Wednesday, 29 August 2018

MAHUSIANO NI INTIMACY I

❤❤ *RELATIONSHIP IS ALL ABOUT INTIMACY(MAHUSIANO UJUMLA WAKE NI UKARIBU)*❤❤
     *Sehemu ya I*
     By Ev Elisha Kazimoto
    Whatsapp 0755444078
   Facebook Elisha Kazimoto.
_Shalom wana mahusiano,kwa mara nyingine Mchambuzi wa Masuala ya Mahusiano na Ndoa  Psychologist & Counselor Ev Elisha Kazimoto,nakuletea Kipengele cha Kisaikolojia kinachoblinda Mahusiano na Kuonyesha uhai,harufu nzuri katika mahusiano yoyote,yawe ya kiurafiki,kiuchumba,kindoa hata Kiroho,ukikosa haya umeokosa vitu vikubwa mno,waweza jikaza kusafiri katika ulimwengu wa Mahusiano ila utafika umechoka au waweza usifike mwisho wa safari,au ukafika na makovu mengi na majeraha mengi_.
❣Ukweli ni kwamba wana mahusiano wengi,wanaendesha mahusiano yao *_Kiugumu ugumu_* na si kwamba wanafurahia,au hawaoni kuwa ni mapungufu,ila hawana namna ya kufanya,wengine ni matokeo ya kimfumo,wengine ni matokeo ya Kihistoria,wengine ni matokeo ya Kutopenda kujifunza mambo mapya,wengine ni *Ujuaji wa Kutojua* haya yote yamefanya mahusiano mengi ya wana mahusiano Kuishi kiugumuugumu( _Hapa si wana wa Giza wala wana wa Nuru_)wote wanapita katika ugumu ugumu.
❣Kisaikolojia, *Mahusiano yanajengwa na Ukaribu* na ndo maana ya mahusiano (Ukaribu/Intimacy )ndo uzaa neno Mahusiano kama hakuna Intimacy/ukaribu Kisaikolojia hakuna Mahusiano kuna *Kushikiriana* Neno KUSHIKIRIANA hakina Taste ya Love(maana yake kuna Conditions/Mazingira Hali zinazo wafanya Kuwa wote ila isingekuwa hizo hakuna sababu ya kubaki katika mahusiano hayo).
❣Kisaikolojia kuna mahusiano *Hai*, Mahusiano yaliyo *Poa* mahusiano yaliyo *Kufa* katika aina zote hizi watu wapo wanaoishi katika aina hizi zote, Aidha yaliyo Hai, au uwe kwa yaliyo Poa,au yaliyo Kufa.
❣Raha ya Mahusiano yoyote yawe na Intimacy/Ukaribu, ukaribu ukikosekana ndo unazaa Kupoa,kupoa kunazaa Kufa. *_Marafiki wengi wanaoelekea uchumba au uchumba umeyeyuka na wengine kuishi kwa Stress/Msongo wa Mawazo kwa namna ya mahusiano yalivyo,hawafurahii mahusiano ila wanaenda kwasababu Anatamani aolewe,au aoe,au kwakuwa ameisha lipa mahari,au kwakuwa amepita mahusino mengi sasa anaona na haya nayo avunje atakuwa wa nani sasa,au umri umeenda ngoja ajikaze waende hivo hivo ila HANA RAHA NA MAHUSIANO HAYO_*
❣Ndoa nyingi zimebaki zikishikiriwa na WATOTO, KIAPO CHA MADHABAHUNI,KUOGOPA UPWEKE AKIAMUA KUACHANA NA MWENZAKE, BASI WOKOVU HAURUHUSU KUACHANA WALA KUCHEPUKA. Hayo ndo yameshikiria ndoa, ila SI INTIMACY/UKARIBU.
❣ *Wana Mahusiano yoyote, Intimacy Ndo inayoshikiria Mahusiano ya uchumba na Ndoa, hata Wokovu wetu unashikiriwa na Intimacy na Mungu wetu* ukipoteza Intimacy umepoteza Raha na Radha ya Mahusiano na Ndoa.
❣❣ *INTIMACY/UKARIBU UNAZAA MAMBO YAFUATAYO*❣❣
1⃣Intimacy inazaa Upendo kati ya wanao usiana kwa mahusaino yoyote. Ukaribu katika Fikra,katika Matendo usipo kuwepo mtakuwa hamna upendo ila mna KIFUNGO/Kinyume cha Upendo ni Kifungo maana upendo ni Hisia Huru. Sasa kifungo ni Kulazimika Kukaa na huyo kwasababu hakuna namna nyingine(kwa waliookoka)wasiookoka hapo ndo Unapiga chini unatafuta mwingine.
