*Swali*:
habar ndugu
Naomba mnisaidie nini nifanye
nilioa tumekaa na mke mpaka akashika mimba kakaaa miez 9 akiwa anakaribia kujifungua akaomba akajifungulie nyumban kwa uangalizi zaid kwakuwa tuko jilani na kwao mwendo wa vijiji 3
sasa baada yakujifungua anagoma kurudi kwangu
tatizo analodai ni watoto nilio zaaga enzi za ujana nikiwa mwislam nilivo okoka ndo nikamuoa yeye na hayo yote nilimwambia kabla ya kumuoa
saizi mama mkwe ananiambia uyu mwanangu sio wakumsuka twende kilioni au kilimanjalo
na staki mwanagu awe mke wa 4
lakini mihao mabinti nilio zaa nao wote wameolewa na wanafamilia zao
jamani imenivuruga akili nilishukuru kanisani nikiwa nafuraha mke wangu akiwa na mimba ila leo nalia sipati jibu naomba nisaidieni jaman
..........................................
*_Anajibu Msaikolojia na Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa Ev Elisha Kazimoto_*
........
........
*Nihitimishe Mada hii kwa Mtazamo wa Kisaikolojia na Kifamilia*
Mchambuzi Ev Elisha(whatsapp 0755444078)
❣ _Maisha ya ndoa yanahitaji mambo kama 3 kwa watu makini waliokusudia Kuoa au Kuolewa_
1⃣ *Ndoa inamwitaji Mungu* _Hii ni kwa wale wanaoamini katika Mungu na nguvu zake na ukombozi wa mwanadamu kwa njia ya Yesu Kristo_ Hapa mwana ndoa inakulazimu kila siku katika maombi yako kujiombea ( *Mapungufu yako yasiwe mwiba kwa mwenzako*) na kumfanya ajute kuoana nawe,lakini mapungufu yako yasiwe chanzo cha migogoro katika ndoa yenu. Pili unahitaji kumwombea mwenzako(Mapungufu yake uyaone ni sehemu ya ubinadamu kila mwanadamu anamapungufu,ila Mungu akupe Neema ya kuyajaza/kuyafunika ili muishi kwa amani).
👉Katika sekta hii ya kumwitaji Mungu katika ndoa,ni muhimu sana wana ndoa kujua, Amani,Upendo na Furaha katika ndoa ndiyo ustawi wa mafanikio ya familia ya wana ndoa na ndo sumu ya kuua ubaya wowote unaokuja kutoka nje ya ndoa yenu,lakini mnapaswa kujua *_Hakuna kitu kinawindwa katika maisha haya ya mwili kama ndoa_* ni kwasababu ndoa ndo chimbuko la mambo yote mema na mabaya,(ibada safi kwa MUNGU na ibaya ovu ya mashetani vyote vinaitegemea ndoa.)
👉Kwa maana hiyo,kwa changamoto yoyote inayotokea katika ndoa kwa mwenzako *_Usiwahi kwanza kumshambulia mwenzako na kumuona mwenye makosa,kwanza angalia nini MTEGO WA SHETANI kupitia changamoto hii analenga KUKUDHOHOFISHA upande upi?, kiroho,kihuduma,kiuchumi,nk_* tafakari kwa muda,uwe mfupi au mrefu kidogo ndipo uombe Neema ya njia ya kutatua changamoto hiyo.
👉Mbali na hapo jiwe moja mnalo rushiwa na adui la changamoto ndogo au kubwa linaweza kupiga vitu 5 mpaka 7 na kuvijenga inakuwa ni gharama na makovu ya kudumu.. *Jiwe lina kuja moja ila*....
i)Linapiga ndoa inatokea Divorce(kuachana)
i)Linapiga amani mnaanza kuishi kwa kupishana ndani kama basi na bodaboda(kununiana)
iii)Linapiga kiroho chako(aliye na majeraha ya moyo hawezi kumsogelea Mungu kwa furaha)
iv)Linapiga huduma(unaanza kuona huduma ni ngumu,unaifanya kiubishi maana ndani moto unawaka)
v)Linapiga watoto(mnakuwa na malezi mawili tofauti,kuna watoto wa baba na wamama,au wanakosa kauli moja ya wazazi wanapata kauli nyingi)
vi)Linapiga maendeleo, (katika migogoro huwa hakuna maendeleo kuna kupambana kujihami)
*_Mwana ndoa, ndoa yako niyakuombea sana kila siku inawindwa mno ila Mungu niwa Neema anatupa kushinda_*) Point to Note: Kumbuka HUJAOA AU KUOLEWA NA MALAIKA,WALA HAMPO MBINGUNI,kwa hiyo jipange kumsaidia mwenzako kama mwanadamu aliyeko duniani na Si kumlaumu kama malaika aishiye mbinguni.
