yake ni magumu sana kwa mawasiliano, ila maswali yangu kwako ni kama 2,3.
1. *Uko busy mpaka kwamba Huli chakula?* Dakika za kula huwezi kuchati na mwenzako? Akaona unavyo jali?
2. *Huna muda wa mapumziko hata dakika 10,tangu asuhi mpaka usiku?* ukamwambia mwenzako Hi.... Niko busy ila nimeona dk 5 nisikie sauti yako?
3. *Huwa hulali masaa 24 wewe uko busy kazini*?(muda huo wa kulala ndiyo ungemjulisha mpenzi wako mkatumia hata dakika 10 tu kuwasiliana na yeye kwakuwa anajua mazingira yako ya kazi basi,muda huo angekusubiri).
4. *Huna salio kabisa hata la kubip*( miongoni mwa Angalizo la kisaikolojia kabla ya kuingia kwenye mahusiano,ni _"Kabla ya kuanzisha mahusiano lazima ujue Mahusiano ni Gharama"_ huwezi kugharimika kulinda mahusiano,kujenga mahusiano basi Usiingie kwenye mahusiano *Utamsumbua bure mwenzako na kumpa mawazo ya bure* Miongoni mwa vitu vinavyo gharimu Akili ya mtu na moyo wake ni Mahusiano kuwa Hafifu.
*Ukiona Mwenzako katika Mahusiano ya Uchumba anakwambia niko busy,niko busy,siku ya 1,2 4,5 wiki jua kuna viashiria vifuatavyo*
1⃣Umeanza kuchuja moyoni mwake,umeanza kupungua umuhimu na uzito wako kwake.( Jiandae kisaikolojia break up iko njiani)
2⃣Kuna mtu anajaza nafasi yako(nafasi yako imeisha zibwa na mtu ila uwezi ambiwa kwakuwa hamja itirafiana ikatokea sababu ya kukuacha.) _Kaa mkao wa kutokosea ukikosea utalimwa kadi nyekundu ya kukutoa nje_
3⃣Unaandaliwa kisaikolojia kupokea taarifa za kusitisha mahusiano.(anakuandaa uanze kumuondoa moyoni na akilini ili hata akikuacha usiumie)huyo ametumia kanuni ya Yusufu... *kukuacha kwa siri*.
4⃣Hiyo ni ishara na Alarm kwako ya aina ya mme au mke utakaye oana naye alivyo na moyo wa *Kuto jali*( _Jipange kuzoea hali hiyo usije ukapata ulcers bure_)
👉Mlioko kwenye mahusiano yoyote, kwa nini Umtese mwenzako kama huna mpango naye tena kwa nini usimwache huru? Kwa nini uendelee kumpotezea muda kukutafuta huku unamwambia uko busy lakini una mpenda *Huu ni uongo,unajua mtu anayependa anagharimika kutimiza hisia zake na za yule ampendaye?* wewe Hukumpenda Ulimtamani sasa tamaa imeisha umeanza kupiga chenga.
👉Mahusiano yoyote yakipoteza mwelekeo wa Mawasiliano hayo HAYAPO TENA kuna kivuli ila Halisi alishaondoka.
*_Nimalizie kwa kusema,ukiona mwenzako mwanzoni mawasiliano yalikuwa moto,kuonana,kupigiana simu,chatting za hapa na pale saizi inapita siku,3 wiki na mkiongea ni dk 10 na lugha unaisikia siyo ya mapenzi ya dhati ni kavu kavu,majibu ya mkato,vi sms vifupi na vikavu, anza kujindaa kuokoa moyo wako kutoka katika kujeruhiwa VUNJA MAHUSIANO HAYO HARAKA bila huruma Kama hataki kubadirika_*
          Ulikuwa nami mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto*
Whatsapp 0755444078
Call 0657557570

No comments:

Post a Comment