2⃣Intimacy inazaa KUAMINIANA. Ukaribu ndo kunakupa kumjua mwenzako,madhaifu yake na kuyabeba,uwezo wake na kuupa nguvu na Kumwamini. *_Intimacy isipo kuwepo, Hakuna Kuaminiana_* Mahusaino mengi ndoa nyingi WANAISHI BILA KUAMINIANA, Hapo Hakuna pepo,wala uchawi Ni mtu Binafsi Uwezo wake wa Kujenga Ukaribu/Intimacy ni mdogo mno kutokana na Kuishi maisha ya Kimfumo(Kabila,familia,misimamo binafsi),Historia za misha ya awali alikopita,Kutokubali mabadiliko ya Kujifunza, Ujuaji wa Kutojua.
👉Kuaminiana kuna kua kulingana na LEVELS za Mahusiano mliyopo na Time ya kukaa katika mahusiano.
👉Mahusiano ya urafiki yana kuaminiana kwa kawaida,uchumba kuaminiana kunaongezeka maana na Intimacy imeongezeka, Ndoa ndo Kuaminiana kunaongezeka sana maana na Intimacy imekuwa kubwa kiasi cha Ku share Miili. _Ila maajabu ya Kisaikolojia ni kwamba, wan ndoa ndo Hawaaminiani kwa level ya juu sana_ Shida hapa ni Ugumu wa Fikra, Imani Potofu.
3⃣Itimacy ina zaa Kumfurahia Mwenzako na Amani. Ni ukaribu wenu ndo unaopelekea kumfurahia mwenzako, awe karibu au mbali moyo unamfurahia,moyo Amani naye. Huu mdo ustawi wa mahusiano na ndoa.
👉Kama hakuna Ukaribu, mwenzako awe mbali au awe karibu unamuona wa kawaida,na uhisi chochote juu yake( *Mahusiano yaliyo kufa*)
4⃣Intimacy inazaa *Mawasiliano hai* huu ji ugonjwa wa wana mahusiano na wan ndoa. (Problems in Communication )Mahusiano yoyote yaliyo hai nadhihirika katika mawasiliano na katika mawasiliano tunaangalia ( *Propose/Sababu ya kuwasiliana, State of Communication/Hali ya mawasiliano(lugha,sauti, na Awamu za mawasiliano/levels)*
👉Mawasiliano kwa wachumba na wana ndoa baadhi yamekuwa ni *Makavu,ni Viporo* kwa kisingizio cha Ubize,mambo ya kitoto,ya kujishaua,ya wale waliooana wenye mchecheto bado( *Hizi uwa ndo lugha za watu walioona wao Wamefeli kwenye kipengele hicho*) sawasawa na wanaosema HAKUMA MTAKATIFU DUNIANI, baada ya wao kufeli kuishi maisha matakatifu wanahisi na wengine wote wameshindwa.
👉Wana mahusiano wengi na wana ndoa wamebaki kuwasiliana *_Matatizo,Maagizo na kwa Dharula ikitokea_* (Purpose)
👉Na wengine wanawasiliana kwa Sauti isiyo Vutia,isiyoonyesha utaofauti wa Intimacy na mtu baki,na wengine kwa lugha ya Ukali na Kufoka(State of communication)
👉Wengine wanawasiliana kwa kipindi Kirefu kuondoa LAWAMA(Level/Times)
👉Mfano,mwenzako mmeachana kwa muda kikazi au kimajukumu(hasa mliokazini) yale masaa 12 ya kazi mpaka 14 _Unawasiliana na mwenzako mara ngapi kwa sms,au call?_ au Umesafiri kwa siku1 hadi mwaka nk, mara ngapi unawasiliana na mwenzako kwa siku nzima 24hrs? *_Hiyo inaonyesha Intimacy yenu au Distance yenu na aina ya mahusiano mlio nayo_*
👉 Kuna wengine wanao wasiliana kwa *_Care & Love,(Purpose ),Kwa lugha ya kupenda,kuthamini,(State of communication)na mara kwa mara(Level/Times)_* hawa watu Mahusiano yao yatakauwa Imara, pamoja na changamoto nyingine kuwakumba lakini Mahusiano yao ni Imara.
❣ *Mahusiano siyo kujivunia Kutoa Matumizi yote ya Familia(mama au baba),hiyo ni Sawa na Kujivunia kutoa sadaka na zaka kanisani lakini HUNA MPANGO NA IBADA* ibada ni Fellowship na Mungu(Intimacy)ndo lolote analolifanya   kwa Mungu lina maana. Hivyo hivyo, Mwenzako anahitaji INTIMACY kwanza ndo lolote utakalo fanya litakuwa na Maana Kwake.
*_Hii ni sehemu ya Kwanza ya Lecture hii ya Mahusiano ujumla wake ni Ukaribu,usikose sehemu ya pili ya mwendelezo wake_*
Mchambuzi ni Mwanasaikolojia na mchambuzi wa masuala ya ndoa na Mahusiano Ev Elisha Kazimoto
Whatsapp 0755444078
Facebook Elisha Kazimoto

No comments:

Post a Comment