*Kwa hiyo baba huyu kama anamjua Mungu ayatafakari haya,na kuyafanyia kazi Bado nafasi ipo ya kubadiri mabaya kuwa mema.*
♦Bado uko na mimi Mwanasaikolojia na mchambuzi wa Masuala ya mahusiano na Ndoa *Ev Elisha Kazimoto* tuigeukie sehemu ya Saikolojia.
2⃣ *Kisaikolojia* _Ndoa ni Hisia ya upendo kwa mwenzako,zinazo kuonyesha upekee,uzuri,ubora wa mwenzako na uwezo wake wa kutimiza furaha yako ya maisha_. 👉Kama *Ndoa ni Hisia* basi hisia huja,hisia utoweka,hisia ulindwa,haya mambo 3 ni muhimu kuyajua kama mwana ndoa.
👉 *Hisia uja, Hisia Ulindwa* Hisia kwa lugha nyingine zinatengenezwa, kuna mazingira yakiwekwa namna flani yanatibua hisia,kazi ya mwana ndoa ni kuhakikisha anajitahidi To develop(kutengeneza) hisia zilizo mfanya mwenzake aone yeye anafaa kuwa mwenza wake na kujitahidi kila mara kutafuta vitu vipya na kuboresha vilivyopo ili kuhakikisha hisia za mwenzake zina kaa juu yake.
👉 *Biblia ina sapoti Saikolojia hapa ona kitu hiki anachokisema mtume Paulo ni cha kisaikolojia cha kulinda Hisia,kuchochea hisia*
33 bali yeye aliyeoa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mkewe.
1 Wakorintho 7:33
34 Tena iko tofauti hii kati ya mke na mwanamwali. Yeye asiyeolewa hujishughulisha na mambo ya Bwana, apate kuwa mtakatifu mwili na roho. Lakini yeye aliyeolewa hujishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi atakavyompendeza mumewe.
1 Wakorintho 7:34
👉Ukiyajua hayo changamoto nyingi zitapungua katika ndoa yako. Wengi wa wana ndoa wamesahau kipengele cha Saikolojia wamezama rohoni na rohoni nako hawafanyi yote yanayo takiwa wamebaki katikati, wengi wao *_Wakioa na kuolewa wanaona WAMETIMIZA NDOTO basi wanabaki kuishi kawaida bila kuhangaika kwa mwenzako.Ndo maana mtu anaweza ona mwenzake kawaida,asijiangaishe kutafuta namna gani ampendeze ila tu bora liende,na ikiwa bora liende ndo Kuumizana kunaanza kuja na mtu hajali kwamba amekuumiza,anaendelea na maisha yake. Huu ni UDHAIFU WA KUTOJUA SAIKOLOJIA,kila siku tunajifunza tufanye vizuri,si kwamba tumejua yoote yatosha ila Tunaongeza maarifa siku kwa siku ili tulinde Furaha yetu_* hapo ndo tunazitendea haki nafsi zetu.
👉 *Hisia Ufa* Kufa kwa Hisia ni kifo kibaya katika ndoa(kwakuwa ndoa ilikuwepo baada ya Hisia Kuzaliwa kati yenu na kuwa hai), Hisia ikifa ndo mwisho wa Mategemeo yako yote ya kimaisha katika kuwa na mwenzi. ( Hisia kufa ni matokeo ya Kurundika changamoto na makosa madogo madogo yasiyo tafutiwa ufumbuzi),lakini pia Hisia ufa ikiwa ni matokeo ya Kutojali Hisia za mwenzako na zako zinakufa juu yake. *_Ndo maana wana ndoa wengi waweza ona wanaishi,lakini wanaonana kama mtu baki tu,basi tu nimezaa naye watoto,_*) _Yaani asikii shahuku,mvuto,hamu kwa mwenzake kama aliyokuwa nayo wanachumbiana au wameoana wiki za kwanza_ (Kataa kumzoea mwenzako kiasi cha kupoteza hisia zote juu yake) Watu ambao hisia zimekufa utaona mambo yafuatayo:-
i)Haoni faida,furaha,na umuhimu wa kushiriki tendo la ndoa na wewe,anaweza shiriki au akatamani kushiriki na hata watu baki wa nje,watoto, vijana wakike au wakiume wadogo,wazee tena kwa shangwe kubwa ila kwako hakuna.
ii)Hana muda hata wa kuongea na mwenzake(chatting /kupiga story) hakuna kitu kama hicho,ila anaweza piga story na wengine kwa furaha na vicheko ila kwa mwenzake ni *Maswali na majibu* ( _Hiki kiko wapi,.... Pale...., pesa ya mboga....... Njoo uchukue..._) hiyo ndo life style ( Tafsiri ya kisaikolojia ni Hisia zimekufa juu ya mwenzake)
iii)Kumzungumza vibaya mwenzako kwa watu wengine nje. Yaani kati ya viashiria vibaya sana kwa ndoa iliyokufa hisia ni mwana ndoa kuzungumza Udhaifu wa ndani kwa watu wengine si kwa kumsaidia ila kama kumkomoa,kumwaibisha aonekane ovyo,si lolote,...Kumbe anajivua yeye mwenyewe. Hisia zikiwa bado hai wana ndoa wanakuwa na lugha moja,wanafichiana Aibu,wanalindiana Heshima.(Soma Matendo ya Mitume 5:1-12) *_Baadhi ya wengine waweza kupigana,kutofautiana ndani ila wakienda nje kwa watu utadhani wanaishi mbinguni_* hawa si kwamba ni wazuri kwa wafanyacho,kuna kona ya saikolojia na kiroho bado imewashinda ila HISIA HAZIJAFA, zinapotea na kurudi.Wanahitaji wasaidiwe ili walinde hari ile wanayoonyesha kwa watu ikae na nyumbani mwao.
👉Kwa mantiki hiyo, baba huyu inabidi afanye Assessment (uchanganuzi) wao wapo level gani hisia zimekufa au bado na maisha yao kabla ya kwenda nyumbani yalikuwaje,kuna changamoto zilikuwa zinajitokeza wanazi handle(tatua)vipi,au zilijirundika zikatengeneza sumu baada ya kwenda kwao zimeanza kurudi moyoni na akilini ndo zinampa ugumu wa kurudi. Akisha fanya uchambuzi huo na kujua apate nafasi ya kwenda kukaa na mke wake waongee kama wana ndoa kiufundi siyo kimamlaka aone kama anaweza fyonza sumu yote na kupanda sura mpya ya mabadiriko.
3⃣ *Ndoa Kijamii/Kifamilia* Hapa niongee na mke,mme na wazazi wote mnaosoma uchambuzi huu. _Ndoa niya watu wawili walopendana katika shida na raha,wao ndo wanayatazama maisha yao na kuyapenda au kuyachukia,na wao ndo wana mikakati ya kuyaboresha, wengine wooote ni washauri wasio na Maamuzi kwa ndoa( *Biblia imesema ndoa na hiheshimiwe na watu wote*) wazazi,ndugu,marafiki yaani wote... Inapotokea wazazi,ndugu,watu wakaruhusiwa Kuisemea ndoa yako,kuwa na maamuzi ya ndoa yako,kuwa nauwezo wa kuzuia au kuruhusu hisia zako mpaka hapo ndoa yako ipo matatani haiwezi simama_ kumbuka Binadamu wote tumeumbwa kwa hisia na mitazamo tofauti tofauti, *_Unachokipenda wewe mwingine anakichukia,unachokiona wewe kinashida,mwingine anakiona kawaida sana, unachokiona tabu mwingine anakiona ni changamoto ya kawaida_* sasa hapa ndo watu upoteza ndoa, maana wewe mwenzako ulimpenda, anawatoto,anamaisha ya chini, ila wazazi,ndugu,marafiki wanakwambia HAIWEZEKANI ukaishi maisha hayo kaa hapa nyumbani, nawe unakubali.. Tafsiri ni kwamba hujui Hisia zako na maana ya ndoa.
👉Lakini anayekushauri usirudi kwa mmeo,au muachane yeye *Ana mume wake,au mke wake* hawajaachana,si kwamba wao hawana changamoto,zipo nyingi ila wanavumiliana,wanalindana wanaenda bado wapo pamoja,ila wewe unashauriwa usikae kwa mmeo.(TUMIA AKILI)
👉Na mwingine anakujaza jeuri,ila kaachana na mwenzake hana la kukujenga kulinda wewe msiachane,mpaka awe mtu mwenye busara sana wakutumia mapungufu yake kuongoza wengine.
👉Mwingine hajaingia kwenye ndoa ndo anakuteka na kukujaza jeuri,hajui umuhimu na uchungu wa ndoa(TUMIA AKILI)
*_Kwenye Post yangu moja nimesema, Ukiona Umepata ndoa,Jaribu kutumia Akili yako yote na nguvu zako zote kuilinda,kuna watu miaka inasonga 30s,40s,50s hawana ndoa wana viruka njia(au wapo kama wao wametulia,tabia safi,elimu ipo,pesa ipo) ila no Partner wanatamani walale waamuke wakute wanaitwa Mr/Mrs ndoto hiyo haijawai timia,wanatamani wampate hata huyo mwenye mapungufu lakini haji...Linda ndoa yako._*( By Ev Elisha Kazimoto 0755444078)
👉 _Kuishi kama *Single Mother, single Father Siyo dili* kuna wengine kwa tabia zao Feki na ovyo wamejikuta wameachika halafu wanatamba na kujisifu eti maisha ya kuishi peke yako Raha Sana, Hakuna Stress..... Uongo mkubwa,miongoni mwa watu wenye Stress kubwa na Chungu, kuliko ambaye hajaolewa ni Walioachika Kizembe halafu Hawajaolewa tena,hawa wana stress ambazo ni sumu hata kuwa sikia usitamani kusikia story zao_ kuna wale waandaaji wa vicheni pati hawa watu *Si wakupewa Maiki kuzungumza* wana sumu mbaya kwa watoto wetu wa kike,uchungu wote wa kuachika wanaumimina kwa wadada wanaoenda kuanza maisha mapya ya ndoa,wanajifanya wanawapa mbinu za kukomaa wao kama wao watengeneze maisha wasitegemee mme kumbe anakupa mbinu ya kuachika. *Wewe Mama Rudi kwa Mmeo* mama yako anayekushikiria hapo yuko na Mme wake ambaye ni Baba yako.
*_Mwisho niseme baba huyu, atulie aombe,aende amwambie mama mkwe na baba mkwe na mke wake wote 3 hivi, Mke wangu njoo,rudi nyumbani tujenge maisha yetu,tulee watoto wetu, maisha ni yetu wawili,tulipendana katika mazingira haya,na umaskini na utajiri ni vipindi vya maisha kama ulivyo usiku na mchana,ambacho hatujui ni masaa(saa ngapi),ifike asubuhi au usiku ila mchana unakuja twende nyumbani. Wazazi wape neno la Hekima, kwamba wazazi wetu,tunategemea ninyi mtushauri na kutuunganisha katika changamoto zote za kimaisha ili nasi tuwaandalie watoto wetu maisha ya baadaye,maisha ni mabadiriko yanayo ratibiwa na Mungu huwezi jua baada ya muda mimi nitakuwa msaada wenu,kutoka katika changamoto hizi zote maisha yaweza badirika kwakuwa uchafu wote nilisha uacha na sasa nina Mungu muda wowote naweza kunena lugha mpya ya maishavmapya ya mafanikio. Mruhusuni mwanenu ambaye ni mke wangu twende tujipange na maisha,kukaa hapa si Suluhisho ila nikuanzisha historia mpya ya kuitwa aloachika,aliyeshindwa ndoa. Na maneno mengine mengi sema na mkeo akuelewe. Akigoma Rudi ukae nyumbani kimya mwombe Mungu mkeo atajileta mwenyewe bila kufuatwa_*
Imeandaliwa na Mwanasaikolojia na mchambuzi wa masuala ya ndoa na Mahusiano *Ev Elisha Kazimoto*
Whatsapp 0755444078
Facebook Ekisha kazimoto
No comments:
Post a Comment